Ukitaka kujipima kama una upendo wa kweli na uvumilivu basi fuga mbuzi wa kienyeji

Ndio maana wahuni wana tusi lao la kuita watu Mbuzi watakua wamemkagua sana...
 
Mbuzi anapenda kula miti dawa, hivyo supu ya utumbo wake ni dawa
 
Usiombe uchunge mbuzi kipindi cha masika ukijani jani umeanza kutoka,...

Sisi tulikuwa na mbuzi kama 100 Kijijini kwetu ila alikuwepo mbuzi aliyekuwa anakula mpka ugali na nyama yaani lilikuwa li lafi balaa...
 
Menikumbusha mzee wetu aliwahi leta mbuzi kwaajili ya sharehe ya Christmas one week before.. Ili achinjwe siku ya sherehe ila sababu ya show zake ilibidi achinjwe mapema kabla hata sherehe haijafika. Akasubiri sherehe akiwa kwa friji...
 
Kuna kipindi niliuza mabeberu yote, yakabaki majike 6 nilitaka nibadilishe mbegu.

Sasa kumbe Kuna jike mmoja akaingia kwenye heat, halafu hakuna beberu.

Usiku nasikia ooooh oo psi , psi oooooh psi psi. Nikaamka najiuliza huyo beberu katokea wapi. Kumbe ni yule jike anatongoza na kupanda wenzake.
 
 
Jamaa umetupanga hapa!!
Yaani jike alikuwa kama yule marehemu wa Mgodini?
 
Baba angu mdogo anafuga mbuz anao wengi ni kisiran huyoo anawapenda mbuz wake balaa
 
Umenikumbusha mbali mkuu kuna mahali niliwahi ishi mwenye nyumba wetu alikuwa na hii mifugo, basi ilikuwa inakutwa na mauti mara kwa mara na mwenyewe hajui inasbabishwa na nn.
Kumbe ndgu mchungaji kila mbuzi wanapomsumbua anawasubiria wakishaingia bandani tu ni kipgo kwa kwenda mbele na alishia kuwamaliza tu kw kuwaua maana hawasikii kfupi jmaa roho mbaya
 
Wachungaji msiasahau wale mliokuwa mnakula mbususu za mbuzi machungani enzi za kubalehe….
Hilo haliongelewi humu, halafu huyo mdada mbuzi / ng'ombe analeta mahaba Hadi nyumbani wanawastukia, wazee wanatambua ila watakauka na mhusika anafikiri NI Siri kumbe nyumba nzima wanajua maana yule mbuzi (ke) kila anapomuona mchungaji (jamaa yake) wake lazima amfuate na hata wakiwa machungani anakuwa nyuma nyuma pamoja na mchungaji yeye hana kiherere kama wengine [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Watu tumechunga sana mbuzi, tumepigwa sana kwa makosa ya mbuzi, mpaka tumekomaa kiaskari. Ila unakuja mjini unakuta mtu anajioona mwambaa. Unamuangalia unasema hiiii!!
 
Menikumbusha mzee wetu aliwahi leta mbuzi kwaajili ya sharehe ya Christmas one week before.. Ili achinjwe siku ya sherehe ila sababu ya show zake ilibidi achinjwe mapema kabla hata sherehe haijafika. Akasubiri sherehe akiwa kwa friji...
Hawa wetu hasa walikuwa kwa ajili ya Idd ilipofika tukamgomea mzee asichinjwe hata mmoja na watoto wote tukaanza kulia mzee alizoea kualika watu pale msikitini yaani akifika anamuwahi Shekh na kumwambia atangaze saa Saba wakitoka msikini wote wapite nyumbani kuna chochote hiyo ni kila Idd. [emoji3][emoji3][emoji3] siku hiyo kaenda kachelewa kwa makusudi halafu akakaa nyuma Shekh asimuone ili akitoka awe wa mwanzo mwanzo pasiwe na mwaliko, [emoji3][emoji3] Shekh kaangaza akamuona pale pale Shekh akatimiza wajibu Assalam Alaykum baada ya swala ya dhuhuri mzee X. anawakaribisha nyumbani kama kawaida msikose" mzee kusikia Hilo hakuna kusikiliza mawaidha Tena ikabidi amtume mmoja wetu atuambie upesi tukutane nyumbani tukatumwa kilo mbili mbili za nyama buchani basi hakutugusa Tena na hao mbuzi Hadi tulipoondoka akawapeleka kwa mtu wakakae hakuwafuata tena

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Mbuzi kagoma kwenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…