copernicucci98
JF-Expert Member
- Jul 28, 2018
- 1,232
- 2,362
Point kubwa sana. Ngoja tusubiri deni liishe, waondoe hiyo kodi "fee" ya kuvuka kama mchangiaji hapo alivyosemaShida kweli kweli na ma gharama yani ina maana wewe kuvuka itakulazimu upoteze 90-100K per months kwenda na kurudi kwako! Huu ujinga ndio unanifanya kigamboni sitaki hata kupasikia
Sisi wa mkoani tunacomment wapiKigamboni (sasa ni wilaya) ni sehemu ya jiji la Dar es Salaam ambayo tofauti na maeneo mengine ilichelewa kuendelezwa kimiundombinu mpaka kufika miaka ya 90 .Watu walichelea kuishi huko kutokana na kupaona ni maporini palipostahili kuishi wanyama.
Hivi leo,mambo ni tofauti sana,mji unakua kwa kasi ya ajabu, barabara zinajengwa kutangulia makazi ya watu,ni sehemu pekee katika jiji la Dar es Salaam ambako ukiingia unasahau kuhusu foleni za barabarani , hali ya hewa ni nzuri kutokana kutokuwepo kwa ujenzi holela wa nyumba, ni karibu sana na city centre na kuna fursa nyingi za kuanzisha biashara.
Binafsi nilifika kwa mara ya kwanza na kuhamia kigamboni mwaka 2015 kutoka Survey maeneo ya karibu na Mlimani city nilipoishi kwa takribani miaka minne,ila mpaka kufikia leo sijawahi kujutia kuishi huku wala kuwaza kuhamia mahali pengine katika mji huu kutokana na sifa nilizozitaja hapo juu na kwa bahati nzuri Mungu amenijaalia kujenga kakibanda huku huku.
Kwa ambao hawajawahi kufika huku hudhani kwamba Kigamboni ni kisiwa na kwamba usafiri pekee wa kufika huku ni wa kuvuka maji kwa pantoni, la hasha! Kigamboni si kisiwa bali imetenganishwa na sehemu nyingine ya jiji kwa sehemu ya bahari iliyoingia nchi kavu (ghuba) ambayo ni bandari ya Dar es Salaam na Kwa sasa ukiachilia usafiri wa wa pantoni kuna daraja na baraba mbili ambazo unaweza kupita bila hata kuiona hiyo bahari.
Karibuni sana Kigamboni.
Mchango utaisha ukiwa ushazikwa miaka 30 mbele haina maanaPoint kubwa sana. Ngoja tusubiri deni liishe, waondoe hiyo kodi "fee" ya kuvuka kama mchangiaji hapo alivyosema
U spoke my mind... Kigamboni kuna uhalifu si wa kitoto... Wahuni wanajificha Kimbiji hukoUkitaka mwisho wako wa Kutembea kutokana na Vibaka na Majambazi kuwa wengi na Kula Kwako Bata ( Kustarehe ) kuwe ni Saa 12 Jioni, basi kaishi Kigamboni.
Kwa mandhar ni pazuri ila kwa huduma ni pahovyoIla ni kuzuri kwelikweli asikwambie mtu ...I love that place
Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Jamaa angu ni kilema sasa hivi walimcharanga mapanga... Mwingine alipigwa tukio akiwa amelala wakaiba nyaraka za ofisi kesho yake akaweka electrical fence... Wote GezauloleAcha fix wewe. Mimi kuna siku nakaa huko Juliana,samaki samaki Hadi saa Saba nane na ninarudi Kigamboni usiku sina mlinzi geti nafungua mwenyewe. Niliishi miaka mitatu bila geti
Kigamboni huijui vizuri wewe,wakati wa msimu wa joto Kigamboni hakufai ni joto kweli, wanaoishi vizuri labda wenye eisii tu,wakati wa baridi Kigamboni ni balaa........Kigamboni (sasa ni wilaya) ni sehemu ya jiji la Dar es Salaam ambayo tofauti na maeneo mengine ilichelewa kuendelezwa kimiundombinu mpaka kufika miaka ya 90. Watu walichelea kuishi huko kutokana na kupaona ni maporini palipostahili kuishi wanyama.
