Ujumbe wa Netanyahu kwenda kwa mamlaka ya Lebanon na watu wake

Annunaki

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2021
Posts
2,042
Reaction score
3,674
Benjamin Netanyahu amewatahadharisha na kuwasihi raia wa Lebanon 🇱🇧 akiwaomba kushikamana na kutumia wakati huu kuiondosha Hezbollah, Netanyahu amesema kwamba kundi hilo la kigaidi limekuwa likifadhiliwa na Iran ili kulinda interests za Iran mashariki ya kati ikiwa ni pamoja na kuishambulia kijeshi Israel 🇮🇱.

Anaomba walebanoni watumie wakati huu kuifanya Lebanon 🇱🇧 iwe kitovu cha amani mashariki ya kati kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Soma Pia: Benjamin Netanyahu: Ukitupiga tunakupiga, hakuna sehemu ndani ya Iran ambayo hatuwezi kufika

View: https://x.com/netanyahu/status/1843694164690846055?t=vWVZnHVLdy0g5URP0Hk3bw&s=19
 
Kila siku kwenye Media yeye apambane awaondoe huko kwenye mashimo walipojificha. Nasio apige majengo ya raia. Au na Hezbollah hawana sare?.

Waruhusu Palestine kua taifa huru, hapatakua na vita, vinginevyo hawatokaa kwa amani hapo middle east. Wapalestine & Hezbollah hawana cha kumpoteza. Wataua viongozi wao wote lakini watakuja wengine hata kwa majina mengine. Yeye apambane tu mpaka awafute.
 
Hayo unayoyaita majengo ya kiraia ndipo wanapojificha hao Hezbollah
 
Kila siku kwenye Media yeye apambane awaondoe huko kwenye mashimo walipojificha. Nasio apige majengo ya raia. Au na Hezbollah hawana sare?.

Waruhusu Palestine kua taifa huru, hapatakua na vita, vinginevyo hawatokaa kwa amani hapo middle east. Wapalestine & Hezbollah hawana cha kumpoteza. Wataua viongozi wao wote lakini watakuja wengine hata kwa majina mengine. Yeye apambane tu mpaka awafute.
Hezbollah siyo Jeshi, ni kikundi cha magaidi ambayo wengi wao utawakuta wale wanaoahidiwa maisha mazuri huko warabuni, kisha hujikuta wapo kwenye magenge hayo ya kiharifu

Genge hili halina sare maalumu kiasi cha Majeshi ya Israel yawafahamu

Kwa hali hiyo hawawezi kuachwa kisa wamejificha majumbani na watu wema!

Ni mjinga tu anayeweza kuacha kushughurikia joka ndani mwake kisa limekaa karibu na ndoo ya maziwa
 
Israel wameshalaaniwa. Wanapenda sana vita.

Ni hulka ya shetani kupigana na kuchukiana.

Washindwe kwa jina la Yesu wa Nazareth Myahudi mpenda vita kama Mayahudi mengine
Kwani anapigana peke yake, au anaopigana nao, nayo ni Mayahudi. Au anayopigana nayo, menyewe yanapigana tu ila hayapendi vita?

Eti Mshangazi?
 
Yani huyu punguani anaua raia alafu awaombe saport watakubali kweli?

Amekosea kidogo, alitakiwa aseme wamwondoshe yeye ili amani ya mashariki ya kati iwepo
 
Kiongozi wa magaidi kajiteka wengine hawataki kuteuliwa kua viongozi w magaidi. Israel akipata jina la kiongozi mpya anaua kabla hajaja ofisini.
All the best
Kuna kazee flani leo kutoka kundi la Hezbollah, kamesimama kuwatia shime wapiganaji wa Hezbollah na kuhimiza mapambano yaendelee,
Sijui usalama wake kaamua kuutoa rehani?

Maana Israel kapukutisha viongozi wakuu wa Hezbollah zaidi ya 10 kwa muda mfupi kwa mbinu zote za kijeshi na kigaidi yeye anatumia tu kuangamizia viongozi.
 
Benjamin Netanyahu amewatahadharisha na kuwasihi raia wa Lebanon 🇱🇧 akiwaomba kushikamana na kutumia wakati huu kuiondosha Hezbollah, Netanyahu amesema kwamba kundi hilo la kigaidi limekuwa likifadhiliwa na Iran ili kulinda interests za Iran mashariki ya kati ikiwa ni pamoja na kuishambulia kijeshi Israel 🇮🇱.

Anaomba walebanoni watumie wakati huu kuifanya Lebanon 🇱🇧 iwe kitovu cha amani mashariki ya kati kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

View: https://x.com/netanyahu/status/1843694164690846055?t=vWVZnHVLdy0g5URP0Hk3bw&s=19

Hayo mabomu anayodondosha huko Beirut hayatofautishi kati ya raia na Hezbollah ila yanaua wote na kujaribu nchi
 
Back
Top Bottom