Ukimya wa Baraza la Maaskofu TEC juu Paroko na Mauaji ya Albino unaashiria nini?

Sijaleta ufafanuzi wowote hapo kiongozi. Na zaidi ya yote awe ni paroko au asiwe paroko, shehe au asiwe shehe kwangu mimi siyo issue ya kulumbania maana najua karibia binadamu wote tumechafukwa na muda wowote tunaweza kufanya chochote na watu wakabaki midomo wazi.
 
Wanafanya utafiti wa hizi tuhuma am sure hawawezi kuwa wamekaa kimya kwa maana ya kwamba kwa sasa hakuna wanachofanya.

Lazima huyo paroko wanamfuatilia na kucheki mambo mengi ili wajiridhishe ndio wanaweza kutoa taarifa rasmi japo kumbuka hata kumekuwa na shutuma dhidi ya mapadre kutia mimba na kubaka pamoja na kulawiti lakini waliona haina haja ya kujitetea sana sababu utaratibu wa kanisa ni kwamba ukiwa na hizi tuhuma wao wanakusimamisha utumishi mpaka itakapodhihirika vinginevyo na ikidhihirika ni kweli basi unatimuliwa.

So unaona kwamba kwa utaratibu wa kanisa hakuna haja ya kujitetea sababu hayo ni matendo binafsi ya mtu. .
 
Unataka TEC waingilie upelelezi wa polisi? Wacha sheria ichukue mkondo wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…