Ujio wa DP world: Magari sasa kushuka bei na kuwa sawa na bajaji

Hivi unajua kikokotoo (calculator) cha TRA kwenye gari ni tofauti na inayotumika hata hapo Zanzibar tu? Achilia mbali nchi jirani sitaki kuzitaja. Ndiyo maana magari katk nchi nyingi zinazotuzunguka yako cheap!
Kwahio DP World wanachukua Bandari au TRA ?
Unadhani shida zetu kwa hii nchi ni ukosefu wa ukusanyaji wa Kodi, Ukosefu wa vyanzo, Mwananchi kutokukamuliwa au mirija na walaji wengi ?

Misaada tunapewa mingapi kila siku ? Mabwenyewe / watawala wanazimaliza bila kufanya kile kinachotakiwa kufanyika....

Ni sawa sawa pipa linavuja, badala ya kuziba hilo pipa ili unachokiweka kisimwagike unadhani kuendelea kujaza kutapunguza uvujaji (kumbe ule uzito unaongeza ukubwa wa tundu hence kuvuja)
 
Naona unatupaka wese kwa mgongo wa chupa 🤣🤣🤣!!! Nyie tupangeni tu.
 
TRA siyo msahafu useme sheria na viwango vya Kodi haviwezi kubadilika endapo DP. World watakuwa wanatupatia trilioni 6 kwa mwezi toka kwenye tozo na ushuru wa bandari
Kwahio TRA wanangojea DP World ili wabadilshe mambo ?

Hivi mpaka sasa budget inajitosheleza au tunahitaji bado misaada ? Kwahio unadhani Hizo pesa utapunguziwa wewe ambaye unaweza kutoa ili tuendelee kukopa ?

Hivi hapa tupo serious tunaongelea issues au umeamua kuja na riwaya za Alinacha
 
Kodi ni TRA sio DP World

DP world hana uwezo wala ubavu wa kushusha kodi

Umeonyesha ujinga ulio nao kwa hii hoja yako .Unao wa kukutosha Hujui hata kazi ya TRA ni nini
 
Assessment zote zinafanyika kupitia mifumo ya TRA kama ni hapo bandari ya Dar wanafanyia kupitia TESWS.

Bandari kuna port charges, kulipia cleaning and forwarding agency fees ,inspection fees hizi zote zinafanyika na mamlaka tofauti mfano inspection ni Tbs, .

Kodi za imposition, railway development kadhaa zinalipiwa kwa mfumo wa TRA.

Nataka kuonyesha hao DP World hawana impact yeyote katika kuzuia kodi za magari ni mamlama mawili tofauti tambua hilo...TBs Wanachukua chao, TRA chao ,waondosha shereha chao ,Icds chao na TPA Chao
 
Ndio upuuzi wenu mmeleta huku
 
Acha kutuona. MAZUZU

Kitu kinachofanya magari kupanda bei ni

🇹🇿 Import duty

🇹🇿 V.A.T

🇹🇿 EXCISE DUTY

🇹🇿CUSTOM PROCESSING FEE

Hizo ni kwa mujibu wa sheria ya Kodi na zitaendelea kuwepo. Hao DP wao watapakua haraka tuu baadaye upambane na. T.R.A

Kitakachofanya MWANANCHI wa kawaida aifurahie bandari yake sii kampuni ya kupakua mizigo Bali ni maamuzi MAGUMU ya KUBADILISHA sheria na kuzifanya bandari zetu kuwa FREE PORT HARBOUR. Si ni Mali yetu? Inawezekana kwani Kuna mtu anatupangia?
 

Ogopa matapeli bandari haiuzwi.
 

Kamwe gari haliwezi kushuka bei na kuwa sawa na bajaji.
 
TRA ndio wapuuzi wa haya mambo na kujifanya kuweka vikwazo chungu nzima ili wahongwe. Ni wauwaji wa uchumi wa Taifa na wala sio wakusanya Kodiak!
Kama kweli tunataka kukuza hili TRA waondokane na mfumo wa wala Rushwa hasa huko ofisini.
Rais fanya wajibu wako Kuna mengi huku chini yako.
TISS mko wapi!
 
Nataka kuonyesha hao DP World hawana impact yeyote katika kuzuia kodi za magari ni mamlama mawili tofauti tambua hilo...TBs Wanachukua chao, TRA chao ,waondosha shereha chao ,Icds chao na TPA Chao
Ukubwa na wingi wa Kodi utapunguzwa ili mtanzania aishi kama peponi baada ya DP World kuanza kukusanyateilioni 6 kwa mwezi kupitia tozo na ushuru wa bandari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…