UKAWA wanavyobabaika: Historia ya 'juisi ya maembe' kujirudia?

UKAWA wanavyobabaika: Historia ya 'juisi ya maembe' kujirudia?

Mkuu Mkandara
Nimekuwekea video ili uache utaratibu wako wa kuwatisha Watanganyika ni wamoja ndani ya muungano, nje ya hapo wataanza Ukurya na Unyakyusa. Nimekuweke uone hali ya Zanzibar kama alivyosema Yahaya Kassimu. ''muungano ukivunjika na ninyi manrudi kwenu,pale mnapaita tu, Wallahi mtaondoka'' .
Je, huoni tatizo hapo? Ni akina nani wataondoka.

Pili, nimekuwekea usikilize wakikiri kuwa ndani ya muungano wanapata kila wanachodai.
Wewe unapata wapi ushujaa wa kusema wanaonewa ikiwa wao wenyewe wanasema hakuna uonevu.

Tatu, maelezo yako umekubaliana na Warioba. Usichokitaka ni jina Tanganyika.
Unaposema tumeweza kuendesha S2 bila matatizo unajidanganya.
Suala la muungano lina mtatizo na wewe ndiye muumini wa Tanganyika kuvaa koti.

Huwezi kuwa na JMT ndani yake Tanganyika ikafanya kazi. Haliwezekani,ndilo tatizo la miaka 50. Utatengaje shughuli za waziri au katibu mkuu katika kushughulikia Tanzania na Tanganyika.
Hesabu zinakataa, mantiki hairuhusu. Unagoma tu lakini unaelewa ukweli.

Muundo uliousema ndio waWarioba, kinachokutisha ni kuzinduka kwa Tanganyika. Unafahamu uwepo wa Tanganyika utaondoa loophole za kutumia herufi ZAN katika kuiba, kudoea. Hilo ndilo linakutesa, na umeshalisema hapa JF(Kumbu kumbu ipo). Unakumbuka kauli ya ''wazanzibar hawajui, wataumia sana Tanganyika ikirudi""

Kuhusu ulinzi na usalama, nimekuuliza makusudi ili kukuonyesha misaada na mikopo si muhimu kuliko wanachokipata. Hawana bajeti ya ulinzi na usalama ambayo kwa bilioni 400 ingechukua zaidi ya Bilioni 150. Ukiweka na wizara zingine wasiokuwa nazo, znz ingebaki bila bajeti ya kulipa mshahara wa sheha.
Leo yote hayaonekani kinachoonekana ni pesa kutoka Washington.

Nikupe mfano kwa hili, kuna mtu alikuwa anamuomba mwenyezi mungu amsaidie kupata kazi.
Amesali usiku kucha kwa miaka 2 bila kupata kazi.Kwa miaka 2 alikuwa na afya akitembea kutafuta kazi.

Baada ya miaka 2 akaacha kumuomba mungu kwasababu hajamsaidia katika maombi ya kupata kazi. Akasema hakuna haja ya kuendelea na swala au maombi yake.

Masikini ya mungu, kumbe huyu jamaa hakujua mungu alikuwa anasikiliza na kujibu swala na maombi yake. Kwa miaka 2 hakuugua hata siku moja. Kuna uwezekano angepata kazi na kuugua kipindi hicho na pesa zote za mshahara kuishia katika matibabu. Mungu alimsaidia kumwepusha na maradhi kwasababu maradhi ndilo tatizo lililomkabili, si kazi.

Mfano huo ni sawa na wazanzibar,wanaona kukopa washington ni fahari kama yule mtu aliyekuwa anatafuta kazi. Hawajui kuwa kutokuwa na bajati za ulinzi na usalama, mambo ya ndani, mambo ya nje, elimu na mzigo wa kubeba muungano ni mkubwa kuliko kupata pesa kutoka kwa Christine Lagard zenye riba. wapo mgongoni wakiendelea na safari na hawaoni, wanachotaka ni kutembea chini waonekane wanaweza.

Muda umefika, wapewe nafasi ya kukopa IMF na kupata misaada kutoka Uarabuni na Ulaya bila kikwazo. Wapewe mamlaka za kumiliki wizara zao, wapewe kila wanachokitaka.
Sisi tunaizindua Tanganyika, ni nafuu kuzuia pesa zetu kwenda znz kuliko kuwakataza kukopa.

Tanganyika ni muhimu kwa wakati huu kuliko wakati mwingine.
Hakuna wa kuizuia, wapo wa kuichelewesha. Tanganyika itazinduka katika meza ya majadiliano au kinyume chake wazanzibar watalipa gharama kubwa kuizindua.

Hakuna kurudi nyuma ni Tanganyika tu. Hilo litatokea iwe mwaka huu au kesho lakini lazima litokee na wznz waelewe hivyo.

Likitokea mezani ni nafuu kwao, wakisubiri tuwatake waizindue Tanganyika wataumia sana.
Labda tumetazama video tofauti maana kama ni ile uloiweka, Yahya Kassim anazungumzia kundi la Wazanzibar na wale wanaodai utengano, wasiotaka muungano huu kwa madai ya serikali 3. Ameileza hofu ya Wazanzibar na matakwa ya Wazaniabr ya kwamba wale wanaosema hakuna hofu sii wakweli na katoa mifano.....Sasa ikiwa wewe umeelewa tofauti, basi ipo kazi kubwa sii kwangu tu bali mijadala mingineyo yote utaitafsiri upendavyo.

Hata swala la Mkataba kwa maana ya ndani ni kuwepo na mamlaka kamili baina ya serikali hizi ili kila serikali iweze kupanga na kuchagua maendeleo yao. CUF kama chama hata kikishinda uchaguzi wa Znz, ndani ya mfumo huu hawawezi kupewa mamlaka hayo ya kidemokrasia ili wao waendeshe shughuli za serikali ya Zanzibar, hivyo kwa kushindwa kupata suluhu kwa miaka yote ndio maana wametaka kuchukua mamlaka hayo kupitia marekebisho ya katiba yao ambayo inawapa mamlaka kama nchi. (NB: Katiba iliyopo haitambui ukweli kwamba Zanzibar ni nchi!) na kwa kufanya marekebisho hayo inaiwezesha Zanzibar wawe na mamlaka ya shughuli za serikali yao kama ilivyo Tanganyika ina mamlaka hayokwa miaka 50 ya Muungano. Wazanzibar wengi wameelewa na kukubali kupokea marekebisho hayo kimsingi.

Sasa kuitaka Tanganyika ambayo hadi sasa hivi ina mamlaka kamili ya kuendesha shughuli zake haileti maana zaidi ya Ukorofi, ni swala potofu la walozoea vya kunyonga tunashindwa vilivyochinjwa kihalali! kwa sababu Zanzibar imehitaji mamlaka ambayo hawana kama republic ndani ya muungano na sio fair kwa nchi kutokuwa na mamlaka ktk demokrasia ya kweli. Hivyo basi ni muhimu kutazama undani wa kuwapa mamlaka haya kutaathiri vipi muungano na hakuna njia isipokuwa kuweka mambo yote ndani ya Muungano (wizara zote) ila mamlaka ya kuendesha shughuli za serikali ndio yapewe hizo serikali zilizopo hadi chini kabisa na sio kila kitu kiwe chini ya serikali ya CCM. Bado huelewi!

Nakuomba muulize mtu yeyote anayeishi ktk nchi zenye Muungano, swala sii serikali ngani maana zipo nyingi, huu ni muundo tu unaotazama ukubwa wa nchi, watu, rasilimali, uwezo wa nchi na kukata ktk matabaka mengi ili kurahisisha ufanishi wa shughuli za maendeleo. Je nini haswa sababu za mamlaka kamili ya ki republic kutolewa kwa nchi (sub soveregn countries)? - sidhani kama unaweza kunambia kwa unagaubaga maana inaonyesha huna unachojua juu ya hili. Sidhani kama unaelewa a republic ndani ya muungano inatakiwa kuwa na mamlaka gani na kwa shughuli gani na mambo ya Utawala huwa chini ya nani..

Tunaposema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT), ina maana a National REPUBLIC of Tanzania ambayo kama nilivyokwisha sema toka Malecela, Sumaye, Lowassa na leo Pinda ni mawaziri wakuu ambao kwa uhalisia wametumikia serikali kwa maslahi ya Tanganyika kwa muda wote wakiwa madarakani kutokana na kuendelea kutumia mfumo usiouwiana na mabadiliko ya Kisiasa na Kuchumi. Lakini tunaliona kosa tu pale Zanzibar wanapotaka nao kuwa na kiongozi wa shughuli za serikali yao ambaye ana mamlaka kamili kama kwetu.

halafu swala la mikopo kwani Tanganyika inapokopa nje hailipi riba? kwani haiwfanyi makosa hayo hayo unayoyafikiria kwa Zanzibar maana unachowacheka ni sawa na Nyani asoona makalio yake mwenyewe. Ikiwa mambo yote yatakuwa ya Muungano, serikali kuu italazimika kupitia bunge la JMT kupitisha mikopo yote na kwa uhakika kila mmoja wetu atahusika, hii ni katika kuondoa Usiri wa CCM ambao wanautumia kwa maslahi yao au ya chama. Umeona wapi chama tawala kina miradi ya biashara kama sii mfumo mbaya wa Utawala halafu wewe unatazama UZanzibar na Utanganyika! Damn vipofu kweli hawaambiwi tazama, hupewa fimbo wakapapasa ardhi!...
 
Mkandara;9904077]Labda tumetazama video tofauti maana kama ni ile uloiweka, Yahya Kassim anazungumzia kundi la Wazanzibar na wale wanaodai utengano, wasiotaka muungano huu kwa madai ya serikali 3. Ameileza hofu ya Wazanzibar na matakwa ya Wazaniabr ya kwamba wale wanaosema hakuna hofu sii wakweli na katoa mifano.....Sasa ikiwa wewe umeelewa tofauti, basi ipo kazi kubwa sii kwangu tu bali mijadala mingineyo yote utaitafsiri upendavyo.
Mkuu Mkandara
Sijui kwanini unakuwa huna uaminifu katika mjadala. Please! Kwanini unakuwa hivi mkuu?

Hivi watu wanaokujua wataamini ni yule Mkandara wa kila siku wanayemjua.
Hata kukiri ukweli unaona adha, kipi utakachosema ukaaminiwa tena.

Naweka video ili watu wasikilize, halafu naweka muda ili walio na haraka na wale wanaotaka 'point' muhimu wafuatialie

Video hii hapa anayetaka aidurusu kwa dakika na sekunde nilizoonyesha halafu asome bandiko la Mkandara kuwa maneno hayo hayapo au hayana maana ya ubaguzi.

https://www.jamiiforums.com/great-t...juisi-ya-maembe-kujirudia-10.html#post9904077

''1.13, mh makamu mwenyekiti, znz imepataikana kwa mapinduzi. Tanganyika imepatikana kwa kura lakini wale waliowaondoa hawapo na wanaweza kupanga bila woga

Tuje znz, sisi kweli tuna woga, hapo nyuma hata kigongoro cha mhogo kinag'olewa. Lakini pia tuna woga, siku ya kupiga kura tunaambiwa utawala wa mtu mweusi mwisho.
Lazima tuingie woga atawale nani. Dhidi ya sisi nani atawale.

2.35 Leo unakwenda uarabuni wanasema serikali tutaipa znz, wao nani?
2.47 Waarabu wanakuja na kusema ardhi hii ni ya baba yangu. Tusiogope kwanini? Tukaishi wapi sisi
6.44 Kiongozi wenu ana ajenda ya siri, ......na hili sisi hatutaki, litatuathiri wazanzibar. Siku akipata madaraka atapinda
9.02 Nawaambia wananchi wa znz wasidanganyike. Nakuambieni tuone wznz tulivyoendelea Tz bara.....
9.39 Na watu wanasubiri,siku mkivunja muungano na kule mtahama mtaelekea kwenu, hatutokubali walalh wallah mnaelekea kwenu pale mtaputa tu mnaelekea kwenu''

Hayo hapo juu ni maneno ya Yahya Kassimu mzanzibar

My take

Mkandara nimeleta video hii ili kukueleza kuwa usiwatishe Watanganyika. Nje ya muungano uliovunjwa na wznz, watabaki salama kwasababu sasa hivi wameduaa, wenzetu wanatuacha.

