Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 11,208
- 20,517
Kweli.. watu hawana time na miujizaSana sana Dar es salaam ndiko yalikojaa majinga.Sisi huku mikoani wachungaji matapeli wamebaki na makanisa yao ya mabati miaka na miaka.
Kweli.. watu hawana time na miujizaSana sana Dar es salaam ndiko yalikojaa majinga.Sisi huku mikoani wachungaji matapeli wamebaki na makanisa yao ya mabati miaka na miaka.
Hakuna mtu amewahi kupona kansa duniani mpaka sasa. Wanapigwa mionzi au chemotherapy na wana ongeza muda wa kuishi tu kati ya miaka 2-15 kutegemea na hali ya mgonjwa ilivyokuwa.Tuseme una kansa. Hela za kwenda kutibiwa hospitalini huna. Sanasana unakunywa mitishamba kwa kuambiwa ambiwa tu na watu lakini hupati nafuu yo yote. Halafu unaona shuhuda watu wamepona kansa kwa kuombewa na Mwamposa. Utaacha kwenda?
Baadhi ya wanaokwenda pale siyo wajinga bali hawana pa kukimbilia. Ukiongea na baadhi yao ndiyo utaelewa wanachopitia. Huduma mbovu za kijamii, umasikini uliokithiri, ufisadi wa kihayawani....
Umeongea ukweli Ndungu.Tumshukuru Mwamposa anawapa watu wetu matumaini! Umati huo mkubwa wa watu usipokuwa na majibu ya maisha yao nchi haitatawalika hii.
Mbona wengi wanaoenda kwa Mwamposa wanaenda kuombewa waondokane na umasikini na waendeshe magari bila kufanya kazi.Wewe unadhani watu wanapenda kwenda? Ukiwa na shida ndio utaona sio ujinga wakati wa kwenda kutafuta msaada kwa waganga au kwenda kuombewa. Hata wewe unaweza kupata shida ukafika sehemu ambayo hukutarajia kufika hata siku moja. Ukilitambua hilo usimbeze mtu anayetafuta suluhishi la matatizo yake kwa njia yoyote ile?
Gharama za siri ndiyo zipi?kama ni rahisi fanya wewe..kuna gharama wameingia tena kubwa sana nyingine za siri nyingine zinahusu pesa ndo anachomaanisha YoungPastor
Kwani tofauti ya Kiboko ya Wachawi yule Mkongo alikuwa anawatoza 500,000 kingilio kule Buza kabla hajatimuliwa na Serikali ni nini? Mwamposa ana survive kwa vile ni mwana CCM mwenzao, lakini wote MATAPELISio kweli kuna mwanangu anapiga hizo mishe ,na ana vichwa hapo mwanza wa kutosha , yeye mwenyewe ana kiri tukiwa bar kuwa wajjnga ni wengi
Hata wajinga hasajaacha kuzaliwa, bado wanaongezeka piakwanini uwasemee watu walochagua upande wao?, ni kwamba haujui watu wote hatuwezi kufanana kiakili na kimtazamo,, istoshe haya maneno ya utapeli hayajaanza kusemwa leo mbona bado wanajazana?
Je, unakubaliana na hoja kwamba wanaojazana kule ni mapumbavu yaliyokata tamaa ya maisha?Ndugu yangu akuna kitu kigumu kama kupata waumini
Wengi humu mnapenda sana kuongea kama hamna akili vichwani ila ukwel ni kwamba akuna kazi ngumu kama kupata waumini
Unaweza wachukulia poa sana hawa wachungaji wakubwa km kina mwamposa joe david na wengneo ila wametoka mbali sana hao waumini unao waona leo wamewatengeneza kwa muda mrefu sana na kwa nguvu kubwa sana
Usione leo hii wanawaibia kwa urahisi waumini wao ukazani ni kazi rahis aisee ni kaz sana wamefanya adi leo hii unawaona wanapiga pesa kirahisi
Tuwaheshimu sana hawa wachengaji ndio wanawaibia waumini wao ila jua wametumia nguvu na muda mwingi sana adi leo hii kuaminiwa na waumini wao
Asante
Nakubali kuhusu matatizo ya watu, lakini Mwamposa anatajirika kupitia sadaka zao. Imagine amejenga 4Star hotel pale Sistila Mbalizi Mbeya wakati maelfu ya anaowaombea wanatembea kwa mguu kutoka Kawe hadi Ubungo hata nauli hawanaHao watu unaowaona huko sio wajinga kiasi hicho unachofikili.
Ni vile tu wewe hauna matatizo hasa yakiroho.
Walio wengi wanapata suluhu ya matatizo waliyonayo.
