Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Hivi serikali kivuli kazi yake ni nini? Mpaka sasa walikuwa na mkakati mbadala gani?
Wapinzani wataendelea kuikosoa na kuielimisha Serekali ila kiburi cha serikali ya Ccm mavuno yake ndio hayo.Hela wanazotumia kununua Wapinzani zingeweza kununua vivuko hata viwili.
 
Miilii bado ipo maelezo yanasema kuna wengine wamekandamizwa na mizigo kwa chini tusubiri tuone
 
Haya ndio tulikuwa tunayasema na sasa yanaanza kutimia!

Kwahiyo watu wasipochanga hayo hayatafanyika?

Hivi nani ni mshauri wa hawa watu?!

Nini wajibu wa serikali katika matukio ya aina hii?

Bajeti ya kitengo cha maafa chini ya waziri mkuu inafanya kazi gani?

Ndio maana wengine tunawafurahia sana watu kama Zitto na Lissu kwa jinsi wanavyowasema wenye mamlaka.

Watanzania amkeni hasa wale wanaodhani wapinzani wana chuki tu na hii serikali.

Kweli kama ni serikakali ya wanyonge, basi watanzania Mungu katupendelea!
Hukumuona chakubanga anatafuta kuonekana ili apate cha kusema?
 
Ujumbe huu umfikie chakubanga
Sasa nn maana ya rambi rambi? Hii serekali inataka kujiongezea mzigo wa dhambi kila siku!! 7rambirambi ni kwa ajili ya kuwafariji wafiwa hiyo ya kujenga ukuta kwani serekalini hakuna MFUKO WA MAAFA?
 
Upo sahihi mkuu ila tunashangaa kwa hawa wakubwa kutumia akili ya sungura
Bwana Mkubwa, naona umefungua kinywa mapema mno. Sidhani kama watu watachanga tena. Rambirambi huliwa na wafiwa. Laiti ungelisema zitawasomesha hata mayatima walioachwa. Ni mawazo yangu tu jamani mnisamehe kwa domo kaya hili
 
Sasa kama bado wanaendelea na zoezi la kuopoa maiti atathibitishaje kabla ya zoezi kukamilika? Halafu huo ujinga wa kusema kwamba CDM wanapinga kila kitu sijui mmeutoa wapi?

CCM waliambiwa kwamba kuna hatari iko siku iko kivuko kitazama wakapinga, leo aliyewaambia ukweli ambao ndio umetokea ndio mnamwita mpingaji, nyie vipi?
Narudia tena, mimi sio wakupinga kila kitu kama cdm. Kuendelea kuopolewa ndio wamefika 300? mhe waziri kaongea kulingana na idadi ya maiti na manusura, sasa mbunge wenu hao watu 300 kawatoa wapi?. Asubiri idadi ifike ili aonge figure.

Subiri tume itakuja na majibu. Utapata majibu ya kwanini kimezama, mbunge ameongea sababu nyingine na ajali imeletwa na sababu tofauti.
 
Back
Top Bottom