Kwa hiyo usipowaunga mkono UKAWA ina maana unawaunga mkono CCM? huoni kama unacheza mchezo mchafu sana wa kisiasa badala ya kutazama hoja iliyopo ubaoni? Je kutokubaliana na serikali 3 inaondoa hata hilo neno sikubaliani na mengi ya CCM au?.......................................
Mkuu Mkandara, hakuna suala la UKAWA. Tafadhali rejea nyuzi za mwaka 2011 haya ya UKAWA, Tanganyika imekuwa sehemu ya mijadala ninayoshiriki sana.Kwa hiyo usipowaunga mkono UKAWA ina maana unawaunga mkono CCM? huoni kama unacheza mchezo mchafu sana wa kisiasa badala ya kutazama hoja iliyopo ubaoni? Je kutokubaliana na serikali 3 inaondoa hata hilo neno sikubaliani na mengi ya CCM au?
Wee nambie hawa wajumbe wanaotaka muundo wa serikali ubadilishwe, wamepata wapi ridhaa ya wananchi kuhusu hilo ikiwa dhamana walopewa ni kuandika katiba Mpya! Ni kutokana na ubishi wenu mmefikia hata kuhoji uhalali wa Muungano wenyewe kisha mnadai hamtaki kuuvunja...Hii akili kweli na nani alowatuma kwa kazi hiyo!
Mkuu Mkanadara kama unanisoma vema, mimi sizungumzii Ukawa leo nilishazungumzia kabla ya kuwepo kwakwe.Ukisema hakuna Ukawa hapa una maana gani? sio wewe ulo quote maandishi yangu na kusema nina wasuppoort CCM kwa S2? sasa iweje unaanza kukataa maneno yako mwenyewe na kuingiza hoja ambayo haihusiani. Matatizo yako na hao kina Mdondoaji takashi GHIBUU hayahusiani na mjadala wetu. Laukama ungejua mfumo wa S2 tusingekuwa hapa kwani yaonyesha wazi unatoka kapa na kwa bahati mbaya wewe mwenyewe una majibu yako hutaki kufundishwa ama kuambiwa nje ya majibu ulojitungia kichwani. Hivyo sitoweza kuendelea kuzungumzia kitu kile kile day in day out! - nimechoka.
Labda nikuulize wewe na hao UKAWA. Ni nani alowapa dhamana ya kuandika mkataba mpya wa Muungano wa JMT! Hizi serikali 3 zinahusiana vipi na Katiba mpya tuloiomba sisi wananchi hadi wakajikabidhi mamlaka ya kujadili na hata kuitaka hati ya Muungano maana yaonyesha hawaamini kuwepo kwa Muungano halali lakini wapo mbele kupokea posho za kuandika katiba ya JMT, Jamhuri wasioamini kuwa halali! Hii mijitu imesoma na kujifanya mianasiasa iloapa kuulinda Muungano usokuwa halali mioyoni mwao. Ujinga huu hata uwe na degree 10 hautasaidia kitu maana watu kama hawa wamefungwa macho na masikio yao japo wanaona na kusikia!
Ebu tuambie, kati ya hao wajumbe wa baraza maalum la Katiba ni kina nani wanawakilisha Upande wa Tanganyika au Zanzibar ktk swala hili la Muungano. Ni nani kati yao ana utaalam na uzoefu wa kuandika Katiba maana nijuavyo hakuna hata mmoja wao alowwahi kuandika haya sura mojawapo leo wapo mbele kudai muungano wa shirikisho!
Huyo Warioba na kundi lake nani kawapa dhamana ya kuuliza juu ya Muungano wetu! unapotaka kusuluhisha wana ndoa unaweza vipi kuanza na kuuliza cheti cha ndoa? na ili iweje? Ujinga huu mkuu wangu sitoukubali na sitouendekeza maana hao jamaa ulowataja ndio kila siku waliokuwa wakisema Muungano wetu sio halali, na sasa wewe umeungana nao japo zamani ulipingana nao. Huoni kama umevutwa walipotaka kukuweka na ukabakia uchi wa nyama...
