Ujenzi wa barabara inayounganisha mikoa mitatu ya Dodoma, Tanga na Singida itapitia maeneo gani?

Dodoma na Singida zipo katikati ya Tanzania,Tanga ipo pembezoni mwa Nchi huwezi kufika Dodoma na Singida pasipo kupitia Mikoa ya Iringa,Morogoro,Manyara,Tabora na Mbeya.

Waziri atakuwa anadhani bado yupo huko Kwao Zanzibar.
Mkuu pole sana.
Chukua ramani ya Tz uipitie upya.
Barabara imeanzia Handeni Tanaga, inapitia Kondoa..Dodoma hadi Singida.
kazi imeanza kitamboa baadhi ya maeneo
 
Unataka ukanunue viwanja karibu na barabara
 
Hiyo barabara itaunganisha mikoa ya Manyara, Dodoma na Tanga directly lakini pia na Singida indirectly.
Kwa Mkoa Manyara itapitia inapopita barabara ya kokoto/vumbi kutoka Katesh hadi Kondoa.

Ikifika Kondoa itakuwa imeungwa na barabara ya Dodoma-Arusha pale Bucha round about karibu na kituo cha kupooza/kuwasha umeme cha TANESCO. Hapo itashuka kilometre kadhaa then itaingia kushoto kama unaenda kiteto. Nadhani itapita Kongwa, Kiteto, Handeni hadi itakapoungana na T2( Chalinze-Segera) au Segera-Himo.

Ikishafika Katesh inakuwa imeungwa na Singida kwa barabara ya Singida-Babati. Na ikifika barabara ya Segera-Himo, inakuwa imeungwa na Tanga moja kwa moja.
 

..KENYA wanalilia hiyo barabara ijengwe ili bandari ya Mombasa iongeze ushindani kwa bandari ya D'Salaam kwa mizigo inayokwenda Rwanda, Burundi, na DRC.

..pia kuna geti kule Serengeti nalo wanataka lifunguliwe ili watalii watoke Nairobi waingie Maasai-Mara, halafu Serengeti, na baadae warudi Nairobi.

cc Geza Ulole
 
Si barabara hii wanaolilia ni ile ya Mombasa-Taveta -Holili! Haipitii Tanga!
 
Una akili ya kijasusi. Kuna maendeleo mengine tukiyafanya ni hasara. Mimi naona kwa sasa hiyo mikoa imeungana. Wilaya ziungwe ungwe lakini sio kuwa na Highway from Tanga to Singida. Itakuwa shortcut kwa Mombasa na tutajimaliza kiushindani.
 
Dodoma na Singida zipo katikati ya Tanzania, Tanga ipo pembezoni mwa Nchi huwezi kufika Dodoma na Singida pasipo kupitia Mikoa ya Iringa, Morogoro, Manyara, Tabora na Mbeya.

Waziri atakuwa anadhani bado yupo huko Kwao Zanzibar.

Dodoma na Singida zimeunganishwa kwa lami.

Bila shaka hii barabara itaanzina njia panda ya Kiteto kupitia Wilaya ya Kongwa maeneo kama Ngomai(Kongwa) Engusero, Kibaya, Mbigiri, Pori kwa Pori (Kiteto, Manyara), halafu itaingia wilaya ya Kilindi-Songe then Handeni-Mkata.

NB: Njia ya kwenda Kiteto-Kilindi-Handeni inayoanzia barabara ya Dodoma-Morogoro haina lami. Kwa hiyo nidhani kazi itakuwepo hapo
 
Ila Mbarawa anatupoteza kinamna. Simuamini tena.
 
Acha mihemuko. Ukitoka Dodoma, unaelekea wilaya ya Chemba. Unapita kata ya Farkwa ambapo patajengwa bwawa, unapita kata ya Kwa mtoro then unatokezea Ikungi (Makiungu) ndio unaingia Singida mjini. Ni bonge moja la short cut...
 
Sasa Kuna shida gani mzigo wa Mombasa au Dar ports kupitia Bandari ya Tanga?

Wajenge haraka Sana
 
Acha mihemuko. Ukitoka Dodoma, unaelekea wilaya ya Chemba. Unapita kata ya Farkwa ambapo patajengwa bwawa, unapita kata ya Kwa mtoro then unatokezea Ikungi (Makiungu) ndio unaingia Singida mjini. Ni bonge moja la short cut...
Hayo huwa Ni majinga unajichosha tuu bure Mimi nimeamua kuyaacha na upuuzi wao.
 
Haitafika barabara ya Moro- Dodoma bali itapitia Wilaya Chemba..kwa Mtoro kuelekea Singida ambapo itapitia Makyungu na itaishi njia panda ya Makyungu na Arusha road
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…