Elections 2015 UKAWA na Lowassa unganeni mchukue nchi, wakati ndio huu, mkipuuzia huu ushauri basi tena!


Hizi ni hoja nyepesi. Mimi wala siop timu Lowassa kama unavyodhani. Mimi maisha yangu hayamtegemei mwanasiasa, kwani ninaweza kuishi popote duniani kwani Mungu amenibariki. Kinachoniuma ni mfumo kandamizi wa CCM hadi wananchi walio wengi hawapati mahitaji ya msingi kwa miaka nenda rudi. Sasa hali imekuwa mbaya zaidi hasa kiusalama (rejea vamizi kwenye vituo vya polisi hapa nchini).

Huo uchafu wa Lowassa unaouongelea ni upi ambao Magufuli au viongozi wengine wa CCM hawana? Aceni kudanganya watu ili mkoloni mweusi CCM aendelee kutunyonya. UKAWA wanatakiwa kuelewa kwamba ushindi ni strategies na ikipatikana opportunity unachukua na ukiacha ujue imekula kwako. Lowassa na opportunity kwa UKAWA na Watanzania wote kwa ajili ya kuondoa mfumo kandamizi wa CCM.
 
fuvu la paka

Unahisi kwa moyo wote huyo uliyemtaja yuko kwa ajili ya kuwatumikia wananchi? mi nadhani wangemtumia huyo kama daraja la kuvukia kuwatumikia wananchi?

Waswahili walisema adui muombee njaa
 
Last edited by a moderator:
Umezungumza lakini ujue nafasi ya makamu wa rais ipo kikatiba. kuibadilisha ni lazima uitishe bunge.

Clemence, hilo wanaweza kutafuta mtu mwenye influence kwa upande wa Zanzibar ili awe mgombea mwenza wa Lowassa. Na hilo litatoa nafasi kwa Prof. Lipumba kugombea ubunge Tabora ili aje kuwa waziri wa Fedha.
 
fuvu la paka

Kama lengo ni kuiondoa CCM nakubaliana na wewe. Lakini kama ni kuwatumikia wananchi kuna mambo mengi sana ya kuyachunguza kabla ya kufikia hapo.....kumbuka Lowasa ana marafiki akina Karamagi, Rostam, na mafisadi underdogs wengi mno ambao sidhani kama Ukawa wanaweza kukubali kuungana nao.....labda Lowasa atangaze kuachana nao kitu ambacho hana ubavu nacho.
 
Last edited by a moderator:

Tena wasichelewe, asikudanganye mtu, nimegundua wananchi wengi hawaujui ufisadi wa LOWASA ni kama hadithi za kusadikika na kufikirika tu.
Huyu mtu ameivumilia sana CCM, na ana kitu kikubwa sana cha kuongeza kwenye upinzani.
 
Uzi wako una mantiki nzuri sana, sema UKAWA wanaanzaje kumsafisha kwa wananchi ili aeleweke vizuri?
Mkuu kusafisha Lowasa ni kazi ndogo tu ni hivi "NDG WANANCHI LOWASA SI FISADI ILA ALIBEBESHWA MZIGO WA DHAMBI WA CHAMA ILI CHAMA CCM KIENDELEE KUTAWALA,ILA UKWELI NDG WANANCHI SISI KAMA UKAWA TULIKUWA TUNAMCHAFUA NDG LOWASA ILI CCM WAMWACHIE AJE HUKU UPINZANI TUENDELEZE MAPAMBANO YA KUKING'OA HIKI CHAMA KONGWE,PIA NDG WANANCHI KUMBKENI SIASA NI MCHEZO WA KIHUNI HIVYO TULIMUHTAJI SANA LOWASA AONGOZE MAPAMBANO HAYA KWANI LOWASA NI MTU SAFI,SAHIHI,TUNAMPENDA NA TUNAMUAMINI ATATUPELEKA KTK MABADILIKO YANAYOTARAJIWA NA UKAWA" hili ndio dodoki pekee la UKAWA kwa lOWASA mkuu!!
 

mkuu, nitafute baadae upate kinana mbili...
 
Narudia tena. LOWASSA ni Asset na Ukawa ni Asset. Hivyo,Lowassa (Asset) + Ukawa (Asset) = USHINDI WA URAIS + WABUNGE + MADIWANI. Wenye uelewa wataona hilo.


👏👏👏👏 excellent perception...!!!

Nitashangaa sana Dr. Slaa agome kuungana na Lowassa ktk kuikomboa nchii hii.. nitamuona Dr. Slaa hajui siasa..na sio mtu kabisa...


Ukawa + Lowassa...NI USHINDI TU...

I bet, there is no way CCM can come close to win tht combination...!!!

Yaani USHINDI ni kabla hata ya October...


Ukawa + Lowassa ni UKOMBOZI WA WATANZANIA...

Lazima Dr. Slaa ageuze mawazo ya mgando sasa, awe kama MBOWE.. maana Mbowe is very very clever ktk mtaji wa kisiasa kama Lowassa, na ana spirit ya ushindi wa wazi....

I know, kwa sasa Mbowe au Prof. Lipumba hawana shida ya kuungana na Lowassa, tatizo ni Dr. Slaa...

Lazima Dr. Slaa akubali haraka, aone kama Kenya walivyofanya na UKAWA + Lowassa, CCM ni kifo...!!!

Yaani hakuna namna CCM itapona hapo...!!!

Yetu macho, CCM byebyeee....
 

