Mkuu nadhani kuwa mkakati huo wa UKAWA kama upo utakuwa na mapungufu zaidi.Mkuu Nguruvi3,
Kuna mtu huku "saiti" tukiwa kijiwe cha kahawa na kashata amejenga hoja kwamba pengine ukimya wa UKAWA ulilenga kuacha kwanza Rais Kikwete azungumze anachotaka kuzungumza kabla na wao hawajaanza kujibu mapigo. Nini mtazamo wako juu ya hili.
Nguruvi3, serikaili ya tanganyika ndio serikali kuu na ndio maana wanasema tumevaa koti la Muungano. Kama hujui undani wa maneno hayo inabidi urudi nyuma kwanza kabla ya kuendeleza malumbano.Alaa kuuumbe! sasa bendera, na serikali ya Tanganyika ipo wapi?
Kumbuka Ontario wanavyo halafu wana mambo ya federation. Sasa tuambie sisi, kwavile unakubali kila nchi ilikuwa huru na ina haki ya mambo hayo, vipi, serikali ya Tanganyika ipo wapi?
Hebu nionyeshe mfano mmoja wa huko majuu unaolingana na muundo wetu.
Ok, sasa niambie kwa kutumia S2 tunawezaje kufanya mambo na kuondoa dhana ya kuvaa koti la muungano?Nguruvi3, serikaili ya tanganyika ndio serikali kuu na ndio maana wanasema tumevaa koti la Muungano. Kama hujui undani wa maneno hayo inabidi urudi nyuma kwanza kabla ya kuendeleza malumbano.
Ikiwa mambo yote ya Tanganyika yanashughulikiwa na serikali kuu wewe unaitafuta Tanganyika yenye bendera yake ya nini, ili iweje? Hivi unaweza nambia ni serikali gani ilopinga OIC kwa Znz kama sio serikali ya Tanganyika? Walokataa mahakama ya kadhi ni kina nani kama sio serikali ya tanganyika?..Hiyo bendera itabadilisha kipi ktk kero ama mapungufu ya Katiba iliyopo.
Nimeshasema wazi kuwa ikiwa kila waziri ktk serikali kuu una mamlaka ya shughuli za Tanganyika huoni kama hapa tumevaa koti la muungano. Abrahaman Babu katuletea reli ya Tazara leo hii sii mali ya Muungano ila Tanganyika kwa sababu ya hayo mambo yasokuwa ya muungano - huoni kama hapa tunatumia jina la Muungano kutufaidhisha bara lakini Znz wanapotaka mambo yao inabidi kwanza yapitishwe na serikali kuu.
Uliona wapi mfumo wa kidemokrasi ambao shughuli za serikali bado mamlaka yake yanatoka serikali kuu. RC hana nguvu isipokuwa kwa rais, Meya wa jiji hana mamlaka isipokuwa kupitia RC wa rais, waziri pia ni mbunge mwanasiasa sii lazima awe na uwezo wa kuongoza. Haya ndio maswala ya kuzungumzia sio muungano hata kidogo.
Pwenye demokrasia, mamlaka ya kuendesha shughuli zote za serikali hupewa vyombo vilivyoundwa kwa ushiri9kiano na serikali kuu sio hii habari ya serikali 2 au 3. Kama Mfumo utaendelea kuwa kama ulivyo haijalishi kama tutakuwa na serikali 3 au Muungano maana bado CCM watajkuwa na mamlaka yote yanayotakiwa wao kuendeleza mfumo wa ujima. Tutakuwa kama China japo wanaendelea lakini ni asilimi 1 tu ndio wanatajirika wakiwaacha mabillioni ya wananchi ktk umaskini wa kutupwa.
Leo hii China inaongoza kwa umalaya na kusafirisha nje Malaya, bwimbwi linauzwa kama njugu tena kwa bei kubwa kuliko Ulaya, Cocaine na Opium inatajirisha cartekl za kichina kiasi kwamba watu hawaendi tena Thailand kutafuta dogo. Lakini hutamkuta mtoto wa kiongozi wa China akiteseka wote wanaspoma Ulaya na Marekani ni matajiri wa kutupwa na kwetu dalili zinaanza kujitokeza kutokana na nguvu ya chama tawala.
Hapa ndipo tunapotakiwa kujikita, hakuna sababu ya kubishana na kupishana na CCM kwaa kila jambo kwa sababu tu hatuwaamini ama sisi ni wapinzani. Tutachekesha kesho kama kweli tutaendelea na Ubishi huu.
Swadakta! hujawahi kuniuliza swali hili na japo majibu yangu yamo ktk maandishi yangu mengi tu.Ok, sasa niambie kwa kutumia S2 tunawezaje kufanya mambo na kuondoa dhana ya kuvaa koti la muungano?
Hapa ndipo hutaki kutueleza. Tufafanulie wewe na CCM mnataka S2, tuna solve vipi problem hamtuelezi.
Nafasi hii ni ya swali moja, JMT na SMZ zitafanyaje kazi ili kutenganisha mambo ya muungano na yasiyo ya muungano kuondoa dhana ya kuvaa koti la muungano?
Mkuu wewe unataka majibu gani kama sii yale unayotaka kuyasikia. Unauliza swali wakti majibu unayo ama unataka kufahamishwa?..Mkuu Mkandara nimekusoma hapo juu na nakuhakikishia hujajibu swali na sijui kama kuna msomaji amekuelewa.
Nitarudi kufafanua, isipokuwa ukweli unabaki kuwa hujajibu swali la jinsi tunavyojivua koti.
Nikupe dondoo, 2/3 ya bajeti ya znz inatoka Tanganyika, wewe unaamini kujenga bandari ndilo suluhissho.
Hiyo sales tax kwasasa haitoki znz wewe unaamini itatoka tukiendelea na muundo huu.
Hujagusia kuwa ile ni nchi (katiba 2010) wewe unaamini ni Watanzania. Nani kakwambia wznz wanahitaji Utanzania? Wangekuwa wanahitaji utanzania wasingekuona wewe kama kicheche. Hivi unawajua au unawasikia.
Nitarudi, ninachokuhakikisha umeandika lakini hakuna jibu, hukujibu kabisa just beating around the bush.
Mkandara walk the talk
Mkandara amegeuka, hapo nyuma amesema anakubali serikali 3, wiki moja baadaye anasema hataki S3.(Rekodi ipo jf ikihitajika)Mkandara;9388985]Kuhusiana na swala la S2, nimesema wazi kwamba sioni sababu ya kuwa na serikali 3 kwa sababu lengu la muungano wetu ulikuwa ufikia S1. Hivyo kama kero kubwa ya Wazanzibar ni Tanganyika kulivaa koti la Muungano basi tulivue na sii lazima tuvue nguo zote. Tulivue koti kuelewa koti hilo sii mzigo ila mzigo kwetu ni lawama zenye logic kuvaa koti wakati wa jua kali kuombea wafadhili watutowe!
Mkandara Kwanza tutambue na kukubali kwamba Zanzibar ni NCHI kwa sababu Znz ina sii tu serikali yake, bali ina mahakama yake na bunge lake. Mihimili hii mitatu ndio nguzo thabiti za utawala wowote wa NCHI. Hivyo ni makosa makubwa kusema Zanzibar sio nchi ati tuna serikali 2 ktk nchi 1, huu ni Uongo na unafiki maana hatusemi Znz sio tu wana serikali yao, wanazo pia Mahakama na bunge lao. Sisi tuna nchi 2 zilizoungana kuunda TAIFA MOJA. Hutawasikia kina Warioba wakitamka hili neno TAIFA japo watasema tunao wimbo wa TAIFA na Bendera ya TAIFA. Huwezi kusema bendera yetu kuwa ni bendera ya NCHI ama tuna wimbo wa NCHI (Tanzania)[/QUOTE Mkandara kasome tena taarifa ya Warioba. Tume imezungumzia vizuri sana kuhusu utaifa na hatari iliyopo.
Kasome taarifa msimwekee maneno na CCM wenzenu mzee wa watu. Taarifa hujaisoma
Mkandara kasome tena taarifa ya Warioba. Tume imezungumzia vizuri sana kuhusu utaifa na hatari iliyopo. Kasome taarifa msimwekee maneno na CCM wenzenu mzee wa watu. Taarifa hujaisomaMkandara: Kwanza tutambue na kukubali kwamba Zanzibar ni NCHI kwa sababu Znz ina sii tu serikali yake, bali ina mahakama yake na bunge lake. Mihimili hii mitatu ndio nguzo thabiti za utawala wowote wa NCHI. Hivyo ni makosa makubwa kusema Zanzibar sio nchi ati tuna serikali 2 ktk nchi 1, huu ni Uongo na unafiki maana hatusemi Znz sio tu wana serikali yao, wanazo pia Mahakama na bunge lao. Sisi tuna nchi 2 zilizoungana kuunda TAIFA MOJA. Hutawasikia kina Warioba wakitamka hili neno TAIFA japo watasema tunao wimbo wa TAIFA na Bendera ya TAIFA. Huwezi kusema bendera yetu kuwa ni bendera ya NCHI ama tuna wimbo wa NCHI (Tanzania)
.Mkuu tena anasahau alituambia kuwa Tanganyika ilikufa na kuwa Tanzania (Rekodi ipo JF ikihitajika tutaitoa)Mkandara: Tanganyika ipo na ndio serikali kuu kwa sababu tunatumia bado katiba ile ya CCM iloboreshwa kuondoa matumizi makubwa ya serikali.
