Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwanakijiji na Mswahili Pendekezo La Dua mmelisikia tunasubiri na nyinyi mpendekeze watu wenu mmoja mmoja.Ili tuendelee na Tufikie tamati katika hili.Kutoka TRA mimi niko tayari na mahojiano kumuuliza Commissioner - Harry Kitillya, Mswahili atapendekeza jina la mtu mwingine kutoka TRA
mtukwao,
maneno mazito hayo... ndugu zetu humu hawataki kukubali kuwa wanaongozwa na ukabila. Wakati wanadai kuna ukabila TRA , ukabila wao wenyewe unawekwa hadharani. Wanapopandikiza mbegu za kuwachukia wachagga, wakati huo huo wanarutubisha chuki ya kikabila ndani yao wenyewe. Leo hii tukisikia kiongozi mchagga amepewa nafasi basi tunajiuliza "kwanini Mchagga?"
Dhambi hii ya ukabila haikomi! Imeanzia kwa wachagga itaenda kwa Wahaya, Wanyakyusa, Wangoni (wa kunyumba) na ni kama mtu kula nyama ya binadamu! Ni mwiko mkubwa ambao ukishauvunja ni vigumu kujikomesha. Ndugu zetu hapa wanajifanya wanasukumwa na uzalendo! kumbe kinachowasukuma ni wivu usio na msingi na chuki isiyokaribishwa! Hawa ndugu tukiwapa nafasi wachague watu kwenye nafasi fulani, la kwanza watakalojiambia ni "wachagga, wahaya, wanyakyusa" hapana!! Wakiona jina la makabila hayo watayakwepa!
Bado tunaendelea kuwapinga, kuwakosoa, na kuwaonesha makosa yao! ili hatimaye wajirudi!
I couldnt agree with you more. Sometimes some people seem to have the solutions to everything.I have long decided not to engage in this kind of debate..but now am forced to comment kwamba, huu mpango wa mahojiano ambao MJJ kwa nia njema anauandaa, utazaa yale yaliyotokea mara baada ya ziara ya Jeikei London majuzi...You wait and see!
Mwanakjj.
wewe umempendekeza nani? sisi tumetaja watu wetu hapa tunaomba na wako umtaje humu. umepata namba ya benny?
pia contact zangu unataka za namna gani? ni PM
Tanga? Nafikiri ni kaskazini tata................................How would you like this one?Waswahili tutawatambua kwa vigezo au vitambulisho vipi?
Ni sahihi pia tukisema kuwa mafanikio yote yaliyopatikana ni kwa sababu ya ushiriki katika mpango huo wa waswahili wenzao pekee?
Hivi Tanga sio Kaskazini?
Joseph Senga
MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umefikia hatua ya kujivunia mafanikio yake, baada ya nchi kadhaa za Afrika, kuendelea kuja nchini kujifunza namna ya uendeshaji wa mifuko yao ya jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF, Ramadhan Dau, aliwaelezea waandishi wa habari ofisini kwake jana wakati akiwatambulisha maofisa wa Mfuko wa Jamii kutoka Sierra Leone kwamba nchi nyingi za Afrika Mashariki na Kati zimeendelea kupata mafunzo mbalimbali ya mfuko huo kutoka kwa maofisa wa NSSF.
Pamoja na Sierra Leone, nchi nyingine ambazo tayari zimefaidika na mafunzo kama hayo ni pamoja na Kenya, Uganda, Ghana, Gambia na Namibia kwa kuwaleta maofisa wake kujifunza jinsi ya uendeshaji wa mifuko yao.
Sisi Tanzania tuko katika nafasi ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa ubora wa huduma na uendeshaji wa shirika letu la NSSF na hawa wageni mnaowaona hapa wamekuja pia kwa lengo hilo hilo la kujifunza jinsi tunavyofanya kazi zetu, alifafanua.
Aliongeza kuwa hatua hiyo ni ya kujivunia kwa mfuko huo pamoja na Watanzania wote, kwa kuwa nchi nyingi za Afrika hazijaweza kufikia hatua ya utoaji wa huduma kama ilivyofikiwa na Tanzania hasa katika kuwahudumia wanachama wake.
Ujumbe wa maofisa saba wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii na Bima kutoka Sierra Leone, uko nchini ukiwa ni ugeni wa NSSF kwa lengo la kujifunza mambo kadhaa ya uhifadhi na maendeleo ya mfuko huo. Ujumbe huo utakuwa nchini kwa muda wa siku sita.