Hivi leo, mambo ni tofauti sana, mji unakua kwa kasi ya ajabu, barabara zinajengwa kutangulia makazi ya watu, ni sehemu pekee katika jiji la Dar es Salaam ambako ukiingia unasahau kuhusu foleni za barabarani, hali ya hewa ni nzuri kutokana kutokuwepo kwa ujenzi holela wa nyumba, ni karibu sana na city centre na kuna fursa nyingi za kuanzisha biashara.
Binafsi nilifika kwa mara ya kwanza na kuhamia Kigamboni mwaka 2015 kutoka Survey maeneo ya karibu na Mlimani city nilipoishi kwa takribani miaka minne ila mpaka kufikia leo sijawahi kujutia kuishi huku wala kuwaza kuhamia mahali pengine katika mji huu kutokana na sifa nilizozitaja hapo juu na kwa bahati nzuri Mungu amenijaalia kujenga kakibanda huku huku.
Kwa ambao hawajawahi kufika huku hudhani kwamba Kigamboni ni kisiwa na kwamba usafiri pekee wa kufika huku ni wa kuvuka maji kwa pantoni, la hasha! Kigamboni si kisiwa bali imetenganishwa na sehemu nyingine ya jiji kwa sehemu ya bahari iliyoingia nchi kavu (ghuba) ambayo ni bandari ya Dar es Salaam na Kwa sasa ukiachilia usafiri wa wa pantoni kuna daraja na barabara mbili ambazo unaweza kupita bila hata kuiona hiyo bahari.
Karibuni sana Kigamboni.
Uwongo Kigamboni bado ni remote place eneo kubwa... Hakuna unafuu kule...Vibaka walikua ni beach boys,maeneo ya mikadi,machava na ferry .wengi walishakamatwa,mji mwema,geza ulole,shagwe,uko kwa kishua saivi,kibaka hauwezi muona.
Hapa ndio si pa kuweka mguu... Beto nje nje wahuni wengi tena ni boda bodaViwanja vinauzwa KIGAMBONI mwembe mdogo karibia na chuo cha afya kigamboni college
1. Umbali kutoka ferry mpk site ni killometer 23
2. Viwanja vimepimwa ila vipo katika michakato ya hati kwahy ukinunua unapata kwa jina lako rasmi
3. Umeme umefika tayar kumetulia hali ya hewa ni safi sana
Meter 8* 22 mil 1.5
Meter 15*20mil 2.5
Meter 35*35 mil 5
Kuhusu punguzo ondoa shaka kila kitu ni maelewano.View attachment 1821559
Hawakomi kule mkuu... Kuna wizi ssa ivi kama unakula bata unasikia mwenye gari namba flan umepak vibaya ukijichanganya ukienda unakutana na chumaHii ni kweli mi kuna siku nimelala mara naskia kuna gari nje linapita lakini nyuma kuna geti linafurutwa linapiga kelele sana, asubuhi watu wakasema inaonekana walienda sehemu kufanya yao wakakutana na vikwazo, wakatoka nduki
Watu hapa wanasema kumepoa ila ni bahati yao hawajakutwa na matukio.. Huyo jamaa aliepigwa panga alikaa coma mwezi[emoji20]Yeah wanajua kuna watu wanapesa za maana, hasa, mkuu mimi nilienda kumsalimia ndugu ila story nilizokuwa naskia tu duu, nikaona hapa acha nilirudi nilikotoka
I read somewhere about posthumoral life..Mchango utaisha ukiwa ushazikwa miaka 30 mbele haina maana
Kwa dar temeke ndio ipo nyuma sana kimaendeleo kulinganisha na manispaa nyingine za darKigamboni kumenikalia kushoto sana. Temeke ndo baba lao bwana. Nyie nendeni nnje ya miji uko mking'atwa na nyoka msitusumbue manake mmewafata wenyewe hao nyoka.
Ujambazi hakuna, mi nimewahi acha nyumba ina kila kitu bila mlinzi miezi 2 ila hawakuiba hata AC zilizokuwepo nje