Pamoja na kilio cha wznz kama Yahya, gin inshatoka katika chupa. Hatukkubali kubeba mzigo wa matatizo yao.
Wapewe kila wanachotaka, sisi Tunataka Tanganyika na hilo hakuna wa kulizuia.
Kama hawatakubali kukaa mezani kwa mambo 7, wajiandae kulipa gharama kubwa sana kuizundua Tanganyika.
Gharama hiyo watailipa kwa jasho au kwa chozi lakini watalipa. Wana hiari.

Sisi tumeshakubali hiari ya kuwapa kila kilicho chao na wanachokitaka. Na wao wana wajibu wa kuzindua Tanganyika.
Wakishindwa kutimiza wajibu wao, tutawataka na si kuwaomba, waizindue Tanganyika kwa gharama zao'''

Hili la video nimefunga, kuendelea kujadiliana na wewe kuhusu jambo la wazi kama hili kutawachanganya wasomaji, nani honesty na nani dishonesty.
 
Last edited by a moderator:
Hata swala la Mkataba kwa maana ya ndani ni kuwepo na mamlaka kamili baina ya serikali hizi ili kila serikali iweze kupanga na kuchagua maendeleo yao.

CUF kama chama hata kikishinda uchaguzi wa Znz, ndani ya mfumo huu hawawezi kupewa mamlaka hayo ya kidemokrasia ili wao waendeshe shughuli za serikali ya Zanzibar, hivyo kwa kushindwa kupata suluhu kwa miaka yote ndio maana wametaka kuchukua mamlaka hayo kupitia marekebisho ya katiba yao ambayo inawapa mamlaka kama nchi.

(NB: Katiba iliyopo haitambui ukweli kwamba Zanzibar ni nchi!) na kwa kufanya marekebisho hayo inaiwezesha Zanzibar wawe na mamlaka ya shughuli za serikali yao kama ilivyo Tanganyika ina mamlaka hayokwa miaka 50 ya Muungano. Wazanzibar wengi wameelewa na kukubali kupokea marekebisho hayo kimsingi..
Huko nyuma umewalaani CUF kwa kutaka kuvunja muungano(rekodi ipo).

Hapa unawapongeza kwa katiba ya 2010 ambayo imevunja muungano.
Mkuu you're everywhere fumbling! You must have a position in debate. Totally inconsistent and rampant. Mkuu vipi?
Upo katika rekodi, ukisema katiba ya 2010 ni makosa naifanyiwe kazi si kubadili muundo.
Leo unarudi kusema wananchi wameelewa, yaani waznz wameelewa kuvunja katiba ya JMT!!!.
Hili ndilo linatupa nguvu zaidi kwasababu ukweli kuwa muungano haupo ni ushahidi wa maneno yako.

Pili, mabandiko mawili yaliyopita umesema Tanganyika haipo (rekodi ipo), halafu unasema kuwa kwa miaka 50 Tanganyika imekuwa inafanya mambo yake. Ni Tanganyika ipi iliyokuwa haipo na ghafla ikawepo?
Ndio maana nasema mantiki tu inakuzia katika mjadala usiendelee kutete unachokitetea.

Tatu, waziri mkuu unayesema ni wa JMT anashughulikia mambo yakiwemo ya ZNZ.
Waziri mkuu huyo wa JMT ambaye unataka ashughulikie mambo yote ya muungano hatambuliki Zanzibar.

Waziri mkuu ndiye mwenye wizara zote ikiwemo ya Ulinzi na usalama, mambo ya ndani, muungano n.k.
Leo unasema anashughulikia mambo ya Tanganyika.

Alaa! hivi umebadilika tena na kusahau kuwa ni wewe unayetaka mambo yote yawe chini ya JMT?
Inawezekanje kama PM ni wa JMT lakini anashughulikia mambo ya Tanganyika.
Logic inakupiga mweleka hata kabla ya kuanza kujadili. Ni logic tu.

Lakini pia hiyo Tanganyika unayosema 'ipo na haipo' haina mamlaka ya kushughulikia mambo yake.
Kwa mfano, SMZ haiajiri Mtanganyika hata kwa bahati mbaya.

Wapi serikali ya Tanganyika na sera zake za uajiri?
Huwezi kuchukua ajira za Watanganyika ukasema ni za muungano na zile za wznz zikawa za wznz!
Huu ndio ubaguzi tunaoelekea kuukomesha.

Angalia hesabu zinavyokupia chenga tena za subset
Tume ya Warioba imeundwa na wajumbe 30. Miongoni mwa hao 15 ni kutoka znz kama nchi.
15 ni kutoka JMT ambayo znz ipo. Wajumbe kutoka Tanganyika wapo wapi?
Hesabu hizi, ziangalie zina kung'onga mkuu. Ni hesabu na loigic ndogo sana, wapi unatatizika mkuu?

Angalia hesabu hii
ZNZ inapata mikopo asilimia 88 ikidhaminiwa na Tanzania ambayo znz imo.
Maana yake ni kuwa znz hiyo hiyo inarudi upande wa pili kujidhamini.

Katika asilimia 88 tueleze ni kiasi gani kinaingia katika muungano?
Na kwanini mkopo wa Tanzania ambayo unasema ni Tanganyika, itumike katika muungano?

Ni hesabu hizo hizo mbovu zimezaa kitu kinaitwa ajira asilimia 21
Swali, wamefikia asilimia 21 kwa kigezo gani? Mchango wa taifa, watu, ardhi au kitu gani tusichokijua.

Lakini kwa hili napenda nikuonyesha mantiki inavyokataa, achilia mbali hesabu.
Waliokuja kutoka Znz ni Makamu wa pili wa Rais wa znz na wajumbe wake kutoka znz kwaajili ya masilihi ya znz.

Upande wa pili ni JMT ambayo aliyekuwepo ni Waziri mkuu wa Tanzania na si Tanganyika, Makamu wa pili wa rais wa JMT Tanzania. Waziri ofisi ya muungano ambaye ni mznz. Waziri wa fedha ambaye ni mznzibar.

Hoja si uzanzibar, hoja ni kuwa kuna uwakilishi wa nchi ya ZNZ.
Upande wa Pili kuna uwakilishi wa JMT ambayo wznz wapo kama nilivyoonyesha.

Matokeo yake ni kuwa suala la ajira lenye ubaguzi kule znz limefanywa la muungano kwa kutumia jina la JMT.
Waliokaa kugawana asilimia 21 ni wazanzibar waliovaa koti la JMT wakasidiana na wenzao wanaowakilisha znz kupata asilimia 21 za Tanganyika.

Watanganyika hawana habari bali kusikia tu kuwa JMT imeamua asilimia 21 ziwe za ZNZ.
Hakuna Mtanganyika aliyeshiriki.
Kama yupo nitajie mmoja tu aliyeingia kwa masilahi ya Tanganyika kama wale waliokuja na makamu wa Rais wa znz.

Katika hali hii huwezi kuwa na JMT na Znz tukawa salama.
Mbegu za chuki na hisia walizopanda wznz zimejenga Utanganyika kwa nguvu.

Sasa Watanganyika wanaelewa kuliko ilivyokuwa huko nyuma.
Hizo asilimia 21 itafika siku Watanganyika wamechoka, na wznz watatimuliwa kwa nguvu!
Huu ni ukweli msiotaka kuusikia lakini kama unapenda ukweli, huo hauna shaka.

Huwezi kwenda kwenye nchi ya mtu ambayo hutambui katiba yake, ukajichotea mapesa kwa jina la muungano, ukatumia fursa kwa jina la JMT halafu wenye nchi wakakaa kimya daima. You can fool some people.........................

Mkandara haya tuyasema siyo taboo, itasaidia kupeusha balaa. Hata kama hatutasema yatatokea.
Hakuna kipindi cha muungano ambacho Watanganyika wamejitambua kama leo.

Hii ni disaster in the making, tuna wajibu wa kuepusha balaa.
Miaka 50 tuliambiwa muungano imara, kwasababu ya taboo hatukuruhusiwa kusema.
Leo tunajua muungano ulivunjwa na znz mwaka 2010. Kwanini tusiseme kinachokuja mbele ambacho ni dhahiri shahiri

Kama kusema Tanganyika imevaa koti la muungano ni haki na halali, tunaogopa nini kuwaambia wazanzibar kuwa Tanganyika wanataka kuvua koti na hivyo wajiandae kuchukua vipande vya koti?
 
Nguruvi3,
Huko nyuma umewalaani CUF kwa kutaka kuvunja muungano(rekodi ipo).

Hapa unawapongeza kwa katiba ya 2010 ambayo imevunja muungano.
Mkuu you're everywhere fumbling! You must have a position in debate. Totally inconsistent and rampant. Mkuu vipi?
Upo katika rekodi, ukisema katiba ya 2010 ni makosa naifanyiwe kazi si kubadili muundo.
Leo unarudi kusema wananchi wameelewa, yaani waznz wameelewa kuvunja katiba ya JMT!!!.
Hili ndilo linatupa nguvu zaidi kwasababu ukweli kuwa muungano haupo ni ushahidi wa maneno yako.
Mkuu wangu unaposoma maandishi ya nmtu jaribu sana kumuelewa ana maana gani.. Kwa mfano naposema Chadema kutoka bungeni ilikuwa kosa haifanyi mimi nipinge pia sababu walizotumia kuondoka bungeni. Na wala nikikubaliana na sababu za Chadema kupinga matokeo ya Uchaguzi haihalalishi pia mimi kukubaliana nao ktk actions watakazo chukua, hivyo ndio kusema napopinga Katiba mpya ya Zanzibar ya mwaka 2010 ni kutokana na Utapeli ulotumiwa baina ya CCM na CUF wala sii CUF peke yao. Na kumbuka katiba hiyo ni ya Zanzibar sii ya CUF na chama tawala CCM, hivyo kila kitu kimetengenezwa kwa mariudhiano lakini ni ushindi mkubwa kisiasa kwa CCM na utawala wake dhidi ya Upinzani visiwani.

Pili, Ikiwa wewe utachukua sheria mkononi na kumuua mtu alo m rape mwanao, basi mimi sintokubaliana na hatua yako ya kuchukua sheria mkononi na pia sintokubaliana na kosa kubwa alolifanya yule Mhalifu, hivyo sina upande naoutetea hapo!. Haiwezekani kwa kila nachopinga basi lazima niwe napongeza hatua ilotumiwa au upande wa pili, wala makosa mawili hayawezi kuleta Usawa wala haki. Ila tu mimi nitaelewa uchungu ulokuwa nao na sababu zilzizokusukuma wewe ukafikia maamuzi hayo na nikayaeleza na kulaani kitendo cha ku rape iwe kwa mwanao au mtoto yeyote na ndivyo navyoitazama Zanzibar ni kama vile tume i rape kwa miaka 30 ya mageuzi. Hivyo mimi kuelewa machungu yao hai halalishi ama kuniweka mimi kuwa nakubaliana na hatua walizochukuwa japo ni haki yao kupewa haki na sheria wanazodai.

Rudi nyuma ukasome vizuri maandishi yangu nimesema wazi toka wakati CCM na CUF wakifanya makubaliano niliyapinga na kusema ni makosa makubwa kwa vyama viwili kufanya makubaliano ili kuibadilisha katiba ya Zanzibar pasipo kuvishirikisha vyama vingine. Hii inaonyesha jinsi gani CCM wanavyo control mustakabali wa nchi hii.

Halafu kila mara unapenda sana kuwasema Zanzibar kama wao ni maskini ebu nipe data za ukweli toka banki kuu maana nijuavyo mimi mwaka huu kwa robo ya kwanza kufikia March wao wame export nje zaidi ya Usd 78mil. na population yao ni kama mil 1.3 tu wakati sisi bara tume export Usd 870 mil tukiwa na population ya mil.49, sasa wewe gawa mil 78 kwa watu mil.1.3 na Ile ya mil 870 kwa watu mil 49 uone nani anafanya vizuri. Na kisha jiulize kwa nini mapato haya yanarecordiwa na benki kuu iliyoko Bara na sio Zanzibar, halafu nambie hizo fedha za mauzo kwa nini ziko banki kuu Dar na sio Unguja, Zanzibar kama unavyodai tunawalipia madeni.

