Umeongea busara mkuu huu ndio utuHapa nami kuna jambo naliona kama mtego kwa Chama dola lissu akifika mshindeni kwenye sanduku la kula na si kumgasi ,mkijalibu MWAFAA tena ikiwezekana mpeni ulinzi madhubuti yani hata mbu usimsogelehe ,ila sina shaka na hili maana najua wapo watu hapa tz wanaelewa zaidi nilisemalo kuliko mimi.na najua kama lisu anafika watachukulia hili kwa umakini wa hali ya juu ,Tanzania kwanza ushabiki wa vyama badae
Kama sio maarufu mnashuhulika nae wanini? Halafu awekwe lockup kwakosa gani? Inakuwaje mnataka Sheria imhukumu kwa vikosa vidogo vya kumsingizia halafu hamtaki sheria hiyohiyo isiwapatilize waliotaka kumuua?Hayo ya wakati uliopita siyakatai alikuwa maarufu - lakini sasa siyo maarufu tena! Mimi kweli darasa la saba nilisoma pia na PhD nayo ninayo. Ila ukubali Lissu hana umaarufu wa kutikisa nchi hata chembe!
Kupigwa risasi alikofanyiwa na kuwekwa lockup akikanyaga nchi kipi cha kutikisa nchi?
Mkuu,hawa watu wamenyimwa maarifa ili utawala wao ufike mwisho.Kama sio maarufu mnashuhulika nae wanini? Halafu awekwe lockup kwakosa gani? Inakuwaje mnataka Sheria imhukumu kwa vikosa vidogo vya kumsingizia halafu hamtaki sheria hiyohiyo isiwapatilize waliotaka kumuua?
Yani itakuwa haki akirudi mumshulikie kwa makosa ya uongo lakini msimpe haki yake kwa mauwaji aliyotaka kufanyiwa?
Lisu mnampa umaarufu wa bure nyie wenyewe mnayomfanyia ndio yanafanya Jamii inayopenda haki na amani izidi kumpenda Mara dufu.
Mlichomfanyia ni ushetani kama haitoshi mkamfukuza na ubunge hamridhiki bado akija mumkamate hapana jitafakarini mtaliharibu taifa kumbukeni vitabu vya dini ambavyo kila siku rais Magufuli anasema aombewe navyo vimeandika HAKI HUINUA TAIFA.
Yani wanataka kutuharibia nchi yetu kwa makosa Yao jaribio lolote litakaloelekezwa kwa lisu litaifanya nchi yetu iwe tested kwa mara ya kwanza toka vita ya idi amini shida yetu ni moja watawala wetu Wana wa underestimate sana watanzania. Wanaamini wanaweza fanya lolote lile na wakaidhibiti hali yoyote kwa nguvu za dola tumuombe Mungu sana awape hekima ili wasiliingize taifa majaribuni. Waliyomfanyia lisu yanatosha wamuache apige siasa zake akipata sawa akikosa sawa atazeeka kwa amani ndani ya nchi yake Kama mrema Yuko wapi mrema wa miaka ya tisini? Lisu wamuache Tena wamlinde kwa upendo wote serikali ifanye Kama baba afanyavyo kwa mtoto wake mtoto wako akikosea humuuwi japo naamini lisu Hana kosa lolote.Mkuu,hawa watu wamenyimwa maarifa ili utawala wao ufike mwisho.
Lissu ana ushawishi mkubwa sana hasa kwa siasa zetu za majukwaani akichambua tu hapa muswada wa sheria ya usimamizi wa rasilimali ama ule wa gesi ama mpango wa taifa wa miaka 5 unaweza choma bendera ya CCM dakika hiyo hiyo.Hayo ya wakati uliopita siyakatai alikuwa maarufu - lakini sasa siyo maarufu tena! Mimi kweli darasa la saba nilisoma pia na PhD nayo ninayo. Ila ukubali Lissu hana umaarufu wa kutikisa nchi hata chembe!
Kupigwa risasi alikofanyiwa na kuwekwa lockup akikanyaga nchi kipi cha kutikisa nchi?
Mwenye maskio na asikie.na #TUNDU_LISSU
Kuhusu sarakasi za Mahakama ya Kisutu, nina haya ya kusema;
Acheni hofu. Kama nitakamatwa na kuwekwa mahabusu, hilo litakuwa ni jambo jema kuliko jambo lingine lolote Magufuli na watu wake watayatendea mapambano ya kudai demokrasia katika nchi yetu.
Wakifanya hivyo basi kampeni yote ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu itakuwa juu ya kukamatwa kwangu.
Ni hivi: kabla ya September 7, nilikuwa na kesi 6 za jinai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Nilikuwa sijawahi kukosa kwenda mahakamani kuhudhuria kesi hizo. Sijawahi kuogopa kesi zao za kijinga.
Kitu pekee kilichonifanya niache kuhudhuria kesi ni kile ambacho dunia nzima inakifahamu. Nilishambuliwa na kujeruhiwa vibaya na kusababisha niondoshwe nchini kwa ajili ya matibabu.
Walionishambulia na waliowatuma, kuwalipa na kuwawezesha hadi sasa wanaitwa 'watu wasiojulikana.' Waliotakiwa wanitibu kwa mujibu wa sheria za nchi yetu walikataa kunitibu. Badala yake wakanifuta Ubunge kwa visingizio vya kijinga tu.
Sasa nikirudi nchini kwa hiari yangu baada ya miaka mitatu ya kujihangaikia mwenyewe wanikamate na kuniweka gerezani kwa visingizio vingine vya kijinga.
