PreGE2025 Ukiachana na Musukuma, hawa ndio wabunge wengine 12 ambao wameishia darasa la 7. Mbunge wako yupo?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Bibi chau mwenyewe elimu yake ina makando kando mengi akiwa anaongea tuu unajua kabisa huyu alienda shule kuongezeka kimo na umri tuu
 
Hawa ndio tunaambiwa tukawapigie kura!
Wabunge wameshindwa na hawataki kuwatetea wananchi wao wanaotekwa, kuteswa na kuuawa!
hapana jamani tunahitaji marekebisho ya katiba tupate wabunge watetezi na wenye akili za kuwaza.
 
Hapa tunaongelea maendeleo na ustawi wa nchi,huwezi kuwa na wabunge ambao hawana elimu halafu utegemee wawe na michango ya kulipeleka Taifa mbele.
Tunaishi katika Ulimwengu wa ushindani,lazima uwe na watu wenye maarifa.
Uelewa wako ni mdogo sana. Nimeeleza hapo juu kwa ufasaha sana na nikatoa na mfano wa tajiri Ford, usichojua ni kwamba maarifa na elimu ni vitu viwili tofauti kabisa unaweza ukawa na elimu lakini bado ukakosa maarifa.

Kwa taarifa yako matajiri duniani wengi hawana elimu kubwa sana hata hapa Tz wengi waliofanikiwa kimaisha ni elimu ndogo tu wakiwemo darasa la 7 na wenye Phd ni watumishi tu.
 
Mantiki yako ni nini hasa mkuu.
 
Vitabu vyote vitakatifu vimeongelea juu ya watu kusoma na kuyatafuta maarifa.

Dunia ina mifumo yake ambayo ili isetiwe inahitaji watu waliosoma vizuri na kuyapata maarifa vizuri.
Huwezi ukawa na Bunge ambalo moja ya kazi yake kubwa ni kuisimamia Serikali na ikasimama kama mhimili unaojitegemea halafu unasema Mbunge awe anajua kusoma na kuandika tu.
 
Mantiki yako ni nini hasa mkuu.
Mantiki yangu ni kuwa tusiwabeze wabunge walio na elimu ya chini (darasa la saba) kwa kuwa kuna ushahidi tosha kuwa pia wenye elimu ya chini wamesaidia maendeleo duniani kwa kiasi kikubwa tu.
 
Kusoma na kuandika ndio elimu mama ya mambo yote duniani kwa maana nyingine ndio base hivyo ukiwa na exposure kubwa ya mambo ya duniani hiyo inatosha sana pia uweze kuishi vizuri na jamii inayokuzunguka hapo utakuwa umetoboa.
 
Uko sahihi kabisa, lakini hao walioisaidia dunia na hawakwenda shule wengi wao ukiwapima utagundua ni magenius ambao wamepewa tunu hiyo na Mwenyezi Mungu.

Je hawa wakwetu ambao hawakwenda shule na wapo kwenye mifumo nao ni magenius? Wana kitu special ambacho tunaweza kuwaita magenius?

Unaweza kuitwa genius katikati ya wajinga ambao hakuna wanachojua na wewe kwasababu ya kuwa na hela na kupita kwenye mifumo iliyooza ukawa kiongozi?...
 
Ngoja nikupe mfano wa hapa kwetu, wabunge Kishimba, Musukuma n.k wana elimu ya kawaida lakini michango yao bungeni ina mantiki kuliko wabunge wengi wenye Phd pia kimaisha wako vizuri tangu wakiwa nje ya bunge.
 
Kusoma na kuandika ndio elimu mama ya mambo yote duniani kwa maana nyingine ndio base hivyo ukiwa na exposure kubwa ya mambo ya duniani hiyo inatosha sana pia uweze kuishi vizuri na jamii inayokuzunguka hapo utakuwa umetoboa.

Bado pamoja na kusoma,kuandika + exposure havijufanyi uingie baadhi ya maeneo maana maeneo mengine huhitaji utalaam zaidi ya kusoma, kuandika na exposure.

