Ukiishi kwa ndugu, rafiki, jirani zingatia haya

😂 kama masikhara hivi jibu jepesi ambalo linamuachia dogo maumivu mazito. Hapo juu kuna member anakwambia halafu baada ya bro kufariki unakuta shemeji anaanza kulalamika mnamtenga.
 
[emoji23] kama masikhara hivi jibu jepesi ambalo linamuachia dogo maumivu mazito. Hapo juu kuna member anakwambia halafu baada ya bro kufariki unakuta shemeji anaanza kulalamika mnamtenga.
[emoji1][emoji1] mambo wanatengeneza wao halafu wanakuja kulalamika wanatengwa
 
Jitahidi kwenda sawa na mama mjengo,unaamka asubuhi unasaidia kazi ndogondogo ndo unaanza shughuli zako za kuingia zoom,siyo unaamka tu hujasafisha hata choo unaingia zoom, utsfurushwa mapema,unafgia uwanja unatoatoa majani,kama maji ni ya kuchota basi unachota,unasafisha bafu,wafanye watoto wakupendw kwa kuwasaidia homework,unawahimiza shule,unawafundisha fundisha,jitahidi kila unapoamka unafanya jukumu walau moja la kifamilia kama miongoni mwa niliyoyataja ndo uanze harakati zako,na ukitaka hela za nauli ongea na mama mjengo kwanza,hapo hata ukisema unataka kuhama watakuzuia,
 
Mkuu hapa anazungumziwa mgeni ambaye ameenda kuangalia life linaendaje eneo hilo sio mgeni ambaye ameenda mapumziko ya kikazi 😂.

Mchele kilo tano na nyama kilo tatu kama ndio zinapima "ustaarabu" wa mgeni mbona kama ni kumbebesha mzigo hustler. Upo sahihi lakini kwa kiasi kikubwa ingawa pia baadhi ya familia kushiriki chakula ni muhimu sana. Mfano mama angu ni lazima ushiriki mezani la sivyo uwe na sababu maalum.
 
Hili ni kosa. Ndo hapo nnaposema mwanaume unahitaji hekima kudeal na mambo ya nyumbani kwako. Kama umeona kosa lazma uchunguze shida iko wapi na udeal nayo kiume. Kama n mke wako, deal nae maana hajakupanda kichwani, vivyo hivuo kwa mdogo wako.
Muhimu hakuna anaepata free pass ya kufanya anavotaka
 
Hapa nakuelewa. I think watu wengi hawajaelewA msimamo wangu. Simaanishi kwamba mke afanye anachotaka kwenye mji, hapana! Issue yangu ni kwamba, ndani kuna utaratibu na huo utaratibu utatakiwa ufuatwe. Na pia haimaanishi mke anapokosea asionywe, la hasha hata yeye rungu linamkuta.
What im saying ni kua, nyumba haitakiwi kuendeshwa kwa madharau from pande zote. Ukiona wawili wanshindwana ni jukumu lako kama mwanume kufanya ucchunguzi na kudeal logically na tatizo lililopo. Kama ni mke, akutane na vyake, kama ni ndugu na yeye pia.
Ninachiendelea kukataa ni madharau.!
Na pia ndugu, kama umeamua kuoa lazma umemchunguza mwenza wako na mapungufu yake unayajua, na kama umekubali kuendana nayo sidhani kama unashindwa kudeal nayo
 
Hapana usijali, mimi mwenyewe sikupendezwa na vitendo alivyonisimulia Mimi nimemsaidia kuona aibu.ni tabia mbaya kwa kweli Mambo madogo yanaanzaga hivihivi mwishowe bifu kali
 
Hapa tumeelewana chief na hiyo ndio concern yangu usiwepo upande ambao umejihesabia haki. Mpaka/utaratibu ni muhimu kwenye hii case, Mme asimame kama mme na kiongozi wa familia, Mke asimame kama mke na mtekelezaji wa miongozo toka kwa mme hivyo hivyo mgeni asimame kama mgeni na afuate taratibu za wenyeji.
 
Yeye kwa madai yake ndugu za mumewe pale hawamthamini wanamchukulia Kama Kaka Yao ndio kila kitu na yeye Ni nothing,Sasa anadai atapambana nao bega kwa bega wapunguze Uhuru,eti Uhuru umezidi..huyo mgeni eti alivyofika siku mbili tatu akaenda kwenye shoe rank akaanza kuchafua viatu vya braza akajichagulie,,,Sasa bibie kamaind
 
Hapana usijali, mimi mwenyewe sikupendezwa na vitendo alivyonisimulia Mimi nimemsaidia kuona aibu.ni tabia mbaya kwa kweli Mambo madogo yanaanzaga hivihivi mwishowe bifu kali
Hakika tuko pamoja na uendelee kumrekebisha anavyokosea na kumpongeza anavyopatia.
 
Daah kweli hatari sasa dogo anachukua viatu vya Braza na Braza wala hana noma ha mind wala nini sasa shida iko wapi hapo

. viatu ni vitu vidogo sana na si vya kwake huyo ni mchoyo
 
Naam naam naaam. Hii ndo sawa.
Familia lazma ikae iweke muongozo kwenye kila kitu. Hapo mdo kutakua na amani na maendeleo. Na kila upande ukisimamia eneo lake kutakua hakuna muingiliano wa majukumu na amani itatawala.
 
Mambo ya kusemana vyakula ni umaskini tu, usukumani kwetu njoo utakunywa maziwa yakutosha utakula nyama zakutosha utakula wali wa kutosha alaf hakuna anae jali. Ukiwa unaondoka unapimiwa na debe kadhaa za mpunga. Ujanja ujanja ndio kitu pekee hatutaki baki nao huko huko kwenu
 
Haya yote mnayasema tu! Matoto ya siku hizi ni kama majinga fulani hivi! Hayawezi kujituma tena yanataka yaishi kama yalivyokuwa yanaishi kijijini! Hizo ni ng'ombe zikae huko huko kijijini!
Mkuu kwa hii comment utakua na roho mbaya sana, mchoyo na mkatili.
 
Hapa mada inaongelea kama mtu anatafuta maisha na hana njia nyingine zaidi ya kuishi au kufikia kwa ndugu. Unafikiri kuna anaependa kukaa kwa ndugu?
 
Hapo kwa kina Junior ndio penyewe na pagumu sana. Junia anaweza kukulamba kofi bila sababu halafu unajikuta unapaniki na kumpa 👊 ya kichwa!
 
Ukiona watu wengi wanalalamikia wageni ujuwe wapo maeneo ambayo hayazalishi vyakula. Ni ngumu kusikia mtu wa Mwanza,Mbeya,Moro au Iringa analalamika.

Kwa Dar ni sahihi kabisa maana hao bei ya mlo mmoja kwa familia ya watu 4-6 inaweza kuwa ya siku 1 au 2 kwa Mbeya,Iringa au Mwanza.
 
Kuwa mwema - jua mipaka yako, wajibika, watendee kwa haki.

Usitake sana kutendewa haki, siyo kwenu hapo na upo kwa muda tu.

Jitambue.
 
Ni kujiongeza tu kwa kile kinachowezekana hata kama kujiongeza kwako hakutaonekana we jitahidi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…