makaveli10
JF-Expert Member
- Mar 27, 2013
- 31,583
- 92,670
Ulicheza kama pele.Katika kete nilizocheza vizuri maishani mwangu ni kujenga Kigamboni baada ya kuuza Madale.
Ila kila shetani na mbuyu wake.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ulicheza kama pele.Katika kete nilizocheza vizuri maishani mwangu ni kujenga Kigamboni baada ya kuuza Madale.
Ila kila shetani na mbuyu wake.
Duh kweli ni gharama mkuu wapunguze beiUtalipa darajani 2000tsh kila unapopita kwa mwezi bei gani?
Uzuri wa Kigamboni ni kuwa hata kama unafanya kazi mjini, foleni unapishana nayo kwa kushangaa upande wenye foleni.Kigamboni (sasa ni wilaya) ni sehemu ya jiji la Dar es Salaam ambayo tofauti na maeneo mengine ilichelewa kuendelezwa kimiundombinu mpaka kufika miaka ya 90 .Watu walichelea kuishi huko kutokana na kupaona ni maporini palipostahili kuishi wanyama.
Hivi leo,mambo ni tofauti sana,mji unakua kwa kasi ya ajabu, barabara zinajengwa kutangulia makazi ya watu,ni sehemu pekee katika jiji la Dar es Salaam ambako ukiingia unasahau kuhusu foleni za barabarani , hali ya hewa ni nzuri kutokana kutokuwepo kwa ujenzi holela wa nyumba, ni karibu sana na city centre na kuna fursa nyingi za kuanzisha biashara.
Binafsi nilifika kwa mara ya kwanza na kuhamia kigamboni mwaka 2015 kutoka Survey maeneo ya karibu na Mlimani city nilipoishi kwa takribani miaka minne,ila mpaka kufikia leo sijawahi kujutia kuishi huku wala kuwaza kuhamia mahali pengine katika mji huu kutokana na sifa nilizozitaja hapo juu na kwa bahati nzuri Mungu amenijaalia kujenga kakibanda huku huku.
Kwa ambao hawajawahi kufika huku hudhani kwamba Kigamboni ni kisiwa na kwamba usafiri pekee wa kufika huku ni wa kuvuka maji kwa pantoni, la hasha! Kigamboni si kisiwa bali imetenganishwa na sehemu nyingine ya jiji kwa sehemu ya bahari iliyoingia nchi kavu (ghuba) ambayo ni bandari ya Dar es Salaam na Kwa sasa ukiachilia usafiri wa wa pantoni kuna daraja na baraba mbili ambazo unaweza kupita bila hata kuiona hiyo bahari.
Karibuni sana Kigamboni.
Hivi kisarawe pako poa?Nawaangalia watu wanaongea tu, Kisarawe hawaijui hawa. TATIZO Usalama wa ule msitu huwa unanipa mashaka sana nyakati za usiku
100%Kigamboni (sasa ni wilaya) ni sehemu ya jiji la Dar es Salaam ambayo tofauti na maeneo mengine ilichelewa kuendelezwa kimiundombinu mpaka kufika miaka ya 90 .Watu walichelea kuishi huko kutokana na kupaona ni maporini palipostahili kuishi wanyama.
Hivi leo,mambo ni tofauti sana,mji unakua kwa kasi ya ajabu, barabara zinajengwa kutangulia makazi ya watu,ni sehemu pekee katika jiji la Dar es Salaam ambako ukiingia unasahau kuhusu foleni za barabarani , hali ya hewa ni nzuri kutokana kutokuwepo kwa ujenzi holela wa nyumba, ni karibu sana na city centre na kuna fursa nyingi za kuanzisha biashara.
