Sijajua hizi mada za EM na KAYUMBA zimekuja sana kipindi hichi ,Ada na Kodi zinasumbua watu tangu enzi za nyerere siyo awamu ya samia tu ,mimi nakumbuka enzi tunasoma ada ilikuwa elfu 8 na ilikuwa ngumu kupatikana inafikia hadi wazazi wanaenda kuongea na mwalimu kwahiyo hakuna jipya.
Nilichogundua kinachowatesa watu ni kufanya mambo kuwaridhisha raia nje ,ukiwa na mawazo hayo kichwa kitapasuka na usikute hata hao raia wenyewe hawana time na wewe kabisa ni perception yako tu.
Ukweli kila mtu afanye anavyopenda kama wewe unaona KAYUMBA ipo fresh wapeleke na usione waliopeleka EM wanapoteza pesa na ukiona mtu anasomesha KAYUMBA mwache awapeleke ni maamuzi yake mwenyewe.