Tunapozungumzia mifumo madhubuti ya kuongoza na kutawala watu na kujenga future ya Taifa + ukuaji wa generations to generations HAPA TUNAZUNGUMZA ZAIDI YA KUJUA KUSOMA, KUANDIKA NA EXPOSURE, bali tunazungumzia maarifa na watu wenye Elimu na ujuzi wa nyanja mbalimbali.
 
Mwanasiasa haitaji elimu ya juu kuwawakilisha wananchi anachohitaji ni maarifa na exposure tu. Yeye anapeleka maoni ya wananchi ambao wapo walio na elimu ya juu na utaalamu mbalimbali ambao ndio watamsaidia huyo mbunge. By the way mbunge hawezi kuwa mtaalamu wa kila sector.
 
Ngoja nikupe mfano wa hapa kwetu, wabunge Kishimba, Musukuma n.k wana elimu ya kawaida lakini michango yao bungeni ina mantiki kuliko wabunge wengi wenye Phd pia kimaisha wako vizuri tangu wakiwa nje ya bunge.

Kishimba na Musukuma ni wafanya biashara, kuwa mfanya biashara kila mtu anaweza kuwa kadili alivyobalikiwa na Mwenyezi Mungu, kuwa mfanya biashara hasa za uchuuzi ukafanikiwa hakukufanyi tukakuita Genius.

Umetoa mfano wa Henri Ford, huyu sio mchuuzi huyu ni technologist aliyefikiri na kubuni jambo kama walivyo akina Gates, Musk nk. Hawa tunawaita genius.

Huku mitaani wapo watu wenye hela zaidi ya huyo Musukuma na Kishimba lakini hatuwezi kuwaita genius maana hufanya uchuuzi ambao ni jambo la kawaida mtaani.

Sijawahi kuona mchango wa maana wa Kishimba au Musukuma bungeni zaidi ya vituko na uchekeshaji ambao ni kawaida kwenye Bunge letu maana haliko serious.
Kwa jamii yetu ilivyo lazima tuwaone Musukuma na Kishimba wana mchango ya maana maana Bunge letu sio moja ya Mabunge yenye kujadili sensitive issues zaidi ya mambo ya kawaida sana yanayohitaji akili yeyote ile.

Jaribu kusikiliza mabunge ya nchi zilizoendelea kama utaona michango ya kijinga inayofanana na Musukuma au Kishimba ambao ukiwasikiliza utagundua shida yao kubwa ni kutaka kuaminisha watu Elimu haina maana na watu wasisome.
 
Mwanasiasa haitaji elimu ya juu kuwawakilisha wananchi anachohitaji ni maarifa na exposure tu. Yeye anapeleka maoni ya wananchi ambao wapo walio na elimu ya juu na utaalamu mbalimbali ambao ndio watamsaidia huyo mbunge. By the way mbunge hawezi kuwa mtaalamu wa kila sector.

Hakuna pia maarifa na exposure inayoweza kupatikana kwa mjinga, kama ambavyo tunasema unaweza kusoma lakini hujaelimika.

Nakataa, Mwanasiasa hawezi Tu kuwa mtu yeyote mtaani eti kwasababu ana exposure na maarifa.... Maarifa gani na exposure gani?

Mtu akiwa na maarifa ya wizi/uchawi/utapeli na exposure kwenye ujingaujinga basi anaweza kuwa Mwanasiasa?..

Lazima tuwe na mipaka maarifa gani na exposure gani?.
 
Taja kazi tatu za bunge! Halafu tujadili kama elimu inahitajika au la
 
Kishimba na Musukuma ni wafanya biashara, kuwa mfanya biashara kila mtu anaweza kuwa kadili alivyobalikiwa na Mwenyezi Mungu, kuwa mfanya biashara hasa za uchuuzi ukafanikiwa hakukufanyi tukakuita Genius.

Umetoa mfano wa Henri Ford, huyu sio mchuuzi huyu ni technologist aliyefikiri na kubuni jambo kama walivyo akina Gates, Musk nk. Hawa tunawaita genius.

Huku mitaani wapo watu wenye hela zaidi ya huyo Musukuma na Kishimba lakini hatuwezi kuwaita genius maana hufanya uchuuzi ambao ni jambo la kawaida mtaani.