Hilo litakuwa jambo jema sana. Itabidi wawaeleze wananchi wa Tanzania na waieleze dunia inayofahamu mambo haya kwa nini wamefanya hivyo. Na watoe maelezo hayo katikati ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge na waeleweke kwa wapiga kura.
Mimi binafsi nitafurahia sana wakifanya hivyo, maana hatutazungumzia kitu kingine chochote katika kampeni za Uchaguzi Mkuu.
Tundu Lissu.
Wishful thinking😀Maneno meeeengi,ameshindwa nini kuja?mgombea urais chadema ni mbowe,huyo mpiga kelele atafukuzwa kwenye chama muda siyo mrefu.Yeye ni karai tu kama yalivyo makarai mengine.
Asilimia kubwa sana ya kesi dhidi ya viongozi wa upinzani hapa Tz, ni kesi za kisiasa, japo zimefunguliwa kama jinai. Inaonekana ni mkakati wa ccm ya Magufuli, kuwatoa mchezoni wapinzani, kwa gharama ya kodi zetu.Huo Ni mtazamo wako tu tena wa kishabiki
Uvunje Sheria useme ni kesi ya kisiasa? Sababu wewe Ni mwanasiasa una haki ya kujunja Sheria,kusema uongo,kufanya fujo? Huu Ni uwana si hasa!!! Kifupi acha apambane na Hali yake tuAsilimia kubwa sana ya kesi dhidi ya viongozi wa upinzani hapa Tz, ni kesi za kisiasa, japo zimefunguliwa kama jinai. Inaonekana ni mkakati wa ccm ya Magufuli, kuwatoa mchezoni wapinzani, kwa gharama ya kodi zetu.
Kuna nyakati majaji wametoa karipio kali dhidi ya mbinu hizi chafu. Mfano lile sakata la Lema kukaa mahabusu miezi 4, kutokana na mchezo mchafu wa mawakili wa serikali wakishirikiana na mahakimu wabovu wanaohongwa na serikali ya Magufuli. Halafu katika dhihaka ya karne, huyuhuyu mhongaji mkubwa wa wapinzani ili waunge mkono juhudi, na anayehonga mahakimu wawanyime haki wapinzani, ndio anajiita mpambanaji wa rushwa!
Hatimaye suala la Lema lilihitimishwa kwa karipio kali kwa hakimu na mawakili wa serikali.
Mfano mwingine ni pale hakimu alipoondoa dhamana kwa Freeman Mbowe na Esther Matiko. Jaji aliyerejesha dhamana zao alitoa karipio kali. Kesi yenyewe pia ni feki. Ile ya akwilina
Sugu alitiwa hatiani katika kesi feki, akafungwa na hakimu huyo asiye na maadili ya uhakimu akapewa ujaji. Rufaa ilicheleweshwa makusudi. Hatimaye ikaonekana Sugu alifungwa kimakosa.
Katika kesi dhidi ya viongozi wa CHADEMA baada ya uchaguzi wa marudio Kinondoni, ambapo Akwilina aliuwawa na risasi za polisi, tuseme viongozi hao walivunja sheria. Vipi kuhusu aliyempiga risasi Akwilina? Maana Polisi wanamjua, ila kesi ilifutwa. Vipi kuhusu wale waliowanyima haki mawakala wa CHADEMA?Uvunje Sheria useme ni kesi ya kisiasa? Sababu wewe Ni mwanasiasa una haki ya kujunja Sheria,kusema uongo,kufanya fujo? Huu Ni uwana si hasa!!! Kifupi acha apambane na Hali yake tu
Kisheria wahusika wa Yale maandamano ndio wanawajibika bila ujinga wa kufanya Yale maandamano haramu huyo marehemu asingekufa,Askari Hana hatia walioandaa maandamano walistahili kunyongwa kabisaKatika kesi dhidi ya viongozi wa CHADEMA baada ya uchaguzi wa marudio Kinondoni, ambapo Akwilina aliuwawa na risasi za polisi, tuseme viongozi hao walivunja sheria. Vipi kuhusu aliyempiga risasi Akwilina? Maana Polisi wanamjua, ila kesi ilifutwa. Vipi kuhusu wale waliowanyima haki mawakala wa CHADEMA?
Tunajua kwamba wapo ambao wapo juu ya sheria. Inaonekana kufanya siasa za upinzani ni kosa la jinai. Ndio maana polisi wanashindana kuwanyanyasa wapinzani ili wapandishwe cheo
Kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, na Katiba yetu, maandanano ni sehemu ya kazi za vyama vya siasa. Ila katika udikteta uchwara wa Magufuli, amevunja Katiba na amevunja sheria kwa kuyazuia. Ila naandamano ya kumpongeza magufuli, hayo sawa kabisa, ruksa.Kisheria wahusika wa Yale maandamano ndio wanawajibika bila ujinga wa kufanya Yale maandamano haramu huyo marehemu asingekufa,Askari Hana hatia walioandaa maandamano walistahili kunyongwa kabisa
Ni haki kwa kufuata taratibu,sio unakurupuka tu tuandamane kisa Ni haki yakoKwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, na Katiba yetu, maandanano ni sehemu ya kazi za vyama vya siasa. Ila katika udikteta uchwara wa Magufuli, amevunja Katiba na amevunja sheria kwa kuyazuia. Ila naandamano ya kumpongeza magufuli, hayo sawa kabisa, ruksa.
Unasema maandamano ya kijinga? Unajua sheria inayoongoza kazi za polisi? Ndio maana mara nyingi hata polisi hulalamika, mambo ya siasa malizeni huko!