Ukiona unapitia dalili hizi katika maisha, jua kuwa Mungu anakupeleka next level ya maisha yako

Ukiona unapitia dalili hizi katika maisha, jua kuwa Mungu anakupeleka next level ya maisha yako

Next level nini, ni kiwango ambacho Mungu anakuinua kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine yenye ukubwa na mamlaka.

Je ni watu gani Mungu uwainua kuwapeleka next level ya maisha?

Wanaitwa choosen one au black sheep wa family, Mungu uwainua watu hao hili kuvunja generation curse au pattern(vifungo vya ukoo au family mfano mila fulani ambazo ni kinyume na Mungu, belief, limitation za kifamilia kama elimu, biashara, kazi, n.k


Ukiona unapitia hatua hizi katika maisha yako basi Mungu anataka kukupeleka kwenye next level(born to greatness)

Preparation(Maandalizi)
Hapa unapitia vitu kama hivi
-rejection(mfano kukosa ajira kila ukijaribu kuomba, hiyo ni direction ya Mungu kukupeleka kwenye kusudi lako la Maisha
-betray(kusalitiwa na watu wengi)
-hali ngumu sana ya kimaisha tofauti na wengine
-kukataliwa toka utoto
-kupoteza kazi


Isolation(Mungu kukufundisha kumtegemea yeye pekee)
Hizi ndio dalili
-kupoteza interest ya vitu ulivyokuwa unavipenda zamani mfano gossip issue
-kuwa na interest na mambo ya Mungu
-kupoteza marafiki wa zamani, uhusiano wa zamani kuondoka bila sababu yoyote
-kupoteza ndoto zako zamani
-kupoteza kazi, biashara
-kupoteza pesa
-kupenda kuwa peke yako
-watu kutokuelewa hiwe family, friend
-kupata favor
-kupata heshima


Testing(Mungu kukujaribu)
-Hapa Mungu anakupima imani yako kupitia changamoto mbalimbali(heavy)

Elevation
Hapa Mungu anakuinua ili uishi kwenye kusudi lako maishani

Ukiona unapitia nyakati ngumu sana maishani kama betray, rejection, loss, tofauti na changamoto za watu wengine jua Mungu anataka kukuinua kwa purpose kubwa maishani mwako usikate tamaa.

Dhahabu kabla aijatengeneza kitu cha thamani uwa inapitia kwenye moto mkali , Usikate tamaa ushindi wako upo karibu.
Naomba nikusaidie kufupisha.

ILI MBEGU IOTE LAZIMA IOZE
 
Infro hebu tuache tupumue walau mara moja kwa mwezi😤
Hili ni jukwaa huru la kila mtu.

Mtu akitaka aachwe apumue, labda asije Jamii forum.

Lakini ukija Jamii Forums, Tambua kwamba umekuja kwenye Public forum. Utakutana na chochote hata usichokipenda.
 
Sidhani kama Mungu angekua anainua watu 70% ya Tanzania ingekuwa masikini.
Exactly.

If prayers really work Africa would be the richest continent in the world.

If prayers really work, Africans would be the richest people on earth.

Lakini  Kiko wapiiiiii?

Waafrika wanao ongoza kukesha makanisani na misikitini ndio maskini choka mbaya, mafukara, makabwela, hohe hae, Pangu pakavu tia mchuzii.
 
Kinyume chake pia ni kwamba unaweza pitia magumu Hadi unakufa,...No gain no pain, No discipline no results, No risk no rewards, Kipindi uko na Imani na mungu hakikisha unakomaa Sana, tena Sana siyo kidogo yaani namaanisha ninaposema kukomaa lazima uwe fit physically na Mentally, wewe ni kazi, mungu,afya, kulala Tu.

Usilete mbwembwe kabisa kama umetokea familia ya kawaida ambayo wewe ndo unaonekana kama jicho la familia, Usinajisi au kuingiza akili yako kwenye vitu vya hovyo, tunza akili na mwili wako. Vitu ambavyo si lazima na havikuongezei achana navyo kabisa maana vitakupotezea malengo, jua kabisa hakuna yoyote wa kuja kukuokoa....(huu ni ushauri Kwa wale waliotokea background za kawaida kabisa na bado wako juu ya mawe)
 
Hiyo njia siyo rahisi aisee..
Unaweza kuwaza kucomit suicide
Unahitaji uwe mvumilivu haswa wa shida za Kila aina,fedheha ,aibu,upweke na mambo ya Kila aina uwe imara kuyabeba.
Yaaan ni hakuna rangi unaacha kuona, ila unakuwa very strong maana Dunia ni ngumu sana asee, bila Sir God kukushika mkono, wafwaaa!😢
 
Hapo ndio unatakiwa ukazane kabisa, usirudi nyuma wala usikate tamaa! umekaribia mafanikio yako na mwanga uko mbele yako! Vumilia..

Binafsi nilipoanza tu ilinibidi nijikane nafsi, nilipitishwa kwenye moto! Kuna muda nakosa pesa ya chakula tu imagine! Ofisi inakaa wiki mbili hakuna biashara hata mia! Nilihama nyumba yangu nikapanga chumba kimoja yani inshort kila kitu kilisimama! Hayo mahusiano ndio nilishasahau! Nilikuwa na triangle yangu kanisani-nyumbani-kazini ndani ya mwaka mwambo yote ndipo yalipojifunga! Nikaongea na mtumishi wa Mungu, akanitia moyo sana maana nilikata tamaa na sikuwa na mtu wa kuongea naye!

Kwahiyo nikawa mtu wa maombi mimi na madhabahu! Naamka usiku saa 9 nasali, nina group la maombi kila siku saa10 tunaanza kusali! Kama roho akinituma kwenda maombi binafsi nafanyia madhabahuni narudi kwangu asbh! Nimelala sana madhabahuni..nilijitahidi pia kufunga kila j5! Kuna interview nilifika oral kw amaelekezo muhimu! Kiukweli ukikaza buti utamuona Mungu!

kiukweli hiki kipindi sio kirahisi kinahitaji watu wajasiri sana! Nakupongeza sana! Tena sana usije ukarudi nyuma! Kuvuka hapo sio lelemama! Na ukipita hapo mtu kukurudisha nyuma atapbana sana!! Mungu akutetee mpendwa..❤️
Ushuhuda wako unajenga, endelea kumpenda Mungu
 
Back
Top Bottom