Ukiona unapitia dalili hizi katika maisha, jua kuwa Mungu anakupeleka next level ya maisha yako

Ukiona unapitia dalili hizi katika maisha, jua kuwa Mungu anakupeleka next level ya maisha yako

Hapo ndio unatakiwa ukazane kabisa, usirudi nyuma wala usikate tamaa! umekaribia mafanikio yako na mwanga uko mbele yako! Vumilia..

Binafsi nilipoanza tu ilinibidi nijikane nafsi, nilipitishwa kwenye moto! Kuna muda nakosa pesa ya chakula tu imagine! Ofisi inakaa wiki mbili hakuna biashara hata mia! Nilihama nyumba yangu nikapanga chumba kimoja yani inshort kila kitu kilisimama! Hayo mahusiano ndio nilishasahau! Nilikuwa na triangle yangu kanisani-nyumbani-kazini ndani ya mwaka mwambo yote ndipo yalipojifunga! Nikaongea na mtumishi wa Mungu, akanitia moyo sana maana nilikata tamaa na sikuwa na mtu wa kuongea naye!

Kwahiyo nikawa mtu wa maombi mimi na madhabahu! Naamka usiku saa 9 nasali, nina group la maombi kila siku saa10 tunaanza kusali! Kama roho akinituma kwenda maombi binafsi nafanyia madhabahuni narudi kwangu asbh! Nimelala sana madhabahuni..nilijitahidi pia kufunga kila j5! Kuna interview nilifika oral kw amaelekezo muhimu! Kiukweli ukikaza buti utamuona Mungu!

kiukweli hiki kipindi sio kirahisi kinahitaji watu wajasiri sana! Nakupongeza sana! Tena sana usije ukarudi nyuma! Kuvuka hapo sio lelemama! Na ukipita hapo mtu kukurudisha nyuma atapbana sana!! Mungu akutetee mpendwa..❤️
Hapo ndio unatakiwa ukazane kabisa, usirudi nyuma wala usikate tamaa! umekaribia mafanikio yako na mwanga uko mbele yako! Vumilia..

Binafsi nilipoanza tu ilinibidi nijikane nafsi, nilipitishwa kwenye moto! Kuna muda nakosa pesa ya chakula tu imagine! Ofisi inakaa wiki mbili hakuna biashara hata mia! Nilihama nyumba yangu nikapanga chumba kimoja yani inshort kila kitu kilisimama! Hayo mahusiano ndio nilishasahau! Nilikuwa na triangle yangu kanisani-nyumbani-kazini ndani ya mwaka mwambo yote ndipo yalipojifunga! Nikaongea na mtumishi wa Mungu, akanitia moyo sana maana nilikata tamaa na sikuwa na mtu wa kuongea naye!

Kwahiyo nikawa mtu wa maombi mimi na madhabahu! Naamka usiku saa 9 nasali, nina group la maombi kila siku saa10 tunaanza kusali! Kama roho akinituma kwenda maombi binafsi nafanyia madhabahuni narudi kwangu asbh! Nimelala sana madhabahuni..nilijitahidi pia kufunga kila j5! Kuna interview nilifika oral kw amaelekezo muhimu! Kiukweli ukikaza buti utamuona Mungu!

kiukweli hiki kipindi sio kirahisi kinahitaji watu wajasiri sana! Nakupongeza sana! Tena sana usije ukarudi nyuma! Kuvuka hapo sio lelemama! Na ukipita hapo mtu kukurudisha nyuma atapbana sana!! Mungu akutetee mpendwa..❤️
Hakika mkuu
 
Asante kwa hoja yako , Kitu unachotakiwa kujua kuna watu wanateseka sababu ya vizazi vyao au family kuna maagano au kuna mambo waliyofanya kinyume na Mungu yanapelekea watoto waendelee kuteseka mpaka atapokea mtu mmoja kuvunja, na Wengine wanafanikiwa sababu vizazi vyao vya nyuma vilikuwa na mahusiano mazuri na Mungu hivyo wanaendelea kufanikiwa.

Kitu chengine ukiona Mambo magumu tenga muda jitafakali angalia tabia zako je ni sahihi mbele za Mungu, kama sio badilika , kuwa na moyo wa shukrani, upendo kwa wengine, kuwa na mahusiano na mtu mmoja pekee na tabia zengine then surrender kwa Mungu(hapa sali mfano mida ya saa 9 usiku mpala 11 hapo Mungu anaweza kupa direction ya changamoto zako kupitia ndoto.

Chengine badilisha mtazamo wako kuusu maisha acha kujitamkia maneno mabaya , jitamkie ushindi atakama unapitia magumu utapata direction ya maisha

Note kuenda kanisani , sijui kukesha sio 100% solution, solution unaweza pata kwa kuangalia mfumo wako wa maisha ukoje then badilsha na Mungu atakusaidia
Umenena vyema kbsa mkuu
 
kuamka kiroho siyo lelemama aisee,siyo jambo la kiimani,,,ni jambo halisi linalotokea kwenye akili na mwilini [Emotionally and physically] l.

Kuna namna unatakiwa kufanya ili hyo hali ipite vizuri,hapo ndo utasikia kitu kinaitwa Meditation..unapaswa uijue meditation inavyo fanyika.uki mess up unaweza kuishia kuwa kichaa..na kuna vichaa wengi sana ambao wametokana na hiyo hali.

Binafsi natoa hyo elimu bure kabisa,kwa muhitaji..
Mkuu shusha nondo hapa tujifunze
 
Asante kwa hoja yako , Kitu unachotakiwa kujua kuna watu wanateseka sababu ya vizazi vyao au family kuna maagano au kuna mambo waliyofanya kinyume na Mungu yanapelekea watoto waendelee kuteseka mpaka atapokea mtu mmoja kuvunja, na Wengine wanafanikiwa sababu vizazi vyao vya nyuma vilikuwa na mahusiano mazuri na Mungu hivyo wanaendelea kufanikiwa.

Kitu chengine ukiona Mambo magumu tenga muda jitafakali angalia tabia zako je ni sahihi mbele za Mungu, kama sio badilika , kuwa na moyo wa shukrani, upendo kwa wengine, kuwa na mahusiano na mtu mmoja pekee na tabia zengine then surrender kwa Mungu(hapa sali mfano mida ya saa 9 usiku mpala 11 hapo Mungu anaweza kupa direction ya changamoto zako kupitia ndoto.