Na kuhusu Tanganyika, wewe unaposema inailipia Zanzibar madeni ni Tanganyka gani hiyo ikiwa haipo? Na kama unasema Tanganyika ipo kwa nini leo unaitaka Tanganyika ambayo ipo na hao UKawa wenzako maana hatuelewani kabisa japo mimi nakuelewa na natumia njia hizo hizo kuandika hoja zangu!
 
Halafu kila mara unapenda sana kuwasema Zanzibar kama wao ni maskini ebu nipe data za ukweli toka banki kuu maana nijuavyo mimi mwaka huu kwa robo ya kwanza kufikia March wao wame export nje zaidi ya Usd 78mil. na population yao ni kama mil 1.3 tu wakati sisi bara tume export Usd 870 mil tukiwa na population ya mil.49, sasa wewe gawa mil 78 kwa watu mil.1.3 na Ile ya mil 870 kwa watu mil 49 uone nani anafanya vizuri. Na kisha jiulize kwa nini mapato haya yanarecordiwa na benki kuu iliyoko Bara na sio Zanzibar, halafu nambie hizo fedha za mauzo kwa nini ziko banki kuu Dar na sio Unguja, Zanzibar kama unavyodai tunawalipia madeni.

Na kuhusu Tanganyika, wewe unaposema inailipia Zanzibar madeni ni Tanganyka gani hiyo ikiwa haipo? Na kama unasema Tanganyika ipo kwa nini leo unaitaka Tanganyika ambayo ipo na hao UKawa wenzako maana hatuelewani kabisa japo mimi nakuelewa na natumia njia hizo hizo kuandika hoja zangu!
Kama wata maintain kiwango hicho cha bilioni 80 kila robo, mwisho wa mwaka watakuwa na bilioni 320(assumption) ambayo ni sawa na bilioni 576 Tsh.(1:1600 exchange)

Bajeti yao ni Tsh Bilioni 710 mwaka huu, kwa maana kuna upungufu wa 134 Bilioni kwa assumption tu.
Hizo bilioni 134 zinapatikana wapi? Bilioni 134 ni sawa na kota moja na nusu ya mwaka. Watapata kota nyingine katika mwaka ulio na kota 4

Ukumbuke idadi ya 1.3million people, hawana bajeti ya ulinzi na usalama na ulinzi, mambo ya ndani, ya nje na gharama za taasisi za kimataifa. Bado hujaondoa gharama za serikali yao.

Ukiangalia haraka haraka, ni kweli unachosema, ukiangalia kwa utulivu, mantiki na hesabu hapa umeharakaisha. Huwezi kuwa na data moja uka draw conclusion. Hata mstari hauchorwi kwa point moja.

Kuhusu pesa zao kuwa Benki kuu, nadhani fedha na benki kuu ni mambo ya muungano.
Sio Mkandara unayesema mambo yote ni ya muungano, leo unapotaka bank kuu ya znz unataka kutueleza nini,.
Bank kuu ya Tanganyika ipo wapi?Unaona unacyojichanganya kila asubuhi.

Ukitaka wawe na bank kuu znz, basi iwepo ya Tanganyika. Ni wendawazimu wawe na bank kuu yao halafu yetu iwe ya pamoja. Kwasasa tunaelekea kukomesha ukupe huo. Na tutaukomesha tu, suala la muda.

Pili, kipi cha ajabu pesa zao kukaa bank kuu? Si wanapata 4.5 ya pato la taifa kutoka bank kuu.
Hiyo 4.5 wangekuwa wanaipata kwao, robo ya kwanza wangekuwa na 4.5% ya Bilioni 80 kama ingekuwepo.

Kwa vile wanapata pato la taifa, hapo wanatumia JMT kuchukua zile 4.5% ya bilioni 800 ulizosema za kota ya kwanza Tanganyika. Unaona jinsi wanavyopata mteremko! Unaona jinsi hesabu zinavyokusuta haraka sana.

Kuna tatizo gani wakiweka pesa bank kuu ya Tanzania?
Huo ni mradi ili wakirudi wanchukua bilioni zao 80 na bilioni za mishahara na bajeti.
Hivyo wanaweka 1 wanachukua 9.Na pia, kuna ajabu gani ikiwa 88% ya deni lao lipo bank kuu ya Tanzania.

Washauri waweke madeni yao znz, nasi tutawasadia wapate bank kuu yao.
Mkandara ZNZ ni masikini tu huwezi kulinganisha na Tanganyika.
Wangekuwa wanafaidika na pato unalosema wasingehamia Tanganyika.

Tanganyika ndio nchi pekee duniani iliyobeba mzigo wa wznz kukliko taifa jingine. Huko kwao hakukaliki FYI.
Umasikini usiuangalie kwa pesa, jiulize miaka 20 ijayo kisiwa kitaongeza?
Halafu jiulize miaka 20 poPulation yao itapungua?

Hakuna namna unaweza kulinganisha znz na Tanganyika, wamebebwa tu hakuna lolote wanalotusaidia. Tumeshawambia njia nyeupeee, wanasubiri nini.

Hili la Tanganyika si wewe uliyesema ipo miaka 50 ikiwa na madaraka kamili. Leo unauliza ipo wapi.
Mkuu utetezi unakupeleka mbio, tulia tu maana siku si nyingi zitamwagwa data hapa.
 
Kama wata maintain kiwango hicho cha bilioni 80 kila robo, mwisho wa mwaka watakuwa na bilioni 320(assumption) ambayo ni sawa na bilioni 576 Tsh.(1:1600 exchange)

Bajeti yao ni Tsh Bilioni 710 mwaka huu, kwa maana kuna upungufu wa 134 Bilioni kwa assumption tu.
Hizo bilioni 134 zinapatikana wapi? Bilioni 134 ni sawa na kota moja na nusu ya mwaka. Watapata kota nyingine katika mwaka ulio na kota 4

Ukumbuke idadi ya 1.3million people, hawana bajeti ya ulinzi na usalama na ulinzi, mambo ya ndani, ya nje na gharama za taasisi za kimataifa. Bado hujaondoa gharama za serikali yao.

Ukiangalia haraka haraka, ni kweli unachosema, ukiangalia kwa utulivu, mantiki na hesabu hapa umeharakaisha. Huwezi kuwa na data moja uka draw conclusion. Hata mstari hauchorwi kwa point moja.

Kuhusu pesa zao kuwa Benki kuu, nadhani fedha na benki kuu ni mambo ya muungano.
Sio Mkandara unayesema mambo yote ni ya muungano, leo unapotaka bank kuu ya znz unataka kutueleza nini,.
Bank kuu ya Tanganyika ipo wapi?Unaona unacyojichanganya kila asubuhi.

Ukitaka wawe na bank kuu znz, basi iwepo ya Tanganyika. Ni wendawazimu wawe na bank kuu yao halafu yetu iwe ya pamoja. Kwasasa tunaelekea kukomesha ukupe huo. Na tutaukomesha tu, suala la muda.

Pili, kipi cha ajabu pesa zao kukaa bank kuu? Si wanapata 4.5 ya pato la taifa kutoka bank kuu.
Hiyo 4.5 wangekuwa wanaipata kwao, robo ya kwanza wangekuwa na 4.5% ya Bilioni 80 kama ingekuwepo.

Kwa vile wanapata pato la taifa, hapo wanatumia JMT kuchukua zile 4.5% ya bilioni 800 ulizosema za kota ya kwanza Tanganyika. Unaona jinsi wanavyopata mteremko! Unaona jinsi hesabu zinavyokusuta haraka sana.

Kuna tatizo gani wakiweka pesa bank kuu ya Tanzania?
Huo ni mradi ili wakirudi wanchukua bilioni zao 80 na bilioni za mishahara na bajeti.
Hivyo wanaweka 1 wanachukua 9.Na pia, kuna ajabu gani ikiwa 88% ya deni lao lipo bank kuu ya Tanzania.

Washauri waweke madeni yao znz, nasi tutawasadia wapate bank kuu yao.
Mkandara ZNZ ni masikini tu huwezi kulinganisha na Tanganyika.
Wangekuwa wanafaidika na pato unalosema wasingehamia Tanganyika.

Tanganyika ndio nchi pekee duniani iliyobeba mzigo wa wznz kukliko taifa jingine. Huko kwao hakukaliki FYI.
Umasikini usiuangalie kwa pesa, jiulize miaka 20 ijayo kisiwa kitaongeza?
Halafu jiulize miaka 20 poPulation yao itapungua?

Hakuna namna unaweza kulinganisha znz na Tanganyika, wamebebwa tu hakuna lolote wanalotusaidia. Tumeshawambia njia nyeupeee, wanasubiri nini.

Hili la Tanganyika si wewe uliyesema ipo miaka 50 ikiwa na madaraka kamili. Leo unauliza ipo wapi.
Mkuu utetezi unakupeleka mbio, tulia tu maana siku si nyingi zitamwagwa data hapa.
Mkuu usinione naendelea kulumbana na wewe kwa sababu nyingine zaidi ya kwamba wewe ni mwandishi mzuri na unaweza kufikisha Ujumbe wangu kwa Watanzania wengine kupitia mada hizi, lakini unayoandika sasa hivi ni madudu matupu maana unashindwa kuelewa hata Jumla ya Pato la nchi au Taifa linatokana na nin. Sasa mimi nimesema kuhusu Export zao, tayari wewe umeunganisha export tu na bajeti, Je umepiga hesabu za mapato ya ndani na kadhalika. Je hiyo Bajeti ya JMT a.ak.a Tanganyika ni kiasi gani nayo ukailinganisha kwa akili hiyo hiyo ya Export? huku zitakuwa ngapi maana huku ndio aibu tupu hata kuzizungumzia!..

Mkuu nakuomba sana tuache malumbano ya kujibishana ili mradi tunabishana, wakati unashindwa kuelewa undani wa hoja zangu na hutaki kupata suluhu bali Utanganyika. Nakuomba tena hubiri kuweka MAMBO YOTA YAWE YA MUUNGANO ili kuliokoa Taifa hili ktk Upuuzi huu wa Kuitaka Tanganyika ili tusiweze kuandika katiba mpya ktk wakati unaotakiwa. Hizi mbinu za wanasiasa wetu iwe wa CCM, CUF au CDM zisikuzibe akili usiweze kuona mbele ya mategemeo ya wananchi wote ktk kuipata katiba mpya.

Na hakuna hii kitu Katiba ya Wananchi (UKAWA) inayodai serikali 3 ambazo ni ongezeko la ajira kwa viongozi wenyewe, ongezeko la matumizi ya kodi za wananchi ktk matumizi ya ndani bila kuhakikisha Ufanisi, Uwazi na Uwajibikaji. Hawa wanajipanga kisiasa zaidi kuhakikisha wao wanaweza kuunda coalition yao against CCM leo lakini kesho ktk Uchaguzi wakaanza vita ya wao kwa wao.. Hizi Politics zenu hazina maana kabisa kwa sababu nawaelewa watu hawa wanavyofikiria na wanavyoweka maslahi yao mbele ya wananchi.

Nadhani nitakomea hapa maana nimeshindwa miye! walonisoma na kunielewa wanaweza kuendelea..
 
Mkuu usinione naendelea kulumbana na wewe kwa sababu nyingine zaidi ya kwamba wewe ni mwandishi mzuri na unaweza kufikisha Ujumbe wangu kwa Watanzania wengine kupitia mada hizi, lakini unayoandika sasa hivi ni madudu matupu maana unashindwa kuelewa hata Jumla ya Pato la nchi au Taifa linatokana na nin. Sasa mimi nimesema kuhusu Export zao, tayari wewe umeunganisha export tu na bajeti, Je umepiga hesabu za mapato ya ndani na kadhalika. Je hiyo Bajeti ya JMT a.ak.a Tanganyika ni kiasi gani nayo ukailinganisha kwa akili hiyo hiyo ya Export? huku zitakuwa ngapi maana huku ndio aibu tupu hata kuzizungumzia!..

