Ukitaka hela za haraka fungua kanisa kuna majinga mengi; kinachoendelea Kawe kwa Mwamposa kinasikitisha

Hakuna mtu amewahi kupona kansa duniani mpaka sasa. Wanapigwa mionzi au chemotherapy na wana ongeza muda wa kuishi tu kati ya miaka 2-15 kutegemea na hali ya mgonjwa ilivyokuwa.

Ingekuwa Mwamposa ananuwezo wa kutibu kansa kwa maombi basi angekwenda tu pale Ocean Road. Ile hospitali kila wakati ina wagonjwa siyo chini ya 500 wanauguza kansa za ngozi, tezi dume, matiti, kizazi, koo nk

Acheni KUDANGANYWA, mbona mama yake Mwamposa alipougua mwaka jana Mwamposa alionekana Airport akimpeleka Ujerumani kutibiwa??
 
Mbona wengi wanaoenda kwa Mwamposa wanaenda kuombewa waondokane na umasikini na waendeshe magari bila kufanya kazi.

Huoni matangazo yao yanavyosema? Utasikia tangazo linasema 'Vuka mwaka na utajiri', mara 'Anza mwaka na ajira' na matangazo kama hayo.

Hakuna tajiri hata mmoja aliyefanikiwa kwa kwenda kuombewa na wachungaji bali wame hustle kwelikweli.
 
Sio kweli kuna mwanangu anapiga hizo mishe ,na ana vichwa hapo mwanza wa kutosha , yeye mwenyewe ana kiri tukiwa bar kuwa wajjnga ni wengi
Kwani tofauti ya Kiboko ya Wachawi yule Mkongo alikuwa anawatoza 500,000 kingilio kule Buza kabla hajatimuliwa na Serikali ni nini? Mwamposa ana survive kwa vile ni mwana CCM mwenzao, lakini wote MATAPELI
 
kwanini uwasemee watu walochagua upande wao?, ni kwamba haujui watu wote hatuwezi kufanana kiakili na kimtazamo,, istoshe haya maneno ya utapeli hayajaanza kusemwa leo mbona bado wanajazana?
Hata wajinga hasajaacha kuzaliwa, bado wanaongezeka pia
 
Je, unakubaliana na hoja kwamba wanaojazana kule ni mapumbavu yaliyokata tamaa ya maisha?

Maana hoja inazungumzia upumbavu wa watu kujazana kwenye maombi ili wafanikiwe badala ya kuchapa kazi.

Hujui kwamba inafikia mahali waumini wanaambiwa mwaka huu hauishi bila kupata nyumba ama gari na mtu anaamini huku hana mipango yoyote ya kumuingizia hata laki mbili kwa mwezi.

Huu ni upumbavu sio upumbavu?
 
Hao watu unaowaona huko sio wajinga kiasi hicho unachofikili.

Ni vile tu wewe hauna matatizo hasa yakiroho.

Walio wengi wanapata suluhu ya matatizo waliyonayo.
Nakubali kuhusu matatizo ya watu, lakini Mwamposa anatajirika kupitia sadaka zao. Imagine amejenga 4Star hotel pale Sistila Mbalizi Mbeya wakati maelfu ya anaowaombea wanatembea kwa mguu kutoka Kawe hadi Ubungo hata nauli hawana
 
Mpaka nitakapomuona kiwete niliyekuwa namfahamu mtaani kwangu ametupa magongo na kutembea nsipo nitaamini. Lakini hao wagonjwa wa kupangwa bado hujanisahwishi
 
Namjua Mwamposa toka akihubiri pale Vatican Hotel Sinza. Na najua alikwenda Nigeria huko ambako wanapewa huo uchawi wa kuvuta wafuasi.

Nawe ukitaka njoo DM nikuelekeze
 
Nasadiki kwa Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume. No matter what
 
Shukrani kwa kuliweka vizuri
 
Hata hapa jf ..nikipima watu wa hapa ni nacho kiona ni UANITHI WA AKILI MKUBWA SANA
 
Mpaka kanisa lako lianze kukulipa siyo mchezo pia,labda uwe na "miujiza" toka siku unalizindua na promo za kufa mtu.

Watu wako reluctant mno kujiunga na makanisa mapya!
Miujiza si unatengeneza tu ...utapeli wa makanisani huwa ni organise ya watu zaidi ya 10
 
Hujaelewa nilichosema. Hata wewe leo hii ukiambiwa una aggressive (pancreatic) cancer na huna uwezo wa kwenda kupata hiyo chemo unayoisema, mbona kwa Mwamposa utakwenda tena utawahi kabisa na kukaa mbele ili mibaraka na miujiza isikupite. Kwa sasa unaweza kujiona msomi una logic lakini ukimaliza options zote za matumaini hakuna kitu ambacho utaacha kufanya ili kujaribu kupata suluhisho la kinachokusumbua. Hata placebo effects za muda mfupi tu zinakutosha.

Nenda ukaongee na watu wanaosafiri kutoka Musoma, Karagwe, Kigoma na kwingineko na kusafiri safari ndefu kuja kwenye hii mikesha. Watu wana matatizo makubwa na hawana matumaini. Na ogopa sana mtu anayekaribia kupoteza matumaini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…