Chengine badilisha mtazamo wako kuusu maisha acha kujitamkia maneno mabaya , jitamkie ushindi atakama unapitia magumu utapata direction ya maisha

Note kuenda kanisani , sijui kukesha sio 100% solution, solution unaweza pata kwa kuangalia mfumo wako wa maisha ukoje then badilsha na Mungu atakusaidia
Kwanini watu wanateseka Tanzania?
Kwanini hakuna Huduma bora za Afya Tanzania?

Kwanini kuna changamoto kubwa ya usafiri Tanzania?

Kwanini kuna ufisadi na ubadhirifu wa mali Tanzania?

Je, yote hayo ni KWASABABU YA MAAGANO, ama kwamba WATU walikwenda kinyume na Maagizo ya MUNGU?

Kwanini watu wanatekwa, wanauWawa, wanabambikiwa kesi za uongo, halafu watu wanaishia kusema TUMEMUACHIA MUNGU?

Yaani Maelfu ya watu wameuliwa oktoba 29 bila hatia halafu unasema kwamba hicho ni kipindi cha mpito kwamba mazuri yanakuja?

Hebu tuwe serious kidogo, yaani viongozi wauwaji wanakaribishwa kwenye nyumba za ibada (kanisani na msikitini) wanapewa na vipasa sauti wanaongea kila kukicha na bado Mungu mwenye nguvu, uweza, upendo, na huruma anaangalia TU.

Mataifa yenye maendeleo makubwa ya kiuchumi kama Sweeden, Netherlands, na Denmark ndiyo mataifa ambayo yana idadi kubwa ya SECULARS. Ila mataifa yanayoongoza kwa imani juu ya Miungu kama Nigeria, Kenya, Tanzania, Ghana, Uganda ndiyo yanayoongoza kwa umasikini, ufisadi, ukandamizwaji mkubwa wa demokrasia, mauaji ya kisiasa.

BADO TU HAMUONI KUWA KUNA TATIZO KUBWA KWENYE IMANI JUU YA MIUNGU HASA KWENYE HIZI DINI ZILIZOPO AFRICA?
 
Mataifa yenye maendeleo makubwa ya kiuchumi kama Sweeden, Netherlands, na Denmark ndiyo mataifa ambayo yana idadi kubwa ya SECULARS.

BADO TU HAMUONI KUWA KUNA TATIZO KUBWA KWENYE IMANI JUU YA MIUNGU HASA KWENYE HIZI DINI ZILIZOPO AFRICA?
TULIA WEWE!

Marekani na Europe haijajengwa atheists! ! ! Atheists walichochangia kwenye hii dunia ni uharibifu na sasa matokeo ni anguko kuu la dunia nzima.

Ni Wakristo ndio waliojenga hizo nchi mnazozihusudu.

Kanisa ndo ndilo lilijenga na kudhamini vyuo vya kwanza kabisa.

Wasomi / wagunduzi wengi wa kwanza walikuwa Wakristo!

Ukristo ndo ilikuwa State religion ya nchi za Europe wakati nchi hizo zina explore dunia na kupanua mamlaka zao.

Ukristo ndo uli shape maadili ya hawa watu wa dunia ya kwanza mnaowaona wastaarabu!

Ukristo ndo umejenga mifumo ya kimahakama na sheria za kimataifa otherwise hata huko Europe vijijini wanawake walikuwa wanakeketwa, watoto walikuwa wanatolewa kafara, bado wangekuwa kwenye mode ya survival for the fittest. n.k.


Na ni kwasababu Ukristo umeachwa, wamemuacha MUNGU, ndo unaona sasa anguko linawaijia! !

Yani ni sawa na mtu alijenga nyumba yake akaweka na furniture zake, baadae wewe ukahamia ukabadilisha furniture ukaweka zako halafu useme wewe ndo umejenga kwasababu kuna furniture zako! Sio wewe uliyejenga hiyo nyumba.

Sio miaka mingi tangu hizi nchi ziachane na Ukristo sasa Jamii zao zinaanguka kuanzia kwa kukaribisha maadui ambao watawamaliza, na wao wenyewe wanakufa tu naturally:

Msingi wa mahusiano ya mume na mke imeharibika, so institution ya familia imeharibika,

watu wamerudi kuwa wanyama, huku wakijifanya wamemuinua mwanamke huku Porn industry ndo imekua wanawake wanadhalilishwa, who's daughters are these? Nimesoma story ya mmoja juzi alivyoacha hiyo industry akaanza kuiongelea jinsi alivyokuwa akilia kila akitoka ku record, baadae alikutwa kafa, wamemuua,

watu hawazai tena wanaishia taratibu,

hata wakizaa watoto wenyewe hawajui jinsia zao wanalishwa mavidonge huko mwishowe wanaenda kuua wenzao,

watu hawaoni maana maishani wanaishia kutajirisha wanasaikolojia wawape maana,

hawaamini MUNGU lakini wanashinda mitandaoni kuongelea Mungu ambaye hayupo hii generation ya kipekee ambayo watu wake wanaishi kwa ajili ya kitu ambacho hakipo, in other words mental case.

Mnafikiri ni kwanini Wamarekani walimchagua Trump kama waliona njia za wasioamini ndo zinafaa? ? Waliona bora wamchague chizi muamini Mungu kuliko kuchagua wendawazimu wasioamini Mungu.

Walishaona mauzauza ambao nyie atheists mnaleta kwenye jamii, imagine mijitu imetenga mwezi mzima kutangaza sodomy. Kuna sjerehe yoyote humu duniani inayodumu mwezi mzima? Lakini mkaona kutangaza sodomy ni muhimu sana mtasherehekea mwezi mzima, halafu wanataka wapite mtaani kuambia watoto wa watu kuwa wako proud kuwa wachezea vinyesi, na hawaishii hapo niliona video mmoja wa alikung'utwa mwaka jana alikuwa anapita uchi kabisa barabarani watoto wapo eti pride month. Akawa anawarecord anawaambia atawashitaki kwa kumpiga.