Mkuu nakuomba sana tuache malumbano ya kujibishana ili mradi tunabishana, wakati unashindwa kuelewa undani wa hoja zangu na hutaki kupata suluhu bali Utanganyika. Nakuomba tena hubiri kuweka MAMBO YOTA YAWE YA MUUNGANO ili kuliokoa Taifa hili ktk Upuuzi huu wa Kuitaka Tanganyika ili tusiweze kuandika katiba mpya ktk wakati unaotakiwa. Hizi mbinu za wanasiasa wetu iwe wa CCM, CUF au CDM zisikuzibe akili usiweze kuona mbele ya mategemeo ya wananchi wote ktk kuipata katiba mpya.

Na hakuna hii kitu Katiba ya Wananchi (UKAWA) inayodai serikali 3 ambazo ni ongezeko la ajira kwa viongozi wenyewe, ongezeko la matumizi ya kodi za wananchi ktk matumizi ya ndani bila kuhakikisha Ufanisi, Uwazi na Uwajibikaji. Hawa wanajipanga kisiasa zaidi kuhakikisha wao wanaweza kuunda coalition yao against CCM leo lakini kesho ktk Uchaguzi wakaanza vita ya wao kwa wao.. Hizi Politics zenu hazina maana kabisa kwa sababu nawaelewa watu hawa wanavyofikiria na wanavyoweka maslahi yao mbele ya wananchi.

Nadhani nitakomea hapa maana nimeshindwa miye! walonisoma na kunielewa wanaweza kuendelea..
Hapo ulipoishia umeachanganya watu sana na wengi hawajakuelewa. Huwezi kuwa na flip flpo kila bandiko wakakuelewa.

Ninachoandika ni ''madudu'' kwasababu hutaki kusikia Tanganyika. Nafurahi kwasababu kwa fikra kama zako tunaweza kuwaonyesha watu wapi tatizo lilipo. Mfano, watu wanaelewa kuwa S2 haziwekani, si kwa model yenu ninyi CCM . Mantiki na hesabu zimekataa, na sasa wengi wanaona ukweli waliokuwa hawaujui.

Tunaweza kuwaonyesha Watanganyika wizi wanaofanyiwa na ka nchi kwasababu ya uzanzibar wanaopaswa lakini Utanganyika ni marufuku.Tumeona jinsi hoja zisivyojibika isipokuwa tu kutuaminisha znz ni sehemu muhimu sana. Tumeonyesha umuhimu wa znz katika kuchota na si kutia.

Tumeona propganda za kuwatisha Watanganyika ambazo tumezijibu na wewe ukiwa mpiga propaganda mkubwa kama alivyo Shivji, Nape na Mwigulu. Hatutapumzika kundi dogo la wasomi likitumia kalamu kuwaadhibu raia wetu wasio na hatia kwa fear of unknown. T
unaaminishwa na Mkandara, Pinda na Nape kuwa Tanganyika haikuwepo imetokea mwaka 1961.

Tunaaminishwa ni haki ZNZ wakavunja katiba kwasababu ni wazanzibar!
Eti ni haki walale na kulipwa mishahara kwasababu ni waznz

Mkandara, huwezi kuwa na JMT na ZN ukawa na haki hata siku moja. Haki haitakuwepo pale ambapo mznz atakuwa mznz, akitaka kuja kuchota anakuwa Mtanzania. Kinachochotwa ni mali ya Mtanganyika iliyobatizwa jina la Tanganyika. Na ili itumike vizuri husillimishwa kwa jina la JMT.

Mwaka 2010 niliandika JF kuwaonya wznz kuwa wanachokitaka si dhahabu ni magugu.
Leo Watanganyika wametambua uhuni na kila uchafu unaofanywa na watu 1.3 nusu yao wakihemea dhiki Tanganyika.

Tanganyika kuzinduka si suala la mjadala , ni suala la kuwaambia wznz wakae mezani.
Wakikataa tutawapeleka mezani kwa nguvu ili waizindue Tanganyika.

Hatuhitaji bora katiba, tunahitaji katiba bora. Hata kama ni 2018 ilimradi tunapata kitu kilicho na thamani that's OK. Kwetu wengine UKAWA ni juzi, tumeanza kuitetea Tanganyika miongo mingi
Tutaendelea kuitetea kwa kutumia njia zote, mwisho wa siku itazinduka.Itazinduka mezani au itazinduka mitaani lakini itazinduka.

Wazanzibar waelewe gharama zinazowasuburi majadiliano yakishindikana.
Hilo si siri tena waelezwe kwasababu huwezi kuzuia watu wanaosema wazi '''Njia nyeupee'

Katika historia hakuna siku kiongozi amesimama na kwaambi wznz jambo zito.
Siku hizi hata muda wa kusema nao hakuna, njia ni nyeupee!

Na wala hawana uthubutu wa kutisha tena.Hakuna anayewazuia, wakaitaka hata leo waende zao, who cares!

Njia nyeupeeee, tuone kama mtu wa Ukerewe au Muheza ataathirika na kuondoka kwa mznz.
Tunashindwa kufanya mambo ya maana tunajadili namna ya kuishi na watu laki 5.
 
ZANZIBAR WAKATAA KUPITISHA (RATIFY) MSWADA WA FEDHA

Soma kipande hiki :
Raza awapaka mawaziri wa SMT | Zanzibar Yetu

Bunge la JMT lina idiadi ya wabunge wa znz wapatao 81. Uwakilishi wao kwa uwiano ni mdoho kuliko ule wa wenzao wa Tanganyika. Mfano, mbunge wa jimbo la znz anawalilisha hadi watu 10,,000 na mbunge wa Tanganyyika nawakilisha watu milioni 1.5 sawa na idadi ya wznz wote dunaini. Hili lilifianyika ili kuwapa uwezi wa wingi wa kuajadili.
SMZ haina gharama za wabunge hao huo ni mzigo wa Tanganyika.

Bunge la JMT linatakiwa kuridhia sheria ya kuanzisha sarafu moja ya EA. Tulitarajia bunge la JMT likisharidhia basi Tanzania imeridhia. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mawaziri wawili walikwenda znz kueleza kuhusu jambo hilo.
BLW limekataa kwasababu eti wzn hawakushirikishwa.

Hapa sijui walioko Dodoma ni watu wa nchi ipi na hao wanaotakiwa kuridhia ni wa nchi gani.
Kinachoudhi sana ni kuwa Bunge la JMT limekuwa na mamlaka madogo kuliko BLW.
Kwamba lazima BLW liridhie jambo linalohusu Tanzania tukifahamu kuwa znz haina jingine zaidi ya jina.

Tunapofika hapo tunajiuliza kuna sababu gani za kuhudumia wabunge 81 kwa gharama ya bilioni 10 kwa mwaka na bilioni 50 kwa miaka 5? Pesa hizi ni nyingi kuliko pesa zinatolewa kwa mikoa ya Tanganyika ambayo ni mikubwa kuliko znz.

Mfano, mkoa wa Dar kwa mwaka wa fedha umepokea bilioni 10 ambazo ni sawa na gharama za wabunge 81 wanaowakilisha znz. Hivi kuna sababu gani za watu 81 wamegewe pande kubwa kuliko watu milioni 5 wa jiji la Dar.

Kiasi cha wabunge 81 ni sawa na 1/8 ya mapato ya znz. Hawa hawawakilishi masilhi yoyote ya Tanzania bali znz. Sasa kama imefika mahali SMZ haiamini kuwa wanaweza kushiriki mijadala Dodoma, eti hadi mswadaupate ruhusua yao kwanza.Kuna sababu gani za kulipa watu 81 ambao hawaamini hata na nchi yao?

Suala la fedha ni la muungano, sasa sijui inakuwaje wznz wanataka walijadili wao kwanza na kwamba lazim

Ukiangalia yote hayo, kiburi cha znz kinatokana na ukweli kuwa wamelelewa katika hali hiyo kwa miaka 50.
Mchango wa wznz ni herufi za jina, zaidi hapo mchango mwiingine ni kuchukua na kuchota. Wapi wanapata kiburi cha kutaka kujadili mambo ya fedha kama wao na si muungano.

Watanganyika, mumeona jinsi naibu waziri Adam Malima alivyodhalilika. Ndivyo watakavyodhalilika wengi siku za baadaye midhali watu wataendelea kuwachekea hawa wznz. Mbona njia ni nyeupee! manaogopa nini kuwaambua wakae kwa adabu au waende zao. Mimi nadhani umefika wakati wa kuwaambia ukweli hawa wenzetu.

Hakuna nayetaka kuvunja muunganio huko znz, lakini pia wengi hawana adabu. Tanganyika haitategemei znz kwa lolote kwa chochote, kinyume chake ustawi wa znz unategemea znz. Hilo ndilo linasababisha mambo kama S3 na mikataba.
Wznz wanafahamu wazi kuwa nje ya muungano ni maumivu kwao. Watanununuliwa wao na kisiwa chao chote.

Lazima tusimame na kuwaambia inatosha, kama wanatuhitaji basi watangulize adabu, waache kiburi kwasababu sisi hatuna sababu za kuwahitaji na wala hatuna cha kuhofia hata wakiondoka wote leo hii. Kiuchumi kisiasa na kiutamaduni Tanganyika hailingani na znz hata kwa 1/10th.
 
SERIKALI YAZIDI KUBABAIKA KUHUSU UKAWA, PINDA HAELEWEKI ANAZUNGUMZIA NINI

Takibani mwezi mzima Spika Samwel Sitta ana harakati za kutafuta muafaka na upande wa pili(UKAWA).
Pamoja na Sitta wapo viongozi na kila mbinu zinatumika ikiwa ni pamoja na kuwagawa, kuwatisha na kuwarubuni UKAWA

Nguvu kubwa imeelekezwa Chadema kwa ushawishi Tanganyika,CUF wakiwa na ushawishi visiwani.
Kumekuwepo na mbinu nyingi, inatosha kusema UKAWA wanaandamwa na taasisi zote unazojua wewe msomaji

Jambo la kushangaza ni viongozi wa CCM kusema hakuna muafaka na wala UKAWA hawahitajiki.
Uzezeta huu wa kufikiri ni zao la uongozi hafifu wa Kikwete.
Tunajua katiba mpya haitawezeakana bila ukawa kuwemo, hesabu haziruhus.Mpango wa kubadili sheria kuondoa 2/3 umekwama

Ni wajibu wa Rais Kikwete kusimama kama leader na stateman kuhakikisha taifa linarudi katika mstari.
Ni kitendo cha udhaifu kwa rais kupokwa madaraka ya kikatiba ya nchi na kundi la wahuni wachache ndani ya CCM.
Wahuni hao ndio wale wale tunaosikia katika Escrow ambako nako pia wamempiga kufuli mkuu wa nchi.

WAZEE WASEMA:
SALIM AZUNGUMZA KWA HISIA NA DIPLOMASIA KALI
WARIOBA AMUONYA KIKWETE KIUTU UZIMA


Katika mahojiano na vyombo mbali mbali vya habari, waziri mkuu na katibu mkuu wa OAU Dr Salim ameongea kwa hisia kali kuhusu masuala ya nchi. Si kawaida ya Dr Salim, inavyoonekana imebidi aseme.
1. Kwanza amekanusha kugombea urais akisema kuna jambo la ziada linatakiwa na huko nyuma hakujua.
2. Akaeleza alivyotumikia taifa kwa miaka mingi na uadilifu na kusikitishwa kuitwa Msaliti
3. Kaongelea kuhusu tume kumpa Rais taarifa za kila mara

Salim ni mwanadiplomasi, anapoongea unatakiwa kumsikiliza kwa umakini.
Kuhusu suala la Urais alichokisema ni kuwa sifa si muhimu ni lazima uwe na pesa.
Kwenye mahojiano hayo ya Nairobi kama laivyokaririwa na gazeti la the citizen alizungumzia kukithiri rushwa.
Ukimsoma , Salim alihusisha mambo mawili,uchaguzi na rushwa na kwa namna fulani kumlaani kuachia hali kuendelea.

Kuhusu kutumikia taifa, Salim alieleza kuanzia alipokuwa balozi hadi katibu mkuu.
Alichotaka kukieleza ni utumishi wake wa kutukuka kwa viongozi kama Nyerere na Manguli wengine wa Afrika.
Ujumbe ulikuwa ni rahisi, kuwa yeye hawezi kuisaliti nchi yake kwasababu kuna mengi ameifanyia.

