Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Tatizo lako mkuu huwa unaongozwa sana na Chuki na hisia. Mimi siamini Kama eti wewe hujui kilichokwamisha mradi kwa yale makubaliaono ya kwanza kule Tanga na Kama kweli hujui basi si mfuatiliaji wa mambo hata kidogo na Kama ni mfuatiliaji utakuwa unajua Ila tu unabisha na kupinga Kama ilivyo kawaida yako siku zote.
Hii hoja yako nimeiona mara kadhaa kwenye ule uzi wa taarifa rasmi ya tukio la leo, nikashangaa imekuwaje wewe ulie mtu makini ukashindwa kujua kilicho endelea na kinachoendelea. Sikutaka kuijibu kwakweli unajua wakati mwingine ni burudani kuona watu wanavyojifanya wajua na wenye akili kubwa kumbe hakuna kitu wanajidanganya wenyewe.
Naona umesema naongozwa na chuki kama defending mechanism yako, ni kipi kipya hivi sasa mpaka niamini kilichofanyika leo? Hivi kwa akili ya kawaida kabisa Tanzania wanaweza kupata 60% kisha Uganda wapate 40%? Je hao total wanapata kiasi gani? Huo mradi sio wa kwetu bali sisi tulitoa njia tu ya huo mradi kwa kutegemea commission ya mauzo ya mafuta, na Museveni alishindwana na Total ndio maana mradi ukasimama. Ila hiki cha leo ilikuwa ni kampeni zaidi kuliko mkataba husika.