Binafsi nilifika kwa mara ya kwanza na kuhamia kigamboni mwaka 2015 kutoka Survey maeneo ya karibu na Mlimani city nilipoishi kwa takribani miaka minne,ila mpaka kufikia leo sijawahi kujutia kuishi huku wala kuwaza kuhamia mahali pengine katika mji huu kutokana na sifa nilizozitaja hapo juu na kwa bahati nzuri Mungu amenijaalia kujenga kakibanda huku huku.
Kwa ambao hawajawahi kufika huku hudhani kwamba Kigamboni ni kisiwa na kwamba usafiri pekee wa kufika huku ni wa kuvuka maji kwa pantoni, la hasha! Kigamboni si kisiwa bali imetenganishwa na sehemu nyingine ya jiji kwa sehemu ya bahari iliyoingia nchi kavu (ghuba) ambayo ni bandari ya Dar es Salaam na Kwa sasa ukiachilia usafiri wa wa pantoni kuna daraja na baraba mbili ambazo unaweza kupita bila hata kuiona hiyo bahari.
Karibuni sana Kigamboni.
Hapana sio kweli,mie juzi nilikuwa uko maeneo ya mji mwema,kufika saa tatu hakuna gari hata moja,ni vibajaji tuHiyo ilikua zamani sio sasa,gari zinakwenda kibada ,kongowe saivi nyingi tu ,mpaka za kariakoo kupitia darajani
Hiyo standy, kama unaitumia tu kurahisisha unapoenda mkoa, na siyo kibiashara inakupoteza,hapana mku, kigamboni hapafai kabisa, kama ni kwa sababu ya bahari tu sawa lkn kuna changamoto ya usafiri sana, nilifikia huko niliona tabu zake, nilitakiwa kuamka saa 9 usiku kwenda stendi ya Magufuli mbezi, siwezi kuishi mbali na kituo cha mabasi ya kwenda mikoani.
Mpango mzima sasa ni Mbezi, Luguruni, kibamba, kiluvya na kibaha.
Hongera kuna fikra za mtandaoni ukizifuata huwezi kujikomboa Dar, wengi tunapasifia kinondoni kawe, kwenye nyumba za kupanga, bora ujenge huko kigamboni kongowe miembe saba kibaha, alafu rudi upange magomeni, utakua na cha kujivunia mjini.Ndio napotaka kununua kiwanja huko.. Hata iwe maporini kabisa
Uwe na pesa yako piaDaraja la nyerere ni chap tu ila uwe na usafiri wako
Mji unakuwa Kigamboni size yake kama wilaya mbili za Dar. So kujaa itachelewa ila na maendeleo yamewahi fikaHongera kuna fikra za mtandaoni ukizifuata huwezi kujikomboa Dar, wengi tunapasifia kinondoni kawe, kwenye nyumba za kupanga, bora ujenge huko kigamboni kongowe miembe saba kibaha, alafu rudi upange magomeni, utakua na cha kujivunia mjini.
Kuna watu niliwakuta mjini enzi hizo Standy ya magari ya bagamoyo iko pale kariakoo mnafani, mpaka leo wako na maisha yaleyale, ilimradi wanaishi Kariakoo.
Ukipata muda tembea kuanzia Mji mwema Hadi Mikwambe uone viwanja vilivyopo barabara hio peke yake achana na zile hotels za baharini. Ikifika weekend napata shida niende wapi. Kigamboni sihami tena nazidi kusogea mbele kule nishafika Dege eco village
Pls Nipe kazi ya kubrand hiyo product kasie mahaba
Viwanja vinauzwa KIGAMBONI mwembe mdogo karibia na chuo cha afya kigamboni college
1. Umbali kutoka ferry mpk site ni killometer 23
2. Viwanja vimepimwa ila vipo katika michakato ya hati kwahy ukinunua unapata kwa jina lako rasmi
3. Umeme umefika tayar kumetulia hali ya hewa ni safi sana
Meter 8* 22 mil 1.5
Meter 15*20mil 2.5
Meter 35*35 mil 5
Kuhusu punguzo ondoa shaka kila kitu ni maelewano.View attachment 1821559