Ukabila ni jambo lisilo semwa sana nchini lakini lipo sana kazini/maofisini

Ukabila wa wachagga kwenye taasisi za umma ama Serikali unatisha sana na hawana aibu hata kidogo nawaambia ni hatari sana, ipo siku inakuja tutataja hizo taasisi
Hivi unashindwa nini kutaja!!!
Wewe mwenyewe hujiamini halafu uko front kuwasema wanaojiamini.
Sasa ukimfichia siri huyo mkabila umefanya la maana?
 
Kuna kampuni huko Arusha mwaka Fulani ofisi karibia staff wote ni wameru na wachaga ilikuwa kampuni ya Sola Hadi kero kwa wengine tusiokuwa wa huko kaskazini
Inatangazwa internal job watu wanatoka external wanapewa kazi na haijulikani usahili kafanya lini na wapi kisa ni kabila lao anapewa shavu yalitushinda wengi tukaamua kuacha na kwenda kujiajiri mtaani.
 
Mmeishaambiwa ''no reform no election'' lakini utakuta makamanda wakitangulia unakuta nyuma yao wapo wanawake na watoto wao wa kike,ninyi mmelala nyumbani mnasubiri kuja kulia lia kwenye mitandao.Hamkuwaona vijana wenzenu kenya walivyopinga udhalimu wa bunge kwa vitendo,hadi ile sheria kandamizi ikafutwa?
Nyie mnakalia kwenda kwenye mabanda ya kubeti alafu unataka mabadiliko??
''Asiyefanya kazi asile''
 
Inawezekana una hoja. Kunaweza kuwa na elements za ukabila kwa kiwango kidogo kwenye baadhi ya vitengo. Lakini hali sio ya kutisha kama ulivyoweka hapo.
Asilimia 96 unazipataje?
Hata kwa mfano wa nshomile uliotoa, ni asilimia 75 (kwa data zako ulizoleta).

Na inakuwaje wewe umefanya kazi sehemu zenye Nshomile, na wewe mwenyewe umefanya na akina Mwamposa, na Ngoshas na Mangis?
 
Upo sahihi kabisa.
Sio kwa Sekta binafsi tu hata Serikalini, akiingia mkuu mpya anaanza kupanga safu yake kwa kuhamisha na kuingiza watu wake.

Hii haileti afya kiutendaji.
Nachukia sana ukabila na udini.
 
Udini ndio balaa sasa yaani kwenye suala la dini ni janga kubwa kuliko yote.
 
Je nikiwa mmoja wa hao wakina mwamposa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…