Kwa kifupi nyie atheists msitake kutuchanganyia ma file hapa, Hamna chochote cha maana mnachochangia kwenye jamii zaidi ya kuleta uharibufu kwenye jamii bora zilizojengwa na Wakristo.

Uzuri yote yalitabiriwa na mwisho UMEKARIBIA.

MWISHO WA MAUZAUZA UMEKARIBIA!

JESUS IS LORD!

MAKE WAY FOR THE KING OF KINGS!
 
8C707DC9-18C2-470D-8A8C-3D092793B6C7.jpeg

Lax 🤸🏽‍♀️🤸🏽‍♀️
 
Let's hear from the founding fathers of America:

i) George Washington, Rais wa kwanza wa Marekani, alisema:

“Unafanya vyema kutamani kujifunza sanaa zetu na njia zetu za maisha, na zaidi ya yote, dini ya Yesu Kristo. Mambo haya yatakufanya muwe taifa kubwa zaidi na lenye furaha kuliko mlivyo sasa.”

ii) John Adams, Rais wa pili wa Marekani, alisema:

“Kanuni za jumla ambazo mababa wa taifa walitumia kufikia uhuru zilikuwa kanuni za jumla za Ukristo Ninakiri kwamba niliamini wakati huo, na ninaamini hata sasa, kwamba kanuni hizo za jumla za Ukristo ni za milele na zisizobadilika kama vile uwepo na sifa za Mungu.”

iii) John Quincy Adams, Rais wa sita wa Marekani, alisema:

“Katika mfululizo wa matukio ya kibinadamu, siku ya kuzaliwa kwa taifa letu imefungamanishwa bila kutenganishwa na siku ya kuzaliwa kwa Mwokozi. Azimio la Uhuru liliweka jiwe la msingi la serikali ya wanadamu juu ya kanuni za kwanza za Ukristo.”

iv) Maneno kutoka Azimio la Uhuru wa Marekani (Declaration of Independence):

“Tunashikilia ukweli huu kuwa ni wa wazi wenyewe, kwamba watu wote wameumbwa wakiwa sawa, kwamba wamepewa na Muumba wao haki fulani zisizoweza kunyang’anywa, na miongoni mwa haki hizo ni Uhai, Uhuru, na utafutaji wa Furaha... Na kwa ajili ya kuunga mkono Azimio hili, kwa kutegemea kwa uthabiti ulinzi wa Maongozi ya Kimungu (divine Providence), tunaahidiana sisi kwa sisi kutoa Maisha yetu, Mali zetu, na Heshima yetu takatifu.”

v) Na maneno kutoka rais wa mwisho wa Marekani, Donald Trump
:2Head:
(I don't believe I'm quoting this guy):

"I believe people can't be happy without religion, without that belief. Let's bring religion back. Let's bring God back into our lives".

Post in thread 'Je dini zitaeweza kuhimili maendeleo ya teknolojia?' Je dini zitaeweza kuhimili maendeleo ya teknolojia?
 
TULIA WEWE!

Marekani na Europe haijajengwa atheists! ! ! Atheists walichochangia kwenye hii dunia ni uharibifu na sasa matokeo ni anguko kuu la dunia nzima.

Ni Wakristo ndio waliojenga hizo nchi mnazozihusudu.

Kanisa ndo ndilo lilijenga na kudhamini vyuo vya kwanza kabisa.

Wasomi / wagunduzi wengi wa kwanza walikuwa Wakristo!

Ukristo ndo ilikuwa State religion ya nchi za Europe wakati nchi hizo zina explore dunia na kupanua mamlaka zao.

Ukristo ndo uli shape maadili ya hawa watu wa dunia ya kwanza mnaowaona wastaarabu!

Ukristo ndo umejenga mifumo ya kimahakama na sheria za kimataifa otherwise hata huko Europe vijijini wanawake walikuwa wanakeketwa, watoto walikuwa wanatolewa kafara, bado wangekuwa kwenye mode ya survival for the fittest. n.k.


Na ni kwasababu Ukristo umeachwa, wamemuacha MUNGU, ndo unaona sasa anguko linawaijia! !

Yani ni sawa na mtu alijenga nyumba yake akaweka na furniture zake, baadae wewe ukahamia ukabadilisha furniture ukaweka zako halafu useme wewe ndo umejenga kwasababu kuna furniture zako! Sio wewe uliyejenga hiyo nyumba.

Sio miaka mingi tangu hizi nchi ziachane na Ukristo sasa Jamii zao zinaanguka kuanzia kwa kukaribisha maadui ambao watawamaliza, na wao wenyewe wanakufa tu naturally:

Msingi wa mahusiano ya mume na mke imeharibika, so institution ya familia imeharibika,

watu wamerudi kuwa wanyama, huku wakijifanya wamemuinua mwanamke huku Porn industry ndo imekua wanawake wanadhalilishwa, who's daughters are these? Nimesoma story ya mmoja juzi alivyoacha hiyo industry akaanza kuiongelea jinsi alivyokuwa akilia kila akitoka ku record, baadae alikutwa kafa, wamemuua,

watu hawazai tena wanaishia taratibu,

hata wakizaa watoto wenyewe hawajui jinsia zao wanalishwa mavidonge huko mwishowe wanaenda kuua wenzao,

watu hawaoni maana maishani wanaishia kutajirisha wanasaikolojia wawape maana,

hawaamini MUNGU lakini wanashinda mitandaoni kuongelea Mungu ambaye hayupo hii generation ya kipekee ambayo watu wake wanaishi kwa ajili ya kitu ambacho hakipo, in other words mental case.

Mnafikiri ni kwanini Wamarekani walimchagua Trump kama waliona njia za wasioamini ndo zinafaa? ? Waliona bora wamchague chizi muamini Mungu kuliko kuchagua wendawazimu wasioamini Mungu.

Walishaona mauzauza ambao nyie atheists mnaleta kwenye jamii, imagine mijitu imetenga mwezi mzima kutangaza sodomy. Kuna sjerehe yoyote humu duniani inayodumu mwezi mzima? Lakini mkaona kutangaza sodomy ni muhimu sana mtasherehekea mwezi mzima, halafu wanataka wapite mtaani kuambia watoto wa watu kuwa wako proud kuwa wachezea vinyesi, na hawaishii hapo niliona video mmoja wa alikung'utwa mwaka jana alikuwa anapita uchi kabisa barabarani watoto wapo eti pride month. Akawa anawarecord anawaambia atawashitaki kwa kumpiga.

