Ukimuua huyu nyoka kama wewe ni mchimbaji fukia hilo duara rudi kijijijini ukalime

Ukimuua huyu nyoka kama wewe ni mchimbaji fukia hilo duara rudi kijijijini ukalime

Nani mshenzi?

Na wachimbaji gani unaowazungumzia? Hao wanaozurura kila pahala?

Na unaelewa mambo ya kiroho wewe? Au umeanzisha mada kuonyesha jinsi unaamini vitu usivyoweza kuvielezea?

Sasa nakuuliza elezea uhusiano uliopo baina ya huyo nyoka na madini, na nikuelewe, sio kuleta bla bla...
Kama haujui hata dhahabu inafananaje nawezaje kukuelezea vitu ambavyo umeshaweka negativity
 
Kwanini kamuua halafu anawashauri nyie msimuue mnaamin
Huyo nyoka aliemuua alipewa elimu mara ya pili hawezi kurudia hio shimo halitoi kitu niempty kbs mpk sasa
 
Ushirikina wa sisi watanzania. Kila kitu tunakihusisha ma mazingaombwe. Ingekuwa kama ndio hivyo, Barrick na wengine wasingechimba dhahabu.

Maana kuna waliofikia nyoka kama hao na vinginevyo
We umeshawahi kufanya kazi kwenye migodi ya Barrick? Katika kitu ni marufuku kuua ni nyoka pamoja na mnyama yoyote utakaemuona eneo la mgodi huwa hawaui, kuna wataalam wapo kwaajili ya ku deal na hivyo viumbe kuviondoa vikiwa hai.
 
Ujinga bado ni janga namba moja la taifa. Watu bado wajinga sana, akili zao bado zipo stone age.
 
We umeshawahi kufanya kazi kwenye migodi ya Barrick? Katika kitu ni marufuku kuua ni nyoka pamoja na mnyama yoyote utakaemuona eneo la mgodi huwa hawaui, kuna wataalam wapo kwaajili ya ku deal na hivyo viumbe kuviondoa vikiwa hai.

Ujinga bado ni janga namba moja la taifa. Watu bado wajinga sana, akili zao bado zipo stone age.
Wewe ndio mjinga ulireply uzi bila kuitwa, kama hujui mambo ya mgodini pita ivi
 
Hawa nyoka wako wengi tu patamela forest reserve na nimewaua sana tu!.... Acha kupotosha!

Hii post yako iko kibiashara kimkakati sana kwa wachimbaji waaminio haya mambo ili wakutafute.
 
Hawa nyoka wako wengi tu patamela forest reserve na nimewaua sana tu!.... Acha kupotosha!

Hii post yako iko kibiashara kimkakati sana kwa wachimbaji waaminio haya mambo ili wakutafute.
Swali, wewe ni mchimbaji??
 
Mhhh, umesemaje eti mleta mada?

Kwamba nyoka asiuwawe?

Wewe ulikubaliana wapi na huyo nyoka kuwa atakuja au ulimpa lini mualiko kuwa atembelee shimo lako?

Nachotaka kusema hapa ni kuwa unapotosha watu...

Nyoka anaweza akawa nyoka wa kawaida na anaweza akawa wa kiroho, na nyoka huyo ikiwa amekuja kwa maagano uliyowekeana wewe na huyo nyoka hicho ulichokizungumza ndio kinawezekana, la sivyo uko hapa kupotosha watu...

Nyoka ni kifaa cha kiroho ukiachana na anavyofahamika kikawaida, kwa hhiyo ujio wake hauingiliani na shimo ikiwa (hakualikwa)!
Msiwe wabishi mimi nimeenda kwenye machimbo ya dhahabu migodi mikubwa ya Barrick ikiwepo Bulyanhulu pamoja na machimbo madogo ya dhahabu mengi yaliyopo wilaya ya Kahama na Geita pia.

Ni kweli huwa wachimbaji wanaimani hiyo na nyoka huwa hauliwi migodini ukitaka ufukuzwe kwenye machimbo basi uwa nyoka watu wakuone utafukuzwa hapo wanaamini umeleta mkosi na madini hayatapatikana kwahiyo ni marufuku kuua nyoka.

Kwa mzungu Barrick yeye pia ni marufuku kuua kiumbe hai chochote ikiwepo nyoka na nyoka wapo wengi sana hasa hawa Puff adder (kifutu) na ukimuona huruhusiwi kumuua unatakiwa uite wataalam wa kuja kumkamata kumuhamisha akiwa hai, ukiua unaweza kufukuzwa kazi
 
Huyu nyoka ni adimu sana kuonekana hua ni nyoka wa kukulitea bahati kama akiwa duarani basi usimpige muache ataondoka mwenyewe ila akitoka duara hilo litatema mali kama nini utapata gramu za kutosha kabisa.
Mara nyingi hupatikana maeneo ya mgodini narudia huyu nyoka hua ni baraka kubwa na ukimuona mara moja hutokuja tena kumuona kamwe.
Onyo: kuna watu wanajifanya wachaMungu sana ikumbukwe kbl ya babu zetu kuvamiwa na wakoloni walikuwa na imani zao na zilikuwa zinawasaidia kwenye mishe zao.
Mwisho: kila kitu kinautarabu wake, nimezaliwa machimboni nimekulia machimboni sibahatishi.View attachment 3446236
Tayari nimeshamuona hapa nina bahati aisehh
 
Back
Top Bottom