Barakoa 001
JF-Expert Member
- Apr 5, 2014
- 5,436
- 14,927
Witch doctor told me
Nauliza hiyo namba tatu program ya kutegeshea bomu01. Angalia mabadiliko ya haraka kwa mkeo: Kila wikiendi jioni, anavaa vizuri na kuondoka nyumbani. Ukimuuliza anasema: "Kinamama tuna maombi ya kufunga na kuomba mwezi mzima kanisani, ntarudi baada ya masaa mawili." Tambua anaenda kufunga ndoa nyingine!
02. Chunguza matumizi ya perfume: Mke wako alikuwa hajui tofauti ya Rexona na Chanel No. 5, lakini siku hizi anapulizia harufu za kifalme hadi mbwa mtaani wanamsindikiza. Shtuka, kuna mtu lazima anamsaidia kuzinunua!
03. Simu yake janja akiiacha chumbani, akaenda jikoni, iguse hiyo simu. Ukiigusa tu, inalia alarm kama bomu la nuclear kutoka Iran na kumshtua. Anakuja mbio maana hapendi mtu mwingine aiguse, kwa kuwa ameficha picha zake za siri na bwana arusi wake mpya! Na kuifungua simu hiyo huwezi kwa sababu password yake inachunguza kwanza DNA!
04. Kwa muda wa miezi mitatu hajakuomba hela ya kusuka nywele. Badala yake anasema, “Ah siku hizi nimetulia, sihangaiki na mambo ya dunia, yanapita.” Hapo ujue kuna mtu mwingine anatuliza moyo wake kwa mapesa.
Sikiliza ndugu yangu, wewe unayeiba wake za watu kwa mbinu yoyote ile. Hata kama hatukuoni, tambua kuwa macho ya Mungu yanakuona popote pale ulipo. Hata ukijificha kwenye bomb shelters kama za Waisraeli, Mungu anakuona hukohuko mafichoni. Tubu dhambi haraka vinginevyo adhabu ya moto wa milele inakusubiri, kwa sababu ya wizi na uzinzi wako.
Wewe pia mke unayechepuka, huna udhuru. Uzinzi ni uzinzi tu hata kama unaupaka mafuta na kuuita: "mapenzi au mahusiano." Tubu, Yesu yuaja upesi.
"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.." (1 Wakorintho 6:9-10)
Asante Certified HaterDalili za kutukumbusha zingebaki za kurudi kwa Kristo wa Nazareth tu, hizi zingine hazitusaidii we kwa akili yako Unaamini mtu mzima anaibiwa?
Kiboko ya Scott Adkins 😅😅😅Have you given yourself a gift this week?
Samahani madam, hivi ukiwa na mbwa kisha huyo mbwa akahamia kwa jirani, ni jirani ndo mwizi au mbwa wako ndo kahama. Mana suala la mwanamke kuhamisha hisia zake mwenyewe unasemaje kaibiwa?Asante Certified Hater
Dah, ila jina lako hilo. Certified Hater?
Anyway, ngoja nijibu hoja yako. Kuiba ni kuchukua kitu ambacho sio mali yako. Mke wako ni wa kwako tu. Sasa kama mke wako amehamishia hisia zake kwa mume mwingine, hajaibiwa tu hapo?
Hata hivyo uzi huu bado unatukumbusha umuhimu wa kutubu dhambi kabla ya ujio wa Yesu Kristo, kwakuwa Yesu atakaporudi atawachukua watakatifu tu. Wazinzi wataachwa na kubaki kwenye dhiki kuu.
Asante Smooth CriminalSamahani madam, hivi ukiwa na mbwa kisha huyo mbwa akahamia kwa jirani, ni jirani ndo mwizi au mbwa wako ndo kahama. Mana suala la mwanamke kuhamisha hisia zake mwenyewe unasemaje kaibiwa?
Ukiishi maisha yako bila kujipa ya mwingine uta-enjoy sana
Kwahyo nihangaike kumpa nyama nyingi ili asihame? Mbwa anayejua ni wako hata apewe nyama nyingi kiasi gani hawezi kuhama kisa nyama za njeAsante Smooth Criminal
Duh, ila na wewe jina lako linatisha bwana! Smooth Criminal?
Sawa, usijali. Ni chaguo lako!
Hebu jiiulize kilichomfanya mbwa wako akahamia kwa jirani ni nini? Ni wazi kwa jirani anapewa nyama nyingi. Huyo mbwa kama angekuwa anafukuzwa akifika tu kwa jirani angehamia? Hivyo jirani ni mwizi kwa sababu amemshawishi mbwa wako ahamie kwake kwa kumpa nyama nyingi. Hapo vipi?
Umesema Kuiba ni kuchukua kitu sawa sawa. Sasa binadamu ni kitu?Asante Certified Hater
Dah, ila jina lako hilo. Certified Hater?
Anyway, ngoja nijibu hoja yako. Kuiba ni kuchukua kitu ambacho sio mali yako. Mke wako ni wa kwako tu. Sasa kama mke wako amehamishia hisia zake kwa mume mwingine, hajaibiwa tu hapo?
Hata hivyo uzi huu bado unatukumbusha umuhimu wa kutubu dhambi kabla ya ujio wa Yesu Kristo, kwakuwa Yesu atakaporudi atawachukua watakatifu tu. Wazinzi wataachwa na kubaki kwenye dhiki kuu.