Kwa kifupi nyie atheists msitake kutuchanganyia ma file hapa, Hamna chochote cha maana mnachochangia kwenye jamii zaidi ya kuleta uharibufu kwenye jamii bora zilizojengwa na Wakristo.

Uzuri yote yalitabiriwa na mwisho UMEKARIBIA.

MWISHO WA MAUZAUZA UMEKARIBIA!

JESUS IS LORD!

MAKE WAY FOR THE KING OF KINGS!
Nafikiri bado wewe ni mchanga sana katika kuifahamu na kuijua historia ya Secularism (Separation of Church & State) pamoja na Human Rights.

Secularism ndiyo iliyobadilisha kwa kiasi kikubwa mwenendo wa maisha ya watu Ulaya na Marekani kuanzia karne ya 18.

Inawezekana huwafahamu watu kama Thomas Paine, Thomas Jefferson, na Voltaire. Hawa wanatajwa katika historia kama miongoni mwa waanzilishi wa demokrasia na secularism tunayoijivunia leo duniani. Muhimu zaidi, wengi wao walikuwa Deists, si Wakristo.

Kabla ya mageuzi yaliyoletwa na secularism, Ukristo ulikuwepo lakini historia pia inaonyesha kuwa ulihusishwa na matukio makubwa ya mauaji na mateso kwa misingi ya dini. Mfano ni witch hunting and witch trials, mauaji ya heretics, pamoja na matukio kama Spanish Inquisition na St. Bartholomew's Day Massacre. Hata fikra tofauti zilikuwa hatarini; mfano Baruch Spinoza alilazimika kukimbia baada ya kupinga baadhi ya mafundisho ya kidini. Pia huko Amerika, Biblia iliwahi kutumika kuhalalisha utumwa.

Sikatai kwamba Ukristo umechangia kwa kiwango fulani katika kujenga misingi ya maadili tuliyonayo leo. Hata hivyo, hoja yangu kuu ni kwamba demokrasia na secularism ndizo zimewezesha mataifa mengi kupata maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii.
Mfano wake ni kwamba:
  1. Utumwa (slavery) ulisitishwa kwa misingi ya haki za binadamu zilizoimarishwa na secularism na demokrasia.
  2. Ukoloni uliwekewa kikomo kutokana na wazo la haki za binadamu.
  3. Wanawake wamepata nafasi ya kuongoza jamii kutokana na misingi hiyo ya haki na usawa.
  4. Maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia yamechochewa na mazingira ya uhuru wa fikra.
  5. Leo kuna freedom of speech, jambo lililoimarishwa na mfumo wa secularism na demokrasia.

Hoja yako ya ATHEISTS ni BATILI na ina thibitisha ni jinsi gani hufahamu misingi ya ATHEISM na SECULARISM.

1. Informed Atheists yeyote hawezi kusapoti Transgenderism kwasababu ni Unscientific [Gender/Sex in Human beings is Binary (You are either a Male or Female)].

2. Porn Industry; Informed Atheists hawezi kusapoti mtu kuingia huko kwa kulazimishwa - huo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za Binadamu. Ikiwa mtu mwenye umri wa miaka 18 na zaidi ameingia kwenye Porn Industry kwa hiari yake mwenyewe baada ya kufanya uchunguzi wa kutosha hapo hakuna ukiukwaji wowote wa haki za binadamu.

3. Binadamu ni Mnyama na kuna shahidi nyingi za kutosha juu ya hili kupitia nadharia ya Evolution (Human descended from a Wild Ancestors) - Hii ni sayansi na sio imani ya kidini.

4. Unapoona Watu hawazaliana kwa kiwango kikubwa hiyo ni ishara kwamba wameELIMIKA na wameSTAARABIKA na hayo ndio matokeo ya SECULARISM, jamii iliyostaarabika na kuelimika hupata MAENDELEO katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Hii ni tofauti na AFRICA, watu wanazaliana sana ila hawajastaarabika na kuelimika kwa sababu DINI zao zinawanyima ELIMU ya KUFIKIRI.

5. Informed Atheists hawahusiki ni propaganda zozote zinazoharibu MAADILI kwenye JAMII. Ni nadra sana kumkuta Atheists anasapoti matendo OVU kama VITA, MAUAJI ya KISIASA, MAUAJI ya KIDINI, nk. Kwa ATHEISTS: Mmomonyoko wa MAADILI siyo: Watu kufanya Ngono wapendavyo, wala siyo Kunywa Pombe Wapendavyo, Wala siyo Kuzaa au Kutokuzaliana, Wala siyo Kuchora Tatoo, wala siyo mitindo ya Mavazi, Wala siyo kutembea NUSU uchi. Kwa Atheists swala la MAADILI ni juu ya MATOKEO ya Matendo, na Wala siyo juu ya machukizo, na kutokuwa machukizo mbele ya macho ya BWANA.

6. Kuhusu watu kutotambua maana ya MAISHA hili ni suala linalosababishwa na factors nyingi, kusema watu wanakosa maana ya Maisha kwa sababu ya ATHEISM ni Upotoshaji wa kiwango kikubwa. Kwanza DINI inawapa watu maana ya MAISHA ambayo ni ya kipotoshaji; mfano - unapomwambia MTU kwamba yeye aliumbwa kumtumkia MUNGU ili baadae atakapokufa akaishi MILELE na MUNGU ni UONGO mkubwa.



Unamzungumzia Trump raisi wa marekani, mbona unawaacha Maraisi wa Afrika ambao kutwa kukicha wapo makanisani na misikitini kufanya sala na kuabudu, ila wakitoka kuingia ofisi za umma kutumikia wananchi wao wanageuka MAFISADI, na WAUWAJI wakubwa.

1. UFISADI, MAUWAJI, UBADHIRIFU WA MALI ZA UMMA, UONEVU, DHULMA, nk. vyote vimeshamiri TANZANIA, cha AJABU wanalaumiwa ATHEISTS. TANZANIA ni nchi iliyowahi na mpaka sasa inaongozwa na Maraisi ambao DINI zao ni aidha UKRISTO, au UISLAMU, sasa inakuaje MUNGU mpenda haki anaruhusu viongozi hao wawe ndio chachu ya UFISADI, MAUWAJI, UBADHIRIFU WA MALI ZA UMMA, UONEVU, DHULMA, nk?

