Ukikutana na Engineer yeyote hana kazi, mchongo wala ramani yoyote ya maisha tafadhali mpige makofi

Ukikutana na Engineer yeyote hana kazi, mchongo wala ramani yoyote ya maisha tafadhali mpige makofi

Yaani mtu mwenye uwezo wa kutoboa mlima kati kati akapitisha daraja hajui afanye mishe gami anakuja kutuuliza sisi hapa jukwaani kweli,
Haya ni matumizi mabaya ya akili,

Tuacheni sisi tuliosoma bachelor of chinese na political science tuteseke mtaani ila sio hawa viumbe
unajua ni kwanini iliwezekana kujenga hayo madaraja na barabara zinazokushangaza !?
Yes ni kwasababu walikua na resources zote zinazohitajika ili kukamilisha mradi husika . haya ilete hiyo kampuni kubwa inyime resources zinazotakiwa ili kufanikisha mradi husika then mwambie afanye huo mradi kama atafanikisha .
kwahiyo bwana mdogo sio kwamba engineers hawana ideas,lakini je resources za kuleta hiyo idea into reality zipo!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahhah mama,hadi umepiga picha halafu ni basic math tena “C” ,nilidhani C ya advanced math kumbe Basic poor you,usiwanange sasa maengineer bongo
Umeona ulivyo mjinga hujui hata kusoma, hiyo ni Basic mathematics???? Hebu soma tena
 
Una uhakika gani kuwa nilifeli hesabu? Kwa taarifa yako hesabu hazikuwahi kunishinda na Advance nilisoma PURE MATHEMATICS kama mbadala wa BAM, siku nyingine uwe na adabu mkuu.

Watu waliosoma Advanced math hawana mawazo finyu kama yako hayo,nawasiwasi hata kama a level ulisoma hesabu
 
Kati ya watu wanaofikiria kwa kutumia mattercall mtoa uzi ni mmojawapo!!
 
Watu waliosoma Advanced math hawana mawazo finyu kama yako hayo,nawasiwasi hata kama a level ulisoma hesabu
Nimeanza kuamini inawezekana kweli kuna ma ingineer wa mwendokasi
 
Kati ya watu wanaofikiria mattercall mtoa uzi ni mmojawapo!!
Sawa mr engineer ahsante kwa mchango wako ila nikikutana na wewe rejea kichwa cha habari
 
Mkuu nakuunga mkono, Engineer kukosa kazi ni uzembe wa hali ya juu maana mazingira yetu ya kiafrika bado fursa za Kihandisi ziko nyingi sana.
Vijana wengi wanakosa ubunifu wa kuanzisha jambo jipya,
Engineer kukosa pesa ni uzembe na upumbavu mkubwa sana maana akitumia knowledge kwa 20% atafanikiwa tu.
 
Ok sawa mkuu ahsante kwa mchango wako kiufupi hii mada ipo nje ya uwezo wako.

Ahsante?


Ila usiwaonee wivu maengineer kwasababu kichwa chako hakikufit kuchukua hiyo course,swala la kuwadharau watu kisa unaweza kupata chai na chakula cha mchana hapo kwa shemeji yako sio vizuri.Changamoto za nchi yetu na uchumi vinajulikana
 
Kazi ni ngumu siku hizi.
Sio Engineers wote wana kazi.
Kazi nyingi siku hizi zinafanywa kwa force account kutumia mafundi /technicians.

Miradi mikubwa wanapewa wenye nyenzo na mitaji mikubwa, hawa at least wanaajiri Graduates /Engineers kwa Uchache.

Sekta Binafsi inayojiri % kubwa ya wataalamu wa kada za majenzi ni kama vile iko ICU miradi mikubwa ya kawaida ya Serikali imeelekezwa kwa TBA (Ushauri na Usimamizi),Suma wao wanajenga.
Kampuni nyingi za ujenzi/ushauri zilizokuwa zinafundisha na kuajili wataalamu zimefungwa/suspended.

Achilia mbali kazi za Kiserikali huku sekta binafsi wenye kazi nyingi ambao wengi walikuwa ni wafanyabiashara wali/wamefunga biashara zao sababu ya Task Force iliyokuwepo na still bado hali haijatengemaa.

Kuna Tatizo kubwa la Ajira kwa kada ya Uhandisi,Usanifu na Ukadiliaji Majenzi.

Suluhisho :Sheria na kanuni zilizounda body za CRB, AQRB, ERB pamoja na PPRA, BLERA na TRA zipitiwe upya au zitumike ipasavyo ili kuondoa simtofahamu iliyopo ili kulinda taaluma na kuondoa utaratibu wa Serikali kufanya kazi zake yenyewe kwa kutumia local fundi.
Mkuu hongera sana, angalau wewe umetufungua akili kidogo wengine walikuwa wana react tu hawajibu chochote kwa hoja
 
Back
Top Bottom