Kwana hata Yesu si alituthibitishia hili,nashauri watu wasome maandiko [emoji23]
Mathayo 6 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁹ Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;
²⁰ bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;
²¹ kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.
…
²⁴ Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
²⁵ Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
²⁶ Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?
²⁷ Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
²⁸ Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
²⁹ nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
³⁰ Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
³¹ Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
³² Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
³³ Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
³⁴ Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.