Elections 2015 UKAWA na Lowassa unganeni mchukue nchi, wakati ndio huu, mkipuuzia huu ushauri basi tena!

Elections 2015 UKAWA na Lowassa unganeni mchukue nchi, wakati ndio huu, mkipuuzia huu ushauri basi tena!

Serena-Naomba ieleweke kwamba mpaka sasa majimbo ya CHADEMA hasa za maeneo wanakokaa wasukuma (Kanada ya Ziwa) kwa kiasi kikubwa yatarudi CCM kwasababu ya Magufuli kuwa msukuma. Asiyetaka kukubaliana na mimi asubiri October


Mimi sikubaliani na wewe juu ya Wasukuma ,Wasukuma wa sasa wanamwamuko mno kuliko kipindi cha nyuma wako tayari kuonekana wanamuunga mkono Magufuli kwa sasa na wakati wakapeni na wakajitokeza kwa wingi kurudisha kadi za vyama vya upinzani lakini siku ya kupiga kura wanapigia upinzani.

Kwa mfano matokeo ya Ubunge 2010 Ilemela na Nyamagana walishinda Chadema dhidi ya CCM iliyokuwa na Masha na Dialo wasukuma. Jimbo la Kwimba mhindi aliwashinda wazawa wa Kwimba kwenye mchakato wa CCM ktk kura za maoni.

Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2014 hasa kwenye maeneo ya wakazi walio na mchanganyiko na kabila nyingine pia wazawa (wasukuma) waliopeperusha bendera ya ccm dhidi ya Chadema walishindwa vibaya.

Wanachotakiwa UKAWA wawe na ilani inayouzika kwa urahisi kwa makundi yote wakulima, wafugaji, wafanyakazi, wavuvi, Elimu, Afya na hasa ileeze nini watafanya kuwaondolea wananchi hali hii ngumu ya maisha. Kwa mfano mwaka huu wasukuma wanaolima pamba kama zao la biashara bei ni mbaya kuliko kipindi cha Mwinyi na Mkapa ambapo kipindi hicho pamba ilikuwa dhahabu yao.
Msimu huu bei ya pamba kwa kilo ni sh800 (ongezeko la sh 100 ya bei ya mwaka jana) na bei hii tangu msimu wa mwaka 2011 haijawahi kuvuka hapa.Kipindi cha Mkapa walikuwa hawanunui mbegu za pamba lakini kwa sasa mbegu wanauziwa.
 
Kama tutaendelea kujidanganya kwamba UKAWA pekee yao watachukua hii nchi basi tutakuwa watu wajinga zaidi duniani..

No way, lazima mtu mwenye nguvu kutoka chama tawala ajiengue nao then ajiunge na wapinzani hapo ndipo kutakuwa na urais wa upinzani kushinda chama tawala. Tumeyaona hayo yakitokea kwenye nchi zetu nyingi tu za kiAfrika. UKAWA tukitaka kwenda Ikulu ni lazima tukubali kushirikiana na Lowassa.. Ni dhahiri EL ana mtaji wa watu wengi sana nyuma yake, kuli'ignore kundi kubwa hivo lililopo nyuma yake utakuwa ni ujinga wetu na kamwe tusitegemee kwenda Ikulu tena miaka ya karibuni..

Wale wanaobeza UKAWA kushirikiana na EL watakuwa ni wapumbavu wasiotakia upinzani mafanikio.. Narudia, kama viongozi wa UKAWA wanaweza kunegotiate na EL wafanye hivyo haraka..
Uko sahihi kabisa na hapo ndo kuna hoja ya msingi. Wanaotukana hawana nia njema na mabadiliko ya kweli. Wanaosema Lowassa ni fisadi watuambie ni nani msafi ndani ya CCM. Kuna watu wanafikiri kuitoa CCM madarakani kazi nyepesi??? wapo wengine wanadhani ni kuhubiri ufisadi majukwaani kunatosha???? Nataka niwaambie wale wote wanaobeza hoja yangu kwamba kuitoa CCM madarakani na mfumo wake unaotufanya tuendelelee kuwa maskini ni zaidi ya majibizano ya hapa mtandaoni, ni mikakati thabiti ikiwemo na ya kutafauta mtu mwenye back up, kitu ambacho Lowassa atasaidia sana.
 
atumtaki ndani ya ukawa

Sema haumtaki wewe usitusemee na sisi kwa sasa tunachotaka ni kuiondoa ccm madarakani hyo ndio mission yetu kwani mbona tumeungana na nyie chadema na atusemi kitu? hapa mission ni kuitoa ccm huyu fuvu yupo sawa kabisa ukawa sio chama ila ni muunganiko wa vyama na wanasiasa wasioitaka ccm madarakani .AMKA BRO
 
Kwel kabisa aje ukawa hata kule kusema chama flan kimependelewa kutakuwa hamna yan weng tunataman ukawa wamsimamishe lowasa ni rung tosha la kuuwa chichiem
 
Kama tutaendelea kujidanganya kwamba UKAWA pekee yao watachukua hii nchi basi tutakuwa watu wajinga zaidi duniani..

No way, lazima mtu mwenye nguvu kutoka chama tawala ajiengue nao then ajiunge na wapinzani hapo ndipo kutakuwa na urais wa upinzani kushinda chama tawala. Tumeyaona hayo yakitokea kwenye nchi zetu nyingi tu za kiAfrika. UKAWA tukitaka kwenda Ikulu ni lazima tukubali kushirikiana na Lowassa.. Ni dhahiri EL ana mtaji wa watu wengi sana nyuma yake, kuli'ignore kundi kubwa hivo lililopo nyuma yake utakuwa ni ujinga wetu na kamwe tusitegemee kwenda Ikulu tena miaka ya karibuni..

