Ujinga ni tatizo kuu hapa Tanzania

Ujinga ni tatizo kuu hapa Tanzania

Kazi ya Serikali ni kukusanya kodi, kusimamia Sheria na kutoa huduma za msingi tu. Hayo mengine Serikali mnaionea
Kukusanya Kodi nako wanafeli mbona? Hivi unajua hasara tunayoipata kupitia transfer pricing maana TRA inaweza audit 10% tu ya hayo makampuni makubwa!!

Tuseme tu public sector haina ufanisi kabisa pengine ni kuajiri watu wasio na experience au shida ni hizo ajira za kudumu mtu anajua whether akiperform or not mshahara upo na promotion ni mandatory.
 
Enzi za Mao, China ilikuwa nchi ya kikomunisisti iliyoamini katika Sera za Ukomunisti.

Pamoja na Ukomunisti wa China, Rais wa kwanza wa China, Mao aliamini kuwa ni lazima apeleke vijana nje ya China wakajifunze Dunia inaendaje na ikoje ili warudi kufanya mabadiliko China.

Moja ya vijana hao alikuwepo Den Xiapoing ambaye alikuja kuwa Rais wa China baada ya Mao. Den alipelekwa Ulaya na akajifunza sana namna uchumi wa Ulaya ulivyokuwa unaenda.

Alipokuja kurudi China, Den alianzisha mfumo wa Private Property na Uwekezaji wa Sekta binafsi katika mfumo wa Uchumi wa China. Kipindi chake ndo makampuni mengi ya Marekani yalienda kufungua viwanda na kufanya uwekezaji China.

Kwa wachina wengi walimuona Deng ni msaliti wa Mao kwa kuwa wengi walikuwa wanaamini kila kitu ni cha wachina na mwekezaji kutoka nje ni mwizi. Den aliwajibu haijalishi kama paka ni mweupe au ni mweusi ili mradi anakamata panya basi huyo anatufaa

Pamoja na wachina kupata shida kuelewa Sera za Den Xiapoing ila leo ndo wachina wanamsujudu kama The Father of Modern China.

Ukiacha China kuna nchi za Singapore na Umoja wa Falme za Kiarabu ambao Dubai ni nchi mojawapo za umoja huo.

Hizi nchi nazo miaka ya 1960 ilikuwa kama sisi! Ila watawala wao walipata akili kuwa kwa akili za kuwaza sisi ndo sisi hatutafika popote. Kupitia rasilimali ya mafuta Dubai walibadilisha Sera zao kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi. Leo hii kila mtu Duniani anakwenda kutalii Dubai na si kwa sababu ya mafuta tu ila kutokana na namna ikivyojengwa , inavyopendeza na ilivyo na uchumi mkubwa na maendeleo makubwa.

Ukija Tanzania. Hapa ndo shida ilipo. Nchi hii ilianzishwa katika misingi ya kijamaa. Misingi hii iliwaaminisha watu kuwa kila kitu ni Serikali na Serikali ni kila kitu. Mfumo huu ambao unaamini katika state capture umedumaza akili za Watanzania wengi sana kiasi ambacho kuna Watanzania leo hawajifunzi hata dunia ikoje, inaenda wapi na itakuwa wapi miaka hata 50 mbele.

Akili hizi zinaamini kuwa Sera ya uwekezaji ni kuuza nchi, Uwekezaji ni uuzaji wa nchi. Sera hii imewafanya Watanzania kuwa nyuma sana. Nchi yetu kuwa nyuma sana, mifumo yetu ya huduma kuwa nyuma sana.

Leo hii Tanzania, unatoka Dar hadi Kigoma kwa masaa zaidi ya 15 kwenye treni ambayo muda wowote unaweza kuambiwa leo hakuna usafiri. Ndani ya hiyo treni vyoo vichafu, huduma ni mbovu ila mtanzania hana shida ili mradi tu inamilikiwa na Serikali

Leo hii nchi yetu ina bandari zinayoweza kuhudumia ipasavyo nchi hadi 8 zinazotuzunguka, ila meli zinakaa wiki 2 hadi 3 kushusha mizigo, wafanyabiashara wanapoteza mizigo yao, hakuna mapato makubwa nchi inaweza kupata na kufanya maendeleo makubwa ila watu wanaona sawa tu ili mradi iwe chini ya Serikali. Hawajali hata wakiambiwa meli zinakimbia zinaenda Bandari za nchi jirani ili mradi waone au wasikie Serikali ndo mmiliki. Huu ni ujinga uliotukuka sana.

Kibaya zaidi pamoja na ujinga huu wa Watanzania, nchi jirani zinazotuzunguka zinakimbia sana ili kukamata fursa za kiuchumi sisi tusiwe na kitu. Rwanda amejenga Bandari kavu kubwa sana ili mizigo ya Congo Mashariki ipite kwake . Bandari hii kawapa wawekezaji. Sasa Rwanda anajenga uwanja wa Ndege mkubwa zaidi Afrika Mashariki ambao utaendeshwa pia na Sekta binafsi.

Huku Kenya amejenga Bandari ya Lamu ambayo ataiendesha kwa sehemu kubwa kupitia sekta binafsi, Msumbiji kaomba vikosi vya Rwanda vilinde Bandari zake ili wawekezaji waweze kuwekeza na zifanye biashara. Hawa wakifanya haya Serikali ikichukua hatua kuboresha utendaji wa Bandari kuna watu wanaaza kusema nchi inauzwa.

Serikali ikiwasikiliiza hawa watu kuna hatari kubwa sana huko mbeleni nchi yetu kuja kuwa kituko cha mwisho zaidi kuliko hata sasa, kutokana na kusikiliza wajinga huku nchi ikitakuwa ikimbie iendane na mabadiliko ya Dunia ya sasa.

Kwa Dunia inavyokwenda sasa, Tanzania haipaswi kurudi nyuma tena! Ujinga usipewe tena nafasi Tanzania!
Hapana hatukatai uwekezaji.
Tunachopinga ni kwa nini Mwarabu?
 
Wapi duniani limewai kufanya jambo baada ya wananchi wote kuridhia?
Si lazima watu wote kuridhia, bali ni wengi kuridhia. Kama viongozi wetu hatuwaamini, wanatoa wapi ujasiri wa kufanya jambo ambalo tunaona kabisa haliko wazi, na lina maelezo yenye utata?

Ifahamike hiyo mali sio ya viongozi bali ya umma, na utata unaongezeka zaidi kwani hao viongozi ni wa upande mwingine wa muungano, na huko wanakotokea mali zao sio sehemu ya uhuni huu. Tuna uzoefu na hii mikataba ya wizi boss.
 
Mkataba wa mda gani? Ulee nielezee
Unauliza hapa kwani hujasikia majibu ya Serikali?

Haya ngoja nikwambie. Ule ni framework agreement. Hakuna mradi specific unaotekelezwa kwa mujibu wa mkataba ule na ndo mana hauna muda. Muda utawekwa kwenye mkataba husika wa utekelezaji wa mradi husika.

Umeelewa?
 
Kukusanya Kodi nako wanafeli mbona? Hivi unajua hasara tunayoipata kupitia transfer pricing maana TRA inaweza audit 10% tu ya hayo makampuni makubwa!!

Tuseme tu public sector haina ufanisi kabisa pengine ni kuajiri watu wasio na experience au shida ni hizo ajira za kudumu mtu anajua whether akiperform or not mshahara upo na promotion ni mandatory.
Shida kubwa kwenye Serikali ni wajuzi kupigwa vita na taasisi kutozingatia succession plan. Kiutaratibu Kamishna Mkuu wa TRA lazima awe na utaratibu wa kuandaa watu kuchukua nafasi yake, pia makamishna wasaidizi wanatakiwa kuwaandaa hawa wa chini na sidhani kama hili linafanyika
 
Enzi za Mao, China ilikuwa nchi ya kikomunisisti iliyoamini katika Sera za Ukomunisti.

Pamoja na Ukomunisti wa China, Rais wa kwanza wa China, Mao aliamini kuwa ni lazima apeleke vijana nje ya China wakajifunze Dunia inaendaje na ikoje ili warudi kufanya mabadiliko China.

Moja ya vijana hao alikuwepo Den Xiapoing ambaye alikuja kuwa Rais wa China baada ya Mao. Den alipelekwa Ulaya na akajifunza sana namna uchumi wa Ulaya ulivyokuwa unaenda.

Alipokuja kurudi China, Den alianzisha mfumo wa Private Property na Uwekezaji wa Sekta binafsi katika mfumo wa Uchumi wa China. Kipindi chake ndo makampuni mengi ya Marekani yalienda kufungua viwanda na kufanya uwekezaji China.

