Ujenzi wa Reli ya SGR uishie Tabora

Acha iishe tuu reli ni muhimu sana, na zisipotumika hapo zitaishia kujenga matundu ya choo for same amount of money
 
Mlikuwa wapi kulisemea hili mwanzoni mpak now mradi upo on-air
Yaani ulitaka amkosoe JPM? Hajitaki? Angeishia kutukanwa na kuitwa kila aina ya majina, na wasiojulikana nao wangemtembelea! IRA UDSM ilivunjwa yote na maprofesa wake kutukanwa kisa tu walimshauri "Mungu Mtu" yale asiyotaka kusikia kuhusu mradi wa Rufiji! Prof. wangu wa UDOM alitukanwa hadharani kisa tu aliongea ukweli kuhusu Makinikia
 
Mkuu kavulata , kwanza asante kwa mawazo yako. Sii wengi humu wanajua how SGR can operate profitably!. Ili SGR iweze kuleta faida ni lazima iwe na kitu kinachoitwa linkages. Mfano hiki kipande cha Dar Moro ambacho kiko tayari, kiteendeshwa kwa hasara muda wote hadi SGR itakapo link na Rwanda, Burundi, Uganda na DRC.

Karibu mitaa hii

Pia kasome
P
 
Ipo TAZARA, kwa nini isitumike kwa ufanisi?
 
SGR inakwenda kuwasaidia Wapiga Kura Mwanza. Full stop!
Chuki ilikuwa kubwa mno mno mno dhidi ya kanda nyingine, hasa kaskazini, Mashariki na kusini, nchi ilikuwa ikijengwa upande mmoja zaidi. Tulishuhudia miradi mikubwa ikimiminwa kuelekea kanda moja na idadi ya mikoa ikiongezwa upande huo. Hata kuhamia Dodoma kwa nguvu ilikuwa kusogeza huduma karibu na kanda pendwa sio vinginevyo.
 
Ahsante mkuu, hata mm kuna uzi humu niliwahi kuandika kuhusu ni nini kitasafirishwa kwenye SGR ili tupate faida? Tukumbuke kuwa faida ya SGR itakokotolewa baada ya kutoa faida iliyokuwa ikitokana na usafirishaji kwa njia malori, mabasi ya abiria na reli ya kati (opportunity costs). Ndio maana mimi nikapendekeza reli hii ghali sana kujenga na kuendesha ya SGR ingeishia morogoro, Dodoma, Singida au Tabora tu kusaidia kuondoa msongamano wa malori bandari ya DSM na "Bagamoyo" kwa kuisogeza mizigo Morogoro, Dodoma, Singida au Tabora ili biashara ya malori, mabasi na reli ya kati isife
 
Kila mjinga leo anatoa ushauri wa kichekesho.
Kuna ombwe pahala ukiona hivyo. Itafika pahala kila mtu atajitengenezea ndama wake wa dhahabu na kumfanya Mungu wake.
 
Wanasema reli ni huduma hata kama faida isipokuwepo, tutasafirisha ng'ombe na wapiga kura wetu.
 
Tunatakiwa tujue Kwanza sababu ya uelekeo wa sgr kuwa huo na sio huko unakosema, pengine Kuna sababu za maana zaidi kuliko unavyofikiria
Hata hivyo kutoa mawazo mbadala baada ya mradi kuanza hakusaidii taifa, mawazo yako ungeyaibua kabla ya upembuzi yakinifu watu wakajadili hapa pengine wangeyaona wahusika.
 
Ungekuwa ujinga uliopitiliza kujenga SGR kando ya TAZARA kuelekea Zambia tena kama ulivyo kujenga SGR na barabara nzuri kandokando ya reli ya kati hadi Mwanza. SGR, barabara na reli ya kati lazima zicheze pamoja kwenye uwanja mmoja kila mtu na nafasi yake ili kupata synergism. Lazima kuwe na kazi Meli, kazi ya SGR, kazi ya Barabara na kazi ya reli ya kati, maana vyote ni vyetu na hatutaki vife. Kuna kodi, ajira na huduma kwenye meli, SGR, malori na reli ya kati pia. Do not strengthen the weakest by weakening the strongest.
 
Wazo mama la kujenga SGR kuelekea mwanza haikuwa biashara na faida bali huduma ya haraka sana ya bei nafuu kutoka mwanza kuja Dsm.
 
Reli ikiishia tabora,hatutapa mapato ya fedha za kugeni wacha tuimalize tu hadi kigoma

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Akili ndogo kweli
 
Mzigo wa Rwanda, Congo DRC, na Zambia unaoingia kupitia bandari kwa mwaka ni tani ngapi kwa kila mmoja?
Umeandika kitu Cha kufikirisha Sana, maana huwezi kukosoa bila kuwa na data ya mizigo inayotoka sehemu husika.
Mwenye data atuletee Kwanza hapa tuone
 
..Dar to Kapirimposhi ni reli ya Tazara.

..Tujiulize kwanini reli hiyo inaendeshwa kwa hasara?
Kabisa, reli ya TAZARA ni Ipo vizuri kuliko Reli ya Kati, lakini inaendeshwa kwa hasara kubwa, na hii reli ya TAZARA inafika hadi huko Kapirimposhi
 
Reli ikiishia tabora,hatutapa mapato ya fedha za kugeni wacha tuimalize tu hadi kigoma

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Hapa tunaongelea ukosefu wa hela ya kujengea SGR yote sawa na mpango. Ndio maana tunashauri badala ya kuicha hela yetu ipotee bure kwa kutokamilika kwa ujenzi na badala ya taifa kukopa zaidi ili kujenga SGR the least evil ni kukamilisha ujenzi hadi Tabora tu. Pale Tabora zitafutwe ekari kama 1000 hivi za kujenga bandari kavu ya mizingo ya Mwanza na vitongoji vyake, kigoma, DRC, Rwanda, Burundi ili kupunguza umbali wa kuja bandari ya dsm. Tukifanya hivyo kutakuwa na faida zifuatazo:
1. Wateja wetu wataishia Tabora tu.
2. Barabara zetu kutoka dam hadi tabora zitapunzika sana.
3. Biashara ya malori, mabasi na reli ya kati ambayo yalikuwa yakose kazi itaendelea.
4. Mji wa Tabora utaendelea kiuchumi na kijamii.
5. Ajira itakuwa kubwa kanda ya kati pale
6. SGR itafanyakazi kuliko kutelekezwa kabisa.
7. Madeni ya ujenzi wa SGR yatapungua
8. Tutapata uzoefu wa kuendesha SGR (pilot study)
9. Faida tutakayopata itamalizia vipande vilivyosalia (capacity building)
 
Ipo Reli ya Tazara, inakufa tu pale. Wafanyabiashara weengi wanaiogopa sababu ya Delay ya mizigo. Kumbuka Biashara ya Reli kusafirisha mizigo inaua biashara ya Malori ambayo meengi ni ya viongozi katika hizi nchi, yaaani Zambia na Tz.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…