Suala la tume ya Warioba, Salim ameiongeleaakionyesha wapi tatizo lilipoanzia.
Kwanza, alipochaguliwa kuwa mjumbe aliongea na Mwenyekiti na katibu mkuu wa CCM kuwa hataweza kuhudhuria vikao vya chama kwasababu ya kutumikia tume.

Hii maana yake ni kuwa, Salim alijitoa kwa ajili ya nchi na kuweka nchi mbele ya chama.
Kwamba, masilahi yake hakutaka yaingiliwe na wanasiasa uchwara na wengine wakiwa watoto wadogo sana kama Nape.
Salim anaendelea kusema kila hatua waliofikia, walimweleza rais Kikwete na hivyo alijua kila jambo.

Ukisoma kwa majumuisho, Dr Salim anachosema ni hivi:
Yeye ni mtu mwadilifu kiutendaji na kudhihirisha kwa kumwambuia Kikwete kwa ushahidi.

Anasisitiza yeye si sehemu ya kundi la rushwa la Serikali ya Kikwete na hivyo kumwita msaliti kama wanavyofanya akina Nape, Masauni, Nahodha na wengine ni kumkosea heshima.
Anabainisha kuwa msaliti ni Rais Kikwete aliyejua kila kilichoendelea lakini akawageuka dakika za mwisho.

Warioba
Naye amefanya kikao baada ya bunge kwa mujibu wa gazeti la mwananchi.
Akihojiwa ofisini kwake anasema alialika wajumbe wa tume na wasomi mashuhuri wakiwemo wazee wawili, Kingunge na ProfShariff.

Ujumbe aliousema Warioba ni kuwa lazima mchakato uendelee kwasababu wananchi wanadai.
Akamwambia kuwa kuna uwezekano wa vurugu. Hapa anamuonya kuhusu kubeba lawama zinazoelekea.

Warioba akapigilia msumari kwa kusema 'Mapungufu ya S3 yasemwe lakini isiwe sababu ya kuficha udhaifu wa S2''
Anachosema Warioba ni kusisitiza msimamo wa tume yake. Tena ameendelea kusema, haiwezekani kutozungumzia kuvunjwa kwa katiba na migongano iliyopo ya S2. Ni hatari kufumbia macho jambo hilo.

Warioba anamuonya Kikwete kuwa S2 haziwezekani, ni utaratibu ulioshindwa na umeleta migongano tofauti na wasemavyo vijana wa Kikwete.

Ukisoma maoni ya wazee wengi, wanajitahidi kumheshimu rais kwa kumweleza kiutu uzima.
Tatizo linakuja kuwa Rais hawezi kwenda kinyume na matakwa ya mafisadi na kundi la wahuni linaloendesha nchi kwa remote.

Busara za akina Salim na Warioba zinaonekana hovyo. Inasikitisha Mkandara wakishindwa kuona tatizo la kikatiba na mgongano
Hawaoni hatari ya uzanzibar uliopamba moto na counter attackinayowakabili hivi karibuni kwa garama kubwa.

Huwezi kuwa na S2 zilizoshindwa miaka 50 ukasema zimefanikiwa, huwezi kufeli kwa kufanikiwa
Warioba na Salim waliokuwa ngazi za juu wameliona hilo, inakuwaje mtu kama Mkandara asiwezkulewa?

Unapokuwa nawatu wenye mawazo kama akina Mkandara, wanaoishi kwa matumaini tu na wanaowasikiliza akina Nape na Mwigulu ni jambo la hatari sana. S2 zimeshindwa miaka 50, akitokea mtu na kudai zimefanikiwa mtu huyo ni hatari kuliko S2
 
MBINU ZA KUWAGHILIBU UKAWA ZINAPIKWA
WAZANZIBAR WANAHIDIWA MBINGU NA MWEZI

Kwa hisani ya gazeti la Raia mwema
Raia Mwema - Warioba kama Sitta

Mikutano ya CCM imeshindwa kujibu hoja, vitisho vimeshindwa, serikali imeanza mbinu za kuwalaghai UKAWA na WAZANZIBAR

Katika kikao cha tume ya Warioba kilichofanyika white sand kwa mujibu wa Raia mwema, Jaji Warioba alieleza undani wa majadiliano ya wasomi na watu wenye ushawishi wapatao 20.

Warioba alitumia nafasi hiyo kueleza mambo mawili makubwa
1. Kwamba, kinachojadiliwa katika S3 ni mapungufu na wala si marekebisho, akimaanisha hoja ya S3 ina nguvu, ili kupunguza nguvu kinachojadiliwa ni mapungufu na wala uzuri wa S2. Warioba anasema hivyo akionyesha kuwa S2 hazina utetezi wala hoja.

Hili tumelijadili sana hapa jamvini,tukitaka waumini wa S2 watueleze uzuri wake,utekelezaji, tukizingatia ongezeko la migogoro . Hakuna anayeweza kutushawishi bali kutukana na kuwananga wapinzani. Udhaifu huo unaonyesha jinsi S2 zilivyoshindwa kutetewa, Warioba kusema wazi, kinachoonyeshwa ni mapungufu, si mazuri au marekbeisho ya S3.

2. Hoja nyingine ni ile ya kumtaka rais Kikwete na Shein wanusuru mjadala.
Warioba kasema rais ana wajibu kunusuru hali iliyopo,akioongea kidiplomasia zaidi.
Alichomaanisha ni kuwa wajumbe waliokutana wanakubalia S3 ni jibu la matatizo yaliyopo.
Kikwazo kilichopo ni jinsi gani ya kurudi katika hoja.

Kikwazo kiliwekwa na rais Kikwete alipofungua bunge na kuweka msimamo na chama chake wa S2.
Warioba kasema, Rais anawajibika akimpa Rais wajibu huo kwa maana kuwa yeye ni sehemu ya tatizo lililojitokeza, na hakuna namna nyingine ila ni kufanya liwezekanalo kunusuru mchakato.

SITTA AWARUBUNI WAZANZIBAR
Waziri na Spika wa BMLK amesema katiba ina mambo mengi ya kuzungumza na wala siyo muundo au idadi ya serikali.
Anachokifanya Samwel Sitta ni kile tulichokieleza kuwa mzee huyu kapoteza thamani ya kuaminiwa na jamii katika uzi mwingine.

https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/index2.html

Sitta anafahamu idadi ya serikali si hoja, kwa makusudi anajaribu kuelekeza mjadala eneo hilo.
Hoja ni muundo wa muungano. Kuna uwezekano tukakubaliana kuwa na serikali 1, S2,au S3 kama yatakuwepo majibu muafaka ya matatizo yanayoendelea kujitokeza.
Hivyo hoja ni muundo si idadi ya serikali kama anavyopotosha Sitta.

Sitta ameendelea kusema yapo mengi ya maana ndani ya katiba na si muundo wa muungano.
Kama ni hivyo, iweje chama chake kiweke msimamo mkali, Spika Sitta akitumiwa kuharibu taratibu, kupindisha kanuni na sheria?
Hapa anajaribu kudanganya umma kuwa suala la muundo wa muungano ni dogo.

Hata kama tutakubaliana na hilo, yale mazito bado CCM haiyakubali.
Tumesikia msimamo wa mwenyekiti wa CCM kuhusu ukomo wa wabunge na tume ya maadili ya viongozi ambao CCM wamepinga kuanzia huko nyuma.

Samwel Sitta akasema, kuna suala zito kama nafasi na mamlaka ya znz katika muungano.
Na pia kile alichokiita 50-50.Hapa anajaribu kuwaambia wazanzibar kuwa kuna pipi za mamlaka kamili na uwezekano wa kugawana mambo 50-50Anachokitaka ni kuvunja nguvu ya UKAWA kwa upande wa Zanzibar kwa kuwapa peremende na pipi.

Ukweli ni kuwa 50-50 haiwezekani. Watanganyika wameamka kuliko wakati mwingine.
In fact leo wengi hawataki kusikia muungano. Baada ya kubaini madudu na ukupe wa Zanzibar haitawezekana kukawa na kitu 50-50.

Hivi unawezaje kuwa na 50-50 na znz?
Kwa kutumia kigezo gani, idadi, ukubwa au hadhi ya nchi. Kama ni 50-50 je wazanizbar wana uwezo wa kuingia gharama za 50-50?

Watanganyika hawakubali kitu hicho kwasababu 50-50 ni kuwaumiza tu.
Leo tunajua ndani ya muungano Mtanganyika hafaidi chochote zaidi ya kuwa mtoaji tu.
Utawezaje kushawishi 50-50 kirahisi namna hiyo.

Kwa znz kuna uwezekano wa kukubali pipi na peremende.
Wao hawaangalii kile wanachosimamia, huangali jambo linalovuma.
Kwa Tanganyika 50-50 haikubaliki na hapo ndipo utakuwa mwanzo na mwisho wa muungano.

Kwa miaka 50 Watanganyika wamebeba muungano na znz mgongoni.
Leo Samwel Sitta ana ubavu gani wa kutushawishi kuhusu 50-50.
Ni kwa lipi na tija ipi kwa Mtanganyika atakayoipata kwa 50-50 ya Sitta.

CCM wanaweza kufanya mbinu hizo, lakini gharama kubwa inawasubiri.
Kwanza, kwa mwamko wa Watanganyika, nafasi za wabunge wengi zipo matatani.

Suala kubwa kuelekea 2015 ni muungano na hawatakuwa na majibu watakapokuwa mbele ya mahakama ya wananchi.
Uwezekano wa kuwa na bunge la wapinzani kama watajipanga ni mkubwa zaidi.

Pili, wananchi wa kawaida watachukua hatua zao kila upande ukilinda masilahi yake.
Hatudhani Watanganyika wapo tayari kupeleka muswada znz ukaamuliwe na wazanzibar.
Na wala hawapo tayari kuona katiba ya nchi inasiginwa na wazanzibar kama walivyofanya kwa kutumia katiba yao ya 2010.

Na tatu, Sitta atakwendaje znz kuwashawishi kubadili katiba yao ili kuondoa manung'uniko yaliyopo sasa?
Katiba ya znz ili ibadilishwe inahitaji kura za maoni.
Kwa hulka ya wazanzibar, wakiwa Dodoma ni CCM wakishapanda meli misimamo yao inabadilika kila uchao.

Mfano,Mohamed Raza alipokuwa Dodoma alitaka S2. Huyu ni muumini wa znz huru miaka mingi toka enzi za komando.
Juzi amerudi BLW na kuwasha moto kupinga hoja za S2 kuhusu mswada wa ratification ya fedha.
Alichosema Raza ni kuwa znz ni nchi na hivyo haikubali taarifa za ku-ratify bali ishiriki.
Sasa itawezekanaje ikiwa znz inataka S2?

UKAWA lazima wawe macho. Mbinu zinatumika kuwaondoa katika hoja yao ya msingi.
Hoja si idadi au aina ya muundo wa muungano.

Hoja ya ukawa ni kuwa kinachojadiliwa ni maoni ya wananchi kupitia tume ya Warioba.
Kama kunahitajika maboresho, ni lazima yawe katika framework ya tume ya Warioba.

UKAWA wakikubali kurudi kwa ghiliba nyingine yoyote watakuwa wamepoteza meli na mzigo.
Hawataeleweka wakaiweka msimamo tena.

Ni lazima watambue kuwa Rais Kikweta na kundi lake la CCM la akina Nape, Chenge, Mwigulu n.k. wana rasimu yao.
Anayeisimamia ni kikweta na hivyo wakikubali kila kitu kibubusa busa watakuwa wameidhinisha katiba ya CCM ya maficho.

Kwanini hoja ziwe kwa UKAWA na si kuwataka CCM warudi kati na kati?

Tusemezane.
 
BOMANI NAYE ALONGA
ASEMA SUALA LA MUUNGANO LIACHWE KWANZA

Mwanasheria mkuu mstaafu wa serikali Jaji Bomani, amesema ni wakati mambo mengine yajadiliwe na suala la muungano liwekwe pembeni kama alivyokaririwa na vyombo vya habari.

