PreGE2025 Ukiachana na Musukuma, hawa ndio wabunge wengine 12 ambao wameishia darasa la 7. Mbunge wako yupo?

PreGE2025 Ukiachana na Musukuma, hawa ndio wabunge wengine 12 ambao wameishia darasa la 7. Mbunge wako yupo?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hapo bado

Waliofeli Form 2
Waliofeli Form 4
Waliofeli Form 6

Na waliopata degree wakiwa full time Waziri tena wizara nyeti ya Fedha. Hiyo degree umeisoma, umenunua ?????
Unamaanisha aliepata phd akisomea full time?
 
Karne hii kama hutambui umuhimu wa elimu, tena elimu bora, wewe utakuwa na tatizo la afya ya akili.

Kuwa na mtu wa elimu ya shule ya msingi ambaye ameajiri watu milioni moja hakuhalalishi kuwa na mtu wa namna hiyo kwenye chombo cha maamuzi.
Kwani elimu imeanza karne hii tu? Wewe utakuwa na utindio wa ubongo. Au tatizo lako ni kutokujua maana ya elimu? Elimu ipo tangu dunia hii iumbwe na ndio maana basic ya elimu haijabadirika vinavyobadirika ni nakishi tu ya elimu.
 
Wewe tatizo lako ni slavery mentality inakusumbua akifanya Mwaafria hutaki kusifia ila akifanya mzungu unasifia, huo ni utumwa wa kiakili. Nisawa na kumwona mzungu anasafiri na drone na mwaafrika akisafiri na ungo. Drone utasema technolojia, ungo utasema uchawi haufai! 🤣🤣🤣

Hahaha, jamaa amemtaja Henry ford ambaye ndio mwanzilishi wa magari ya Ford.
Yupo Ellon Musk mwenye Tesla, wapo akina Lamborgin, wapo akina Adidas, wapo akina Bill gates, wapo walioanzisha Boeing, Airbus nk.

Hao wote niliowataja kazi zao zinajulikana duniani kwenye technolojia, Tunaendelea Magari yao, tunapanda ndege zao, tunatumia na kuona matokeo ya technolojia zao.

Ziko wapi technolojia za zetu Africa ambazo ziko wazi kwa kila mtu kutumia na kuona mchango wake kwenye manufaa ya dunia?
Leo hapa tupo busy na internet na kila mtu anachat huku na kule, iko wapi internet ya Mwafrica sasa tujivunie nayo?..

Iko wapi mizigo na abiria vilivyobebwa na ungo? Leo nyungo ngapi zimesafiri kutoka Dar es salaam kwenda New York, zimebeba abiria wangapi na mizigo mingapi, zimetua wapi? nk.

Tunajaribu kuwa na mawazo chanya ili akili zetu zifanye kazi nasisi tuwe na uwezo wa kutengeneza vya kwetu ili tujivunie navyo.
 
Na wamefanikiwa kimaisha kuliko wewe uliye na Phd ya makaratasi wenyewe wana Phd kwa wananchi.

Kasome kitabu cha management ambapo Ford anaulizwa aliwezaje kufaulu kwenye kampuni yake wakati hana elimu na ameajiri wafanyakazi wenye Phd. Jibu lake lilikuwa 'Anawajua vizuri wafanyakazi wake'.

Hivyo kitu muhimu kwenye dunia hii ni kuijua jamii unaoishi nayo kuliko kitu kingine hapo utatoboa, ndio maana unaona hao wabunge wanashinda ubunge kuliko hao wenye Phd. Nenda kagombee huko kwa Musukuma kama utapata hata kura 100!!

Mantiki yangu ni kuwa tusiwabeze wabunge walio na elimu ya chini (darasa la saba) kwa kuwa kuna ushahidi tosha kuwa pia wenye elimu ya chini wamesaidia maendeleo duniani kwa kiasi kikubwa tu.
Hakuna SI Unit ya mafanikio.
Kila binadamu ana maana yake ya mafanikio.

Hao darasa la saba unaosema wamesaidia maendeleo duniani, ni sahihi, lakini hapa tunazungumzia kwenye bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa na mbunge darasa la saba.

Hao wabunge wa la saba, wamechangia nini cha maana humo bungeni!!??
 
Hahaha, jamaa amemtaja Henry ford ambaye ndio mwanzilishi wa magari ya Ford.
Yupo Ellon Musk mwenye Tesla, wapo akina Lamborgin, wapo akina Adidas, wapo akina Bill gates, wapo walioanzisha Boeing, Airbus nk.

Hao wote niliowataja kazi zao zinajulikana duniani kwenye technolojia, Tunaendelea Magari yao, tunapanda ndege zao, tunatumia na kuona matokeo ya technolojia zao.

Ziko wapi technolojia za zetu Africa ambazo ziko wazi kwa kila mtu kutumia na kuona mchango wake kwenye manufaa ya dunia?
Leo hapa tupo busy na internet na kila mtu anachat huku na kule, iko wapi internet ya Mwafrica sasa tujivunie nayo?..

Iko wapi mizigo na abiria vilivyobebwa na ungo? Leo nyungo ngapi zimesafiri kutoka Dar es salaam kwenda New York, zimebeba abiria wangapi na mizigo mingapi, zimetua wapi? nk.

Tunajaribu kuwa na mawazo chanya ili akili zetu zifanye kazi nasisi tuwe na uwezo wa kutengeneza vya kwetu ili tujivunie navyo.
Ungekuwa na akili sawa sawa ungewatafuta hao wanaotengeneza ungo ili uwasaidie kutoka hapo walipo ili ungo uweze kutumika commercially kama vitu ulivyovitaja hapo juu badala ya kuwabagaza na kuwasifu wazungu tu kama na wewe ni mzungu. Hivyo tatizo liko kwenye ubongo wako ndio maana nikasema una tatizo la slavery mentality, jitahidi utoke hapo uwe mbunifu kama waliobuni ungo.
 
Hakuna SI Unit ya mafanikio.
Kila binadamu ana maana yake ya mafanikio.

Hao darasa la saba unaosema wamesaidia maendeleo duniani, ni sahihi, lakini hapa tunazungumzia kwenye bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa na mbunge darasa la saba.

Hao wabunge wa la saba, wamechangia nini cha maana humo bungeni!!??
Kwa hiyo hawajachangia chochote cha maana? Anyway asante kwa mchango wako kwenye mada hii.
 
Kwa hiyo hawajachangia chochote cha maana? Anyway asante kwa mchango wako kwenye mada hii.
Kingekuwepo cha maana walichochangia, ungeweka hapa.
Hao la saba ni vikaragosi vya watawala.
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Hao wote Wana hela

Ndo maana wananchi wanawapenda
Moja wapo ya vikwazo vya kulia Kwa Demokrasia katika nchi changa ni Unaskini wa watu.
Kwamba
1. Watu hawaoni umuhimu wa kuacha kwenda kujitafutia Riziki na kukaa kusikiliza sera na matazamio ya wanasiasa na hivyo kufanya maamuzi sahihi.
2. Wenye fedha wachache bila kujali uwezo wao kiakili na kiuongozi, kutumia fursa hiyo ya Umasikini wa watu kurutubusha rushwa! Ccm huchaguliwa Kwa exchange ya ubwabwa, t-shirt na khanga
 
Wakuu,

Hivi karibuni nimeona watu wanalalamika kwamba tovuti ya Bunge inafuta CV za wabunge makusudi ili tusijue level zao za elimu.

Sasa kabla hawajafuta, ni vyema tujue nani ni nani. Mule bungeni kuna wabunge wengi ambao waliruka umande. Yani mtu alisoma hadi la 7 tu after that akajikuta yuko bungeni.

Wabunge wote hawa wametokea CCM na hakuna hata mmoja ametokea upinzani na wote ni wanaume!

Hawa ndio wanatutungia sheria na kutaka mwandishi awe na Diploma au Bachelor's Degree ili aweze kuripoti habari za Uchaguzi.

Ni Mbunge gani nimemsahau hapa?

1. Daniel Awack Tlemai - Mbunge wa Karatu

YearLevelSchoolAwards
1985 - 1991Primary SchoolQarru Primary SchoolCPEE


2. Nicodemas Henry Maganga - Mbunge wa Mbogwe

YearLevelSchoolAwards
1991 - 1997Primary SchoolNhungwiza Primary SchoolCPEE


3. Hussein Nassor Amar - Mbunge wa Nyang'hwale

YearLevelSchoolAwards
1967 - 1973Primary SchoolBuzanaki Primary SchoolCPEE


4. Kilumbe Shabani Ng'enda - Kigoma Mjini

YearLevelSchoolAwards
1975 - 1981Primary SchoolMuunganoCPEE


5. Robert Chacha Maboto - Bunda Mjini
YearLevelSchoolAwards
1983 - 1989Primary SchoolMuhoji Primary SchoolCPEE


6. Hassan Seleman Mtenga - Mtwara Mjini

YearLevelSchoolAwards
1974 - 1980Primary SchoolChikongola Primary SchoolCPEE



7. Tabasamu Hamisi Hussein Mwagao - Sengerema
YearLevelSchoolAwards
1975 - 1981Primary SchoolNyakato Primary SchoolCPEE

Wabunge wengine ni pamoja na:

