Uke kutoa harufu kali(Vaginal Odor): Chanzo, dalili na tiba zake

Nimeona niirudie hii mada. sababu ni nyingi ila kubwa ni hizo mbli. Candida nimeongezea tu.

Fangasi wa candida
Hawa husababisha muwasho ukeni na kutokwa na ute mzito mweupe, ugonjwa huu unaweza mpata mwanamke yeyote ila zaidi ni wale wafanyao ngono. Kwa kawaida ute huu huwa haunuki. Pia unaweza hisi papuchi inawaka moto nakusikia maumivu wakati wa kugegedwa. Inasemekana kati ya wanawake 100 , 75 kati yao hupata ugonjwa huu maishani mwao.

Kutibu candida nirahisi sana , kuna dawa za kupaka kama clotrimazole cream, na pia kuna vidonge vya clotrimazole vya kuweka ukeni. Pia kuna vidonge vya fluconazole.

Unaweza kupaka clotrimazole au kutumia vidonge kwa siku7-14 kulingana na uzito wa ugonjwa pia unaweza kunywa kidonge kimoja cha fluconazole 150mg au vidonge vitatu (kimoja kila baada ya siku tatu) kulingana na hali

Trichomonas vaginalis
Kati ya wanawake mia kumi wanao hawa wadudu. Wanasababisha papuchi kuwasha, maumivu wakati wa kukojoa na kutokwa na maji ya rangi ya mchanganyiko wa kijani na njano ambayo hunuka vibaya.

Kutibu ni rahisi sana! Metronidazole (frajili) ambayo huwa na 200mg unameza 2g (unameza vidonge 10 kwa pamoja). Au vidonge viwili na nusu asubuhi na viwili na nusu jioni kwa siku saba. Pia unaweza tumia dawa ya tinidazole.

Bacterial vaginosis
Unatoa majimaji meupe yenye harufu ya samaki. Unapiga metronidazole200mg (frajili)vidonge viwili na nusu asubuhi na viwili na nusu jioni kwa siku saba.
Dose ya metronidazole ni ndogohyo,400mg 8hrly kwa siku 5 iko poa
 
3416865a1cb8bb48173e4e07e170e651.jpg

Tatizo la harufu mbaya ukeni

Leo tutazungumzia tatizo linalowasumbua wanawake wengi, tatizo la kutokwa na uchafu unaotoa harufu mbaya sehemu za siri. Kitaalamu hali ya mwanamke kutokwa na majimaji yenye rangi nyeupe au ya njano,ni hali ya kawaida na wala siyo tatizo
endapo majimaji hayo siyo mazito sana na wala hayatoi harufu mbaya. Lakini endapo majimaji yanayotoka yapo katika hali ya ute
mzito wenye rangi nyeupe au kahawia, yanatoa harufu kali na yanawasha, basi hiyo ni ishara ya ugonjwa uitwao Vaginosis.

Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha na kuutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nje ya mwili. Pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maambukizi ya
bacteria au fangasi wanaoleta magonjwa. Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na huwa na rangi nyeupe au ya njano. Pia
huwa na asidi ya Lactic ambayo huzuia kuzaliana kwa vijidudu vya maradhi na huzalishwa kwenye tezi za Bartholin (Bartholin's glands) zilizopo kwenye shingo ya mlango wa uzazi (Cervix).

Kwa kawaida, mwanamke hutoa kiasi cha gramu 2 za seli zilizokufa kutoka kwenye mji a uzazi na gramu 3 za ute mwepesi kila siku. Kiwango hiki huweza kuongezeka au kupungua kutegemeana na mzunguko wa hedhi. Kuna wakati ute huwa mwepesi na unaovutika (kama ute wa yai la kuku) na kuna wakati huwa mzito kiasi na wenye rangi ya njano. Ute huu ni wa kawaida na huwatoka wanawake wote hususan baada ya kuvunja ungo.

Sababu za kutokwa na uchafu huo Kuna sababu nyingi ambazo husababisha mwanamke kutoa ute au majimaji yasiyo ya
kawaida kutoka kwenye sehemu zake za siri. Maambukizi ya bacteria wanaosababisha magonjwa kama Trichomoniasis, Candidiasis, Gonorhear au uambukizo wa bacteria Candida albicans, Vaginosis Bacteria n.k husababisha mwanamke kutokwa na uchafu unaoambatana na harufu mbaya.

Pia mabaki ya vitambaa, tissue au pedi ambazo hazikutolewa wakati wa hedhi huweza kusababisha tatizo hili. Usafi wa
sehemu za siri usipozingatiwa hususani mwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hedhi, huweza kuwa mazalia mazuri ya
bacteria wanaosababisha harufu mbaya.