2. Kutokana na mageuuzi ya Kiuchumi (soko Huria) na kisiasa (vyama vingi, Katiba iliyopo imepitwa na wakati hasa ktk kuuboresha muungano. Hii habari ya Mambo yasokuwa ya Muungano kuwa ndio shughuli za serikali ni makosa kuendelea kutumiwa leo hii kutokana na hali halisi ya leo. Kwa maana ya kwamba hakuna Mambo yasokuwa ya Muungano ktk Taifa lolote unless tunabaguana
Mkuu anasema mambo yote ni ya muungano.Mkandara: Mambo yote ni ya Muungano isipokuwa shughuli zake ndizo huwa za serikali, hivyo ndio kusema wizara ya ELIMU inatakiwa kuwa ni uya Muunngano isipokuwa uendeshaji wa shughuli za elimu ndipo tunapotofautisha kati ya Zanzibar na Bara. Mamlaka hayo watapewa serikali za Zanzibar na serikali ya Bara kama ilivyo. Mwafunzi anaweza kwenda popote kusoma pasipo kubaguliwa yoka darasa la kwanza hadi chuo kikuu. Kilimo na wizara zote ziwe chini ya serikali kuu ambayo itafaidika kwa asilimia 60 ya pato toka pande hizi mbili
Mchango wa znz ni upi kama tunajua wa Tanganyika. Tunachotaka ni kuwa mchango wa Tanganyika umnufaishe mlipa kodi wa Tanganyika si wa nchi jirani uliyosema ya znz.Mkandara: Kama tumeweza kujua mchango wa tanganyika ktk mfuko wa Taifa leo hii ndani ya serikali 2 binafsi sioni saabu ya kuunda serikali ya 3 ili tujue lile lile linalojulikana leo maana gharama za uendeshaji serikali hutokana na kodi za wananchi. Kodi akilipa Bakhresa akiwa Dar inahesabika ni makusanyo ya Bara haihitajiki kuweka jina tanganyika kutambua kodi ya Bakhresa imetoka wapi. Hii ni hawa kwa uwekezaji wa nje maada makao makuu ya Azam yapo bara basi kodi yake inakusanywa na itaendelea kukusanywa Bara ndani ya serikali zozote
Mkuu, wazanzibar hawataki Tanzania, mbonahuwaelewi. Sisi tumejiita Watanzania miaka 50, wao hawataki kabisa. Mkuu somakatiba yao uone kama kuna sehemu wanautambua utanzania3. Kulivua koti hili la Muungano ni pale sisi bara tutakapo wezakutambua kwamba Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.Wana mchango mkubwa sana ktk Taifa hili kulingana na location ya visiwa hivyo.Tusiutazame mchango wa Zanzibar kwa kupima fedha ama bendera ama katiba yaobali tunawezaje kuitumia Zanzibar kuboresha GDP ya Taifa zima. Kwa mfano tukijengabandari kubwa Zanzibar na kuifanya freeport (siisales Tax), Kujenga soko kuu la kilimo, spices, matunda na nyama kwa ajili yaexport kuvuta nchi za asia na Ulaya kutoka na freepot hivyo imports na exportszitalenga kupitia Znz.
Mkuu mikopo na granta si lolote sichochote ukilinganisha na msaada wanaopata sasa hivi. Hatuna sababu za kuwapazaidi ya wanachopata maana wanapata hata wasichostahili.4. Tutalivua koti kwa kuhakikisha kila mikopo, misaada nagrants zinayochukuliwa nje kwa ajili ya ujenzi wa Tanzaniaiwe Bara au visiwaniinafaidisha Taifa zima kwa ile asilimia 60 wanayochukua serikali kuu. Kwa maanahiyo kama Dhahabu ya Geita au reli ya kati, Tazara inachagia mfuko wa Taifabasi mfuko huo ni wetu sote.Na kama Karafuu ya Zanzibar inauzwa nje, basi wajueasilimia 60 ya kodi ama ushuru wake inakwenda moja kwa moja ktk mfuko wa Taifawao watabakia na asilimia 40 ya makusanyo ya kodi. Ugonvi mkubwa baina yetu naZnz umetokana na hili, haya nimesoma kuwa JK kapata mkopo mkubwa toka IMFkuboresha reli ya kati kwa jina la Tanzania, sasa tujiulize iweje pato la relihiyo halitakuwa la muungano hata kwa asilimia 1 kwa sababu tu ati sii mambo yamuungano?. Kwa nini isiwe shughuli za uendeshaji wa reli hiyo ndio uwe nimamlaka ya bara, lakini kitakacho ingizwa 40% ya bara na 60% ya Muungano hukotuna kisu kingine. Kwa haya machache kati ya mengi Kero hazitakuwepo..