Huu ni mwendelezo wa kauli za wazee ili kunusuru mchakato ambao sasa ni dhahiri UKAWA wana upper hand. Tofauti na inavyoonyeshwa na wanasiasa muflisi kama Nape, Ukawa ni sehmu muhimu sana na haiwezi kubezwa kwa mtu anayetumia akili.

WAZEE HAWAKULIONA HILI?

Kikwete alipoanzisha mchakato, wengine tulisema kuna tatizo tukionyesha wazi kuwa suala la muungano litachukua sehemu kubwa sana ya mjadala.

Tulishauri kwanini kusiwe na kura ya maoni kwanza hasa kwa znz ili tujue kama tupo ndani ya meli moja au wenzetu wanashuka, badala ya kuruka kama katiba ya 2010 inavyoonyesha.

Tulihoji Rais kuanzisha mchakato na si mkutano wa kitaifa.
Mkutano wa kitaifa ungetoa dira ya taifa na kisha katiba kuandikwa kwa kufuata dira hiyo.
Haya yote yamefanyika na kuelezwa bila wazee kutia neno.

Leo akina Bomani, Sitta, Warioba n.k. wanakuja kulalamika kukwama kwa mchakato.
Tena wanafanya hivyo wakiogopa kusema ni Kikwete aliyetaka mawazo yake na CCM yawe katiba.

Kwamba, tatizo ni Kikwete kwenda kuhutubia bunge na kuweka msimamo wake dhidi ya msimamo wa watu milioni 43

Wazee wanakwepa ukweli huo na kuwaona UKAWA ni tatizo.
Tatizo si UKAWA, tatizo ni Rais Kikwete aliyeingilia mchakato,kuuvuruga kwasababu tu alitaka kupandikiza mawazo yake.Wazee wasione aibu kusema nchi inaelekea katika vurugu na chanzo ni Rais Kikwete.

Mzee Bomani anaposema watu wajadili mambo mengine waache suala la muungano, nalo pia ni jambo linaloonyesha uzee si lazima uwe hekima, kuna nyakati unaambatana na matatizo.

Bomani hakumbuki tena kuwa muundo wa serikali ndio unasimamia mambo mengine.
Utajadilije haki za akina mama, 50-50 ya Sitta au madudu mengine kama huna structure ya serikali

Matatizo ya znz ndiyo yamefikisha nchi hapa. Uhuni wao wa kudharau katiba na kubadili bila majadiliano ni sehemu tatizo. Kuomba na kutaka kusiko na ukomo kwa wznz sasa ni kero .

Leo unawezaje kujadili tume ya utumishi ambayo haifanyika kazi znz?
Tunawezaje kujadili maadili ya viongozi ikiwa znz wana maadili yao?
Unawezaje kujadili ulinzi wa nchi walkati tuna Amir jeshi mkuu na Amir jeshi mdogo wa Zanzibar

Tunawezaje kuzungumzia kutengeneza ajira ikiwa suala hilo halina nafasi SMZ?
Tunawezaje kumpa waziri mkuu madaraka na nguvu zaidi ikiwa hajulikani huko Zanzibar?

Ni kutokana na kufanya kazi kimazoe zoea kama akina mzee Bomani tena kwa kulipua lipua leo structure ya muungano inachekesha kweli kweli.

Makamu wa Rais wa SMZ hajulikani huku bara ni kituko gani.
Hakuna mahali katika katiba ya JMT imeandikwa uwepo wa makamu wa Rais.
Hatujui Pinda na makamu wa rais wa SMZ nani mkubwa.

Mazoe zoea tu ya kazi kama akina Bomani, ndiyo yametoa nafasi sasa hivi wazaznibar hawakusanyi kodi, hawafanyi kazi na wanaajiriwa bwelele kwasababu Tanganyika inayoitwa Tanzania inawalipia kuanzia umeme, maji hadi mafao ya uzeeni.

Akina Bomani hawakuona hayo, wanataka kutushawishi tuachie kizazi chetu matatizo yaliyopo.

Miaka 50 Tanganyika imeshindwa kupanga mipango ikielemewa na mzigo wa nchi ya Zanzibar. Hakuna namna hilo linaweza kuahirishwa. Kama alivyosema Bomani, vurugu zinaweza kutokea ingawa tuna maono tofauti a namna zitakavyotokea.

Yeye anaamini bora liende ili kuepusha mtafaraku, sisi wengine tunasema, hapa lazima kuwe na muafaka.

Muafaka ni ule wa wengi ambao ni S3 na si watu 600 waliokwenda Dodoma.

Kauli za Bomani ni jitihada za kuwalaghai UKAWA warudi bungeni ili kujadili rasimu ya CCM.

Huwezi kuacha kujadili muundo wa serikali, ukasema umeleta muafaka.
Huko ni kutoa free way kwa CCM, jambo lisilokubalika tena.

Akina Bomani wamwmbie Kikwete hapa tulipo nchi ipo njia panda.

Hii si Tanzania ya mabomu ya machozi. Hayo yamepita sasa ni Tanganyika ya wananchi na wazalendo. Mabomu ni moshi tu unaofuka, Tanganyika ni kitu kinachotakiwa kiwepo.
 
UKAWA: NGUVU HII YA GHAFLA MNATAKIWA KUIANGALIA
BOMANI NA MTUNGI WAMETOKEA WAPI LEO HII?

Jana na leo tumesikia matamko kutoka kwa Jaji Mtungi na mwanasheria wa zamani Mark Boman.

Boman anasema UKAWA warejee bungeni na kujadili mambo mengine ya katiba na wala si muundo.
Kwa maneno mengine anahalalisha uharamia wa CCM bila masharti, akiwaweka UKAWA kama watovu wa nidhamu na tatizo la katiba

Jaji mitungi anasema ni mlezi na katika majadiliano, na uongozi wa UKAWA wamefikia 'mufaka' na hivyo wananchi wawaunge mkono.

Yote yametokea katika muda mfupi sana wa siku mbili kukiwa na taarifa za kikao cha tume ya Warioba iliyokaa kurjea sintofahamu ya bunge la katiba. Hakuna shaka hawa wawili wanalo lao jambo.

Boman na Mtungi wanachokieleza ni kuwa kukwama kwa katiba kunatokana na UKAWA.

Yapo maswali mengi ya kuwauliza wazee hawa.

1. Tulipowaambia suala la muungano linahitaji kutengwa na katiba, na ni muhimu litangulie ili kutofunika mambo mengi, ina maana hawakutuelewa au hawakujua? Na kama hawakuju,a wapi wamejifunza kwa muda wa siku mbili na kuona tatizo.

2. Wakati CCM inapitisha miswada kwa akidi ya wabunge 100 mbona Mitungi na Boman hawakukemea hali hiyo?

3. Wakati Rais anapokea rasimu zote,mitungi akiwemo kwanini hakuona tatizo? na kama aliliona wapi aliposemea?

4. Wakati zinatolewa rasimu ya I na II na rais kuridhia iende bungeni, ina maana wazee hawa hawakujua tatizo lililo mbeleni?

5. Wakati CCM inakaa na kutoa matamko ya S2 ina maana Mtungi na Boman hawakuwa na fahamu au akili timamu za kubaini kuwa hoja iliyopo mbele yetu si ya chama ni ya taifa?

6. Mtungi alipoingiza sintofahamu ya kuwachagulia Chadema nani agombee na nani hafai, huo ndio ulezi wa vyama?
Na je si kuwa alikuwa anatumika kuvuruga Chadema kama sehemu ya kuvuruga UKAWA?

7. Wakati Rais anakataa S3 bungeni na kusisitiza S2 hadi atakapoondoka, wazee hawa hawakuona hatari mbeleni?

8. Wapi katika sheria za msajili wa vyama, Mtungi amepewa dhamana ya kusuluhisha migogoro ya katiba ya nchi?

9. Boman aliokwenda Zanzibar na kusema maoni ya wananchi yasikilizwe, alimaanisha maoni yapi, ya tume au ya JK

10. Kuingia kwao katika timbwili hili, je si kutumiwa na serikali kuwapaka matope UKAWA ili hali wanajua mchakato ulivurugwa na hotuba ya Rais iliyowalenga Warioba na wazee wenzake?

UKAWA WAWE MACHO, JUISI YA IKULU SASA INAHAMAIA KWINGINE

Juzi UKAWA walikwenda ofisini kwa msajili. Baada ya mazungumzo si mwenyekiti wake Mbowe au msemaji walioeleza kilichojadiliwa. Makosa haya waliyafanya wakati wa nyuma walipokwenda na kupewa majagi ya juisi za maembe.
Leo wanawezaje kukana kauli ya Mtungi kuwa kuna muafaka na wananchi waunge mkono.

Ni kwa mintaarafu hiyo, UKAWA wanawajibu wa kufafanua ni muafaka gani walioufikia.
Kinyume chake, historia ya juisi ya maembe inajirudia taratibu.

Ni vema ukawa wakajiuliza, je wao ndio tatizo au lipo tatizo na wao wanatafuta haki na suluhu ya tatizo.
Kitendo cha kukaa kimya bila kueleza kwanini wanakubali kutuhumiwa kuvuruga mchakato ikiwa ni kinyume
cha nia na dhamira zao ni cha kushangaza.

Umma unaaminishwa taratibu wao ndio tatizo na wala si kutofuatwa utaratibu wa maoni ya wananchi.
Uongo huo unapojirudia sana hatima yake ni kugeuka kuwa ukweli.

UKAWA ni lazima wajitokeze waeleze nini hasa kinachowashibu.
Kwa baadhi ya wananchi wasio na uelewa ni rahisi sana kuvutika kwa hoja za kina Boman na mtungi kuliko ukweli uliopo mezani.

Endapo wanataka muafaka, duru ingeshauri waweke wazi masharti yao ambayo ni pamoja na

1. Serikali kufuta kauli ya 'S3 zitakuja baada ya JK kuondoka'
Serikali lazima iseme wazi kuwa kinachoandikwa ni katiba kutokana na maoni ya wananchi

2. Kama hakuna muafaka, wasukume ajenda ya kura ya maoni kwa Zanzibar kwanza ili hatima ya muungano ijulikane.
Wazanzibar waulizwe kama wanataka muungano au hapana.

3. Waendelee kusisitiza kuwa maoni ya tume hata kama yalikusanywa na watu 1500 bado ni muhimu kuliko ya wajumbe 600 ambao wengine hawana uwakilishi bali majina yao na sifa zao za siri kwa aliyewateua.

Bila kuzingatia maoni haya, UKAWA inazidi kujiweka katika nafasi ngumu sana.
Haiwezekani kurudi kujadili katiba nusu, na wala haiwezekani kurudi kama hakuna muafaka wa nini kijadiliwe na kwa misingi ipi.

Hawa akina Jaji Boman na Mtungi wanatumika sasa baada ya kubaini kuwa bila UKAWA hakuna katiba mpya.

Ni ima UKAWA wakubali katiba bora au wafakamie juisi na kupata bora katiba.
Kwa hali ilivyo, hatuna shaka UKAWA wameanza kubabaika kama kichwa kinavyosema hapo juu.

Katika hai ya kubabaika, wasaliti na wanafiki watajitokeza na huenda UKAWA ikabaki katika makabrasha.

Tusemezane.
 
UKAWA WANABABAIKA, SASA WANAOMBA KUITWA KWENYE JUISI YA MAEMBE
KAULI YA DR SLAA KUHUSU KIKWETE KUKOMBOA MCHAKATO, NI MAKOSA


Dr Slaa amekaririwa na gazeti la mwananchi akisema, anayeweza kukokoa katiba mpya ni Rais kikwete.
Kauli hii ya kiongozi wa UKAWA nje inatia wasi wasi na mashaka kama kweli kuna umakini wa UKAWA.

Wakati viongozi wa UKAWA walipokutana na msajili wa vyama Jaji Mutungi, msimamo wao kwa mujibu wa vyombo vya habari ni kutorudi hadi maoni ya wanchi yaheshimiwe.

Dr Slaama ameyarudia hayo katika taarifa yake. Tatizo lililojitokeza ni pale alipomuomba Rais Kikwete aokoe mchakato kwasababu ndiye pekee kiongozi wa juu mwenye uwezo huo.