2. Congo DRC ina watu zaidi ya Millioni 100 na kiongozi wao MKUU ni MKRISTO, inakuaje MUNGU anashindwa kuwaondoa kwenye VITA na MIGOGORO YA KISIASA?

3. NIGERIA ina watu zaidi ya millioni 300, wananchi wake ni wafuasi wa DINI ya UKRISTO na UISLAMU kwa wingi inakuaje wanakimbilia CANADA, MAREKANI, NORWAY, SWEEDEN, DENMARK kutafuta maisha? Inakuaje mpaka TRUMP anaingilia kati mauaji ya waislamu dhidi ya Wakristo huko Nigeria, yaani ina maana Mungu ni mvivu kiasi hicho mpaka anasaidiwa kazi na TRUMP?


MWISHO, Iko hivi UKRISTO umekuwa ni DINI ambayo imekuwa ukiEVOLVE kucope na maendeleo ya Secular Morality, na Teknolojia ndio maana leo hii utakuta Mashoga kanisani wakisali na kuabudu, utakuta Vijana wa kiume na kike wa kikristo wamechora TATOO, utakuta kuna KUTALAKIANA baina ya Wanandoa Wakristo, Utakuta uvaaji wa mavazi ya kisasa kwa wakristo makanisani. Hali hii imeibua aina ya UKRISTO unaofahamika kama LIBERAL CHRISTIANITY, na CULTURAL CHRISTIANITY, lakini pia hii inatoa ishara kwamba baada ya Miaka karne nyingi zijazo UKRISTO wa kale UTAPOTEA KABISA.

UNA UHURU WA KUAMINI CHOCHOTE, ILA FAHAMU KWAMBA IMANI YAKO INAWEZA KUWA UONGO, NDIO MAANA UNAHITAJI UTHIBITISHO KABLA YA KUAMINI, PIA UNAPOWAAMINISHA WATU UONGO HUO NI UOVU.
 
(not debating, just leaving this here for Genuine Truth Seekers)

Proof of Jesus

HAKUNA
mtu aliyeacha nyayo nyingi kwenye historia kama Yesu Kristo, HAKUNA!

Yesu Kristo ndiye Mtu mashuhuri kupita wote kwenye historia, nakuhakikishia.


1) Kwanza dini zote (ikiwemo dini ya atheism) zinamkubali Yesu Kristo, halafu Yesu anajikubali mwenyewe tu.

Wayahudi wanasema Yesu alikuwa Rabi/mwalimu.

Waislamu wanasema Yesu alikuwa nabii.

Wabuddha wanasema Yesu ni mtu aliyeangaziwa (enlightened).

Wahindu na imani za huko Mashariki wanasema Yesu alikuwa udhihirisho wa Mungu, mungu flani aliyechukua umbo la binadamu, mwalimu, mtawa, mtu mtakatifu aliyeamua kuachana na ya ulimwengu n.k.

New age spiritualists wanaohubiri power of the mind, wanasema Yesu alikuwa ni mtu aliyefuzu kwenye hiyo sekta.

Waamini sayansi kuwa ndo itawapa majibu ya kila kitu (wakana Mungu) wanasema Yesu alikuwa jamaa mjanja mjanja, mwanasiasa flani ambaye alianzisha chama chake na kupata wafusi.

Kuna viazi vichache vinasema Yesu hakuwepo kabisa.

YESU KRISTO hamtaji yeyote yule, anasema yeye pekee:

• ndiye Njia inayotafutwa na watu,
ndiye Kweli inayotafutwa na watu,
ndiye Uzima wa binadamu
unakopatikana,

• ndiye Mwanga kwenye ulimwengu
huu wenye giza,

•  ndiye Ufufuo kwani kifo sio mwisho,

• ndiye Mlango wa kuingilia Next
Level,


• ndio Jina pekee tunalopaswa kuliitia,
sio majina ya watu waliokufa,

• ndiye Mchungaji mwema atatupa kila tunachohitaji,

• ndiye Mwana wa Mungu, Muumba aliyeingia ndani ya uumbaji wake mwenyewe, akawa Mwana wa Binadamu

• ndiye Kristo/ Masihi/ Mwokozi, anayetuokoa na uharibifu (dhambi) na kifo ambacho binadamu anahangaika kukiepuka.

1000036340.jpg


(Picha ni za kufurahisha macho. Kuna mtu atakwazika kisa YESU ni ngozi nyeupe. Acha ushamba! Katafute ngozi nyeupe uoe uachane na hizi hoja za bei rahisi. )


2) Hakuna mtu mwenye rekodi nyingi kumhusu kwenye historia kama Yesu Kristo.


-Waongo na wazushi wanasema hamna uthibitisho. Ni nini hasa kinastahili kuwa uthibitisho?

Shida sio kuwa hamna uthibitisho, shida ni hawapendi kuona wanachoona.

Yesu angekuwa ni mwalimu tu mwenye hekima ambaye hakuzaliwa na bikra, hakufanya miujiza, hakufufuka na kupaa mbinguni, hakuna ambaye angepinga kuwa hakuna mtu mwengine kwenye historia ambaye kumbukumbu zake zilitunzwa kwa wingi kama Yesu.

- Kwa sasa tuna takriban hati za zamani 6000 za agano jipya katika lugha ya Kigiriki peke yake! Wastani wa hati moja ni kurasa 450!

- Tukiongeza na nakala zilizotafsiriwa karne za kwanza kwa kilatini, kiCoptic, kiSyriac n.k tunakuwa na makumi ya maelfu ya nakala za agano jipya.

NI AIBU kwa waongo na wazushi!

- Hakuna maandiko yoyote kwenye historia yenye shehena la nakala kama agano jipya! HAKUNA.

1000036915.jpg



3) Vitabu vya Injili viliandikwa na watu walioshuhudia hayo matukio.


