Ujinga ni tatizo kuu hapa Tanzania

Kwa kifupi wapingaji hawana hoja za msingi
 

Well sijui hao wengi lkn ukiona wengi wanapinga ina maana hawataki kwa nini muwalazimishe wakati wengi hawataki? Demokrasia ni kusikiliza wengi isitoshe tumeshaumizwa sana hivyo tutakuwa ni wajinga kama tusipotaka kuwa waangalifu kwani wanaotetea dp world ndio wale wale pia waliotetea kuuzwa kwa shirika la reli kwa wahindi, ndio wale wale waliotetea uwekezaji wa migodi ya dhahabu ambapo sasa yamebakia mashimo na hakuna tulichofaidika, hivyo its human kama ulishaumizwa kuwa mwangalifu …
 
Mbona Dp world Imepewa bandari kadhaa China. Nadhani issue iwe tu mkataba wa kimaslahi ila hata china wao maendeleo Yao yalikuja kwa mitaji ya kigeni.
Kama ni hivyo jengeni hoja kwa kushauri serikali sehemu pa kufanyia marekebisho kwenye mikataba siyo kuleta lawama jumuishi kama mleta mada...inakera sana.
Serikali nayo viongozi wanaleta mikataba mibovu inayoingia na hao wawekezaji huku wakitoa lawama kwa wafanyakazi wanaoendesha taasisi zinazodaiwa kushindwa kujiendesha kwa faida.

Ebu fikiria wanasiasa wanafanya makosa lakini hawachukuliwi hatua za kinidhamu alafu unataka mfanyakazi hapo TPA wao wawe Mungu walionee nchi huruma...Akina Musukuma hawalipi kodi kwenye biashara zao zote lakini ndiye wa kwanza kuilaumu wafanyakazi wa TRA na TPA...ukitaka kuwawajibisha viongozi wa juu wanapiga simu yenye vitisho.
 
Kwa hiyo bi Tozo alipelekwa wapi kujifunza uwekezaji?

Shida mnakwepa ukweli

1. Ukomo wa mkataba
2. Kwa nini Zanzibar hazihusiki?
3. Analeta mtaji kiasi gani kuwekeza
4. Mapato na kodi zetu zimekaaje?
5. Sharti la kupewa ardhi yoyote anayotaka na tuwalipe sisi tutakaowandoa anapopataka boss
6. Kutokuvunja mkataba hata akiboronga.

Hatupingi uwekezaji ila tunapinga mkataba mbovu
 
Una uhakika hayo unayosema yapo hayajatolewa ufafanuzi?
 
Acha mboyoyo, tuambie ni wapi watanzania wameukataa uwekezaji?

Wanachokataa ni utapeli kupitia bandari
 
Kwa Dunia inavyokwenda sasa, Tanzania haipaswi kurudi nyuma tena! Ujinga usipewe tena nafasi Tanzania!
Huelewi unachokiandika juu yake.

Uliambiwa kuwa "communist" ni kujitenga na dunia nyingine?

Huko kwenye "ubepari" kuna mahali popote wanaposema ni lazima kila nchi iwe na mfumo sawasawa na mkuu wa hao mabepari?

Sasa wewe unayekariri, nawala hutaki au huna uwezo wa kutumia akili zako na kudadavua lipi linalofaa kwa wananchi wa hapo ulipo, tuelewe wewe ndiye mtetezi mkuu wa ubepari?

Mbona hata huko kwenye ubepari bado kuna mambo ya kikomunist yanafanyika?

Uliambiwa kwa Tanzania kuwa nci ya kibepari kwelikweli ni lazima iuze kila kitu ilichonacho kwa hao mabepari watakaokuja kukuletea maendeleo hapa?

Huyo Deng, alipofungua nchi, wachina walibweteka kwa kujua mabepari wanaleta maendeleo?

Ni ajabu sana kwa mtu mwenye akili kudhanikwamba maendeleo yaliypo China yamletwa na watu kutoka nje. Hii akili siyo ya kawaida kabisa.

Mwisho, ngoja nikiri kwamba andiko lako refu sikulisoma. Lakini ninajua takataka ambazo wewe hupenda kuzitetea hapa JF.
 
Unaanza kwa kusema sielewi nilichoandika unamalizia kwa kusema hujasoma chote nilichandika. Ndo mana nikisema ujinga kwa watanzania ni tatizo nielewe ndugu.
 
Unaanza kwa kusema sielewi nilichoandika unamalizia kwa kusema hujasoma chote nilichandika. Ndo mana nikisema ujinga kwa watanzania ni tatizo nielewe ndugu.
Nimekueleza msingi wa nilichojibu. Hukusoma hilo?
Nimesoma mistari ya mwanzo nikaona hadithi ni zile zile za siku zote, sikujihangaisha tena kupoteza muda na andiko refu hilo lenye mambo yale yale ninayofahamu unayatetea kila mara humu.

Na kuhusu huo "ujinga" nilitaka kulisemea hilo, lakini nikaghaili.
Ngoja nikuache kwa sasa kuhusu hili la "ujinga."
 
Uwe na jioni njema
 
Ila ni kweli kabisa
Nchi ya kifala sana hii
Nimeshuhudia Warundi wakiingizwa usiku pale NIDA Chang'ombe kwenda kutoa alama za vidole, kulikuwa na afisa wa NIDA na Mlinzi wa SUMA JKT, kila Mrundi aliliwa jiwe tatu 300,000 daadeki, halafu kuna watu humu wanalilia uzalendo kwe kwe kwee😆😆

Kulikuwa na Warundi kama 28 hivi so do the maths.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…