Mkuu wangu hivi kweli wewe mgumu kiasi hiki kuelewa?Mkandara amegeuka, hapo nyuma amesema anakubali serikali 3, wiki moja baadaye anasema hataki S3.(Rekodi ipo jf ikihitajika)
Kero unazozungumzia ni wznz, vipi Watanganyika hawana?
Kubaguliwa si kero. Waziri mkuu kuomba kibali cha kazi znz na kibali cha kuishi si kero?
Mtanganyika kuchomwa moto ili aondoe biashara zake znz si kero?
Mwanafunzi wa Tanganyika kunyimwa mkopo znz si kero?
Mtanganyika kunyimwa ardhi, na znz kutoa ardhi kwa watu wa mombasa, Oman na wataliano si kero? Watanganyika kunyimwa ardhi znz si kero?
Katiba ya muungano ambayo ni ya Tanganyika kwa mujibu wako au serikali ya bara kama unavyosema ni chini ya katiba ya nchi jirani ya znz, hiyo si kero
Tumekuuliza tunavua vipi koti umezunguka hukusema kitu kikaeleweka. Huwezi kuvua koti kwa kuacha kujenga bandari Mtwara ili ijengwe nchi ya jirani. Kwanini tusiache Kenya wakajenga tudhani znz ni muhimu sana. Biashara kati ya Kenya na Tanganyika ni kubwa mara 1000 ya biashara kati ya Tanganyika na znz.
Mwenzenu, hili la UKAWA bado sijalielewa vizuri sana japo najaribu sana kulielewa. Sijaelewa kama ni Muungano unaotaka kuja kuongoza taifa letu au ni muungano ambao unataka kuiondoa CCM; sijafahamu vizuri kama ni Muungano wenye lengo la kuhakikisha tu Tanganyika inarudi na Zanzibar inakuwa na mamlaka yake au ni Muungano unaotaka kuboresha Muungano kwa kuleta Serikali Tatu. Maana nina hofu - na sitashangaa kuwa zitakuwa kweli - kuwa tusije kushuhudia kama ule Muungano wa kwanza wa kina Mwai Kibaki na wengine walipojaribu kuiondoa KANU ambapo walionekana wameungana mwaka 2002; na kwa kweli waliweza kuiondoa KANU madarakani. Lakini sote tunajua matokeo yake yalikuwa nini ilipofika 2007.
Binafsi sijaona kama muungano huu ulifikiriwa sana kabla ya kufanyika (hatukuona wamejiorganize kabla ya Bunge la Katiba wakati wa kura za maoni n.k) ni kama more reactionary than anything. Na kinachowaunganisha ni suala la Tanganyika na Zanzibar hatujui itakuwaje watakapofika kwenye mambo mengine yaliyomo kwenye rasimu kama wataweza kuwa pamoja hasa kama mitazamo ya kivyama itapishana.
Bora wewe mkuu umeliona hilo na wala usidhanie vinginevyo maana kinachofanyika hapa ni Political mind game! inaudhi hasa ukizingatia hawa watu wamepewa dhamana hii kuandika Katiba Mpya.Mwenzenu, hili la UKAWA bado sijalielewa vizuri sana japo najaribu sana kulielewa. Sijaelewa kama ni Muungano unaotaka kuja kuongoza taifa letu au ni muungano ambao unataka kuiondoa CCM; sijafahamu vizuri kama ni Muungano wenye lengo la kuhakikisha tu Tanganyika inarudi na Zanzibar inakuwa na mamlaka yake au ni Muungano unaotaka kuboresha Muungano kwa kuleta Serikali Tatu. Maana nina hofu - na sitashangaa kuwa zitakuwa kweli - kuwa tusije kushuhudia kama ule Muungano wa kwanza wa kina Mwai Kibaki na wengine walipojaribu kuiondoa KANU ambapo walionekana wameungana mwaka 2002; na kwa kweli waliweza kuiondoa KANU madarakani. Lakini sote tunajua matokeo yake yalikuwa nini ilipofika 2007.
Binafsi sijaona kama muungano huu ulifikiriwa sana kabla ya kufanyika (hatukuona wamejiorganize kabla ya Bunge la Katiba wakati wa kura za maoni n.k) ni kama more reactionary than anything. Na kinachowaunganisha ni suala la Tanganyika na Zanzibar hatujui itakuwaje watakapofika kwenye mambo mengine yaliyomo kwenye rasimu kama wataweza kuwa pamoja hasa kama mitazamo ya kivyama itapishana.