Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Kwanza namshukuru sana Mungu kwa neema yake nimekuwa miongoni mwa binadamu ambao wameanza maisha rasmi,kwa ile maana maisha yanaanza ukiwa na miaka 40,kwani niko katika 40's
Nimegundua au kuyasikia mambo kadhaa ambayo pale mwanadamu anapo mdhihaki Mungu hadharani basi hakika majibu huja mapema mno
Mtengenezaji wa meli ya Titanic,kwa uhodari na tekinolojia waliyotumia kutengeneza,waliamini ni meli bora sana ambayo isingewaza kuzama,alipoulizwa umadhubuti wa meli hiyo na waandishi wa habari,alisema ni meli imara na bora sana hata Mungu hawezi kuizamisha.
Kilichotokea nadhani wote tunakijua,imebaki historia tu na watu wanapambana kila kukicha kwenda kuchunguza mabaki yake
Kuna kipindi kilichopita wakati wa kampeni uchaguzi mkuu kati ya marehemu Magufuli na marehemu Lowasa akiwa upinzani,mwanasiasa maarufu mama Serina Kombani alisema Lowasa atakufa mda si mrefu kwa kuwa ni mgonjwa
Lakini kilichotokea nadhani wote tunakijua,alitangulia kufa yeye kwanza nadhani hazikupita wiki au moja akatungalia mbele ya haki
Kuna binti mmoja alikuwa anaenda matembezi au kwenda mji mwingine na gari yake,sikumbuki vizuri ni kama aliambiwa na mama yake amuombe Mungu afike salama,lakini alidhihaki,na nyuma ya gari kulikuwa na mayai,alipata ajali mbaya sana,lkn cha kushangaza hakuna hata yai moja lililo vunjika
Kuna binti mmoja nadhani kama sio Chanika basi mbagala ni mwaka jana tu,aliambiwa na mama yake,uswali swala ya isha kabla hujalala ni mida ya saa mbili usiku,akamjibu mama yake kama unaona kuswali ni muhimu basi swali wewe na Allah wako kilichotokea usiku huo hakuamka tena
Wasomaji wangu Mungu wetu ni mkubwa mno ni mwenye kusikia na kuona kila kitu,kuwa makini sana matamshi yako kwani hakika yeye halali wala hasinzii,anajua yaliyomo kizani na kwenye mwanga
NI hayo tu!