9. Deo Sanga - Makambako
10. Hassan Zidadu Kungu - Tunduru Kaskazini
11. Njalu Daudi Silanga - Itilima
12. Jaffar Sanya Jussa - Paje
WA chama gani vile
 
Yulikaa SEHEMU BAR KARIBIA NA CHOO

JAMAA AKASEMA ANAENDA KUKOJOA

ALIPOFIKA AKAJAMBA KWELIKWELI

TUKAANZA KUCHEKA

ALIPORUDI TUKAMUULIZA MWAMBA VIPI TENA NN KIMYA AKAJIBU

KILA MVUA LAZIMA LAZIMA IJE NA RADI TULIKAA KIMYAA

SO KILA KWENYE PHD LAXIMA WAWEPO LA SABAA TUWE WAPOLE
 
Ungekuwa na akili sawa sawa ungewatafuta hao wanaotengeneza ungo ili uwasaidie kutoka hapo walipo ili ungo uweze kutumika commercially kama vitu ulivyovitaja hapo juu badala ya kuwabagaza na kuwasifu wazungu tu kama na wewe ni mzungu. Hivyo tatizo liko kwenye ubongo wako ndio maana nikasema una tatizo la slavery mentality, jitahidi utoke hapo uwe mbunifu kama waliobuni ungo.

Kwahiyo hao watengeneza ungo wenyewe hawataki kuwa matajiri mpaka tuwafuate, kuwasaidia na kucommercilize huo usafiri wao.

Hao waliotengeneza ndege kuna binadamu waliwafuata na kuwasaidia au ni wenyewe walijifanyia revolution stage kwa stage mpaka kufikia hapo walipo na watu kuanza kuzitumia ndege.

Ford uliyejaribu kumtaja kuna mtu alimfuata au yeye mwenyewe alimove stage to stage na kufika alipo.
Elon Musk alifuatwa na nani?

Technolojia ni suala open sana, sio suala la giza ukiwa nayo lazima ionekane tu na lazima ikue tu na lazima watu waikimbilie huhitaji kelele nyiiiingi kuwaaminisha watu.

Hiyo unayoisema technolojia ambayo watu wanayogizani itakuwa sio technolojia tena maana Karne na Karne tunaisikia wakati wenzao zakwao ziko wazi na watu wanazitumia na watu zinawatajirisha na zinaleta msaada duniani.

Narudi tena, Technolojia ni suala la wazi sio kificho maana yakuwepo nikuwasaidia watu haina maana kama unatechnolojia halafu ni Siri unataka tukufuata gizani.
 
inawezekana wanauwezo mkubwa wakutumia akili, pia itakua wamejifunza maisha kwa vitendo kwa muda mrefu. badala yakuwabeza embu tujifunze kwao
 
Screenshot_2025-06-12-11-12-01-513_com.whatsapp.jpg
 
Actually ndivyo ilivyo, sheria yenyewe inaweka wazi kuwa mbunge ni muwakilishi wa wananchi wa jimbo lao. Sasa kama mna mbunge bogus huyo ni muwakilishi wa wananchi wa jimbo hilo ndivyo walivyo. Ona wabunge bogus angalia na wananchi wake utaona hata wananchi wake ni bogus na mifano ipo haina haja ya kutaja
 
Jamii imekuwa na ongezeko kubwa la wasomi tofauti na zamani kwahiyo ingependeza kama wawakilishi wa wanajamii nao wangekuwa wasomi.
wanasema bunge ni la wawakilishi wa wananchi, kwa hiyo wananchi wote wanawakilishwa bungeni ndio maana kuna mpaka wabunge waganga wa kienyeji, wachungaji, wasanii na wapuuzi wengine usishangae kuona mbunge bogus!
 
Hilo sio la kuuliza, si unaona yanayoendelea bungeni, kungekuwa na watu TIMAMU, isingekuwa hivi.
 
Back
Top Bottom