Ukiona dalili hizi, ujue tayari kuna mtu ameishamuiba mke wako!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
01. Angalia mabadiliko ya haraka kwa mkeo: Kila wikiendi jioni, anavaa vizuri na kuondoka nyumbani. Ukimuuliza anasema: "Kinamama tuna maombi ya kufunga na kuomba mwezi mzima kanisani, ntarudi baada ya masaa mawili." Tambua anaenda kufunga ndoa nyingine!

02. Chunguza matumizi ya perfume: Mke wako alikuwa hajui tofauti ya Rexona na Chanel No. 5, lakini siku hizi anapulizia harufu za kifalme hadi mbwa mtaani wanamsindikiza. Shtuka, kuna mtu lazima anamsaidia kuzinunua!

03. Simu yake janja akiiacha chumbani, akaenda jikoni, iguse hiyo simu. Ukiigusa tu, inalia alarm kama bomu la nuclear kutoka Iran na kumshtua. Anakuja mbio maana hapendi mtu mwingine aiguse, kwa kuwa ameficha picha zake za siri na bwana arusi wake mpya! Na kuifungua simu hiyo huwezi kwa sababu password yake inachunguza kwanza DNA!

04. Kwa muda wa miezi mitatu hajakuomba hela ya kusuka nywele. Badala yake anasema, “Ah siku hizi nimetulia, sihangaiki na mambo ya dunia, yanapita.” Hapo ujue kuna mtu mwingine anatuliza moyo wake kwa mapesa.

Sikiliza ndugu yangu, wewe unayeiba wake za watu kwa mbinu yoyote ile. Hata kama hatukuoni, tambua kuwa macho ya Mungu yanakuona popote pale ulipo. Hata ukijificha kwenye bomb shelters kama za Waisraeli, Mungu anakuona hukohuko mafichoni. Tubu dhambi haraka vinginevyo adhabu ya moto wa milele inakusubiri, kwa sababu ya wizi na uzinzi wako.

Wewe pia mke unayechepuka, huna udhuru. Uzinzi ni uzinzi tu hata kama unaupaka mafuta na kuuita: "mapenzi au mahusiano." Tubu, Yesu yuaja upesi.

"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.." (1 Wakorintho 6:9-10)
 
Inasikitisha sana
FB_IMG_17486260138529094.jpg
 
Mbususu ni mali yake acha ampe amtakaye aichakate
 
Muhimu zaidi zingatia maisha yako na watoto wako kushughulika na mtu mzima ni kujipa stress.
Ye hata akiibiwa haijaibiwa roho yako.
 
Wapo wanamke wanaliwa na chembe ya dalili hawoneshi...

Ukiona mwanamke anaonesha dalili ujue kachoka kuwa na mwanaume aliyenaye, na anafanya makusudi kuumiza hisia za mwanaume...
 
Bila ushahidi huo ni uchonganishi
Uko sawa mkuu, ushahidi ni muhimu. Lakini hakuna jambo jipya chini ya jua. Mbinu za michepuko ni marudio tu. Hivyo ukiona dalili kama hizo, kumbuka: "lisemwalo lipo. Kama halipo, laja." Ila usihukumu bila ushahidi. Ukipiga, ukiua, jehanam inakuhusu.
 
Back
Top Bottom