Ukishuka Airport Dar ukapita barabara kuu unaona jinsi nchi na watu wake walivyochoka. Viongozi mnafeli wapi?

Lucas Mwashambwa ni mtetezi wa kila upuuzi unaofanywa na serikali hii ni chawa mwandamizi wa Samia.
 
Sisi wenyewe wenye nchi tunakuogopa huku kwetu, je wageni??? Daaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Ulishafika huko wakati ule au umeona video tu?
 
Maswali yako hayana mantiki yoyote.
Mwenzako anakufungua macho uone jinsi gani hela zinavyotafunwa na wachache bila maendeleo ya maana sasa unamgeukia yeye kwa maswali hayo kwa hiyo unataka achukue mshahara wake aanze kugawa mitaani kwa Watanzania wote wenye shida?
 
Kuhusu watu kuchoka ukute wana Afya kukuzidi wewe.
Nadhani ungejikita kwenye miundombinu na uongozi mbovu sio kusema Afya za watu.
Au unadhan kuwa na tumbo kubwa ndio afya
Hujaelewa ndugu.
Mtu mwenye maisha mazuri hata akiwa mwembamba anajulikana tu kuna nuru fulani anakuwa nayo tofauti na mtu aliyepigika na maisha kisha akakonda ni vitu viwili tofauti.
 
Kwenye mchakato wa kimaendeleo watu weusi huwa hawafuati plans/targets zilizowekwa wao huwa wanawaza kuiba tu alimbikizie tumbo lake bila kujali mustakabali wa wengine.
Kwa hapo wala simpingi
 
😂😂
 
Sababu kubwa inasababishwa na utofauti wa lifestyles kati ya Dar na mikoani.
Dar kila kitu kinahitaji pesa wakati mikoani vitu vingi ni bure na hata vinavyouzwa bei yake ni chee kitu ambacho inasaidia wengi kumudu.
Ila dar kila kitu ni expensive kuanzia mahali pa kulala,vyakula,usafiri pamoja na starehe zote ni gharama sasa kwa mtu asiye na kazi rasmi inamvuruga anajikuta kila siku malengo yake hayatimii na familia inampelekesha hawataki kujua hilo wanataka huduma na hapo ndipo makasiriko yanapoanza kuja unamuona kila mtu anayekatiza mbele yako ni mchawi
 
Yeah uko sahihi.
Mfano mzuri Tundulisu miaka ile alinusurika kidogo tu kupotezwa na wasiojulikana
 
Angeenda kujenga kwao uholanzi,kiliwapeleka kipi hapo?..walipofika hawakukuta social order?!
Kwa sababu Africa tumejaaliwa rasilimali ila hatujui kuzitumia ndio maana wanakuja.
Ulaya walikosa rasilimali ila wamejaaliwa akili na uono kwa hiyo lazima wataendelea kuja hadi siku tutakapopata uono wa kulingana nao na hiyo itachukua karne nyingi sana hadi tuje kulingana nao kimtazamo.
 
Ukiwa unatoka China, Dubai, Ulaya au nchi nyingine zilizoendelea utatamani kulia wakati ndo ndege inaanza kuingia Dar. Unajiona kabisa umerudi kwenye kupigika hata kama una hela.
Naisubiria kwa hamu hii siku nione pakoje nikifika kwenye hili eneo
 
Huo utafiti uchwara, professorial rubbish.
Umaskini katika nchi zote za Africa Mashariki umejikita vijijini zaidi kuliko mjini, nyumba za udongo/tembe ziko vijijini.
Utapiamlo na unyafuzi hapa Tanzania umejikita kwenye mikoa ya vijijini.
Kote duniani majiji yawakilisha fursa za kila aina kwa kila kundi, sio kila mtu anataka kulima.
 
Jidanganye ,endelea kukaa kwenye mabanda huko Mjini ukijifariji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…