Mzee wa kupambania
JF-Expert Member
- Aug 14, 2022
- 21,111
- 53,092
Unamaanisha nini mkuu?Utapeli waliotakiwa kutapeliwa wamarekani walipoushitukia , hata vazi sutico,linakataliwa nchini ikabidi kaundasuti ziaze kuvaliwa
Tazara yenyewe imechoka kuliko mchoko wenyewe
Marekani,uingereza wote wana kambi Kenya.Hapo wanamtongoza ili akubali waweke kambi hapo Kenya. Mzungu ukiona anajifanya anamheshimu kiongozi wa kiafrika jua anawindwa. Umesahau bwana Membe alivyotumiwa farasi maalum wamkokote UK.
Marekani naona anatafuta mahali pa kuweka uwepo wake akapambane na influience ya Warusi na Wachina Afrika.
Nimeona wameideclare kenya kama ally wao, wachambuzi inakuaje hiiHapo wanamtongoza ili akubali waweke kambi hapo Kenya. Mzungu ukiona anajifanya anamheshimu kiongozi wa kiafrika jua anawindwa. Umesahau bwana Membe alivyotumiwa farasi maalum wamkokote UK.
Marekani naona anatafuta mahali pa kuweka uwepo wake akapambane na influience ya Warusi na Wachina Afrika.
Sasa anamtokea puaniSamia alipokelewa na Mange 😀.
Katika mambo yote uliyoandika hoja ya msingi ni moja tu kwa nini Tanzania hatutoboi kimataifa?Ni kweli kuna uelewa mdogo, lakini watu wote hawawezi kuwa na uelewa mkubwa, ukitaka iwe hivyo na wewe utakuwa na uelewa mdogo. Kuna watu wanajifunza, wengine wadogo, sasa watajuaje mambo bila kujifunza?
Jana niliandika tofauti ya state visit na visits nyingine, nikaitaja hii ziara ya Nyerere, lakini sikuona haja ya kubeza watu.
Zaidi, swali la msingi liko palepale, kwa nini Kenya inashamiri sana kinataifa zaidi ya Tanzania? Kwa nini Kenya imekuwa nchi ya kwanza Afrika kupata State Visit Marekani tangu mwaka 2008, na Tanzania haipati nafasi hizi?
Kuna jibu refu la historia ya Kenya kama koloni proper la Waingereza ambalo halijapitia Ujamaa kama sisi, geopolitics, Wakenya walivyojipanga ku lobby, business culture ya Kenya, masuala ya Kenya kwenda kulinda amani Haiti, siasa za Umagufuli kujifungia zilivyoharibu mahusiano ya kimataifa ya Tanzania, Samia kutojua anataka kufanya nini, Tanzania kuji align zaidi na China, yote haya yanahusika.
Haikupangwa siku nyingi sana; mwaliko ulikuja mwezi wa pili ikiwa ni muda mfupi sana baada ya Mahakama Kuu ya Kenya kuzuia polisi wa Kenya kwenda Haiti. Hata kama kulikuwa na mipango hiyo ya kumwalika, jambo ambalo Marekani inataka kufanya kwa kiongozi mmoja mmoja wa Afrika, huenda ziara hii ya Rutto isingekuwa mwezi huu.Umejitahidi sana kujieleza, na yote uliyoeleza yanajulikana. Ila bila kusita kabisa nabaki palepale. Ziara ya Ruto haikuwa ya kustukiza hata kidogo; hii imepangwa kiutaratibu tokea mwanzo kwa nia ile ile ya Marekani kuwa na eneo lake katika ukanda huu. Kenya haikuanza jana chini ya Ruto kuwa chini ya 'influence' ya Marekani. Kidogo Mwai Kibaki aliwastua sana wakubwa, alipogeukia Mashariki. Na kutokana na kuingia kwa China, Marekani anaona maslahi yake yanalegalega; kwa hiyo sasa ana'catch up'.
Siyo mara ya kwanza Ruto kuingia Jumba Jeupe tokea ashike madaraka. Mipango hii ilianzia hata kabla Uhuru hajaachia madaraka. Huu ni mpango endelevu, siyo wa kustukiza.
Inawezekana hiyo point ya kwa nini Tanzania haitoboi ndiyo ya msingi, lakini hizo point zote zina umuhimu.Katika mambo yote uliyoandika hoja ya msingi ni moja tu kwa nini Tanzania hatutoboi kimataifa?
Na si lazima taifa liwe na uhusiano wa karibu na Marekani au wanachama wa NATO ili liwe na uchumi mzuri.
