Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Kigamboni (sasa ni wilaya) ni sehemu ya jiji la Dar es Salaam ambayo tofauti na maeneo mengine ilichelewa kuendelezwa kimiundombinu mpaka kufika miaka ya 90. Watu walichelea kuishi huko kutokana na kupaona ni maporini palipostahili kuishi wanyama.

Hivi leo, mambo ni tofauti sana, mji unakua kwa kasi ya ajabu, barabara zinajengwa kutangulia makazi ya watu, ni sehemu pekee katika jiji la Dar es Salaam ambako ukiingia unasahau kuhusu foleni za barabarani, hali ya hewa ni nzuri kutokana kutokuwepo kwa ujenzi holela wa nyumba, ni karibu sana na city centre na kuna fursa nyingi za kuanzisha biashara.

Binafsi nilifika kwa mara ya kwanza na kuhamia Kigamboni mwaka 2015 kutoka Survey maeneo ya karibu na Mlimani city nilipoishi kwa takribani miaka minne ila mpaka kufikia leo sijawahi kujutia kuishi huku wala kuwaza kuhamia mahali pengine katika mji huu kutokana na sifa nilizozitaja hapo juu na kwa bahati nzuri Mungu amenijaalia kujenga kakibanda huku huku.

Kwa ambao hawajawahi kufika huku hudhani kwamba Kigamboni ni kisiwa na kwamba usafiri pekee wa kufika huku ni wa kuvuka maji kwa pantoni, la hasha! Kigamboni si kisiwa bali imetenganishwa na sehemu nyingine ya jiji kwa sehemu ya bahari iliyoingia nchi kavu (ghuba) ambayo ni bandari ya Dar es Salaam na Kwa sasa ukiachilia usafiri wa wa pantoni kuna daraja na barabara mbili ambazo unaweza kupita bila hata kuiona hiyo bahari.

Karibuni sana Kigamboni.
Kigamboni sio Dar
 
Usikute ata hapajui vizuri

Watuache na kigamboni yetu

Tena ngoja nizame Longoni beach resort nikanywe beer weekend Leo ulinzi wa kutosha toka NAVY FORCE JWTZ

Sio vibaa vya mtaani kidogo tu ngumi
IMG_20220310_185721.jpg
 
Mbezi malamba mawili is better,karibu na bus terminal,karibu na airport,beach aziko mbali kihivyo,kigamboni ukitaka uione chungu uwe na safari ya mkoani kwa zile gari zinatoka saa 12 asubuhi ndio utajua haujui!
 
Unatufokea?!! Sister du huwezi kukaa huko. Hakuna Kidimbwi,Samaki samaki. Wapangaji wengi wa Kigamboni ni wafanyakazi wa makampuni za mafuta,bandari,serikali kabla ya kuhamia Dodoma na wanafuzi wa IFM,TIA,Mwl Nyerere.
😂😂😂😂Siwafokei bhana,hata Mimi Ni mmoja Kati ya makundi uliyotaja.Kuhusu bata mbona hata huko Kuna Pwezapweza,Cape joint,mmeongezewa na cape Giant na Nolasco.... Yaani huko kuzuri kwenda beach tu sio kukaa pamepoaa....
 
😂😂😂😂Siwafokei bhana,hata Mimi Ni mmoja Kati ya makundi uliyotaja.Kuhusu bata mbona hata huko Kuna Pwezapweza,Cape joint,mmeongezewa na cape Giant na Nolasco.... Yaani huko kuzuri kwenda beach tu sio kukaa pamepoaa....
Duh mbona unavijua viwanja kama mkazi?!
 
Mbezi malamba mawili is better,karibu na bus terminal,karibu na airport,beach aziko mbali kihivyo,kigamboni ukitaka uione chungu uwe na safari ya mkoani kwa zile gari zinatoka saa 12 asubuhi ndio utajua haujui!
Siku hizi buses zinaanzia Kigamboni na kurudi zinaleta watu hadi Kigamboni. Wafanyabiashara wanajiongeza.
 
Huko chocho zote nazijua sio viwanja tu hata kwa wahanga maarufu napajua😂😂😂by the way bado nina watu wangu huko wanashindaga pale kwa mwingira so huwa napay visit mara mojamoja
Ukipita huko siku moja nishtue.
 
Back
Top Bottom