- Thread starter
-
- #21
Hapa wewe ndio inaonekana unapenda ushabiki.
1. Hakuna popote nilipoweka ushabiki. Zote nilizoweka ni facts kutokea kwenye quotes ambazo nimeziweka bayana.
2. Ni ku challenge hapa, onyesha mfano mmoja wa ushabiki au chochote ambacho sikuweka ushahidi!
3. Bila mfano hapa ulichoandika hapa ni kama kupaka rangi hewa tu!
Ushabiki umekuzuia kujadili kitu kwa mizani sawa.
1. Wapi sikujadili nini Kwa mizania sawa?
2. Bila mfano tuhuma Hii na ya pale juu hazina thamani yote.
Hata twende
Unaamini kuwa Hamas walivamia Israel na kuteka ama kuua kila waliyemkuta mbele yao?
1. HAMAS hawakuvamia Israel. Bali walivamia maeneo ya Palestina yanayokaliwa na Israeli.
2. Hapa ni sawa na wewe kumbamba mwizi wako. Labda kama wewe ungemuandalia karamu?!
Unajua kabla ya Oktoba 7 kulikuwa kuna mazungumzo ya kuwafanya palestinians kupata taifa lao?
1. Maeneo ya Palestina yanakaliwa tangia 1948.
2. Israel imekataa jitihada zote za majadiliano na Palestina na HAMAS.
3. Uko wapi ushahidi wako wa mazumgumzo yenye mwelekeo wowote wa maendeleo wakati Israel ikiendelea na ujenzi na kupanua maeneo ya uvamizi?!
Je njia waliyotumia Hamas kuvamia na kuuwa ilikuwa ndio njia pekee na sahihi kwa muda huo?
1. Njia zote za ukombozi zinapofungwa, ni halali kwa victim kutumia njia zozote kujikomboa ambapo hata armed struggle ni justifiable.
2. Maji maji, Mau mau, ANC na Apartheid, pia struggle za SWAPO, MPLA, ZANU PF, nk ni mfano wake.
Kama Maji Maji au Mau Mau ilikuwa halali, iweje lawama kwa wapalestina?
Je aliyevamiwa kikawaida alipaswa afanye nini?
1. Uko sahihi, umeuliza vyema kabisa.
2. Palestina aliyevamiwa tokea 1948, kikawaida ilikuwa afanye nini?
3. Zaidi sana ungejiuliza, kama wewe ukimfumania mwizi wako kwenye eneo lako akiendelea na yake ungemfanya nini?