Ujenzi wa Reli ya SGR uishie Tabora

Ujinga ni kuwaza nchi nyingine na si kuwaza raia wako higi mizigo inayotoka mikoani kwenda mikoa mimgine ni michache sana kulinganisha na mizigo ya burundi?
tuache ushamba reli hii ni ya raia wa kitazzania sio waburundi au waganda.

narudia watanzania tuache ushamba wa wageni
 
Tazara unaijua?
 
Sasa kusini si ipo Tazara, mbona haijawa utilized?,
Kanda ya ziwa pia ina mizigo,, pamba, mahindi, alizeti, viazi etc
 
SGR Kwenda mwanza kwanza haina tofauti na ulivyojengwa uwanja wa ndege mkubwa chato
Mawazo ya kijinga na chuki tu,Kama huduma ktk nchi hazitakuwapo tutakuwa tunarudi kwenye safari ya dar unapita Nairobi wabinafsi nyie nchi yote laxima ijengwe kulingana na Hali ilivyo.ndiyo maana mwingereza alioongeza tawi la Mwanza kwenye reli ya Kati baada ya kuona umuhimu wake.happy new year.
 
Transporter wengi watakosa kazi,,, [emoji23]
 
Sisi hatina dira ni watu wa kukurupuka huko Zambia si kuna tazara lakini haitumiki ipaswavyo hatuna watu wanaoweza kutupigisha hatua
 
Ipo TAZARA, kwa nini isitumike kwa ufanisi?
TAZARA haileti faida kwa muda mrefu. Tulionywa na Waingereza kuwa Mozambique Zimbabwe South Afrika na zitakapopata Uhuru TAZARA itakuwa redundant na hicho ndicho kilichotokea.Labda mradi wa kuchimba udongo wa chuma na mkaa wa mawe Liganga na kuna maeneo mengi tu yenye madini ya kusafirisha in bulk nchini mwetu,ni kuunganisha TAZARA na maeneo hayo.Si madini tu hata mazao ya mashambani,mbao mbolea,na abiria.
 
Wengine tulishaga toa mawazo Kama haya siku nyingi sana

 
Ipo TAZARA, kwa nini isitumike kwa ufanisi?
Habari ya tazara na kushindwa kwake ni suala ya uafrika angalia kiongozi anamtoa kalemani anamuweka makamba unategemea nini hapo zaidi ya mradi kugeuzwa dili za watu binafsi safari tunayo ndefu na tutachoka hasa.
 
SGR ya TAZARA inatosha kabisa kubeba mzigo wa zambia, congo,, shida iko kwenye utashi wa wafanyabiashara wanapendelea malory zaidi kuliko train, sababu kuu itakua ni urasimu nadhani,
SGR inayoenda mwanza, sana sana itapata abiria sana, kwa mizigo sidhani,, wafanyabiashara wanapendelea kutumia malory zaidi kuliko kuhangaika na TRA wakati wa kuutoa mzigo bandari kavu
 
Ili kuacha kukopa wabunge wako tayari walipwe nusu mishahara Na posho ili tupate pesa za kujenga reli kwa pesa yetu wenyewe? Au ndugai anataka nani akamuliwe atoe pesa ya kujenga reli?
Si wananchi?,, Juzi mie balozi wa nyumba kumi kumi amepita, anakusanya mchango kwenda kulipa deni la taifa kila kaya, 50,000 ,, hili deni limetubana sana,,, [emoji23][emoji23]
 
Kipande cha Dar hadi Dodoma kimekamilika?
 
Reli sio kwa ajili ya mizigo tu, ni kwa ajili ya kusafirisha abiria pia.
 
Kwan hiyo bandar inayo jengwa mkoa wa rukwa kazi yake nn na hii teli itapita mpaka mpanda na kuungana hiyo mbandari hapo
 
Lengo la magufuli ilikuwa ni kupeleka sgr usukumani nyengine zote ni geresha tu kama ni uchumi basi train kwanza ingepelekwa kigoma co mwanza sawa sawa na uwanja wa ndege kupelekwa chato.
 
Mkuu,
wazo lako sio relevant tena kwa sasa maana SGR kutoka Ng'wanza kwenda Isaka kazi imeanza na mkandarasi yuko site. Inatafutwa hela ya Tabora-Isaka.



Jan 9, 2021 Mhe. Rais John Pombe Magufuli:
Alishuhudia zoezi la kutia saini ya ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka Mwanza mpaka Isaka. Huu ni mkataba uliosainiwa kati ya Tanzania (TRC) na China (CCECC). Hii ni awamu ya tano ya ujenzi wa reli ya treni ya umeme nchini






JUNE 14, 2021
Rais SSH akizindua ujenzi wa SGR
 
Mbona Tazara ipo , au Bandari ya jiografia huku aka sana
 
Ni kweli kabisa. Sasa kuna huyo aliyeandika kuwa SGR ingeelekezwa huko, ikabidi nimuulize hivyo, labda hakujua kuna TAZARA.
 
Habari ya tazara na kushindwa kwake ni suala ya uafrika angalia kiongozi anamtoa kalemani anamuweka makamba unategemea nini hapo zaidi ya mradi kugeuzwa dili za watu binafsi safari tunayo ndefu na tutachoka hasa.
Habari ya uafrika unajidhalikisha mwenyewe.
Ni muhimu kujua kuwa waziri siyo mtendaji na waizara inaweza kufanya shughuli zake zote kwa ufanisi kupitia wataalam wakiongozwa na karibu mkuu.
Kudanganyana na kelele za kisiasa ndizo huaminisha wasiojua kuwa waziri ndiye muhimu.
Miradi haijengwi na waziri, ni wataalam wa wizara, waziri kazi yake kusimamia sera. Sidhani kama kuna sera ya wizi.
Hata hivyo, awepo Kalemani au Makamba, kwangu na watanzania wengine wenye mapenzi mema kwa taifa tunataka miradi ikamilike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…