Wale wanaobeza UKAWA kushirikiana na EL watakuwa ni wapumbavu wasiotakia upinzani mafanikio.. Narudia, kama viongozi wa UKAWA wanaweza kunegotiate na EL wafanye hivyo haraka..
huu ndio ukweli halisi,naamini MBOWE anajua kucheza vema na mitaji ya kisiasa hasa kwa lengo la kuongeza nguvu na kupiga hatua kufikia matarajio ya waTanzania.
 
Narudia tena. LOWASSA ni Asset na Ukawa ni Asset. Hivyo,Lowassa (Asset) + Ukawa (Asset) = USHINDI WA URAIS + WABUNGE + MADIWANI. Wenye uelewa wataona hilo.
 
fuvu la paka

LOWASA+UKAWA =URAIS
historia mpya na maneno ya nyerere yatatimia kuwa upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm.kwikwikwikwikwi
 
Last edited by a moderator:
Yeye aungane na sisi UKAWA yaani aje atupe sapoti kupiga kampeni na kuhamasisha wananchi ila sio.aje kugombea URAIS,hiyo haikubaliki
 
Nimeamini baadhi ya watanzania ni waumini wa maovu.Hatujui kutafakari kabisa.Mnayemtaja ni Lowasa huyu huyu au mwanae. Kama ukawa wanataka kufa kifo kibaya Lowassa aingie nyumbani kwao.
 
Naona Team Lowasa mnaweweseka na Lowasa wenu. Nani alikwambia UKAWA wanatafuta ushindi kwa njia haramu? Lowasa ni mchafu na UKAWA ni watu wasafi hawako tayari kuchafua njia na nia yao ya kujenga Tanzania iliyo safi kwa kuungana na uchafu. Lowasa ni fisadi na sera za UWAKA ni kuwaondoa mafisadi akiwemo Lowasa itakuwaje wawe na nia hiyo halafu wamchukue fisadi kupambana na mafisadi. Ni njia haramu kuwa naye kwenye mapambano. Mtafutie kwingine na si WAWAKA
 
Ni ushauri mzuri na unapaswa kujadiliwa na viongozi wote wa UKAWA kwa maslahi mapana ya nchi yetu!
 
Nyie mapopoma ni either CCM mnaogopa hiyo theory au hakuna mnachokijua kwenye ulingo wa siasa..

U can never wake up with million bucks just over night.. never on this Earth.. Hatuwezi kukishinda chama tawala kama chama hicho hakitapasuka, haitowezekana. Ndani yao kuna matajiri wakubwa, wana vyombo vya dola, wana mahakama, tume pia ni yao.. Usitegemee kuchukua nchi kama hivyo vyote havitogawanyika. EL ana kundi kubwa na matajiri nyuma yake (ambao kimsingi ndio dhana kubwa ya CCM), EL ana wafuasi mbalimbali walioko juu serikalini na hata kwenye Tume ya Uchaguzi, jeshini na hata Polisi. Tutakuwa wajinga kwa tuna'ignore jambo muhimu kama hilo..
Kamwe usitegemee CCM watangaze tu kirahisi eti UKAWA mmechukua nchi.. hahahaha tutasubiri sana


Ngugu yangu,
Wewe una hoja ya msingi sana. Hakuna namna UKAWA wakashinda uchaguzi bila kupata mtu toka CCM mwenye nguvu. UKAWA wana bahati sana, kwani hawajampata mgombea wao na Lowassa ametolewa kwenye kinyang'anyiro CCM. Hivi, nikiwauliza hawa wanaopinga hili wazo la Lowassa waniambie ni nani ambaye akitoka CCM anaweza akashinda akiwa UKAWA dhidi ya Magufuli mbali na Lowassa? Nataka niwaambie ni kwamba HAKUNA mwingine zaidi ya Lowassa. Si Sitta, Membe, Mwandosya, Makongoro, na hata Mwakyembe anayeweza kufanikisha hilo. Mimi narudia tena, hii ni fursa pekee kwa UKAWA na Lowassa, na wakizembea tu, nataka nikuambie kwamba jinsi UKAWA walivyoshindwa kuinfluence hata Tume ya Uchaguzi iwe huru, na mengineyo hasa kwenye BVR, then, wasahau kabisa kuingia Ikulu na hata wabunge watapungua sana, zikiwemo na kura za urais ambazo zina impact kwenye wabunge wa viti maalumu.
 
huu ndio ukweli halisi,naamini MBOWE anajua kucheza vema na mitaji ya kisiasa hasa kwa lengo la kuongeza nguvu na kupiga hatua kufikia matarajio ya waTanzania.

Tukishindwa mwaka huu, tusitegemee tena miaka ya karibuni..
 
Serena

Umezungumza lakini ujue nafasi ya makamu wa rais ipo kikatiba. kuibadilisha ni lazima uitishe bunge.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo Lowasa ndio atafanya iwe nyepesi ?
Basi asimame peke yake aende kwingine.

CDM imehangaika na mapandikizi Zitto, Shibuda na wengineo na bado makovu hayajakauka , mnataka kuleta makovu mengine?
 
fuvu la paka

Kuungana na Lowasa na kuungana na uchafu ambao CHADEMA imepata umaarufu kwa sababu ya kuuibua na kuukemea. CHADEMA wataonyesha unafiki wa hali ya juu watakapokaribisha fisadi yoyote katika chama chao. Hata watu wa Kaskazini ambako inadaiwa CHADEMA imejizatiti na ambako Lowasa anatoka watakihama chama na bila shaka wataingia CCM.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom