Ukimsaidia Mbongo jambo au fedha, kila tatizo atataka umsaidie tena. Hii ni ishara ya Low IQ

Sahihi mkuu, wabongo wengi tuna unafiki na hatuna ujasiri wa kusema "Hapana" "Sina" "Siwezi"
Matokeo yake tunaishia kuishi kwa kunung'unika
 
Siku nikifanikiwa kwenye hili nahisi nitatoboa... Nimejitahidi sana hapo kwenye ndugu lakini sijaona matunda hata kidogo zaidi nipo vile vile.
 
Huu uzi utafikiri wachangiaji wake, wote ni wazungu au wa mataifa mengine coz kila mtu anawaponda wabongo.

😀😀
Uzungu sio ngozi, ni itikadi tu na namna ya kuendesha maisha. Ukiendesha maisha kibepari we ni mzungu. Mzungu anajua mipaka ya msaada na haogopi kusema hawezi. We uchukie usichukie utajua mwenyewe.
 
Inaelekea wewe tu ni zwazwa, Mtanzania ni mtu wa kumsaidia kweli jamani? Matatizo mengine haya mnajitakia wenyewe jamani.
 
Uzungu sio ngozi ni itikadi tu na namna ya kuendesha maisha. Ukiendesha maisha kibepari we ni mzungu. Mzungu anajua mipaka ya msaada na haogopi kusema hawezi. We uchukie usichukie utajua mwenyewe.
Yani hiyo itikadi ndio inaitwa Uzungu?
Vipi kuhusu mtu ambaye yeye haendeshi maisha yake kwa hizo itikadi,yeye ataitwaje? ataitwa kwa kutumia race gani ambayo ni opposite na hiyo uzungu.
 
Yani hiyo itikadi ndio inaitwa Uzungu?
Vipi kuhusu mtu ambaye yeye haendeshi maisha yake kwa hizo itikadi,yeye ataitwaje? ataitwa kwa kutumia race gani ambayo ni opposite na hiyo uzungu.
Mkomunisti au mjamaa kama alivyokuwa Mwasisi wa taifa hili😂! Hio ndio namna ya wabongo wengi ya kuishi. Tunategemea misaada zaidi kutoka katika ngazi ya familia hadi taifa. Tumelemaa
 
Uzungu sio ngozi, ni itikadi tu na namna ya kuendesha maisha. Ukiendesha maisha kibepari we ni mzungu. Mzungu anajua mipaka ya msaada na haogopi kusema hawezi. We uchukie usichukie utajua mwenyewe.
Naam, uzungu ni Kama sera au iti kadi ya mtu.

Neno hili hali maanishi uzungu wa sura, ila itikadi na mwenendo ulio katika mstari.

mfano, uki wahi kwenye kikao au sehemu yoyote, huo ni uzungu.

kuto kuwa na roho ya korosho kwa masela, kisa pisi. Huo nao ni uzungu.
Neno la misimu hili.
 
Eeh na linatumika sana hilo.

Ukisikia boss wangu mzungu sana, ujue huyo boss kutoa tip ni kawaida na habanii watu kwenye haki na maslahi yao.

Kinyume na hapo boss ni mkoloni.
 
Bro umenena ,hii ni kweli kabisa ukimsaidiq mtu next time tena anarudi kwako.

Chakufanya, uwe hueleweki ukimsaidia next time anakuja sema hauko vizuri.

Mininamfano mzuri, kuna dada aliniomba nimsaidie hela, nikampa, ikawa kila mwisho wa mwezi tarehe za 20s ananiomba kiasi kile kile ,ikabidi niwe nampa miezi mingine simpi saiv kashaacha huo ujinga
 
Eti kaka angu sijui nitakula nini[emoji23]
 
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu ?
By Mzilankende
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…