Ujenzi wa barabara inayounganisha mikoa mitatu ya Dodoma, Tanga na Singida itapitia maeneo gani?

Ujenzi wa barabara inayounganisha mikoa mitatu ya Dodoma, Tanga na Singida itapitia maeneo gani?

Sasa Kuna shida gani mzigo wa Mombasa au Dar ports kupitia Bandari ya Tanga?

Wajenge haraka Sana

..washindani ni bandari za D'Salaam vs Mombasa.

..bandari ya D'Salaam tuna advantage ya kuwa karibu zaidi na Rwanda na Burundi ukilinganisha na Mombasa.

..sasa kuna barabara ya Mombasa -- Taveta -- Holili ikijengwa itapunguza umbali wa kutoka Mombasa kwenda Rwanda na Burundi kupitia Tanzania.

..baadhi ya wachambuzi wa masuala ya usafirishaji wanaona hali hiyo itailetea matatizo bandari ya D'Salaam.

..Naomba kusahihishwa kama nimekosea.

cc Geza Ulole
 
Mkuu ukitaja Mvomero, tayari umetaja mkoa wa Morogoro na Prof mbarawa hakuutaja mkoa wa MOROGORO, bali alitaja Tanga,Dodoma kwenda Singida

Wewe shida Yako ni barabara inapita wapi au waziri kataja kitu Gani?
 
Dodoma na Singida zipo katikati ya Tanzania, Tanga ipo pembezoni mwa Nchi huwezi kufika Dodoma na Singida pasipo kupitia Mikoa ya Iringa, Morogoro, Manyara, Tabora na Mbeya.

Waziri atakuwa anadhani bado yupo huko Kwao Zanzibar.
Dodoma Kiteto kilindi handeni tanga hakuna changa la macho
 
Una akili ya kijasusi. Kuna maendeleo mengine tukiyafanya ni hasara. Mimi naona kwa sasa hiyo mikoa imeungana. Wilaya ziungwe ungwe lakini sio kuwa na Highway from Tanga to Singida. Itakuwa shortcut kwa Mombasa na tutajimaliza kiushindani.

..@Geza Ulole amenisahihisha kwamba barabara tishio ni Mombasa--Taveta--Holili.

..mimi nadhani barabara hiyo ijengwa baada ya SGR kukamilika ili bandari yetu isiathirike.
 
Haitafika barabara ya Moro- Dodoma bali itapitia Wilaya Chemba..kwa Mtoro kuelekea Singida ambapo itapitia Makyungu na itaishi njia panda ya Makyungu na Arusha road
Kwa hiyo itafika Kibaya Kiteto kuelekea Chemba?
 
Kwa hiyo itafika Kibaya Kiteto kuelekea Chemba?
Bila shaka, naomba nisikuhakikishie sana.
Ninachofahamu itapitia kilindi hadi Chemba inaungane na barabara ya Kwamtoro kwenda Singida na itatokea njiapanda Makyungu Singida
 
Dodoma na Singida zipo katikati ya Tanzania, Tanga ipo pembezoni mwa Nchi huwezi kufika Dodoma na Singida pasipo kupitia Mikoa ya Iringa, Morogoro, Manyara, Tabora na Mbeya.

Waziri atakuwa anadhani bado yupo huko Kwao Zanzibar.
😂😂😂😂we jamaa
 
Zipo options nyingi tu...

Singida - Dodoma - Turiani - Handeni ( hii angalau sehemu kubwa ni lami)

Singida - Dodoma - Engusero - Kibaya - Handeni

Singida - Dodoma - Kondoa - Kibaya - Handeni
 
..@Geza Ulole amenisahihisha kwamba barabara tishio ni Mombasa--Taveta--Holili.

..mimi nadhani barabara hiyo ijengwa baada ya SGR kukamilika ili bandari yetu isiathirike.
Yuko sahihi sana.
Tanga to Singida ni mbali ukitokea Mombasa kwenda Burundi na Rwanda
 
..@Geza Ulole amenisahihisha kwamba barabara tishio ni Mombasa--Taveta--Holili.

..mimi nadhani barabara hiyo ijengwa baada ya SGR kukamilika ili bandari yetu isiathirike.
Ile sio shortcut. Pointi kubwa ninayounga mkono hoja yako hapa ni "shortcut".
 
