Ujumbe huu uwafikie Askari wa JWTZ

Ujumbe huu uwafikie Askari wa JWTZ

Nadhani ingekuwa busara kama ange weka full story lakini hapo tutamuhukumu mwanajeshi bila kujua upande wa pili ilikuwaje... Mimi sidhani kama huyo mwanajeshi ni punguani aanze kumpiga TU mtu bila sababu...huyu Kuna kitu kakikoroga...haki vile​
Pamoja na hayo bado hawana mamlaka yakuchukua sheria mkononi.Vyombo vyakushughulika na makosa ya raia vipo.Unaweza ukajichukulia sheria mkononi kwa mtu ambaye humjui alafu akakudhalilisha na jeshi lako.Tutii sheria.Kila mtu aheshimu mipaka yake.
 
Serikali itakubaliana na Mimi kuwa maaskari wengi wa JWTZ Ni waonevu
Tatizo ni kushindwa kujisimamia tu ,ukijisimimamia hamna wa kukugusa , hao mafala mnawapa nafasi na unyonge wenu .
Hamna sheria inayoruhusu mwanajeshi kukugusa ,unless labda uwe umewafanyia vurugu .
Tofauti na hapo usiruhusu kuguswa na mpumbavu yeyote .
Kama anaona umevunja sheria mwambie akashitaki police
 
Nasikitika kuwa toka jana napambana kuwepo na pambano kati ya Dr Restart na jamaa mmoja aliyejitanaibisha kuwa mjeda bwana Elias K kumbe naye ni wale waliokandwa kama bwana Restless Hustler basi pambano tukaliamishia kwa Private Hae Mo-Su .

Masikitiko yangu ni kuwa private Hae Mo-Su hataki kukubali pambano lifanyike nje ya uwanja wa kambi ila yeye anataka afuatwe kambini ili akipigwa asaidiwe na private wenzie .

Nikasema sasa kama na yeye anamuogopa Dr Restart basi hata mimi chapombe niko hapa kupigana aje Mbeya kwa nauli zangu na pia matibabu juu yangu tupimane uwezo lakini bado anademadema .

Sasa natangaza kwa afande yeyote aliyepo hapa na yuko tayari kupimana ubavu na raia basi aje aseme tuandae pambano .

Nb.Tunafanya hivi ili kuwatia moyo raia wote kujua kuwa wajeda wanapigika vizuri tu na wanakaa hawana maujuzi kama tunavyoaminishwa na jamii .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Wajeda si washazoea kuja mob

Ova
 
Kwa muda mrefu, Askari wa JWTZ wamekuwa wakilaumiwa kwa kujichukulia Sheria mikononi mwao.
Chuga Matejoo walikomesha askari wanaojichukulia sheria mikononi, walimkamata mmoja huko migombani baada ya kuleta shida kwa raia kisa amemkula demu wake, huyo askari alizikwa hatunaye tena
 
Kwa muda mrefu, Askari wa JWTZ wamekuwa wakilaumiwa kwa kujichukulia Sheria mikononi mwao. Kwa kuwa wao ni wanajeshi, wanaamini kwamba wanaweza kupiga watu makofi mtaani hovyo bila kuulizwa na mtu.

Pengo la uhusiano mnalolitengeneza kati yenu na raia wa kawaida, mtakuja kuliona nyakati zijazo. Na mtambue kuwa uwezo wenu wa kuilinda hii nchi unategemea ushirikiano kamili na wananchi.

Hatuombi mabaya yatokee lakini siku nchi hii ikipitia kwenye misukosuko ya kiusalama, mkipita mitaani katika kutekekeza majukumu yenu, mtakutana na sisi raia wa kawaida ambao awali mlikuwa mkitupiga hovyo.

  • Mkiishiwa chakula, hatutawapa.
  • Mkiishiwa maji, hatutawapa.
  • Mkitumia ubabe kama mlivyojizosha tutawawekea sumu.

Sifa ya kwanza ya kuwa Askari wa JWTZ ni kuwa Raia wa Tanzania, huwa nashangaa sana mnapojitofautisha na Raia kana kwamba nyie sio Raia! Sasa huo uaskari wameupataje! Au Ukishakuwa Askari, U-Raia unaisha?

Katika Serikali ya Awamu ya Tano, tulishuhudia chuki kubwa kati ya raia wa kawaida na Jeshi la Polisi, baada ya maaskari hao kutumia mamlaka vibaya na ubabe wa kishamba, nadhani hiyo chuki imepungua awamu hii.

Nia yangu ni njema na kama raia mwema, natumai haki yangu ya kikatiba kuwashauri. Badilikeni Masoja, Tanzania yenye ulinzi imara inaanza na raia wema, kisha Maaskari.

Sisi ni wengi kuliko nyie hivyo bila sisi hamtaweza kuilinda hii nchi. Acheni kupiga watu mitaani hovyo.
Wanaacha kushughulika na mambo makubwa yanayoangamiza taifa, wanakamata " MITUMBA"mitaani, M23 piteni na huku!!!!
 
Kuna haja ya kufanya mabadiliko kwenye haya majipu pia.

Marekani huwi mwanajeshi angalau uwe na Bachelor, hii iletwe huku pia tupate jeshi lenye weledi na kujitambua... na wapewe mafundisho kuwa raia sio adui yako au punch-bag la kumalizia hasira zako
Tanzania wale darasa la saba na form 4 feliaz ndio wanakimbilia jeshini kwa asilimia bigi
 
Back
Top Bottom