Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Shida kweli kweli na ma gharama yani ina maana wewe kuvuka itakulazimu upoteze 90-100K per months kwenda na kurudi kwako! Huu ujinga ndio unanifanya kigamboni sitaki hata kupasikia
Point kubwa sana. Ngoja tusubiri deni liishe, waondoe hiyo kodi "fee" ya kuvuka kama mchangiaji hapo alivyosema
 
Kigamboni (sasa ni wilaya) ni sehemu ya jiji la Dar es Salaam ambayo tofauti na maeneo mengine ilichelewa kuendelezwa kimiundombinu mpaka kufika miaka ya 90 .Watu walichelea kuishi huko kutokana na kupaona ni maporini palipostahili kuishi wanyama.

Hivi leo,mambo ni tofauti sana,mji unakua kwa kasi ya ajabu, barabara zinajengwa kutangulia makazi ya watu,ni sehemu pekee katika jiji la Dar es Salaam ambako ukiingia unasahau kuhusu foleni za barabarani , hali ya hewa ni nzuri kutokana kutokuwepo kwa ujenzi holela wa nyumba, ni karibu sana na city centre na kuna fursa nyingi za kuanzisha biashara.

Binafsi nilifika kwa mara ya kwanza na kuhamia kigamboni mwaka 2015 kutoka Survey maeneo ya karibu na Mlimani city nilipoishi kwa takribani miaka minne,ila mpaka kufikia leo sijawahi kujutia kuishi huku wala kuwaza kuhamia mahali pengine katika mji huu kutokana na sifa nilizozitaja hapo juu na kwa bahati nzuri Mungu amenijaalia kujenga kakibanda huku huku.

Kwa ambao hawajawahi kufika huku hudhani kwamba Kigamboni ni kisiwa na kwamba usafiri pekee wa kufika huku ni wa kuvuka maji kwa pantoni, la hasha! Kigamboni si kisiwa bali imetenganishwa na sehemu nyingine ya jiji kwa sehemu ya bahari iliyoingia nchi kavu (ghuba) ambayo ni bandari ya Dar es Salaam na Kwa sasa ukiachilia usafiri wa wa pantoni kuna daraja na baraba mbili ambazo unaweza kupita bila hata kuiona hiyo bahari.

Karibuni sana Kigamboni.
Sisi wa mkoani tunacomment wapi
 
Acha fix wewe. Mimi kuna siku nakaa huko Juliana,samaki samaki Hadi saa Saba nane na ninarudi Kigamboni usiku sina mlinzi geti nafungua mwenyewe. Niliishi miaka mitatu bila geti
Jamaa angu ni kilema sasa hivi walimcharanga mapanga... Mwingine alipigwa tukio akiwa amelala wakaiba nyaraka za ofisi kesho yake akaweka electrical fence... Wote Gezaulole

Sent from my SM-G970U1 using JamiiForums mobile app
 
Kigamboni (sasa ni wilaya) ni sehemu ya jiji la Dar es Salaam ambayo tofauti na maeneo mengine ilichelewa kuendelezwa kimiundombinu mpaka kufika miaka ya 90. Watu walichelea kuishi huko kutokana na kupaona ni maporini palipostahili kuishi wanyama.

Hivi leo, mambo ni tofauti sana, mji unakua kwa kasi ya ajabu, barabara zinajengwa kutangulia makazi ya watu, ni sehemu pekee katika jiji la Dar es Salaam ambako ukiingia unasahau kuhusu foleni za barabarani, hali ya hewa ni nzuri kutokana kutokuwepo kwa ujenzi holela wa nyumba, ni karibu sana na city centre na kuna fursa nyingi za kuanzisha biashara.

Binafsi nilifika kwa mara ya kwanza na kuhamia Kigamboni mwaka 2015 kutoka Survey maeneo ya karibu na Mlimani city nilipoishi kwa takribani miaka minne ila mpaka kufikia leo sijawahi kujutia kuishi huku wala kuwaza kuhamia mahali pengine katika mji huu kutokana na sifa nilizozitaja hapo juu na kwa bahati nzuri Mungu amenijaalia kujenga kakibanda huku huku.

Kwa ambao hawajawahi kufika huku hudhani kwamba Kigamboni ni kisiwa na kwamba usafiri pekee wa kufika huku ni wa kuvuka maji kwa pantoni, la hasha! Kigamboni si kisiwa bali imetenganishwa na sehemu nyingine ya jiji kwa sehemu ya bahari iliyoingia nchi kavu (ghuba) ambayo ni bandari ya Dar es Salaam na Kwa sasa ukiachilia usafiri wa wa pantoni kuna daraja na barabara mbili ambazo unaweza kupita bila hata kuiona hiyo bahari.

Karibuni sana Kigamboni.
Kigamboni huijui vizuri wewe,wakati wa msimu wa joto Kigamboni hakufai ni joto kweli, wanaoishi vizuri labda wenye eisii tu,wakati wa baridi Kigamboni ni balaa........
 
Viwanja vinauzwa KIGAMBONI mwembe mdogo karibia na chuo cha afya kigamboni college

1. Umbali kutoka ferry mpk site ni killometer 23

2. Viwanja vimepimwa ila vipo katika michakato ya hati kwahy ukinunua unapata kwa jina lako rasmi

3. Umeme umefika tayar kumetulia hali ya hewa ni safi sana

Meter 8* 22 mil 1.5

Meter 15*20mil 2.5

Meter 35*35 mil 5

Kuhusu punguzo ondoa shaka kila kitu ni maelewano.View attachment 1821559
Hapa ndio si pa kuweka mguu... Beto nje nje wahuni wengi tena ni boda boda

Sent from my SM-G970U1 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni kweli mi kuna siku nimelala mara naskia kuna gari nje linapita lakini nyuma kuna geti linafurutwa linapiga kelele sana, asubuhi watu wakasema inaonekana walienda sehemu kufanya yao wakakutana na vikwazo, wakatoka nduki
Hawakomi kule mkuu... Kuna wizi ssa ivi kama unakula bata unasikia mwenye gari namba flan umepak vibaya ukijichanganya ukienda unakutana na chuma

Sent from my SM-G970U1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom