Ukiona unapitia dalili hizi katika maisha, jua kuwa Mungu anakupeleka next level ya maisha yako

Ukiona unapitia dalili hizi katika maisha, jua kuwa Mungu anakupeleka next level ya maisha yako

Naomba kuelewesha.
Hivi ukikaa na njaa, ukalia na kutoa machozi, ukihudhuria nyumba za ibada kila mara — je, hiyo ndiyo itamfanya Mungu akutimizie haja zako za kiuchumi?
Yaani mtu akifanya hivyo kwa wingi, ndio moja kwa moja atapata ajira, faida kwenye biashara, na mafanikio mengine?
Tuseme umeomba sana ukaambulia ajira. Wakati huo huo kuna mamilioni hawana ajira, nao pia walisali na kufunga. Je, hapo utaweza kumsifu Mungu aliyewapa wachache ajira na kuwaacha wengi wenye vigezo vyote wakikosa nafasi?
Fikiria hivi:
Jeshi la uokoaji limeagizwa kwenda kuokoa wanafunzi katika bweni linalowaka moto. Katika hali ya kawaida kabisa, jeshi hilo lina uwezo wa kuokoa wanafunzi 100 kati ya 120 waliomo ndani. Lakini katika hali isiyo ya kawaida, likafanikiwa kuokoa wanafunzi 20 tu.
Je, hapo tutalisifu jeshi hilo kwa kuokoa wanafunzi 20 kati ya 120 na kuacha 100 wakipoteza maisha?
Kama kupata alama 20 kati ya 100 ni kufeli, je Mungu kumpa mtu mmoja ajira kati ya 1000 walioomba inakuwaje si kufeli, bali inaitwa kufaulu kunakopaswa kutukuzwa?
Hebu mtueleze, ni akili zipi zinatumika kumwelewa Mungu mwenye upendo na huruma pale anaposaidia wachache na kuwaacha wengi wakiendelea kuumia?
 
Kuna pepo  hapo juu limesema:

"wanao ongoza kukesha makanisani na misikitini ndio maskini choka mbaya, mafukara, makabwela, hohe hae, Pangu pakavu tia mchuzii."

Kwamba hujawahi kuona Wakristo matajiri maishani mwako?

Hizi ndinga zinazojaa huko makanisani ni za kwenu nyie roho waovu?

Kwamba makasri yote unayoyaona jijini ni ya kwenu nyie waabudu shetani?

Kwamba wasomi wote watalaam wote humu duniani ni mapepo wenzenu?

Kwamba waajiri wote, wenye biashara kubwa wote ni watu wenu nyie wa ufalme wa giza?


Embu Tutokee hapa.


Tena bora uwe maskini huku mcha Mungu utabaki na Amani ya Mungu, unamuonea wivu mwenzio anaenda kusifu kwa raha zake peke zake kanisani?

Kuliko kuwa maskini usiyeamini Mungu unaishia kufanya kila aina ya uovu na uchafu kupa utajiri ambao hata huupati,

unaishia tu kupata aibu na dharau na trauma, kuwa mtu wa makasiriko tu maisha yako yote, unaishia ku post mitandaoni kila siku kumlaumu Mungu ambaye hata hayupo maisha yako yote
:2Head:
 
Naomba kuelewesha.
Hivi ukikaa na njaa, ukalia na kutoa machozi, ukihudhuria nyumba za ibada kila mara — je, hiyo ndiyo itamfanya Mungu akutimizie haja zako za kiuchumi?
Yaani mtu akifanya hivyo kwa wingi, ndio moja kwa moja atapata ajira, faida kwenye biashara, na mafanikio mengine?
Tuseme umeomba sana ukaambulia ajira. Wakati huo huo kuna mamilioni hawana ajira, nao pia walisali na kufunga. Je, hapo utaweza kumsifu Mungu aliyewapa wachache ajira na kuwaacha wengi wenye vigezo vyote wakikosa nafasi?
Fikiria hivi:
Jeshi la uokoaji limeagizwa kwenda kuokoa wanafunzi katika bweni linalowaka moto. Katika hali ya kawaida kabisa, jeshi hilo lina uwezo wa kuokoa wanafunzi 100 kati ya 120 waliomo ndani. Lakini katika hali isiyo ya kawaida, likafanikiwa kuokoa wanafunzi 20 tu.
Je, hapo tutalisifu jeshi hilo kwa kuokoa wanafunzi 20 kati ya 120 na kuacha 100 wakipoteza maisha?
Kama kupata alama 20 kati ya 100 ni kufeli, je Mungu kumpa mtu mmoja ajira kati ya 1000 walioomba inakuwaje si kufeli, bali inaitwa kufaulu kunakopaswa kutukuzwa?
Hebu mtueleze, ni akili zipi zinatumika kumwelewa Mungu mwenye upendo na huruma pale anaposaidia wachache na kuwaacha wengi wakiendelea kuumia?
Asante kwa hoja yako , Kitu unachotakiwa kujua kuna watu wanateseka sababu ya vizazi vyao au family kuna maagano au kuna mambo waliyofanya kinyume na Mungu yanapelekea watoto waendelee kuteseka mpaka atapokea mtu mmoja kuvunja, na Wengine wanafanikiwa sababu vizazi vyao vya nyuma vilikuwa na mahusiano mazuri na Mungu hivyo wanaendelea kufanikiwa.