Mpaka nitakapomuona kiwete niliyekuwa namfahamu mtaani kwangu ametupa magongo na kutembea nsipo nitaamini. Lakini hao wagonjwa wa kupangwa bado hujanisahwishiWewe unadhani watu wanapenda kwenda? Ukiwa na shida ndio utaona sio ujinga wakati wa kwenda kutafuta msaada kwa waganga au kwenda kuombewa. Hata wewe unaweza kupata shida ukafika sehemu ambayo hukutarajia kufika hata siku moja. Ukilitambua hilo usimbeze mtu anayetafuta suluhishi la matatizo yake kwa njia yoyote ile?
Namjua Mwamposa toka akihubiri pale Vatican Hotel Sinza. Na najua alikwenda Nigeria huko ambako wanapewa huo uchawi wa kuvuta wafuasi.Ndugu yangu akuna kitu kigumu kama kupata waumini
Wengi humu mnapenda sana kuongea kama hamna akili vichwani ila ukwel ni kwamba akuna kazi ngumu kama kupata waumini
Unaweza wachukulia poa sana hawa wachungaji wakubwa km kina mwamposa joe david na wengneo ila wametoka mbali sana hao waumini unao waona leo wamewatengeneza kwa muda mrefu sana na kwa nguvu kubwa sana
Usione leo hii wanawaibia kwa urahisi waumini wao ukazani ni kazi rahis aisee ni kaz sana wamefanya adi leo hii unawaona wanapiga pesa kirahisi
Tuwaheshimu sana hawa wachengaji ndio wanawaibia waumini wao ila jua wametumia nguvu na muda mwingi sana adi leo hii kuaminiwa na waumini wao
Asante
Nasadiki kwa Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume. No matter whatHata Roman Catholic kuna wapumbavu wengi tu, mna mtukana Mwamposa wakati kanisani kwenu RC nyuma ya mlango mmeweka maji ya chooni mnayaita maji ya baraka mnayatia madole 💩💩💩💩🤣😂 vijana tafuteni pesa mtaingiziwa dudu kwa chuki zenu
Shukrani kwa kuliweka vizuriJe, unakubaliana na hoja kwamba wanaojazana kule ni mapumbavu yaliyokata tamaa ya maisha?
Maana hoja inazungumzia upumbavu wa watu kujazana kwenye maombi ili wafanikiwe badala ya kuchapa kazi.
Hujui kwamba inafikia mahali waumini wanaambiwa mwaka huu hauishi bila kupata nyumba ama gari na mtu anaamini huku hana mipango yoyote ya kumuingizia hata laki mbili kwa mwezi.
Huu ni upumbavu sio upumbavu?
Hata hapa jf ..nikipima watu wa hapa ni nacho kiona ni UANITHI WA AKILI MKUBWA SANAView attachment 3642348View attachment 3642349View attachment 3642350
Ukiona watu wengi hivi ujuwe umasikini ni mkubwa sana, pia elimu ni duni katika jamii. Ibada za kijinga kabisa kuhusu miujiza, ni utapeli kutumia shida na ujinga wawatu kama fursa hadharani.
Tungekuwa na Serikali inayojali, ingetafakari ni wananchi wa kiasi gani walio katika hali ya kukata tamaa na kuhitaji uponyaji, si wa kiroho bali kiuchumi. Wanajaa hapa kupata maneno ya matumaini!
Miujiza si unatengeneza tu ...utapeli wa makanisani huwa ni organise ya watu zaidi ya 10Mpaka kanisa lako lianze kukulipa siyo mchezo pia,labda uwe na "miujiza" toka siku unalizindua na promo za kufa mtu.
Watu wako reluctant mno kujiunga na makanisa mapya!
Huwezi kuondoka nyumbn kuacha watoto(miaka chini ya kumi) ndani siku nzima,ijumaa mpaka jumamosi sababu ya mkesha. SPole sana. Kwanini umemuacha?
Hujaelewa nilichosema. Hata wewe leo hii ukiambiwa una aggressive (pancreatic) cancer na huna uwezo wa kwenda kupata hiyo chemo unayoisema, mbona kwa Mwamposa utakwenda tena utawahi kabisa na kukaa mbele ili mibaraka na miujiza isikupite. Kwa sasa unaweza kujiona msomi una logic lakini ukimaliza options zote za matumaini hakuna kitu ambacho utaacha kufanya ili kujaribu kupata suluhisho la kinachokusumbua. Hata placebo effects za muda mfupi tu zinakutosha.Hakuna mtu amewahi kupona kansa duniani mpaka sasa. Wanapigwa mionzi au chemotherapy na wana ongeza muda wa kuishi tu kati ya miaka 2-15 kutegemea na hali ya mgonjwa ilivyokuwa.
Ingekuwa Mwamposa ananuwezo wa kutibu kansa kwa maombi basi angekwenda tu pale Ocean Road. Ile hospitali kila wakati ina wagonjwa siyo chini ya 500 wanauguza kansa za ngozi, tezi dume, matiti, kizazi, koo nk
Acheni KUDANGANYWA, mbona mama yake Mwamposa alipougua mwaka jana Mwamposa alionekana Airport akimpeleka Ujerumani kutibiwa??