Mpelelezi wa mauaji, James Warner Wallace (J.W.W), mkana Mungu aliyegeuka na kumwamini Yesu anasema akiitwa kwenye tukio la mauaji, maelekezo ya kwanza anayotoa kwa polisi ni kuwa wawatenganishe walioshuhudia hilo tukio. Maana wakikaa wote wataanza kujadili hilo tukio mpaka aje afike atakuta wana maelezo yanafanana fanana.

Lakini wakitenganishwa, akija kuwahoji mashahidi, maelezo yao huwa ni shagala bagala, huenda yakaonekana hata kuwa yanapingana. Lakini hiyo haimaanishi kuwa yanapingana.

Tena ukija kuchanganya maelezo yao yanayoonekana kupingana ndo unapata picha vizuri kwasababu kila mtu anakuwa anasimulia kutokana na mazingira aliyokuwepo wakati wa tukio, alichokuwa ana focus, hamu yake, mtazamo wake, makuzi yake n.k.

- Sasa basi, kitabu cha Luka kinasema kabisa anayoandika daktari Luka ni shuhuda za mashahidi alioenda kuwahoji (Luka 1).

- Mathayo na Yohana wanasema waliyoandika walishuhudia kwa macho yao.

- Injili ya Marko inakubalika na wachambuzi kuwa ni Marko alikuwa akiandika kwa niaba ya mtume Petro aliyekuwa anamsimulia, akimsaidia kutafsiri kwenda Kigiriki.

1000036342.jpg



Je kuna sababu yoyote ya kushuku shuhuda hizi?

a) Utasikia "haiwezani kitabu cha 1 Petro kiwe kiliandikwa na mtume Petro kwasababu kimeandikwa kwa Kigiriki cha kisomi kabisa na mtume Petro alikuwa mvuvi kutoka Galilaya".

Sasa kwanini asijue kigiriki wakati maisha yake yote aliishi eneo ambalo watu waliongea kigiriki! !

Lakini pia inaoneka kuwa Petro alikuwa anamsimulia mtu anamuandikia.

Kama wazee wa kanisa (church fathers) wa karne ya kwanza na ya pili kwenye barua zao walikuwa wanarejea maandiko na wanakubaliana kuwa yaliandikwa na flani na flani, unakataa nini? ?

1000036343.jpg



b) Au utasikia "maandiko yenyewe yameandikwa mamia ya miaka baada ya matukio kwahiyo yamebadilishwa au kutungwa ".

i) Kwanza hatuna nakala halisi zilizoandikwa kwa mikono ya mitume wenyewe, sababu ni wazi:

•Nyenzo walizotumia (ngozi) hazingeweza kudumu.

•Muda mrefu umepita.

Nakala za historia zilikuja kuanza kudumu wakati walipoanzisha taasisi za kutunza nakala hizi, ndomana unapokuja kukutana na nakala yoyote ya historia ya zamani zaidi iliyotunzwa unaweza kukuta ni ya miaka zaidi ya 90, 300, 1000 baada ya kuandikwa kwa nakala ya kwanza kabisa.

ii) Pia Nakala nyingi ziliharibiwa na waliochukia ujumbe wa Wakristo.

iii) Inawezekana pia waliiga utamaduni wa Wayahudi ambao waliharibu nakala za zamani zilizochakaa kila waliponakili maandiko kwenye sehemu mpya.

1000036344.jpg




c) Kama watu wangetaka kubadilisha biblia, ingebidi wapitie njama za viwango vitatu:

i)
Kwanza njama ya hati - ingebidi wachukue zaidi ya hati 6000 za Kigiriki agano jipya wazibadilishe na wafiche ushahidi kuwa wamefuta wino wakabadilisha.

ii) Pili njama ya lugha - Kisha itabidi wakatafute maelfu ya hati za agano jipya zilizotafsiriwa kwenda kilatini, kiCoptic na kiSyriac wazibadilishe zote ziendane na uongo waliyoandika kwenye zile za Kigiriki.

iii) Tatu njama ya maoni ya wazee wa kanisa (early church fathers) - wazee wa kanisa wa karne za kwanza walikuwa na utamaduni wa kuandika maoni/uchambuzi kuhusu biblia.

Tukisema tutupe biblia zote, tunaweza kuunda asilimia 95 ya agano jipya kwa kutumia maandishi ya wazee wa kanisa tu! Kwahiyo wanaotaka kubadilisha biblia ingebidi pia wapitie barua zote za wazee wa kanisa wabadalishe iendane na uongo walioandika kwenye Kigiriki na kilatini, kiCoptic na kiSyriac.

Kusema kuwa Biblia imebadilishwa ndio Conspiracy Theory kubwa kuliko zote kwenye karne yetu (ikifuatiwa na Evolution)

1000036345.jpg



d) Bila kusahau kopi tulizonazo za Injili zinakaribiana umri na nakala halisi, mfano tuna kopi za miaka 100AD.

Linganisha na nakala zingine za kihistoria, mfano za mwanahistoria Josephus ambaye kopi yake ya zamani kabisa tuliyonayo ni ya miaka 1000 baada ya Josephus! ! !

Au za Julius Caesar na vita zake kopi tuliyonayo ya zamani kabisa kumhusu ni ya miaka 900 baada ya Caesar mwenyewe! ! !

Au Aristotle, kopi yake ni ya miaka 1400 baaya ya Aristotle! ! !

1000036912.jpg



e) Je tunaweza kujua wakati ambapo nakala ya kwanza kabisa iliandikwa?


Kwa mfano, kitabu cha Matendo kilichoandikwa na Luka kinaongelea unabii wa kuharibiwa kwa Yerusalemu (Matendo 6:14). So tunaweza kuhitimisha kuwa kiliandikwa kabla ya 70AD.

Kwenye kitabu cha Luka, Luka anasimulia jinsi Yesu alivyotabiri kuwa Yerusalemu itakuja kuharibiwa.

Hakuna kitabu chochote kwenye agano jipya kilichosimulia tukio la kuharibiwa kwa Yerusalemu, zaidi ya kutoa unabii kuhusu kuharibiwa kwa Yerusalemu (70AD)!

Unakuta mtu badala ya mtu kuhitimisha kuwa Yesu anaweza kutabiri kwa usahihi, mtu anasema hivyo vitabu viliandikwa baada ya tukio kwasababu haiwezekani kutabiri! ! !