Tanzania ni taifa lisilofungamana na upande wowote linaweza kuwa na ushirika na taifa lolote duniani iwe ni China au Marekani
Mshirika mkubwa wa kibiashara wa Kenya ni China. Ushawishi wa China kupitia BRI na BRICS ndio unafanya Marekani aimarishe ushawishi wake Africa.Mfano, huwezi kuongelea Ruto kupata state visit Marekani bila kuongelea business culture ya Kenya iliyomtengeneza Ruto, the Hustler in Chief. Inayoweka watu wa kumu inform Ruto nini cha kufanya, .
Vietnam imekuwa na siasa za ujamaa lakini ni mshirikia mkubwa wa kibiashara wa Marekani kuliko KenyaHuwezi kuongelea business culture ya Kenya bila colonial influence ya Waingereza na siasa zilizofuatia uhuru za Kenya ambazo hazijapitia distractions za Ujamaa.
Bado inaiweka Kenya juu na Ruto anakuwa strategic geopolitical player.Mshirika mkubwa wa kibiashara wa Kenya ni China. Ushawishi wa China kupitia BRI na BRICS ndio unafanya Marekani aimarishe ushawishi wake Africa.
Imeanza kuonekana mataifa ya Africa yameanza kuwa na nia ya kujiunga na BRICS
Hii state visit ya Ruto pale Marekani ni issue ya ki-geopolitics
Vietnam imeondoka kwenye Ujamaa tangu mageuzi ya Doi Moi ya miaka ya 1980. Pia Vietnam imejua kujipanga kutumia historia ya vita na US kujenga biashara.Vietnam imekuwa na siasa za ujamaa lakini ni mshirikia mkubwa wa kibiashara wa Marekani kuliko Kenya
Sijaona point yako ya maana hapa?
Vipi kuhusu China mshirika mkubwa wa kibiashara wa Marekani. Vipi siasa za China?
Kwani Tanzania ni nchi ya kijamaa mpaka sasa? Umeona hoja zako jinsi hazina mashiko.Vietnam imeondoka kwenye Ujamaa tangu mageuzi ya Doi Moi ya miaka ya 1980. Pia Vietnam imejua kujipanga kutumia historia ya vita na US kujenga biashara.
Sisi hata hatujui tunaenda wapi.
China tangu mageuzi ya Deng Xiaoping inafuata siasa za uchumi wa viwanda kupata exports. Sisi hatuna hata hizo exports.
Utaenda kuongea nini na Mmarekani wakati huna exports, hutaki majeshi yake, madini unagawa tu kwa makampuni bila shida, huna hata influence regionally, utaenda kuongea deal gani na Wamarekani wakati huna exports?
Tanzania haijui hata inafuata mfumo gani.Kwani Tanzania ni nchi ya kijamaa mpaka sasa? Umeona hoja zako jinsi hazina mashiko.
Why kwa Tz uangalie political historical backgroundna sio kwa Vietnam?
Deng Xiaoping alifanya mageuzi ya kibiashara na siyo ya kisiasa
Mbona Kenya ni taifa lisilofungamana na upande wowote mkuuRuto akisema hafungamani na upande wowote nitamuelewa, kwa sababu anacheza na Wachina, halafu anacheza na Wamarekani.
Ni lini China walibadilisha siasa zao wakati wa Deng Xiaoping mkuu?Tanzania haijui hata inafuata mfumo gani.
Vietnam wana viwanda, wana export processed goods, wanatengeneza nguo, viatu etc.
Sasa unaifananishaje Tanzania isiyo export processed goods na Vietnam?
Unasema Deng Xiaoping alifanya mageuzi ya biashara, si siasa. Ukisoma historia ya class struggle ni historia ya biashara, means of productions.
Biashara ni siasa, ndiyo maana mpaka sasa tunaongelea "diplomasia ya uchumi", usichoelewa nini?
Kwani wapi nimesema si taifa lisilofungamana na upande wowote?Mbona Kenya ni taifa lisilofungamana na upande wowote mkuu
Hata kwenye diplomasia za kiuchumi Tz ni kama Kenya tuKenya wanaelewa kutofungamana na upande wowote katika zama hizi za diplomasia ya uchumi. Tanzania hawajui.
Yule alikuwa wa hovyo kauli zake hazikuwa sawa na sera ya kimataifa ya Tanzania ni ujinga wake tuTulikuwa na rais aliyepiga sana kelele kuwasema vibaya mabeberu,