Hiyo barabara itaunganisha mikoa ya Manyara, Dodoma na Tanga directly lakini pia na Singida indirectly.
Kwa Mkoa Manyara itapitia inapopita barabara ya kokoto/vumbi kutoka Katesh hadi Kondoa. Ikifika Kondoa itakuwa imeungwa na barabara ya Dodoma-Arusha pale Bucha round about karibu na kituo cha kupooza/kuwasha umeme cha TANESCO. Hapo itashuka kilometre kadhaa then itaingia kushoto kama unaenda kiteto. Nadhani itapita Kongwa, Kiteto, Handeni hadi itakapoungana na T2( Chalinze-Segera) au Segera-Himo.
Ikishafika Katesh inakuwa imeungwa na Singida kwa barabara ya Singida-Babati. Na ikifika barabara ya Segera-Himo, inakuwa imeungwa na Tanga moja kwa moja.
Hii barabara ni muhimu sana kwa tanzania hasa kwa bandari ya tanga, lakini pia kwa kenya, bandari ya mombasa.
Hii barabara itatokea handeni na kupita kilindi kiteto kondoa mpaka singida kupitia kwa mtoro na itarahisisha sana isafiri wa tanga to dom
 
Nimemsikia Waziri Ujenzi, Profesa Mbarawa akisema kunaujenzi wa barabara inayounganisha mikoa mitatu ya Dodoma, Tanga na Singida.

Hii barabara mpya itapitia maeneo gani au wilaya zipi ndani ya hiyo mikoa mitatu aliyoitaja?

Mwenye uelewa tafafhali ninahisi Prof. ametupiga changa la macho.

Au ilani ya CCM inasemaje kuhusu hiyo barabara?
Unawasiwasi na mipango ya Profesa? Kitu ambacho kwa akili ya kawaida haiwezekani, Kwa akili za kiprofesa itawezekana. Kaa Kwa kutulia, subiri utekelezaji. Utekelezaji ukikwama kwenye makaratasi usishhangae pia🤣🤣🤣
 
Mkuu ukitaja Mvomero, tayari umetaja mkoa wa Morogoro na Prof mbarawa hakuutaja mkoa wa MOROGORO, bali alitaja Tanga,Dodoma kwenda Singida
Kwahiyo shida utajwe mkoa wa Morogoro?? Haya waziri alisahau kutaja huo mkoa
 
..KENYA wanalilia hiyo barabara ijengwe ili bandari ya Mombasa iongeze ushindani kwa bandari ya D'Salaam kwa mizigo inayokwenda Rwanda, Burundi, na DRC.

..pia kuna geti kule Serengeti nalo wanataka lifunguliwe ili watalii watoke Nairobi waingie Maasai-Mara, halafu Serengeti, na baadae warudi Nairobi.

cc Geza Ulole
Bandari ya Mombasa haiwezi faidika na hiyo barabara kushinda bandari ya tanga
 
Unaweza kukuta kwenye hzo ncha zilizoungana kati ya dodoma na tanga kuna bonge la bonde ambalo litagharimu mahela mengi au haiwezekan kabisa barabara kupita
Hakuna bonde lolote, sema hapo eneo hilo hakukuwa na historia ya barabara, barabara ya kwenda mikoani toka enzi za ukoloni ilianzia dar ama Bagamoyo kwenda Morogoro, na miaka mingi maendeleo ya usafirishaji yalilenga huko
 
Bandari ya Mombasa haiwezi faidika na hiyo barabara kushinda bandari ya tanga

..bandari inayoweza kushindana na Mombasa ni bandari ya D'Salaam.

..Tanga ni bandari ndogo sana kuweza kuilinganisha au kuishindanisha na Mombasa.
 
Nimemsikia Waziri Ujenzi, Profesa Mbarawa akisema kunaujenzi wa barabara inayounganisha mikoa mitatu ya Dodoma, Tanga na Singida.

Hii barabara mpya itapitia maeneo gani au wilaya zipi ndani ya hiyo mikoa mitatu aliyoitaja?

Mwenye uelewa tafafhali ninahisi Prof. ametupiga changa la macho.

Au ilani ya CCM inasemaje kuhusu hiyo barabara?
Katafute Atlas ya Tanzania mkuu.
 
Back
Top Bottom