Dalili za ugonjwa wa kutoa harufu
Wanawake wenye tatizo la Vaginosis huwa na dalili kubwa ya kutokwa na ute na majimaji yasiyo ya kawaida (Uchafu)
kutoka sehemu za siri. Uchafu huu huwa unatoa harufu kali kama shombo ya samaki au kitu kilichooza na huambatana na
maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu.Wakati mwingine uchafu
wenye rangi kama ya kijani hutoka
-Kuwashwa na kuchomachoma sehemu za siri,
mgonjwa asipopatiwa tiba haraka husababisha vidonda
sehemu za siri.
- Mwanamke anapoona anatokwa na ute uliochanganyikana na damu hata kama hayupo kwenye siku zake, hii ni dalili nyingine
ya Vaginosis.
- Maumivu makali wakati wa tendo pia ni dalili za ugonjwa
huu.

Matibabu
Tatizo hili hutibika hospitalini baada ya vipimo vya kitaalamu kuchukuliwa na daktari au nesi mwenye uzoefu wa kutosha
juu ya magonjwa ya wanawake. Dawa za kupaka (Ointment/ Cream) na dawa za kumeza (Pills) huweza kumaliza tatizo hili.

Angalizo:
Dawa za kihospitali muda mwingine zinaweza kukuongezea tatizo badala ya kukutibu, hivyo basi inashauliwa kuzingatia usafi wa nguo za ndani na ukeni kwa ujumla vilevile kuzingatia ulaji wa lishe bora ambayo itakusaidia kuuwezesha mwili kujisafisha wenyewe. Bila kusahau unywaji wa maji kwa wingi.

Kumbuka: Ni makosa kutumia dawa bila kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari au nesi.

Jihadhari
wanawake wengi hupenda kutumia baadhi ya dawa ukeni kwa lengo la kuongeza vionjo kwenye mapenzi pia kuufanya uke
kunukia vizuri vitu hivyo ni kama sabuni za kukaza uke, shabo inayowekwa kwenye maji machafu ili kusafisha wenyewe
huweka ukeni ili kukaza uke, dawa za kusafishia ukeni hasa zenye kemikali, hudi asali na vingine vingi naomba niseme kuwa
njia hizi hufurahisha kwa mda mfupi lakini madhara yake ni makubwa kama hivyo kuanza kutoa harufu mbaya.
 
Nimeona niirudie hii mada. sababu ni nyingi ila kubwa ni hizo mbli. Candida nimeongezea tu.

Fangasi wa candida
Hawa husababisha muwasho ukeni na kutokwa na ute mzito mweupe, ugonjwa huu unaweza mpata mwanamke yeyote ila zaidi ni wale wafanyao ngono. Kwa kawaida ute huu huwa haunuki. Pia unaweza hisi papuchi inawaka moto nakusikia maumivu wakati wa kugegedwa. Inasemekana kati ya wanawake 100 , 75 kati yao hupata ugonjwa huu maishani mwao.

Kutibu candida nirahisi sana , kuna dawa za kupaka kama clotrimazole cream, na pia kuna vidonge vya clotrimazole vya kuweka ukeni. Pia kuna vidonge vya fluconazole.

Unaweza kupaka clotrimazole au kutumia vidonge kwa siku7-14 kulingana na uzito wa ugonjwa pia unaweza kunywa kidonge kimoja cha fluconazole 150mg au vidonge vitatu (kimoja kila baada ya siku tatu) kulingana na hali

Trichomonas vaginalis
Kati ya wanawake mia kumi wanao hawa wadudu. Wanasababisha papuchi kuwasha, maumivu wakati wa kukojoa na kutokwa na maji ya rangi ya mchanganyiko wa kijani na njano ambayo hunuka vibaya.

Kutibu ni rahisi sana! Metronidazole (frajili) ambayo huwa na 200mg unameza 2g (unameza vidonge 10 kwa pamoja). Au vidonge viwili na nusu asubuhi na viwili na nusu jioni kwa siku saba. Pia unaweza tumia dawa ya tinidazole.

Bacterial vaginosis
Unatoa majimaji meupe yenye harufu ya samaki. Unapiga metronidazole200mg (frajili)vidonge viwili na nusu asubuhi na viwili na nusu jioni kwa siku saba.
Mkuu FLAGILY 10 MARA MOJA?tena za mg 2!? UTAUWA WATU WEWE!
 
Mada nzuri asante mkuuu ila hiyo harufu ya samaki inasababishwa na nini na kwa nnn inuke kama samaki.
 
jamani msimeze midawa mingi kwa ushauri wa mleta mada.flagly huwa 2×3 kwa siku 5 au 2×3 kwa siku 7au vidonge 4 mara 2 ila ni kwa USHAURI WA DAKTARI ALIYE IDHINISHWA NA SI VINGINEVYO!
 
Vidonge kumi khaaaaaaa Mungu epushia mbali
 
Back
Top Bottom