Kitu chengine ukiona Mambo magumu tenga muda jitafakali angalia tabia zako je ni sahihi mbele za Mungu, kama sio badilika , kuwa na moyo wa shukrani, upendo kwa wengine, kuwa na mahusiano na mtu mmoja pekee na tabia zengine then surrender kwa Mungu(hapa sali mfano mida ya saa 9 usiku mpala 11 hapo Mungu anaweza kupa direction ya changamoto zako kupitia ndoto.

Chengine badilisha mtazamo wako kuusu maisha acha kujitamkia maneno mabaya , jitamkie ushindi atakama unapitia magumu utapata direction ya maisha

Note kuenda kanisani , sijui kukesha sio 100% solution, solution unaweza pata kwa kuangalia mfumo wako wa maisha ukoje then badilsha na Mungu atakusaidia
 
1) Saa nyingine ukiwa maskini Mkristo umshukuru Mungu, ndomana Mungu anasema ushukuru kwa yote. Hujui maskini ni last born wa Bwana? ? Unafikiri MUNGU hajui unavyohisi?

Acha uwe maskini wa mali, ubaki tajiri wa Uadilifu wa MUNGU.

"Akawatazama wanafunzi wake, akasema: “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, kwa sababu ufalme wa Mungu ni wenu.

Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashibishwa. Mmebarikiwa ninyi mnaolia sasa, kwa sababu mtacheka."

Luka.6.20-21.NENO


2) Kuwa tajiri nao ni mtego, maana mtu anafikiri kapata utajiri kwasababu kwa namna fulani ni bora zaidi.

Sasa inakuwaje Mungu aseme ni rahisi kwa ngamia kuingia kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia kwenye Ufalme wa MUNGU? Si matajiri ndo wangeongoza kuingia?

"Yeyote aliye mwaminifu katika mambo madogo, pia ni mwaminifu katika mambo makubwa. Na yeyote asiye mwaminifu katika mambo madogo pia si mwaminifu katika mambo makubwa.

Ikiwa hamkuwa waaminifu katika mali ya kidunia, ni nani atakayewaaminia mali ya kweli?

Nanyi kama hamkuwa waaminifu na mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?"

Luka.16.10-12.NENO

Sasa mtu kapata utajiri halafu anautumia kutuchapia sisi maskini.

Utajiri wenyewe usikute kapata kwa kuonea maskini, mf. Kulipa vijakazi ujira mdogo.

Utajiri wako ni kwa ajili ya anasa zako na kujitukuza mwenyewe.

Ndomana YESU alisema huwezi kutumikia MUNGU na utajiri, hao ni Mabwana wawili tofauti, Falme mbili tofauti, Ulimwengu miwili tofauti.

3) Na hii ndo namna Mkristo tajiri anatumia utajiri wake:

"Waagize wale ambao ni matajiri wa ulimwengu huu waache kujivuna, wala wasiweke tumaini lao katika mali ambayo si ya hakika, bali waweke tumaini lao katika Mungu ambaye hutupatia vitu vyote kwa wingi ili tuvifurahie.

Waagize watende mema, wawe matajiri katika matendo mema, pia wawe wakarimu na walio tayari kushiriki mali yao na wengine."

1Timotheo.6.17-18.NENO


"Nia yetu si kwamba wengine wasaidike wakati ninyi mnateseka, bali pawe na uwiano.

Kwa wakati huu, wingi wa vitu mlivyo navyo utasaidia kutosheleza mahitaji yao, ili wakati wao watakapokuwa na wingi wa vitu, nao wapate kutosheleza mahitaji yenu.

Ndipo patakuwa na usawa, kama ilivyoandikwa: “Aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, wala aliyekusanya kidogo hakupungukiwa.”

2Wakorintho.8.13-15.NENO


Mkristo akiingia mahali ni Ufalme wa MUNGU umeingia hapo: wenye njaa watakula, wagonjwa watapata matibabu, majobless wanapata ma connection n.k

Pesa za Mkristo tajiri ni kwa ajili ya Ufalme wa MUNGU na si vinginevyo. (Sijasema ukatoe sadaka kanisani ujimalize)
 
Back
Top Bottom