Kwa wachina wengi walimuona Deng ni msaliti wa Mao kwa kuwa wengi walikuwa wanaamini kila kitu ni cha wachina na mwekezaji kutoka nje ni mwizi. Den aliwajibu haijalishi kama paka ni mweupe au ni mweusi ili mradi anakamata panya basi huyo anatufaa

Pamoja na wachina kupata shida kuelewa Sera za Den Xiapoing ila leo ndo wachina wanamsujudu kama The Father of Modern China.

Ukiacha China kuna nchi za Singapore na Umoja wa Falme za Kiarabu ambao Dubai ni nchi mojawapo za umoja huo.

Hizi nchi nazo miaka ya 1960 ilikuwa kama sisi! Ila watawala wao walipata akili kuwa kwa akili za kuwaza sisi ndo sisi hatutafika popote. Kupitia rasilimali ya mafuta Dubai walibadilisha Sera zao kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi. Leo hii kila mtu Duniani anakwenda kutalii Dubai na si kwa sababu ya mafuta tu ila kutokana na namna ikivyojengwa , inavyopendeza na ilivyo na uchumi mkubwa na maendeleo makubwa.

Ukija Tanzania. Hapa ndo shida ilipo. Nchi hii ilianzishwa katika misingi ya kijamaa. Misingi hii iliwaaminisha watu kuwa kila kitu ni Serikali na Serikali ni kila kitu. Mfumo huu ambao unaamini katika state capture umedumaza akili za Watanzania wengi sana kiasi ambacho kuna Watanzania leo hawajifunzi hata dunia ikoje, inaenda wapi na itakuwa wapi miaka hata 50 mbele.

Akili hizi zinaamini kuwa Sera ya uwekezaji ni kuuza nchi, Uwekezaji ni uuzaji wa nchi. Sera hii imewafanya Watanzania kuwa nyuma sana. Nchi yetu kuwa nyuma sana, mifumo yetu ya huduma kuwa nyuma sana.

Leo hii Tanzania, unatoka Dar hadi Kigoma kwa masaa zaidi ya 15 kwenye treni ambayo muda wowote unaweza kuambiwa leo hakuna usafiri. Ndani ya hiyo treni vyoo vichafu, huduma ni mbovu ila mtanzania hana shida ili mradi tu inamilikiwa na Serikali

Leo hii nchi yetu ina bandari zinayoweza kuhudumia ipasavyo nchi hadi 8 zinazotuzunguka, ila meli zinakaa wiki 2 hadi 3 kushusha mizigo, wafanyabiashara wanapoteza mizigo yao, hakuna mapato makubwa nchi inaweza kupata na kufanya maendeleo makubwa ila watu wanaona sawa tu ili mradi iwe chini ya Serikali. Hawajali hata wakiambiwa meli zinakimbia zinaenda Bandari za nchi jirani ili mradi waone au wasikie Serikali ndo mmiliki. Huu ni ujinga uliotukuka sana.

Kibaya zaidi pamoja na ujinga huu wa Watanzania, nchi jirani zinazotuzunguka zinakimbia sana ili kukamata fursa za kiuchumi sisi tusiwe na kitu. Rwanda amejenga Bandari kavu kubwa sana ili mizigo ya Congo Mashariki ipite kwake . Bandari hii kawapa wawekezaji. Sasa Rwanda anajenga uwanja wa Ndege mkubwa zaidi Afrika Mashariki ambao utaendeshwa pia na Sekta binafsi.

Huku Kenya amejenga Bandari ya Lamu ambayo ataiendesha kwa sehemu kubwa kupitia sekta binafsi, Msumbiji kaomba vikosi vya Rwanda vilinde Bandari zake ili wawekezaji waweze kuwekeza na zifanye biashara. Hawa wakifanya haya Serikali ikichukua hatua kuboresha utendaji wa Bandari kuna watu wanaaza kusema nchi inauzwa.

Serikali ikiwasikiliiza hawa watu kuna hatari kubwa sana huko mbeleni nchi yetu kuja kuwa kituko cha mwisho zaidi kuliko hata sasa, kutokana na kusikiliza wajinga huku nchi ikitakuwa ikimbie iendane na mabadiliko ya Dunia ya sasa.

Kwa Dunia inavyokwenda sasa, Tanzania haipaswi kurudi nyuma tena! Ujinga usipewe tena nafasi Tanzania!

