Mikoani kuna Uzi sana...sana tatu unatafuta chakula kwa tochi!
Mkoa gani ulitafuta chakula kwa tochi? Au unaongelea aina ya chakula,ulikosa chips kavu? Kama ulikuwa Arusha ungeenda Granmelia ipo pale mkuu ina hadhi ya nyota tano kama Serena unapokunywa chai. Au kama ni masikini masikini ungeenda maeneo Shivers/Mrina ungepata nyama choma na mad* wa kununua.
Tabora ungeenda hata Tabora Belmonte ni nyota tatu haifikii Hyatt unapokula mchana ila ingefidia kidogo, wazungu weusi wenzako huwa wanalala pale pia, kama ni masikini masikini unataka wa kununu ukachakate ungeenda Oxygen Lounge/Club nadhani bado ipo nilipita muda kidogo.
Mwanza zipo sehemu kibao, Iringa zipo.....Mbeya pia nimeshacheki night life yao.
Issue ni hela hamna, au nyie ni madogo na night life mnaigiza mnataka mkute watu weengiii muanze ukenge ukenge
😀 sababu mmeshazoea kufuata mikumbo ya msafara wa mamba.
Halafu watu wa hivi na mitazamo hii hata hapa Dar ndio nyie tunawakimbia club kubwa tunaenda katika vi bar vya nje sababu brother brother nyiiingiii ni bia ya saba zote za mizinga,na kusimulia historia za zamani, ulegend wa kibwege oooh hapa Kino mi legend, babu yangu sijui hivi, wakati watu wanataka kula life kwa kidogo kilichopatikana.
Ukiwasha sigara, haujafika hata katikati anaitaka, unampa nzima anaiweka mfukoni anasubiri unayovuta. Mwishowe unambwatukia dogo kuwa na adabu, kwanza nani kakuita hapa....umeshapata bia na sigara. Ondoka
NB SIO LAZIMA UWE WEWE NDIO WATU KIBAO WALIVYO