Dr Slaa amesahau kuwa aliyeunda tume ni JK. Serikali iliyopeleka mswada bungeni na kupitishwa na wabunge 100 kati ya 320 ni ya Kikwete. Aliyepokea rasimu zote mbili ni Kikwete.
Aliyeunda bunge la katiba ni Kikwete. Aliyekwenda kuwatukana wazee akina Warioba ni Kikwete.

Katika kuwananga wazee wa watu, Kikwete alisema S3 zitalifanya jeshi lihukue nchi. Kitisho hicho kakitoa Kikwete.

Na kauli muhimu ambayo Dr Slaa hakuisikia ni ya Kikwete aliyosema '' Msimamo ni S2, hizo zingine zisubiri hadi niondoke mwakani''

Hii maana yake ni kuwa Kikwete hayupo tayari kwa namna yoyote ile kukubaliana na mawazo ya wananchi kupitia tume ya Warioba. Leo Dr Slaa anashindwaje kuona ukweli huo?

Kikwete hawakemei akina Nape na Kinana wanaoendeleza tambo za katiba mpya si muhimu.
Hao ni watendaji wake amabo kila siku huibuka kuwatukana UKAWA wakiwa hawana majibu ya hoja.
Kikwete akiwa mwenyekiti wao na Rais wa nchi hajawaekemea hata siku moja ikiwa na maana ameridhia.

Leo Dr Slaa anawezaje kumuomba Kikwete ambaye msimamo wake ni S2 hadi aondoke mwakani, eti aokoe mchakato wa katiba unaoendelea?

Dr Slaa, tunadhani mchakato utaokolewa na wananchi kwa kupitia maoni yao.
Ninyi UKAWA nje na UKAWA BMLK mna wajibu wa kuwafahamisha wananchi kile wasichokijua.

Hili la kumuomba JK asimamie mchakato alioshindwa na aliowafanyaia hila ni la kushangaza sana.

Unaomba mtu mwenye hila akutendee haki. Mtiririko wa mambo Ina maana hukuuona?

Ni kauli kama hiyo imetolewa na Seif kuwa kuwepo na mazungumzo ya katiba mpya.

Hili linaonyesha kuwa ukawa wameanza kubabaika pamoja na ukweli kuwa wana hoja zenye mantiki na umma upo upande wao.

Hatujui kama ni kiu ya juisi za maembe imeanza kuwapata, tunachojua huko ni kubabaika.

Tusemezane.
 
DR SLAA
SOMA BANDIKO LA HAPO JUU LINALOKUKOSOA KWA KAULI ZAKO
HALAFU SOMA HABARI HII


Kwa hisani ya gazeti la Mwananchi
Mbeya. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi amefichua sababu za chama hicho kushikilia msimamo wa muundo wa serikali mbili katika mjadala wa Katiba Mpya, akisema ni "maagizo ya mwenyekiti wa CCM".

Mjadala wa Katiba Mpya ulikumbwa na mtikisiko baada ya Rais Jakaya Kikwete kueleza kitu alichokiita maoni yake binafsi wakati akizindua Bunge la Katiba kwa kueleza kuwa angependa muundo wa Muungano wa serikali mbili tofauti na Rasimu ya Katiba iliyopendekeza serikali tatu.

Mjadala huo ulivurugika kabisa baada ya kundi la wajumbe kutoka vyama vya upinzani waliounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia vikao likidai mjadala umepoteza mwelekeo kwa kuweka kando maoni ya wananchi ya kutaka muundo wa serikali tatu.

Akifungua mkutano wa Baraza la Utendaji la Umoja wa Vijana wa CCM wa Mkoa wa Mbeya juzi jioni, Zambi alisema mwenyekiti wa CCM alishawaambia kwamba msimamo wa chama ni kuhakikisha zinabaki serikali mbili kwenye Katiba Mpya.

''Vijana sasa lazima niwaeleze ukweli kuhusu muundo wa serikali, ni kwamba piga ua, CCM inataka kuimarisha muundo wa serikali mbili na hili ni agizo la mwenyekiti wetu Rais Jakaya Kikwete," alisema huku akishangiliwa.

Alisema suala la Muungano ni maelewano na kwamba baadhi ya shughuli muhimu za Zanzibar zimehamishiwa Bara wakati nyingine za Bara zimehamishiwa Zanzibar.

Hata hivyo, alisema kero iliyopo kwa sasa kwenye Muungano huo ni namna ya kugawana mapato makubwa ambayo alisema Serikali inaendelea kuyafanyia kazi.

"Rais Kikwete katika kutueleza msimamo wa chama, pia alifafanua vizuri suala la serikali tatu kuongeza gharama za uendeshaji, jambo ambalo hata mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba aliliona, ingawa alifafanua kwamba halina namna," alisema.

Zambi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, alisema anamshangaa Mwenyekiti wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe anapotamka kwamba serikali tatu ni lazima.

"Vijana wote na wanaCCM mkoani Mbeya naomba muelewe kwamba sisi chini ya mwenyekiti wetu wa CCM, Rais Kikwete, tumeamua muundo wa serikali mbili tu," alisema.

Alisisitiza kwamba kama wachache hawataafiki msimamo huo kwa busara, Serikali ya CCM itaendelea na katiba iliyopo.

Akieleza sababu za msimamo wake wa serikali mbili wakati akizindua Bunge la Katiba, Rais Kikwete alizungumzia gharama za uendeshaji wa serikali tatu akisema katika muundo wa serikali tatu, Serikali ya Muungano haitakuwa na vyanzo vya uhakika vya fedha na kwamba hilo linaweza kusababisha kushindwa kulipa mishahara kama ya wanajeshi na hivyo kusababisha chombo hicho cha dola kuchukua serikali
 
SITTA AWATEGA UKAWA

KAULI YAKE HAINA UPATANISHI


Wiki hii kumekuwa na wimbi la viongozi wa dini kuwataka UKAWA warudi bungeni. Tumemsikia Askofu wa TEC Muigize, hoja yake ikaweka sawa na Askofu Nagalekumtwa ambaye ni Rais wa TEC.
Juzi tukamisikia askofu wa Tanzania Evangelical church naye akiwataka warudi bungeni.

Wasichokisema ni kuwa UKAWA warudi kujadili nini. Kuna utata na mashaka kwanini wimbi hili la kuwataka UKAWA limekuja na nguvu kubwa. Ukiachilia hao, majaji kama Mutungi na Boman nao wamekuja na kauli kama hizo.

Uhuru wakutoa habari ni wa kila raia, inapofika baadhi ya raia wanatoa maoni yao bila kwenda kina inatia shaka.
Tatizo lililopo ni kutosikilizwa kwa maoni ya wananchi. Hicho ndicho kimewatoa UKAWA bungeni. inginevyo sikuona sababu ya wao kuondoka.

Je, kuondoka kuna uzito? Jibu ni ndio kwasababu katiba inaandikwa kwa muafaka wa kitaifa na si wa chama. Ile habari ya chama kushika hatamu imefika ukomo. Katiba ni ya watu wote na hakuna mwenye haki. Hatuwezi kukubaliana kwa uwiano sawa lakini lazima tubishane kwa hoja na mantiki.

Hili wazo la wengi waliopo bungeni wapewe ndio wenye ukanda ni la ajabu sana. Hivi katiba ya 1977 si imeandikwa na wengi? Kama ni suluhu kwanini tunarudi kuandika katiba nyingine ikiwa wengi walikubaliana nayo?
Jibu ni kuwa mazingira yamebadilika, na wakati unabadilika na hivyo lazima turudi katika muafaka wa kitaifa.

Muafaka huo umekwama kwasababu ile ile ya kutaka kutumia wingi na si mantiki katika kuandika katiba. Spika Samwel Sitta ameonyesha mara nyingi ubabe wa kutaka kutenda kwasababu tu ni mbabe na antaka kile walichoamua wao mafichoni ndicho kiwe.

Jana ametoka na kauli ya kuteua viongozi wa dini na wengine 27 kufikia muafaka. Sitta alienda mbali kwa kusema wale watakaokataa akiwaita watakao vimba vichwa wananchi watajua hawapo upande wa katiba.
Sitta akasema kama UKAWA wakirudi na kutoka , sheria itabadilishwa ili kuondoa 2/3 na kutafuta kitu kingine mbadala ili kupitisha katiba.

Hapa kuna hoja tatu kubwa za kujadili.
1. Kuteua viongozi wa dini
Spika Sitta hawezi kutuaminisha kuwa viongozi anaowatea wa dini ndio wawakilishi wa dini. Na kibaya zaidi huu ni mchakato wa kisiasa, viongozi wa dini waliingia bungeni kama sehemu ya wawakilishi na si wawakilishi wa dini. Lini walichaguliwa na dini zao? Hao waliteuliwa tu ili kuleta uwiano mzuri hasa sehemu zinazohusu imani na wala si wasuluhishi.

Inaendelea....
 
Inaendelea

Hoja ya pili
Sitta anatafuta muafaka, na moja ya taratibu za kupata muafaka ni matumizi ya lugha. Sitta alipotumia neno kuvimba vichwa kukiwa na upinzani, kwa lugha ya upatanishi tayari ameshachukua sehemu katika suala hilo.

Mpatanishi hachukui upande na lugha imeleta ufa mkubwa zaidi. Lugha yake haikupaswa kutumiwa alivyofanya katika wakati huu.

Tatu, Sitta ametoa angalizo kwa uwezekano wa kubadili sheria ili rasimu ipite hata kwa akidi ya watu 100.
Huko ni kurudia historia.Mchakato ulikusudia kuwa na mufaka kuanzia bungeni.

Tunakumbuka Makinda na Ndugai wakalazimisha sheria ipitishwe na wabunge 100 kati ya 320.
Mavuno ya ubabe huo ndiyo tunayoshuhudia. Haielekei kama Sitta amejifunza lolote kuhusu hilo.

UKAWA WATEGWA

Kauli ya Sitta ina maana kubwa kwa UKAWA. Kwanza, kitendo cha kuwatumia viongozi wa dini kina maana kuwawekea mtego ili warudi bungeni kwa kuelewa heshima waliyo nayo katika jamii.

Sitta anaweza kuwaambia kwa ulaghai warudi kitakachojadiliwa ni rasimu ya Warioba.
UKAWA wanaweza kuingia mkenge na kurudi.

Watakapofika bungeni ile 'rasimu' na mbinu zao zitaanza kutumika.
UKAWA wakitoka sheria inabadilishwa kukidhi matakwa ya kupitisha rasimu yao na kutetea mfumo wa serikali 2.

Kama ni hivyo na UKAWA wanalijua hilo kuna sababu gani za wao kurejea bungeni?

Si wakae pembeni ili CCM wapitishe rasimu yao na kisha katiba wanayoitaka.
Hakuna maana ya kurudi bungeni kukiwa na mitego.UKAWA kukaa nje na katiba ya CCM kuandikwa au kurudi na kisha kuondoka ili sheria ibadilishwa havina tofauti.

Kuna mantiki ya kukaa nje ili watende watakavyo, kuliko kurudi kwa kudanganywa na kuondoka kwa kuijengea CCM uhalali wa kuandika rasimu yao kwa ulaghai.

UKAWA wanatakiwa wawe waangalifu, kama ni kurejea, basi iwe kwa kutumia sheria na kuhakikishiwa kwa namna ambazo CCM haitawarudi. Hoja ni kurudi katika rasimu ya Warioba.

Wakibabaika tu na ujanja unaotumiwa , UKAWA watajikuta katika wakati mgumu sana.

Tusemezane
 
UKAWA: KIMYA CHENU KITAWAGHARIMU MBELE YA SAFARI

UONGO UKIRUDIWA MARA NYINGI HUGEUKA KUWA UKWELI


Jitihada za kutumia wanasiasa kuokoa mchakato zinaonekana kushindikana.
Kama alivyoanza Lukuvi kutumia sehemu za Ibada sasa Rais na mwenyekiti anaunga mkono.

Jana alikuwa TAG akiwaomba viongozi wa dini wasadie kuwashawishi UKAWA warudi.
Ni Rais huyo huyo aiyesema May mosi kuwa UKAWA wapo likizo watarudi.

