Ukimsaidia Mbongo jambo au fedha, kila tatizo atataka umsaidie tena. Hii ni ishara ya Low IQ

Mkuu hiyo sio elimu ya pesa Ila ni utegemezi na udhembe uliokithiri. Mtu anaweza kuwa hana nidhamu ya pesa lakini akadeal na matatizo yake pasipo kutaraji mtu mwingine amtatulie
Hivi hamna jinsi ya kuweka hili somo darasani maana hakika umaskini wetu umeanzia hapa na hata ukijaribu kugusia hili UTAONA jinsi utachambwa mara mchoyo mara roho mbaya ila ukweli ni janga la taifa.
 
Hivi utaendaje wakati ni ndg zako mfano Mimi nilikuwa na ndg yangu yeye ni mlevi nikamtafutia kazi hela haweki ni kulewea tu kodi anataka nimlipie. Siku moja akafungiwa nje usiku saa nne anakuja kwangu hapo Kuna ndg wengine wawili . Nikaanglia nikawaambia kamwandalieni chumba cha nje huko yaani ndio akawa amefika hakuondoka tena story ni ndefu ila alikaa miaka kama 2 nikawa nimezuia mshahara wake nikamjengea room 3.

Wanakera sana aisee alafu hizo lawama sasa
 
Kazini kuna kazi. Kama upo kwenye nafasi ya kumsaidia mtu hata mara 100 usichoke wala usilete makasiriko mkuu. Jitahidi umsaidie kadiri ya uwezo wako na pale ambapo haiwezekani mwambie ukweli ili asiendelee kutegemea msaada wako.

Huwezi jua kuna watu hawafanikiwi mpaka wapitie kwa mtu fulani na si kila mtu. Yawezekana huyo brother hana mwingine wa kumsaidia matatizo yake zaidi yako wewe. Dunia duara mkuu wangu. Chonde chonde usikate tamaa yawezekana barka zako zinatoka hapo unapotoa msaada.
 
Mkomunisti au mjamaa kama alivyokuwa Mwasisi wa taifa hili😂! Hio ndio namna ya wabongo wengi ya kuishi. Tunategemea misaada zaidi kutoka katika ngazi ya familia hadi taifa. Tumelemaa
Too much katika jambo lolote lile sio kitu kuzuri hata kidogo. Iwe kwenye kuomba msaada au kunywa beers..
 

kama una uwezo wa kumsaidia mtu, msaidie tu. maisha haya ni ya kupitia. Na fedha na kila kitu tutakiacha hapahapa duniani. Tuliikuja watupu na tutaondoka watupu.
 
Tuangalieni nyumba zetuwatu wanaokwenda kazini na watu wanaolala je tunafanana jibu utalo pata ndio utajua.
 
Kweli kabisa
 
Eeh na linatumika sana hilo.

Ukisikia boss wangu mzungu sana, ujue huyo boss kutoa tip ni kawaida na habanii watu kwenye haki na maslahi yao.

Kinyume na hapo boss ni mkoloni.
huwa tuna waita roho ya korosho au beberu la kihindi.

Mpambania ma deal au haki, tuna kuita samaki shujaa😄😄
 
Hizi ndio comment za great thinker sasa.....
 
Kwani kukataaa unaona Nini??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…