Sijawahi kuona mchango wa maana wa Kishimba au Musukuma bungeni zaidi ya vituko na uchekeshaji ambao ni kawaida kwenye Bunge letu maana haliko serious.
Kwa jamii yetu ilivyo lazima tuwaone Musukuma na Kishimba wana mchango ya maana maana Bunge letu sio moja ya Mabunge yenye kujadili sensitive issues zaidi ya mambo ya kawaida sana yanayohitaji akili yeyote ile.

Jaribu kusikiliza mabunge ya nchi zilizoendelea kama utaona michango ya kijinga inayofanana na Musukuma au Kishimba ambao ukiwasikiliza utagundua shida yao kubwa ni kutaka kuaminisha watu Elimu haina maana na watu wasisome.
Wewe tatizo lako ni slavery mentality inakusumbua akifanya Mwaafria hutaki kusifia ila akifanya mzungu unasifia, huo ni utumwa wa kiakili. Nisawa na kumwona mzungu anasafiri na drone na mwaafrika akisafiri na ungo. Drone utasema technolojia, ungo utasema uchawi haufai! 🤣🤣🤣
 
Taja kazi tatu za bunge! Halafu tujadili kama elimu inahitajika au la
Maswali ya wanafunzi peleka kwa wanafunzi wenzako hapa tunajadiri issues siyo academic questions!
 
Wewe mleta mada una elimu ya kiwango gani?. Unaweza kuwa mwepesi kunyooshea vidole wabunge wakati wewe upo hoi zaidi ya hao wabunge unaowakashifu kupitia huu uzi.

Hao hao wabunge la saba wanakaribia kuimaliza reli ya SGR kwa namna mchango wao wa maamuzi unavyoisaidia TZ.

Hao hao wabunge la saba wamefikisha umeme nchi nzima, hivi sasa uwekezaji wa viwanda unaweza kufanyika nchi nzima kwa sababu miundo mbinu ya umeme imesambaa nchi nzima.

Hao hao la saba wamewezesha ujenzi wa meli Ziwa Victoria na pato la makusanyo ya TRA linaongezeka kila siku.

Tukumbuke hao la saba wanafanya kazi na wabunge wenye shahada za juu za vyuo vikuu, yupo Kimei humo bungeni, yupo Profesa wa wizara ya michezo yupo Hamza Johari mwanasheria mkuu.

Usilidharau bunge zima kisa uwepo wa wabunge wasiozidi 15 ambao ni darasa la saba!.

Hata hao darasa la saba kufika walipofika kuna jitihada kubwa waliyoifanya ambayo wewe mleta mada huwezi kuifanya na kuacha alama kwenye jamii inayokuzunguka.

Kuna wabunge zaidi ya 350 humo bungeni huu uzi unaongelea wabunge 12 walioshia darasa la saba, hao wengine hawatoshi kuwakilisha kundi la wasomi?.

Huyo msukuma ni milionea wa muda mrefu tu, kuna wasomi wangapi amewaajiri kwenye biashara zake ambao maisha yao yanazitegemea mali zake?.

Punguzeni kasumba za kitoto hizi.
Karne hii kama hutambui umuhimu wa elimu, tena elimu bora, wewe utakuwa na tatizo la afya ya akili.

Kuwa na mtu wa elimu ya shule ya msingi ambaye ameajiri watu milioni moja hakuhalalishi kuwa na mtu wa namna hiyo kwenye chombo cha maamuzi.
 
Hakuna pia maarifa na exposure inayoweza kupatikana kwa mjinga, kama ambavyo tunasema unaweza kusoma lakini hujaelimika.

Nakataa, Mwanasiasa hawezi Tu kuwa mtu yeyote mtaani eti kwasababu ana exposure na maarifa.... Maarifa gani na exposure gani?

Mtu akiwa na maarifa ya wizi/uchawi/utapeli na exposure kwenye ujingaujinga basi anaweza kuwa Mwanasiasa?..

Lazima tuwe na mipaka maarifa gani na exposure gani?.
Kwa uelewa wako mtu mwenye maarifa ya wizi/utapeli atakubalika na jamii inayomzunguka mpaka wamchague kuwa mbunge!!?? Fikiri kwanza kabla ya kuandika mkuu!
 
Back
Top Bottom