Viongozi wa dini wameingia kwa nguvu sana katika kusimamia suala la UKAWA.
Kinachostaajabisha ni viongozi hao kuwataka UKAWA warudi bungeni, baasi. Hawana maelezo mengine.

Kususia bunge kwa UKAWA kulikuwa na maana moja, kwamba hawapo tayari kuwa sehemu ya uchakachuaji au kutumiwa kuchakachua mchakato. Walijua kitakachotumika ni mambo ya kura baada ya katiba inayotakiwa na CCM kuwa tayari.

UKAWA waliondoka kama njia ya kidmekrasia ya kupinga utaratibu wa kubadili maoni ya wananchi na kuweka ya watu wasiozidi 600. Walichokitaka si kushinikiza matakwa yao bali kufuata utaratibu wa kuzungumzia kilichoamualia na wananchi.
Hivyo, kuondoka kwao ni kutetea masilahi ya wananchi dhidi ya kundi lililomtisha mwenyekiti wa CCM na kukata kona ghafla.

UKAWA wanasikia kauli kama za Mwenyekiti wa mkoa wa Mbeya mh Zambi kuwa maagizo yanatoka kwa mwenyekiti wa CCM taifa aliyesema piga ua ni serikali 2.

UKAWA wanafahamu Rais alisema ''hizo S3 msubiri nikiondoka''
Hivyo wana kila ushahidi wa kuwa shinikizo wanalopata ni la kuwataka kurudi ili kuidhinisha rasimu nyingine.

Wamemsikia Samwel Sitta akisema uwezekano wa kubadili kanuni ili iwepo simple majority upo kama watatoka tena.

Kinachoshangaza viongozi wa UKAWA wamejificha wakihudhuria vikao vya siri na watu kama Mutungi.
Hawajaonyesha leadership ya kukabiliana na matamko yanayoashiria kuchafua nia na adhma yao.

Tulitegemea kauli ya Zambi ikutane na mapigo mazito ya UKAWA ikiwa ni ushahidi wa jinsi mchakato ulivyoingiliwa.
Tulitegemea wawaulize viongozi wa dini, UKAWA warudi bungeni ili kujadili nini,rasimu ya wananchi au kukamilisha tu ratiba ya kuwepo bungeni.

Viongozi wa dini wamerudia mara nyingi sana na kuna sababu za kuhisi wanatumiwa kueleza kuondoka kwa UKAWA tu.
Hawaendi mbali na kueleza chanzo na kiini cha mzozo wala kurejea bungeni ni ili kufanya nini.

Hizi propaganda za viongozi wa kidini zimerudiwa mara nyingi sana na sasa wananchi wamesahau jinsi Rais alivyovuruga mchakato, jinsi Sitta alivyovuruga utaratibu na kanuni na jinsi CCM ilivyowapiga kufuli wawakilishi wao kwa kura ya wazi.

Kinachoongelewa ni UKAWA kurudi bungeni kana kwamba hilo ndilo tatizo.
Propaganda hizo zinarudiwa sana viongozi wa UKAWA wakiwa kimya.
Sasa zigo linaonekana kuwarudia, wananchi wanasema rudini bungeni kwasababu wameanishwa kuwa wao ni tatizo.

Tunadhani akina Mbowe, Mbati na Lipumba wanatakiwa watoke huko waliko.
Hoja nzito zisijibiwe na maafisa habari wa vyama bali viongozi wa UKAWA.

Wawaeleze wananchi kwanini hawarudi bungeni na wanataka nini ndani ya sheria ili warudi bungeni.
Hoja ni simple, tujadili rasimu ya Warioba.
Tuifanyie maboresho ili ipelekwe kwa wananchi kupigiwa kura.

Na ili kurejea ni muhimu Rais akafuta kauli zake wakati anafungua bunge.
Rais alialikwa kama kiongozi wa taifa na si mwenyekiti wa CCM.
Afute kauli zinazounga mkono chama chake kwasababu hapo si sehemu ya maoni.

Halafu wamwambie Rais amwagize mwenyekiti Sitta wazungumzie rasimu ya Warioba, mazuri na mapungufu yake.

Wasipofanya haya, umma utababaika na hata wajumbe wao wanaowaunga mkono watagawanyika.

Watagawanyika kwasababu hawajui viongozi wao wanasimamia nini na kwanini wapo mafichoni.

Tusemezane
 
UTETEZI HUU KWA RAIS NI DHAIFU
MCHAKATO ALIUHARIBU KWA KOFIA YA CHAMA NA SI SERIKALI
UKAWA 'PRESSURE' HII SI DALILI NZURI YA NINYI KULEGEA, JUISI MEZANI


Tumeshangazwa na Rais Kikwete kusifu jitihada za msajili wa vyama kutafuta suluhu na UKAWA
Msajili wa vyama ni mlezi wa vyama vya siasa si mlezi wa katiba ya nchi.

Katiba ya nchi mlezi ni Rais aliyechukua jukumu la kuanzisha mchakato hata pale taratibu zilipokuwa haziungi mkono hatua hiyo. Rais alichukua hatua bila kushirikisha chama chake, na alivaa kofia ya mkuu wa nchi.

Mkuu wa nchi ni kiongozi wa kila raia bila kujali kitu chochote. Kauli yake ni ya ukuu wa nchi si ya chama.
Kuanzisha mchakato halikuwa suala la kisiasa bali la masilahi ya nchi hata kama lilikuwa na chembe za kisiasa.

Bunge aliloteua Rais ndicho chanzo kingine cha mgogoro.
Wabunge ni wana siasa, kuwajaza bungeni ni sehemu ya mgogoro tunaouona.
Katika mazingira ya kawaida bunge la katiba linapaswa kuwa na wawakilishi wengi wa wananchi wasiofungamana na vyama vya siasa. Kosa la kwanza.

Rais alipokwenda kuzindua bunge ni taratibu tu na wala si sheria.
Tuliona mvutano wa nani atangulie kutoa mada.

Kilichopaswa kufanywa kwa mujibu wa kanuni ni Rais kuzindua bunge ili liweze kuanza kufanya kazi zake.
Alichokifanya Rais ni kuliekeza bunge kuhusu linachopaswa kufanya.

Upo utetezi kuwa Rais ana haki ya kutoa maoni. Ndiyo, haki hiyo alikuwa nayo lakini si haki ya kujibu tume aliyoiteua yeye na iliyokuwa na mawasiliano naye.

Yeye alifahamu rasimu ina nini ndiyo maana alisaini iletwe bungeni.Kitendo cha kuanza kuichambua si kuzindua bunge ni kujibu rasimu, na hivyoalijikuta ameacha wajibu wa ulezi wa taifa na kuingilia ushabiki wa kisiasa. Kosa la pili.

Kitendo cha rais kutoa maoni hakikupaswa kufanywa katika bunge a katiba.
Alichopaswa kufanya ni kuliekeleza bunge wajibu wake ikiwemo kuwaleta wajumbe wote pamoja kusimamia masilhi ya taifa.

Kauli za kukosoa rasimu tena akisema '' hizo S3 msubiri hadi niondoke,jeshoi litapindua nchi' ilikuwa ni ushahidi tayari alishatoa msimamo wake na kuwaelekeza wajumbe waangalie nini na si rasimu iliyopo mbele yao. Kosa la tatu.

Pamoja na hayo, rais alikuwa na nafasi ya kutoa maoni wakati tume inafanya kazi.
Ndivyo viongozi wengine na raia walivyotoa maoni.
Hakukuwa na sababu za yeye kutoa maoni wakati ameshasaini rasimu.
Huko kulikuwa kuingilia mchakato na kuuvuruga. Kosa la nne.

Kuna mahali katika hotuba yake Rais ameongelea rasimu kutoeleza mipaka ya nchi.
Hili lilikuwa sahihi kwasababu ni jambo linalohusu taifa na usalama wake.

Lakini pia ni rais huyo huyo alikuwa kimya wakati zanzibar inaweka mipaka chini ya mamlaka yake.
Wapi hoja ya moani ya rais inapokuwa na mashiko? kosa la tano.

Rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM hakusema lolote wakati chama chake kinatoa msimamo.
Badala yake, rais akatetea vyama kujadili rasimu kwa makundi yao akisema ni sawa.
Hapa alikuwa anapalilia siasa za vyama zaidi ya utaifa. Kosa la sita.

Wakati mawaziri wake wanakwenda kanisani, ilikuwa wakati muafaka wa rais kuonyesha kuwa yeye ni gundi ya taifa.
Rais amekaa kimya na hata waziri kuendelea kumshauri akiwa na uchafu wa kupenyeza udini. Kosa la saba.

Mchakato huu ambao sasa ni wa kisiasa unapaswa kuendeshwa kisiasa.
Siku zote viongozi wameasa kuchanganya dini na siasa kwa matamako makali.

Leo tunasikia mawaziri wakienda makanisani, viongozi wa dini wakitoa misimamo kana kwamba hili ni suala la kiroho.
Na rais anashiriki huko kwenye mikutano ya dini na siasa, halafu anatumabia tusichanganye dini na siasa. Kosa la nane.

Kitendo cha kumsifu Jaji mtungi kuwaleta pamoja UKAWA na serikali, akijua kuwa ofisi ya mutungi ilihusika kuleta tafrani na viongozi wa Chadema, kinatafsiriwa kama mbinu ya kuwatisha.

Na kitendo cha kumsifu ni kueleza kuwa mbinu za Mutungi kuwavuruga UKAWA kwa kuanza na Chadema ni sehemu ya mkakati wa serikali. Kosa la tisa.

UKAWA
Kutokana na kufanikiwa kuwapata viongozi wa kidini, sasa hivi hoja inajengwa, viongozi wa dini ambao tunajua wana heshima wanawasihi UKAWA warudi bungeni. Hili linafuatia wimbi la wazee kama Bomani kufanya hivyo hivyo.
UKAWA wamekaa kimya hoja zao zikibadilishwa na sasa tatizo si hoja za UKAWA bali kurudi bungeni.

Tena wapo wanaosema hoja za UKAWA ni laini. Well, kama ni laini iweje hazina majibu.
Wanachotaka UKAWA si kuboresha rasimu kwa kuondoa au kuongeza, wanachokitaka ni maboresho yawe katika framework ya rasimu iliyowakilishwa.

Mfano, bunge linaweza kupanga namna ya kuongeza au kupunguza madaraka ya Rais wa muungano.
Hii haina maana bunge hilo linaweza kuondoa framework ya rais wa muungano. Kuna upotoshaji ambao UKAWA wameukalia kimya.

Hoja kubwa ni kuwa UKAWA ili warudi bungeni lazima rasimu ya Warioba iwe framework ya maboresho yote na si kuandika rasimu nyingine. Wananchi wamesema wanataka S3, hivyo wajibu wa bunge la katiba ni kuhakikisha kuwa S3 walizotaka zinakuwepo.
Ni jinsi gani zinafanya kazi hilo ndilo jukumu la BMK na wala s i kubadili na kuwa S2.

Kama kuna kubadili na kuwa S2 basi tuonyeshwe maoni hayo yanatoka kwa wananchi wapi?
Na kwanini basi wasifikirie mkataba ambao pia umezungumziwa kwa nafasi kubwa.
Wapi wajumbe wanapata uhalali wa kubadili framework ya tume.

Kubadili framework ya tume kuna maana moja, kwamba BMLK linaandika katiba yao na si kwa mujibu wa sheria iliyounda tume na hadidu rejea.

Kwamba Rais Kikwete kavuruga mchatako hilo suala suala tena, kilichopo mbele ni kujadili hatima ya kuvuruga na mustakabali wa taifa. Lolote litakalotokea na kugharimu damu ya mtanzania, lazima atakuwa kati ya mjadala.

Hivyo jukumu la kurudisha UKAWA ni lazima lizingatie maoni ya tume ya Warioba.

Tusemezane.
 
Nguruvi3, Dah, nilikuwa naandika mara ghafla PC yangu ikazima na nikapoteza hata mada nilokuwa najadiliana na wewe . Nimeitafuta wala siipati hivyo nakuomba niwekee 'like' tu ili niweze kuipata tena mada hiyo ktk orodha ya msg maana nimegundua sasa ni wapi wewe huelewi ama hukosea.
 
Back
Top Bottom