Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Kutoka TRA mimi niko tayari na mahojiano kumuuliza Commissioner - Harry Kitillya, Mswahili atapendekeza jina la mtu mwingine kutoka TRA
 
I have long decided not to engage in this kind of debate..but now am forced to comment kwamba, huu mpango wa mahojiano ambao MJJ kwa nia njema anauandaa, utazaa yale yaliyotokea mara baada ya ziara ya Jeikei London majuzi...You wait and see!
 
Kutoka TRA mimi niko tayari na mahojiano kumuuliza Commissioner - Harry Kitillya, Mswahili atapendekeza jina la mtu mwingine kutoka TRA
Mwanakijiji na Mswahili Pendekezo La Dua mmelisikia tunasubiri na nyinyi mpendekeze watu wenu mmoja mmoja.Ili tuendelee na Tufikie tamati katika hili.
 
mtukwao,

maneno mazito hayo... ndugu zetu humu hawataki kukubali kuwa wanaongozwa na ukabila. Wakati wanadai kuna ukabila TRA , ukabila wao wenyewe unawekwa hadharani. Wanapopandikiza mbegu za kuwachukia wachagga, wakati huo huo wanarutubisha chuki ya kikabila ndani yao wenyewe. Leo hii tukisikia kiongozi mchagga amepewa nafasi basi tunajiuliza "kwanini Mchagga?"

Dhambi hii ya ukabila haikomi! Imeanzia kwa wachagga itaenda kwa Wahaya, Wanyakyusa, Wangoni (wa kunyumba) na ni kama mtu kula nyama ya binadamu! Ni mwiko mkubwa ambao ukishauvunja ni vigumu kujikomesha. Ndugu zetu hapa wanajifanya wanasukumwa na uzalendo! kumbe kinachowasukuma ni wivu usio na msingi na chuki isiyokaribishwa! Hawa ndugu tukiwapa nafasi wachague watu kwenye nafasi fulani, la kwanza watakalojiambia ni "wachagga, wahaya, wanyakyusa" hapana!! Wakiona jina la makabila hayo watayakwepa!

Bado tunaendelea kuwapinga, kuwakosoa, na kuwaonesha makosa yao! ili hatimaye wajirudi!

I am of the take that kuna ukabila sehemu sehemu. For you to come up with stuff like that (where i have highlighted in bold), is quite insulting. That is so below the belt. Mwanakijiji, sometimes if you dont have something to say, its fine to just chill. People may disagree with you, but to call them wivu na chuki...sijui zinatokea wapi. Kuna mtu amekwambia anataka kufanya kazi TRA? Mimi ni mmoja ya watu nilio na marafiki wa karibu wa kichagga, na sijawahi kusikia naambiwa na wivu na chuki. Sijawahi kucompete kazi na mchagga, na haitakuwa ishu kwangu. Please, be a gentleman and take that back!!
 
I have long decided not to engage in this kind of debate..but now am forced to comment kwamba, huu mpango wa mahojiano ambao MJJ kwa nia njema anauandaa, utazaa yale yaliyotokea mara baada ya ziara ya Jeikei London majuzi...You wait and see!
I couldnt agree with you more. Sometimes some people seem to have the solutions to everything.
 
Nampendekeza Benny Lusege ila MMANDA sitaki awemo kwani ni kundi lile lile. na kittilya.
mkandara yuko likizo anafuatilia kwa ndani kabisa tuendelee kumsubiri na awemo kwenye mahojiano.
nimesikia mwanakjj anaumwa kwa vile Redio yetu ndio ina mwaka na mtangazaji ni mmoja tufute subira na kumuombea Dua apone haraka.
 
NSSF yavuka lengo la makusanyo




na Anna Makange, Tanga




SHIRIKA la Hifadhi ya Taifa (NSSF) Mkoa wa Tanga limevuka lengo la makusanyo ambapo limekusanya sh milioni 2,481.20 kwa kipindi cha miezi minane tangu Julai mwaka jana hadi Februari mwaka huu.


Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga, Yahya Mhamali, aliiambia Tanzania Daima kuwa makusanyo hayo ni ya kipindi cha utekelezaji wa malengo ya kazi kwa mwaka 2006/2007 ambapo shirika lake lilijiwekea lengo la kukusanya sh milioni 2473.76 katika kipindi hicho.


Alisema kuwa makusanyo hayo yanatokana na malimbikizo ya michango ya kawaida pamoja na adhabu katika kipindi hicho walikusanya malimbikizo ya michango ya wanachama ya sh milioni 342.57 wakati lengo lilikuwa kukusanya sh milioni 247.44.


Mhamali aliendelea kufafanua kuwa michango ya kawaida ilikuwa sh milioni 2,120.71 wakati lengo lilikuwa kukusanya sh milioni 2,176.96.


Kwa upande wa adhabu, kwa wanachama waliochelewesha ada walikusanya sh milioni 18.9 wakati lengo lilikuwa kukusanya sh milioni 49.5.


Alisema licha ya kukusanya kiasi hicho cha fedha, NSSF pia iliweza kuandikisha waajiri wapya 39 sawa na asilimia 75 ya lengo lililowekwa la kuandikisha waajiri 52.


Aliendelea kufafanua kuwa shirika hilo pia limeandikisha wanachama wapya 2034 sawa na asilimia 119.86 ya lengo la awali la kuandikisha wanachama 1697 sambamba na kuwaingiza katika mpango wa matibabu wananchama na familia zao 1,134 unaogharamiwa na NSSF na kwamba wanachama 2461 walilipwa sh milioni 612.2 kwa ajili ya mafao mbalimbali

PHILLIMON MICHAEL.
HIYO NIMETOA KWENYE Tanzania Daima la jumapili. naona uko kimya siku hizi?
hizo ndio kazi za waswahili unaowachukia.
 