Una hoja hasa kwenye sera na ilani lakini naomba usiwapumbaze CHADEMA na UKAWA kwa matokeo ya serikali za mitaa, kwani unajua influence ya Magufuli kwa kanda ya ziwa??? kama unafikiri utani, wewe subiri October 2015.
 
Sijawahi kuona ushauri wa hovyo kama huu wa kwako hapa.

Hakuna haja ya kuiondoa ccm madarakani ikiwa tutaweka wagombea wale wale mafisadi walioua nchi yetu. Ukiitoa ccm kwa kuwa imekuwa fisadi na mafisadi ndio hao hao kina Lowasa, halafu unampa uongozi wa nchi fisadi gumegume yule yule Lowasa, utakuwa ama una maradhi ya akili ama huna msingi wala sababu ya maana ya kutafuta mabadiliko. Utakuwa unatafuta mabadiliko kwa maslahi yako binafsi na si ya umma kitu ambacho UKawa hakikubaliki.

LAWASA AKIGOMBEA URAISI KWA CHAMA CHOCHOTE HATUMPIGII KURA SISI WATANZANIA HALISI TUNAOTAKA TANZANIA YETU ASILIA.

Hueleweki unapoongelea Lowasa awe mgombea wa UKAWA, huku references and standards zako zote ziko ccm!. Kwa kuwa ccm wote ni mafirauni na hakuna msafi, basi ukawa wasimamishe tu hilo fisadi nao? Wewe vipi lakini?

UKaWA inachukua nchi without haja ya mkono wa mafisadi!.

Hii kumtengenezea njia mwenye safari ya matamanio, imebuma, tafuta mlango mwingine. Labda jaribu kwa Zito au IPPT Maendeleo!, Ukawa kumejaa nahata hivyo access denied!.
 


Hapana, nadhani ukweli tuusimamie, Lowasa sio mwadilifu! Basi hilo lituongoze na si vinginevyo
 
Lowasa ni CCM na katika wakoloni waliotuweka mpaka hapo tulipo. Lowasa alikuwa anatafuta madaraka ili aendelee kuimarisha himaya yake ya kutuibia Watanganyika kwa hiyo hatuwezi kuhamisha hiyo himaya yake na kuinganisha na wapambanaji wanaotaka kumwondoa huyo mkoloni mweusi. Tutakuwa tunajiangusha wenyewe. Jiulize kwa nini CCM wamemuondoa, ni kwa sababu ni mchafu. Wamemwondoa maana walijua wakimweka UWAKA watamponda na kuwaangusha kwa hiyo wametafuta kujisafisha japo bado ni wachafu. UKAWA wanazo siraha za kutosha hawahitaji mtu mchafu kuja kuwapigania. Kwa hiyo kama Watanzania wanahitaji mabadiliko waje bila Lowasa
 

Good observation.
 
Tena wasichelewe, asikudanganye mtu, nimegundua wananchi wengi hawaujui ufisadi wa LOWASA ni kama hadithi za kusadikika na kufikirika tu.
Huyu mtu ameivumilia sana CCM, na ana kitu kikubwa sana cha kuongeza kwenye upinzani.

Na hata hao wapinzani wake (CCM) watakosa hoja ya kumwita fisadi maana walikula wote.. Watamwitaje EL fisadi wakati wao wote ni mafisadi. Hii ndio move pekee ya UKAWA kuweza either kuchukua nchi au kupata wabunge wengi ambao watatupa Waziri Mkuu na Spika wa Bunge..
 
Lowassa fisadi hajawahi kuwa upande wa wananchi,
 

Watu wengine bwana!, hivi ni nani ambaye yuko ukawa na ana nguvu huko hakuwahi kuwa CCM? CCM ina mfumo wake na CHADEMA wana mfumo wao. Si Mbowe wala Dr. Slaa ambaye hakuwahi kuwa mwana-CCM huko nyuma. Wote wametokea huko, lkn mfumo uliopo CHADEMA na ile spirit ya Lowassa ya kufanya kazi ni muhimu sana. Halafu pia mmekalia uchafu uchafu wa Lowassa ni upi??? Hivi kuwa tajiri haupaswi kugombea uongozi wa nchi? Je ni nani wa kulaumiwa kama alikuwa halipi kodi kwenye biashara zake? si ni serikali hiyo ya CCM?
 


Kombe la dunia 2010 Suarez alidaka mpira uliokuwa unaingia golini dakika ya mwisho kabisa ya mchezo.. Unajua nini kilifuata?? Alipewa kadi nyekundu, wapinzani wake wakapiga penalt na wakaikosa, then unajua nini kingine kilitokea?? Mwisho wa mechi akina Suarez wakaibuka kidedea.. Wakati mwingine lazima ukubaliane na facts na kucheza rafu ndogo ndogo ili tu mpate ushindi.. Mara nyingi kwenye mpira anayetafuta suluhu au ushindi kwa hali na mali inawalazimu mpaka kufanya mbinu chafu ili washinde, wanajidondosha kwenye 18 ili wapewe hata penalt..

Tuendelee kujidanganya kwamba ni rahisi kuishinda CCM bila rafu na mbinu yeyote ile.. Ila kumbuka, kinachoongoza nchi si mtu bali ni system na sera. Hata unayemwona msafi UKAWA akipelekwa CCM anaweza kugeuka mchafu kuliko, nani alitegemea ZZK atakuwa hivi alivyo?? Kama umekubaliana na scenario hiyo, basi pia hata yule mchafu CCM anaweza kuwa msafi akiingia UKAWA..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…