Kwahiyo mtu ameshaamua akilini kwake miujiza haiwezekani kwahiyo akiona simulizi la utabiri uliokuja kutimia maana yake liliandikwa baada ya tukio! Hapo tayari umeleta ubaguzi (bias) kwenye kupima umri wa hizi nakala za kihistoria.

Kingine, wakati vitabu vya Matendo na Luka vinaandikwa bado kina Paulo, Petro, Yakobo walikuwa hai (miaka ya vifo vyao inajulikana), wakati vifo vya wafuasi wengine wa Yesu kama Stephano na Yakobo kaka ya Yohana vinatajwa.

Inawezekana mtu aandike historia ya Tanzania ya miaka ya 90 asitaje kifo cha Nyerere?

1000036347.jpg


1000036902.jpg



f) Sasa tutajuaje kuwa nakala hizi za agano jipya zilizonakiliwa vizazi baada ya vizazi hazijabadilika?

Tutafuata mlolongo wa ulinzi (chain of custody).

Kwa mfano, aliyeandika kitabu cha Yohana, alimpa nani hiyo nakala?

Tunawajua baadhi ya wanafunzi wa Mtume Yohana: Ignatius, Polycarp, Papius.

Hawa wanafunzi nao wana wanafunzi wao wanajulikana.

So tunaangalia kwenye huu mlolongo wa wanafunzi, Je simulizi kumhusu Yesu linabadilika? Je Yesu alianza kama mtu wa kawaida kadri muda ulivyoenda akageuka kuwa Mungu mtu?

Hapana! Tangu kitabu cha Yohana hadi barua za wanafunzi wake (wazee wa kanisa) na wanafunzi wao, simulizi ni lilelile: Yesu alizaliwa na bikra, alifanya miujiza, alikufa, akafufuka! ! !


Kitabu kama 1 Wakorintho kinakadiriwa kuwa cha miaka ya 50AD, na kinaongelea Ufufuo wa Yesu (1 Wakorintho 15). So Ufufuo wa Yesu ni habari iliyokuwepo tangu karne ya kwanza, haikutungwa baada ya miaka kupita!


1000036911.jpg



Hata kuhusu vitabu vilivyokuja kurasimishwa kwenye Baraza la Laodicea (363AD), ndo hivyo hivyo vilivyokuwa vinanakiliwa kwenye barua za wazee wa kanisa tangu karne ya kwanza, na vilikuwa vinaitwa hivyo hivyo vinavyoitwa - Injili ya Luka, ya Mathayo n.k.

Baraza halikuja kuamua lolote jipya kuhusu vitabu zaidi ya kukataa vitabu vilivyokuja kuibuka baadae ambavyo wazee wa kanisa hawakuvitambua!


1000036346.jpg



g) Kingine cha kutujuza kuwa nakala hazijabadilika ni uwepo wa mamia na maelfu ya nakala za awali kabisa za agano jipya kwa visehemu au nzima nzima, kwa lugha zaidi ya nne tofauti.

Zingekuwepo kopi mbili tu kungekuwa na utata. Lakini ni maelfu ya nakala tena kwa lugha nne tofauti! !

1000036351.jpg



h) Utasikia "kitabu cha Mathayo hakijasema kimeandikwa na Mathayo kwa hiyo hatujui nani kakiandika na hakiaminiki".


Unajua ni historia kiasi gani itabidi tuitupilie mbali tukitumia hii hoja?

Hakukuwa na utamaduni wa mtu kuandika jina lake kwenye makala zake.

Tumeona hapo juu (f), uhalali wa waandishi wa nakala hizi tunaupata kupitia mlolongo wa ulinzi (chain of custody).


i) Vipi kuhusu zinazodaiwa kuwa ni utata (contradictions) zinazoonekana kwenye zile Injili nne?

Kwanza contradiction maana yake haziwezi kupatanishwa. Kilichopo kwenye Injili ni tofauti (variation) sio contradiction.

Kwa mfano, kwenye ukoo wa Yesu, Mathayo 1:16 inasema baba ya Yosefu ni Yakobo huku Luka 3:23 inasema baba ya Yosefu ni Heli. Mtu anakimbilia kusema ni contradiction.

Lakini Mathayo kafuata ukoo wa Yesu kupia Solomon Mwana wa Daudi (Mathayo 1:6),

huku Luka akifwata ukoo kupitia Nathani mwana wa Daudi (Luka 3:31)!

Njia mbili tunazoweza kupatanisha kisa hiki:

a) Mathayo anafuata ukoo wa Yesu kupitia Yosefu baba yake mlezi huku Luka akifwata ukoo kupitia Maria mama yake.

Ndomana Luka anasema "...na watu walidhani yeye ni mtoto wa Yosefu mwana wa Heli...." (Luka 3:23 BHN).

Yosefu anakuwa mwana wa Heli kupitia ndoa yake na Maria, hivyo Yesu anakuwa mwana wa Daudi kupitia Maria kisheria.

b) Au kupitia ile Sheria ya kurithi mke (levirate marriage), kwamba Heli na Yakobo walikuwa Ndugu, kisha Heli alikufa bila mwana kwahiyo Yakobo akamuoa mjane wake akamzaa Yosefu, kwahiyo Yosefu alikuwa mwana wa Heli kisheria.

Unaweza kutafiti zaidi.

Je maelezo haya hayapatanishi Injili hizo?

1000036352.png



Mfano mwingine, kulikuwa na malaika mmoja au wawili kwenye kaburi la Yesu?

Mathayo 28 na Marko 16 inasema mmoja. Luka 24 na Yohana 20 inasema wawili.

Mpelelezi J.W.W anakwambia hajawahi kusikia mashahidi wawili wa tukio wakikubaliana kila kitu.

Kwanza chochote atakachojibu shahidi kinategemea swali ulilomuuliza, ndomana anaweza asitaje jambo muhimu sana kwenye kesi, ukija kuumuliza kulihusu anakwambia hukuniuliza!

Na ndo anachoona kwenye kisa hiki cha malaika kwenye kaburi la Yesu. Waandishi wanaonekana kujibu maswali tofauti.

Mathayo na Marko hawajasema kulikuwa na malaika mmoja tu! Lakini Yohana na Luka wanasema waliwepo wawili.