Mswahili,
Si Waswahili. Ni Watanzania. Achana na tashwira ya kibaguzi.
 
Sina Uhakika na Hali ya Afya ya Mwanakijiji,Kama bado anaumwa ninaendelea kumpa pole na kumtakia apate na nafuua na kupona haraka.
Nimeona mapendekezo ya washiriki waliochaguliwa na Dua na Mswahili.
1)Dua amemchagua Kamishina-Harry Kitillya
2)Mswahili amemchagua-Benny Lusege na ametoa sharti kwamba mmanda asialikwe kwani anamini ni kundi moja na kitillya.
3)Mwanakiji tunasubiri wewe ukipata nafuu basi uchague mtu mmoja kutoka TRA AMBAO HAWAMO KATI YA HAO AMBAO WAMESHAONDOLEWA AU WAMESHAPENDEKEZWA KWENYE MAHOJIANO.
Mswahili Mkandara hawezi kuwemo kwani uwezo wa vyombo husika ni si zaidi ya watu sita sasa kama unataka mkandara awemo basi uondoe jina ulilopendekeza na umpendekeze Mkandara badala yake.
 
Haya nimerudi, na ninashukuru kwa salamu zenu za heri na nafuu kwenu mtu mmoja mmoja na kwa jumuiya nzima ya JF.

Niliposema "wote" mliotaka kuzungumza nao wamekubali niliwahusisha watu wa majina hayo! sasa sijui nifanye nini ili nipate contact zenu nyinyi. Nitajaribu kupanga kufanya tena mazungumzo hayo J'mamosi hii, hivyo nawaomba Mswahili na wenzako tafadhali nipatieni contacts zenu na nitawajulisha muda wa mazungumzo siku ya Jumamosi.
 
MKJJ

Hamna wasi, confirm muda na contact zangu ni zile zile. Kama kuna tofauti yoyote ni PM.
 
Mwanakjj.
wewe umempendekeza nani? sisi tumetaja watu wetu hapa tunaomba na wako umtaje humu. umepata namba ya benny?
pia contact zangu unataka za namna gani? ni PM
 
Waswahili tutawatambua kwa vigezo au vitambulisho vipi?
Ni sahihi pia tukisema kuwa mafanikio yote yaliyopatikana ni kwa sababu ya ushiriki katika mpango huo wa waswahili wenzao pekee?
Hivi Tanga sio Kaskazini?
 
Waswahili tutawatambua kwa vigezo au vitambulisho vipi?
Ni sahihi pia tukisema kuwa mafanikio yote yaliyopatikana ni kwa sababu ya ushiriki katika mpango huo wa waswahili wenzao pekee?
Hivi Tanga sio Kaskazini?
Tanga? Nafikiri ni kaskazini tata................................How would you like this one?
 
Sierra Leone waja kujifunza hifadhi ya jamii

Joseph Senga
MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umefikia hatua ya kujivunia mafanikio yake, baada ya nchi kadhaa za Afrika, kuendelea kuja nchini kujifunza namna ya uendeshaji wa mifuko yao ya jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF, Ramadhan Dau, aliwaelezea waandishi wa habari ofisini kwake jana wakati akiwatambulisha maofisa wa Mfuko wa Jamii kutoka Sierra Leone kwamba nchi nyingi za Afrika Mashariki na Kati zimeendelea kupata mafunzo mbalimbali ya mfuko huo kutoka kwa maofisa wa NSSF.

Pamoja na Sierra Leone, nchi nyingine ambazo tayari zimefaidika na mafunzo kama hayo ni pamoja na Kenya, Uganda, Ghana, Gambia na Namibia kwa kuwaleta maofisa wake kujifunza jinsi ya uendeshaji wa mifuko yao.

“Sisi Tanzania tuko katika nafasi ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa ubora wa huduma na uendeshaji wa shirika letu la NSSF na hawa wageni mnaowaona hapa wamekuja pia kwa lengo hilo hilo la kujifunza jinsi tunavyofanya kazi zetu,” alifafanua.

Aliongeza kuwa hatua hiyo ni ya kujivunia kwa mfuko huo pamoja na Watanzania wote, kwa kuwa nchi nyingi za Afrika hazijaweza kufikia hatua ya utoaji wa huduma kama ilivyofikiwa na Tanzania hasa katika kuwahudumia wanachama wake.

Ujumbe wa maofisa saba wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii na Bima kutoka Sierra Leone, uko nchini ukiwa ni ugeni wa NSSF kwa lengo la kujifunza mambo kadhaa ya uhifadhi na maendeleo ya mfuko huo. Ujumbe huo utakuwa nchini kwa muda wa siku sita.
 
Tusitafute majibu rahisi kwa maswali magumu. Mimi natokea Mbeya, lakini nimekaa sana Tanga, Pwani (Rufiji), Kilimanjaro, Morogoro na nimesoma iringa na Dar. Kwa hiyo angalau nina picha kidogo ya tofauti ya elimu za mikoa hii. Maendeleo ya shule ya mikoa ya K'njaro, Mbeya na Kagera yanatokana na historia, kwamba wamisionari waliwahi kujenga shule maeneo hayo, kwa hiyo sio rahisi sana kulinganisha mikoa na kuwapaka ukabila pasipo sababu. Mpaka kesho, idadi ya shule za K'njaro haiwezi kufanana na ile ya mkoani Rukwa ama Pwani, wala ile ya Mbeya haiwezi kufanana na Lindi au hata jirani zao Singida. Huu ndio ukweli na si kukimbilia kulaumu ukabila,
Mzee Mwanakijiji pokea tano za chap chap, pia mpe Samvula chole hicho kitabu cha Mwalimu Nyerere asome.
 
Back
Top Bottom