Maumivu yanayotupatapa wanaccm kutokana na huyu bwana ni kuusema ukweli unaouma. Huyu jamaa hasahau na wala hapindishi kitu. Yaani mkuki moyoni inaumiza sana ndio maana hatumpendi.
Ni kweli anapowaambia wananchi ukuaji wa uchumi wetu hauendani na maisha halisi ya wananchi, kweli wananchi wanakubali kwa sababu maisha ni magumu sana wao wananchi wanaijua hali hiyo. Sisi viongozi tunaifanya hatujui maisha kua ni magumu tunapindisha ukweli, sasa Lissu anachoma katikati.
Lissu anaposema vifaa vya ujenzi vimepepanda maradufu, sukari imepanda maradufu ndio ujue anachomaka kati kati. Polepole juzi nadanganya eti vitu havijapanda bei muongo mkubwa, nenda kaulize bei ya nguo ya 2014 kwa sasa usikie bei yake.
Ukweli mchungu, Lissu anawaambia watumishi wa umma wengi hawajalipwa stahili zao na wala hawajaongezewa mishahara miaka mitano, wengi hawajalipwa stahili zao baada ya kuachishwa kazi, kwani uongo?
Huyu Polepole kwakua hajui uchungu wa chama na ameingia juzi tu eti anasema watumishi wamepunguziwa kodi, kwani kupunguziwa kodi ndiyo kuongeza mshahara na ndiyo makubaliano ya kimkataba? Aache kudanganya watu kwanza yeye siyo Mwanaccm ameazimwa kwa muda tu.
Lisu huyu anakera,anakera hadi anachukia.