Sasa kama kuna wawili si kuna mmoja! ! Hakijaharibika kitu.

Ili kuwe na contradiction, Mathayo na Marko waseme alikuwepo mmoja tu.

Ukisoma vizuri utaona Mathayo na Marko walikazia issue ya tetemeko na jiwe la kaburi.

Mathayo
anaonekana kujibu swali "Ni nini kilisababisha tetemeko"?

Marko anaonekana kujibu swali "ni nani aliondoa jiwe kwenye kaburi"?

Luka anaonekana kukazia fikra kupotea kwa mwili kwenye kaburi.

Yohana yeye alikazia fikra ripoti ambayo wanawake hao walienda kutoa.

J.W.W anasema anavyoona jinsi ambavyo waandishi wa Injili hizi hawakujihangaisha kulinganisha masimulizi yao Ili yafanane, ni uthibitisho kuwa masimulizi haya ni ya kutegemeka.

Hata yangefanana neno kwa neno, wazushi wangekataa pia! Wangesema hawa watu wametunga.


1000036353.jpg




4) Masimulizi kwenye agano jipya (na la kale) ni yenye kutegemeka kihistoria.



Kuna taarifa nyingi za zisizo za kikristo za kihistoria kwenye biblia. Yani kama utamsoma Josephus (36-100AD) ukamwamini na usijiulize mara mbili kama yuko sahihi au la, basi hata Injili unaweza kusoma bila kujiuliza.

Ukikuta tofauti kwenye taarifa fulani ya kihistoria (mfano issue ya sensa ya Quirinus wakati Yesu alipozaliwa) sio unampuuza Luka na kumsikiliza Josephus, maandishi ya Josephus hayana mamlaka yoyote zaidi ya Luka.

Kwanza Injili inakuwa na mamlaka zaidi kwakuwa yalionekana kuwa maandiko yenye thamani kubwa kwahiyo yalilindwa sana, yalitunzwa, yalisambazwa na kutafsiriwa!

Tofauti na maandishi ya wanahistoria kama Josephus ambaye hakuwa na watu waliofuatilia na kulinda maandishi yake! ! Kama kuna uongo amesema hakuna wa kumpinga!

Daktari Luka anasema: "....Watu wengi wamejitahidi kuandika juu ya mambo yale yaliyotendeka kati yetu. Waliyaandika kama tulivyoelezwa na wale walioyaona mambo hayo kwa macho yao tangu mwanzo, na waliotangaza ujumbe huo. Inafaa nami pia, Mheshimiwa, baada ya kuchunguza kwa makini mambo yote tangu mwanzo, nikuandikie kwa mpango, ili nawe uweze kujionea mwenyewe ukweli wa mambo yale uliyofundishwa." (Luka 1:1‭-‬4 BHN)


Mtume Petro naye anasema: "Wakati tulipowafundisheni juu ya ukuu wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, hatukutegemea hadithi tupu zisizo na msingi. Sisi tuliuona utukufu wake kwa macho yetu wenyewe." (2 Petro 1:16 BHN)

Mtume Paulo anasema: "....alizikwa, akafufuka siku ya tatu kufuatana na Maandiko Matakatifu; kwamba alimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea wale kumi na wawili. Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya 500 kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa." (1 Wakorintho 15:4‭-‬6 BHN)

Biblia ni nyaraka zenye kutegemeka kabisa za historia.

Sio hekaya au hadithi!

Biblia sio Gilgamesh epic!

Biblia iliandikwa na mashahidi wa matukio halisi ya historia, wakishuhudiwa na mashahidi wenzao wa hayo matukio.

1000036354.jpg




5) Bila kusahau kuenea kwa ukristo karne za kwanza kulihusisha mateso makali sana kwa wakristo.

Walichohitaji ni kumkana Yesu halafu waepuke kifo waendelee na maisha yao,

lakini mamia na maelfu walikubali kuuawa: walisulubiwa, walipigwa mawe hadi kufa, walichomwa moto wakiwa hai, walitupwa waliwe na wanyama!

Kuna faida waliyokuwa wanapata kwa kushikilia hiyo Imani?

Pesa? Mamlaka? Wanawake?

Zaidi ya mateso na kudharaulika!

Au wote walikuwa wanaota?

Ni nini kilichowasukuma?

Na kuna tofauti ya mtu kukufuata kukuua kwasababu ya imani yako, na mtu aneyeenda kujitoa kafara kwasababu ya imani yake.

1000036356.jpg


1000036355.jpg



6) Tuna uthibitisho wa kutosha kabisa wa kukubali masimulizi ya Yesu bila shaka yoyote (beyond reasonable doubt).

Haiwezekani kuwa na uthibitisho bila shaka kabisa (beyond possible doubt).

Hiyo itahitaji kujua KILA KITU na haiwezekani kujua kila kitu.

Hakuna anayeishi maisha kwa kiwango hicho cha bila shaka kabisa maana hata nyumbani tusingetoka hadi mtu uwe na uhakika bila shaka kabisa kwamba hutogongwa na gari kesho, hutopigwa na radi, hutotekwa n.k.

Hata hukumu za wahalifu wabaya kuliko wote wanaohitaji kunyongwa hazihitaji uthibitisho bila shaka kabisa.

Nafasi ndogo iliyobaki kati ya uthibitisho bila shaka yoyote na uthibitisho bila shaka kabisa ndo nafasi ya maswali yako yasiyokuwa na majibu.

Ni nafasi ya wewe kuchukua hatua moja tu, ya IMANI.


Sio Imani kipofu: ni Imani yenye uthibitisho usio na shaka yoyote!

Kuwa na TUMAINI sio kuwa na matamanio ya kufikirika.

Ni kuwa na uhakika wa mambo unayoyatarajia kutokana uthibitisho usio na shaka uliopata.

"Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye."
Yohana.6.28‭-‬29.SRUV

"Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa maana kila mtu anayemwendea Mungu ni lazima aamini kwamba Mungu yuko, na kwamba huwatuza wale wanaomtafuta."
Waebrania.11.6.BHN

"Pimeni kila kitu: Zingatieni kilicho chema."
1Wathesalonike.5.21.BHN


1000036357.jpg
 
Back
Top Bottom