Nafarijika Sana kuona threads kama hizi hapa JF...
JF ya sasa na watanzania Wengi hawana tofauti na wale waliomuua Galileo Galilaya Kwa kusema "dunia ni duara" sio flat...Hadi Viongozi wa dini wakasema "amekufuru"....akanyongwa....
 
Unauliza hapa kwani hujasikia majibu ya Serikali?

Haya ngoja nikwambie. Ule ni framework agreement. Hakuna mradi specific unaotekelezwa kwa mujibu wa mkataba ule na ndo mana hauna muda. Muda utawekwa kwenye mkataba husika wa utekelezaji wa mradi husika.

Umeelewa?
Tatizo mkuu serikali haikuwekeza kwenye kuelimisha watu juu ya mkataba huu, watu wakieleweshwa na kutoa maoni kusingetokea sintofahamu. Bahati mbaya sana both wanaopinga na wanaotetea wanatumia propaganda sio facts so wananchi wameshameza sumu inakua ngumu kuitoa.
 
Mtego huo, shtuka wewe

Unadhani watu wanaugomea kwann?
 
Shirika gani limegawiwa kwa Foreigners?
Issue sio umiliki wa serikali issue ni ufanisi, tatizo la serikali zetu hazina ufanisi kabisa embu niambie taasisi Gani ya serikali yetu Ina ufanisi? Zote zimeoza Sasa why ulazimishe tu umiliki wa serikali hata kama hakuna ufanisi?

TTCL na Vodacom ni mbingu na ardhi, ATCL na Precision ni mbingu na ardhi, kiufupi hakuna government entity inaizidi private sector kwa ufanisi. Hata kampuni kama Deloitte na PWC zinaizidi ufanisi TRA na NAO kwenye ukaguzi.

Nadhani mfumo wa uendeshaji taasisi za serikali ubadilike, ziwe za mikataba zenye KPI otherwise hawa mafisadi hawana uchungu na chochote sababu bandari iingize hasara au faida hawana Cha kupoteza na mishahara ipo pale pale.

Kwa hiyo suluhisho la huo unaouita ufanisi ndio kugawa Kampuni zetu kwa Government owned foreign Companies?
 
Tatizo mkuu serikali haikuwekeza kwenye kuelimisha watu juu ya mkataba huu, watu wakieleweshwa na kutoa maoni kusingetokea sintofahamu. Bahati mbaya sana both wanaopinga na wanaotetea wanatumia propaganda sio facts so wananchi wameshameza sumu inakua ngumu kuitoa.
Suala sio kumeza sumu. Suala ni ujinga. Kuna watu wanaelewa ila wanabisha tu ili mradi wabishe.
 
Vita dhidi ya ujinga aliyoianzisha Mwalimu Nyerere nadhani alikosea ingembidi aanzishe vita dhidi ya IQ hafifu huenda inatibika
 
Shida iko wapi?
Wewe umezifanyia nini hizo kampuni unazoita zetu?

Shida iko, hakuna kinachofanyika/badilika mfano Shirika letu la reli ziaid ya kuibiwa na foreigner kipi kilifanyika? Tangayika packers Wahindi akina patel waliiba mitambo yote na kwenda kufungua viwanda nje leo hii tanganyika packers imebakia viwanja tu vya mahubiri, hotels zetu za kitalii zore wizi mtupu hakuna ufanisi wowote ulioonekana kilichotokea ni malia zilizokuwepo kuibiwa na foreigners besides ingekuwa ni rahisi hivyo kusingekuwa na nchi masikini Afrika au Duniani kwani wote si wangegawa tu Kampuni zao kwa akina taifa gas &Co. na kuwa na maendeleo?
 
Kwa hiyo suluhisho la huo unaouita ufanisi ndio kugawa Kampuni zetu kwa Government owned foreign Companies?
Sio mpaka foreign ila sekta binafsi inaweza kuwa na ufanisi kuliko public sector maana wao ni profit-oriented sio blah blah. Hata hao US wametoa bandari zao kwa mikataba ya miaka mpaka 50 kwa kampuni za UAE Ili kuongeza ufanisi.

Hapa Cha kuweka sawa ni mikataba tu ila kubinafsisha bandari sio kitu Cha ajabu maana hata waliopo hao TPA wamefeli kabisa.

Hata hapo TPA ni rushwa, ufisadi, madawa ya kulevya, magendo n.k yanapitishwa tu hata sahivi?! Mnavyoongelea sovereignty it's as if sahivi magendo hayapiti?
 
Back
Top Bottom