Mkuu tusizungumze vitu pasipo kuweka nukuu za vifungu vya katiba hasa tunapotaka kuzungumzia maswala mazito kama haya. Kwanza, nakuomba unipe kifungu ndani ya katiba ya Zanzibar kinachosema rais wa Zanzibar ndiye Amiri Jeshi mkuu kisha tuendelee! Na nitakujibu yote kwa hatua usiongeze hadith mpya juu ya hili.Mkuu Mkanadara kama unanisoma vema, mimi sizungumzii Ukawa leo nilishazungumzia kabla ya kuwepo kwakwe.
Nazungumzia UKAWA kama ninavyozungumzia vyama vyote. Hilo naomba ulielewe.
Nimeweka uzi na kusema watarudia juisi ya maembe. Nikaonyesha jinsi walivyobofoa siku za mwanzo na huko wanakotarajia.
Nimesimama kutetea Tanganyika kabla ya Mbatia hajateuliwa. Ndiyo maana nasema mengi unayoyaona mbona tuliyashayazungumza.
Nikutoe wasi wasi, muungano unaousema ni halali si halali. Uhalali ni miaka 50 tu,kisheria kuna matatizo mengi.
Uhalali umeondolewa kabisa na katiba ya SMZ ya 2010 iliyomsimika Amir jeshi na nchi yetu kuwa na Maamir jeshi 2.
Ninaweza kuwa sielewei ,ni mapungufu ya mwanadamu.Tupe mfano, ni taifa gani lina Maamir Jeshi 2?
Huko Ontario, Premier wa Ontario anapigiwa mizinga 21 kama Prime minister wa Canada?
Je, kuna majeshi mangapi nchini Marekani, na nani Amir jeshi wa kila states.
Ukinitaji moja tu basi naunga mkono S2. Ukishindwa kutaja hapo kuna mambo 2.
Kwanza unathibitisha kuwa kilichopo ni kasha tupu, muungano ulishaoza
Pili, katika mfumo wa sasa wa S2, kuwa na maamir jeshi 2 wa majeshi tofauti ni hatari kuliko mfumo mwingine wowote
Mkuu nifahamishe kidogo, ni jinsi gani tunagawa shughuli za Tanzania ili kuwa na za znz na zile za Tanganyika ili kuvua koti.
Ukisema Tanganyika ishughulikiwe na Tanzania hapo si kuwa umevaa koti bali utakuwa na kikoi na mkwiji.
Mkuu, wewe na CCM kwa umoja wenu mnasema gharama za muungano zinaongezeka katika S3.
Kwavile sielewi ningependa kujifunza kutoka kwako, S2 gharama zake zina unafuu maeneno gani na kwa njia zipi.
Mkandara, hadidu za rejea za tume ya Warioba zimeeleza kuzungumzia suala la muungano.
Hazikusema muundo au serikali ngapi. Hazikusema gharama au kitu kingine. Zimesema kwa ujumla wake zungumzieni muungano.
Unamhukumu bure Warioba,kama angekuwa ni yeye wakati anawasiliana na Kikwete, JK angesimamisha mchakato.
Hakuna sehemu yoyote na mwanasheria yoyote aliyesimama kusema Tume imeenda kinyume na hadidu za rejea.
Si JK wala si CCM wenye akili timamu wanaosema .Tume imefanya kazi kisheria na hakuna pingamizi.
Ni tume iliyosheheni wanasheria, maprofesa, wanadiplomasia na watu kutoka katika jamii.
Weledi na uadilifu wa watu wa tume huwezi kuuweka katika mizani na wale wanaoandika rasimu ya CCM ya S2 chini ya Andrew Chenge, au washabiki kama Lusinde, Nape, Mwigulu n.k.
Katika bunge la Katiba, Zanzibar inawakilishwa na makundi matatu
1. Kutoka BLW
2. Kautoka Bunge la JMT
3. Kautoka Makundi ya Rais
Tanganyika haina mwakilishi hata mmoja., ahsante kuliona hilo.
Waliopo ni wajumbe wa Tanzania bara ambao unasema wanaserikali ya bara.
Waliopo ni wajumbe wa nchi ya Tanzania bara iliyopata uhuru mwaka 1977. Hakuna mjumbe wa Tanganyika.
Kwavile unaelewa hilo, basi unatuelewa tunaposema muungano wa sasa hauna haki wala usawa.
Hakuna Tanganyika au Mtanganyika anayewakilisha. Na bunge hilo halina Mtanganyika.
Kwavile umetambua hilo, pakuanzia si hapa tulipo. Ni kuanza kuzindua Tanganyika ili isimame na masilahi ya Tanganyika kama ilivyo znz. Halafu tuangalie mambo 7 kwasababu znz haitaki mambo yote kama kule Canada unakosema.
Kama hayo 7 hawataki, wasipigwe mabomu , njia ni nyeupee kabisa, waondoke zao kwa amani.
Kwa suala la cheti cha ndoa, Tanzania ambako mtu anaweza kuingia na kuishi tu bila nyaraka ni makosa kuulizia vitu kama hivyo. Huko Canada ulipo unaweza kuulizwa cheti cha ndoa hata miaka 90 iliyopita.
Cheti cha ndoa ni kutafuta ukweli hata kama ndoa hiyo ilishakuwepo. Swali la kwanza utakaloulizwa huko Canada ulipo au Marekani, uwe katika ofisi binafsi au ya umma ni ID yako na ikibidi proof of marriage kama una claim za aina hiyo. Haijalishi ni miaka mingapi mumeishi, kinachotakiwa ni proof ya marriage. Tanzania unaweza ku prove kwa maneno, huko kwingine ney!
Mkuu, nitakupa maelezo yakiambatana na vifungu.Mkuu tusizungumze vitu pasipo kuweka nukuu za vifungu vya katiba hasa tunapotaka kuzungumzia maswala mazito kama haya. Kwanza, nakuomba unipe kifungu ndani ya katiba ya Zanzibar kinachosema rais wa Zanzibar ndiye Amiri Jeshi mkuu kisha tuendelee!
Mkandara,Mkuu tusizungumze vitu pasipo kuweka nukuu za vifungu vya katiba hasa tunapotaka kuzungumzia maswala mazito kama haya. Kwanza, nakuomba unipe kifungu ndani ya katiba ya Zanzibar kinachosema rais wa Zanzibar ndiye Amiri Jeshi mkuu kisha tuendelee! Na nitakujibu yote kwa hatua usiongeze hadith mpya juu ya hili.
Mkuu wangu ata sijajichanganya hata kidogo isipokuwa nyie ndio mnajichanganya. Na kama kweli ulinisoma kwa makini utanieklewa vizuri sana nachosimamia.Mkandara,
Mimi nahisi suala la Katiba mpya, hasa muundo wa muungano limekuchanganya sana. Sio mkandara tuliyemjua, unajichanganya sana na wengi wetu tumeishia kukusoma tu badala ya kuchangia kwani ingawa unatumia uhuru wako wa mawazo, mawazo yako yanaleta mchanganyiko mkubwa sana kwani you are full of contradictions. Mfano hili la mgongano wa kikatiba baina ya ile ya JMT (1977) na ya znz (2010). Hivi kweli umezisoma katiba hizi kabla ya kumuuliza Nguruvi3 swali alete ushahidi kwamba zanzibar sasa ina amiri jeshi mkuu? Hata Jaji Warioba kajadili hili juzi ITV kwamba wanajeshi wamemwambia wamechoka kupigia mizinga "amiri jeshi wakuu wawili". Nini unataka kujua ukweli zaidi ya hapo?
Kwa mujibu wa katiba ya JMT (1977), ibara ya 33 (2):
Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa:
*Mkuu wa nchi.
*Kiongozi wa serikali.
*Amiri Jeshi Mkuu
Pia ibara ya 4(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ikisomwa pamoja na ibara ya 147(2) na vifungu vya 3,4 na 7 vya nyongeza ya kwanza inaipa serikali ya Muungano:
*Mamlaka ya ulinzi na usalama na uwezo wa kuanzisha MAJESHI katika jamhuri ya Muungano.
Ukisoma ibara ya 121 ya Katiba ya znz ambayo inampa rais wa znz mamlaka alizojadili Nguruvi3 hapo juu, hauoni mgongano uliopo kabisa?
Sent from my iPhone using JamiiForums
Kifungu hiki hakika maana yoyote zaidi ya kusema rais wa Zanzibar atakuiwa kiongozi wa nchi moja kati ya 2 zilizoungana na mamlaka yake hayana tofauti na Mamlaka ya Premier wa Ontario au Quebec nkija ktk kifungu cha Utakuta ya kwamba ylozungumziwa ni SHUGHULI na mamlaka ya rais wa Zanzibar jambo ambalo hata huku Canada kila Premierwa nchi zake ni msimamizi mkuu wa shughuli zote za nchi yake hivyo Wazanzibar wametaka kujitenganisha kujipa majukumu ya Kinchi kutokana na sisi kukataa kwamba wao sii NCHI. Mimi niliwaelewa lakini nyie mkawa mstari mmoja na CCM ktk hilo isipokuwa mnakuja geuka pale mnapoona Zanzibar inataka kutambuliwa kama nchi wakati Tanganyika hamuioni.26.(1) Kutakuwa na Rais wa Zanzibar ambaye atakuwa Mkuu
wa Nchi ya Zanzibar, Kiongozi Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
121.(1) Kutakuwa na ldara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar ambazo kazi zake na shughuli zake zitakuwa kama
zitavyoainishwa katika sheria zinazohusika
Mkuu wangu ata sijajichanganya hata kidogo isipokuwa nyie ndio mnajichanganya. Na kama kweli ulinisoma kwa makini utanieklewa vizuri sana nachosimamia.
Labda nianzie nyuma. Ni serikali ya Tanganyika kupitia Mh. Pinda walosema Zanzibar sio NCHI. Nyie mnakubaliana na hili wakati mimi sikubalinani nalo maana Zanzibar ni NCHI isipokuwa sii TAIFA. NI nchi kwa sababu ina serikali yake, ina bunge lake na ina mahakama zake hivyo kuundwa kwa katiba ya mwaka 2010 ilifuatia majibu ya Pinda kusema kwamba Zanzibar sio nchi. Isome katiba vizuri na pengine kifungu hiki tu kinatueleza kwamba Zanzibar wametumia fursa hiyo kujitambulisha kama wao ni nchi ndani ya Muungano wa kuunda JMT (TAIFA),
Sasa basi kifungu hiki kinachosema
Kifungu hiki hakika maana yoyote zaidi ya kusema rais wa Zanzibar atakuiwa kiongozi wa nchi moja kati ya 2 zilizoungana na mamlaka yake hayana tofauti na Mamlaka ya Premier wa Ontario au Quebec nkija ktk kifungu cha Utakuta ya kwamba ylozungumziwa ni SHUGHULI na mamlaka ya rais wa Zanzibar jambo ambalo hata huku Canada kila Premier ni nmkuu wa shughuli zote za nchi yake hivyo Wazanzibar wametaka kutenganisha na kujipa majukumu ya Kinchi kutokana na sisi kukataa kwamba wao sii NCHI. Mimi niliwaelewa lakini nyie mkawa msitari na CCM ktk hilo isipokuwa mnakuja geuka pale mnapoona Zanzibar inataka kutambuliwa kama nchi kama ilivyokuwa toka zamani.
Katiba ya mwaka 1977 iliwatambua kama nchi lakini baada ya mwaka 1984 mageuzi mengi yalianza kufanyika hadi kufikia 1993 Zanzibar ilipoteza hata rais wa Zanzibar kutambuliwa Bara tukatenganisha makamu wa rais na rais wa Zanzibar. Taratibu viongozi wa Zanzibar wakaanza kupoteza sauti ktk JMT isipokuwa kwa kupitia vyama vya siasa hilo wao hawakuilitaka. 2. Jeshi la JWTZ linagawanyika ktk sehemu 3. Tuna Jeshi la nchi Kavu, la Anga na la majini hivyo KMKM ni sehemu ya jeshi letu kama NAVY ya Marekani. Hivyo sioni tatizo kabisa kama NAVY wasipoiywa The Marines kwa Marekani ama KMKM kuiytwa hivyo wakati jeshi hilo lina Watanganyika, Jeshi la Anga lina Wazanzibar na na nchi kavu pia lina Wazanzibar. Tatizo lenu liko wapi haswa.
Mimi nimekwisha elewa wapi tunakosana kimawazo. 1. Hamkubali kama Zanzibar ni nchi wakati mimi nasema Zanzibaer ni nchi hivyo maswali yenu yote na hoja zenu zoote zinatazama upande wa Zanzibar kutokuwa nchi wakati huo huo mkichanganya NCHI na TAIFA kwa sababu tu hamuelewi nafasi ya Tanganyika.
Mabadiliko yoote ya vifungu vya Katiba ya Zanzibar kufutwa na kuandikwa upya imetokana na hizi fikra za kusema Zanzibar sio NCHI bali mnataka iwe sawa na MKOa wa Tanzania jambo ambalo wao hawalikubali na kama ndivyo basi bora tugawane umaskini.
Nitasema tena binafsi sioni tatizo kabisa kwa Zanzibar kuwa nchi kama ilivyokuwa toka zamani maana hata tukiunda serikali 3 kitakachotokea ni nyi kukubali Zanzibar ni NCHI baada tu ya Tanganyika kuwa nayokuitwa NCHI na sii kuwa ndani ya JMT. Lakini tujiulize kwa Zanzibar kujiita nchi kumewaongezea nini haswa tofauti, Ni MAMLKA YA UENDESHAJI SHUGHULI ZA SERIKALI YAO kama ilivyo ktk states za USA, Canada ama UK.
Haya msikie Nguruvi3 ana vyojichanganya na maswla ya ndoa asoyajua. Canada ukikaa na kimada miaka miwili tu huhesabika kama mke (in common) na ana mamlaka na madai yote ndani ya nyumba kama mkewa ndoa hawahitaji cheti cha ndoa kuhalalisha haki ya huyo mwanamke, leo Zanzibar tupo kwa miaka 50 bado mnasema hawana uhai wao bali ni sehemu ya mume Tanganyika! Acheni jamani kutupotosha..
INi kinyume na inavunja masharti ya artical kama tulivyovunja rais wa Zanzibar kutokuwa makamu wa rais (1984/93) na alivyovunja Mh. Pinda kudai Zanzibar sio nchi na wabara wote wanaunga mkono bungeni hoja ikapita!Mkandara,
Mimi sihoji haki ya zanzibar kujitambulisha kama nchi, hiyo ni haki yao, kama ilivyo haki ya Tanganyika kama mshirika mwingine wa muungano, haki ambayo imeminywa, huku wewe ukisomeka kuunga mkono kuminywa kwa Tanganyika.
Nilichowasilisha hapo juu ni very simple: je, hatua husika ya Znz 2010 haiendi kinyume na Katiba ya sasa ya JMT (1977)? Naomba ujibu ndio au hapana, halafu ndio tujadili upande wako wa hoja.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Pinda hajavunja katiba ya muungano Bali ametetea katiba hii ambayo haitambui znZ Kama nchi hata hivi tunavyozungumza. Vinginevyo pls educate me kauli ya Pinda inavunja vipi katiba ya muungano.Inavunja kama alivyovunja Mh. Pinda kuidai Zanzibar sio nchi na wabara wote wanakunga mkono bungeni!..
Soma kwa makini sehemu ya kwanza na pili ya katiba hiyo (kabla ya marekebisho) kisha ondoa mamlaka ya makamu wa rais kiasi kwamba hatakuwa tena rais wa Zanzibar na hatatambuliwa kama kiongozi wa Tanganyika ama JMT. Kina nani walokiuka katiba ya mwaka 1977?Pinda hajavunja katiba ya muungano Bali ametetea katiba hii ambayo haitambui znZ Kama nchi hata hivi tunavyozungumza. Vinginevyo pls educate me kauli ya Pinda inavunja vipi katiba ya muungano.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu kama unatafuata neno hutafuti maana hapo sikuelewi. Hata hivyo msikilize Warioba akiwa ITV, Mag3 aliweka video nzuri sana hapa. Hakuna kiongozi wa CCM au mwanasheria aliyepinga ukweli wa Warioba isipokuwa wale waliogoma kuelewa au walioamua kutokubali hata kama utwaambiaNguruvi3,
Mkuu katika yote uloandika sioni kifungu kinachosema rais wa Zanzibar ni Amir jeshi mkuu wa jeshi la Zanzibar au Tanzania..Nipe kifungu hicho ama futa maneno uloyaandika kisha tuiendelee. Maana unaniongezea kazi nyignine ya kujibu vitu ambavyo havihusiani na swali langu.
Mkandara anasema znz ni nchi si taifa. Katiba ya znz inasema znz ni nchi na ni taifa. Mkuu Mkandara achukue likizo, kuna kitu kinamchanganya! No siyo Mkandara ninayemjua.Pinda hajavunja katiba ya muungano Bali ametetea katiba hii ambayo haitambui znZ Kama nchi hata hivi tunavyozungumza. Vinginevyo pls educate me kauli ya Pinda inavunja vipi katiba ya muungano.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Hapa pia hueleweki, Rais wa znz kutokuwa makamu hujui utaratibu gani ulitumika.INi kinyume na inavunja masharti ya artical kama tulivyovunja rais wa Zanzibar kutokuwa makamu wa rais (1984/93) na alivyovunja Mh. Pinda kudai Zanzibar sio nchi na wabara wote wanaunga mkono bungeni hoja ikapita!
Mkuu Mkandara, utaratibu gani ulitumika kuondoa Rais wa znz kuwa makamu? Ukishatueleza utaratibu tutakubaliana nawe. Bila kutueleza utaratibu hatutakubaliana nawe.Soma kwa makini sehemu ya kwanza na pili ya katiba hiyo (kabla ya marekebisho) kisha ondoa mamlaka ya makamu wa rais kiasi kwamba hatakuwa tena rais wa Zanzibar na hatatambuliwa kama kiongozi wa Tanganyika ama JMT. Kina nani walokiuka katiba ya mwaka 1977?
Ukisha ondoa hilo tu tayari unaondoa Zanzibar kuwa sehemu ya Nchi Moja ya Tanzania na kuzigawa hivyo tulianza kugawanyika toka mwaka 1984 na mwaka 1993. Ukisha vuruga katiba ya mwaka 1977 kwa kuyaondoa madaraka ya rais wa Zanzibar ktk serikali ya JMT tayari unaiondoa kinyemela Zanzibar na kuipa mguu wa kuwa ni NCHI yenye serikali yake, bunge lake na mahakama, hivyo wana kila haki ya kudai mamlaka kamili kama nchi.
Mkuu wangu kwani Warioba nani? Kasomea law na katiba lakini hajui muundo wa serikali 3 laa sivyo asingeendelea kupendekeza Mambo yasiyokuwa ya Muungano kuendelea ktk katiba mpya. Asingeshauri kuwepo na wizara 7 tu za Muungano hivyo kuifanya serikali kuu kuwa dhaifu na mamlaka chini ya serikali za nchi. Hana alijualo zaidi ya mapendekezo toka makundi ya watu wasokuwa na Utaalam.Mkuu kama unatafuata neno hutafuti maana hapo sikuelewi. Hata hivyo msikilize Warioba akiwa ITV, Mag3 aliweka video nzuri sana hapa. Hakuna kiongozi wa CCM au mwanasheria aliyepinga ukweli wa Warioba isipokuwa wale waliogoma kuelewa au walioamua kutokubali hata kama utwaambia
Mfuatilie Mchambuzi anavyokuhabarisha kuhusu katiba ya 1977, mimi niliamua kucheza na hiyo ya znz unayotetea.
January 12 Sheni kapokea kiapo cha utii, je ni kama nani
Siku hiyo akiwa katika jukwaa maalumu, Kikwete alikuwa anapiga soga na akina Nape Jukwaa kuu
Mkuu una maana huelewi Rais wa znz anapigiwa 21 gun salute.
Hebu niambie premier mmoja tu wa Canada anayepokea gun salute hata 2. Nitajie kuanzia Nova scotia hadi BC.
April 26, wale askari walitoa kiapo kwa Sheni, walikuja Dar kutoa kiapo kwa Kikwete
Hivi mkuu umechanganyikiwa na nini? Si Mkandara tunayemjua.
Kwamba yote hayo huyaoni unachotaka ni neno Amir jeshi.
In fact kuna Amir jeshi wawili, wanajeshi wetu wanalijua hilo.
Nimekuonyesha vifungu na nina simama kusema kuna Amir jeshi wawili, nisichojua ni kuwa Amir jeshi yupi ni mkubwa na yupi ni mdogo.
Mkuu wangu kwani Warioba nani? Kasomea law na katiba lakini hajui muundo wa serikali 3 laa sivyo asingeendelea kupendekeza Mambo yasiyokuwa ya Muungano kuendelea ktk katiba mpya. Asingeshauri kuwepo na wizara 7 tu za Muungano hivyo kuifanya serikali kuu kuwa dhaifu na mamlaka chini ya serikali za nchi. Hana alijualo zaidi ya mapendekezo toka makundi ya watu wasokuwa na Utaalam.
Yeye na Tume yake hawakuichaguliwa kuandaa muundo wa Muungano, zipo tume zilizokwisha pita na ndizo pekee zilizokuwa na mamlaka ya kuujadili Muungano na wakashindwa kutokana na hali halisi. Sina la kujifunza toka kwa Mchambuzi kwa sababu anaitafsiri Katiba apendavyo kama watu wengine wanavyoitafsiri Biblia kiasi kwamba leo tuna madhehebu tofauti kwa biblia ile ile. Hii haiwafanyi hawa kuwa ndio wakweli ama wanaijui Biblia.
Katiba ya mwaa 1977 ipo wazi na ammendments zimefanyika pasipo kuzingatia mfuko wetu wa kisiasa na Kiuchumi. Na pendekezo lolote la kugawana umaskini kwa kuisingizia Katiba ya mwaka 1977 ambayo yeye Mchambuzi hataki ifanyiwe marekebisho ila katiba mpya iandikwe hawezi kunambia mimi niifuate wakati yeye haikubali ila huitumia tu pale anapoihitaji.
Katiba iko wazi na clear kabisa kwa mtu yeyote anayefahamu mamlaka ya nchi zilizoungana na kwamba katiba hiyo haijavunja sheria yoyote. na hakuna mahala popote ndani ya katiba ya Zanzibar inayosema rais wa Zanzibar (dr.Shein) ni Amir jeshi mkuu wa Zanzibar haya mnayaongeza nyie kama mlivyoaminishwa.
Na kama hujui basi nikwambie kwamba hili neno rais ndiye Amirmamlaka ya rais iwe nchi yoyote duniani na kama halipo basi rais huyo hana mamlaka hayo. Katiba lazima ijieleze wazi soma katiba ya nchi yoyote utayakuta maneno haya. Katiba yoyote ni lazima ieleze kwa uwazi mamlaka ya rais kama yeye ndiye Amir jeshi mkuu na maadam mnachukua vifungu vya katiba na kuvitafsiri mnavyopenda haiwezi kunifundisha chochote.
Ni katiba hiyo hiyo imeeleza kuulinda Muungano leo nyie mnaikataa na kusema Muungano unaweza kubadilishwa na kuwa wa shirikisho, kifungu gani ktk katiba ya mwaka 1077 kinawapa nafasi hiyo, leo mnaitumia kutaka kutuvuruga. Nimesema wazi kwamba kuna makosa yalofanyika mwaka 1984 na 1993 ambayo ndio chanzo cha mapungufu ya katiba iliyopo na hayo ndio yamezua kero zote hizi.
Tukiweza kuyarekebisha hakutakuwa na kero tena.Nyie mnalazimisha serikali 3 ambazo sioni sababu ya rais wa nchi, Amir jeshi mkuu kuendesha mambo 7 tu ktk Kinchi ambacho hakijai hata mkononi. Obama anaongoza states 50 ktk mambo yote ya Muungano wa nchi hizo huku shughuli za serikali zikiendeshwa na states zake na wamefanikiwa leo sisi na nchi mbili tu mnataka kuanzisha mgawanyiko kwa sababu hamjawahi kuona ama kuishi ndani ya nchi zenye mfumo mnaoupendekeza.
Sipendekezi muundo wowote wa serikali pasipo kuzingatia matakwa ya wananchi na hakuna kiongozi wala tume ilokuwa na dhamana ya kupendekeza muundo wa Muungano hivyo Warioba na tume yake wamekuwa kama watoto wadogo walotumwa sokoni kununua samaki wakatuletea na unga. Nani alomwambia tunataka kula Ugali?
Kwanza naomba idhini kutoka kwa Mchambuzi niwe wakili ili kumrudisha Mkandara katika hali yake' Mkandara the best'Mkuu wangu kwani Warioba nani?
Kasomea law na katiba lakini hajui muundo wa serikali 3 laa sivyo asingeendelea kupendekeza Mambo yasiyokuwa ya Muungano kuendelea ktk katiba mpya.. Hana alijualo zaidi ya mapendekezo toka makundi ya watu wasokuwa na Utaalam.
Yeye na Tume yake hawakuichaguliwa kuandaa muundo wa Muungano, zipo tume zilizokwisha pita na ndizo pekee zilizokuwa na mamlaka ya kuujadili Muungano na wakashindwa kutokana na hali halisi.
Sina la kujifunza toka kwa Mchambuzi
Katiba ya mwaa 1977 ipo wazi na ammendments zimefanyika.
Na pendekezo lolote la kugawana umaskini kwa kuisingizia Katiba ya mwaka 1977 ambayo yeye Mchambuzi hataki ifanyiwe marekebisho ila katiba mpya iandikwe hawezi kunambia mimi niifuate wakati yeye haikubali ila huitumia tu pale anapoihitaji.
Katiba yoyote ni lazima ieleze kwa uwazi mamlaka ya rais kama yeye ndiye Amir jeshi mkuu na maadam mnachukua vifungu vya katiba na kuvitafsiri mnavyopenda haiwezi kunifundisha chochote.
Ni katiba hiyo hiyo imeeleza kuulinda Muungano leo nyie mnaikataa na kusema Muungano unaweza kubadilishwa na kuwa wa shirikisho, kifungu gani ktk katiba ya mwaka 1077 kinawapa nafasi hiyo, leo mnaitumia kutaka kutuvuruga.
Nimesema wazi kwamba kuna makosa yalofanyika mwaka 1984 na 1993 ambayo ndio chanzo cha mapungufu ya katiba iliyopo na hayo ndio yamezua kero zote hizi.
Tukiweza kuyarekebisha hakutakuwa na kero tena.Nyie mnalazimisha serikali 3 ambazo sioni sababu ya rais wa nchi, Amir jeshi mkuu kuendesha mambo 7 tu ktk Kinchi ambacho hakijai hata mkononi.
Sipendekezi muundo wowote wa serikali pasipo kuzingatia matakwa ya wananchi na hakuna kiongozi wala tume ilokuwa na dhamana ya kupendekeza muundo wa Muungano hivyo Warioba na tume yake wamekuwa kama watoto wadogo walotumwa sokoni kununua samaki wakatuletea na unga. Nani alomwambia tunataka kula Ugali?