Ukitaka kujipima kama una upendo wa kweli na uvumilivu basi fuga mbuzi wa kienyeji

Mbuzi kwa dharau wanaweza kulia bandani bila sababu ukienda kutizama nini kinaendelea eti na wao wanakutizama design kama wewe fala umekuja eeh ukipiga hatua kadhaa wanaliamsha dude tena basi kukutesa tu..
 
bora kondoo mara mia n wastaarabu sana...ila wakianza pigana kaa mbali
 
Hongereni
Mwezi uliopita nilijitia kiherehere kununua ng’ombe wa kienyeji, alitaka kunipa kesi ya mauaji baada ya kumpiga jirani

Nimeishia kumchinja siku ya Eid,
Sitaki tena mnyama Mwenye miguu minne kwangu
Sasa jirani yako analeta umbea kwenye nyumba za watu ng’ombe afanyeje

Ng’ombe ukiona amekupiga kuna mambo mawili

Unapiga umbea sana kumhusu

Unamuangalia demu wake kimatamanio😁😁😁

Hilo la umbea anaweza kukufikiriapo akakupa karipio tu

Ila hilo jingine zea iz no wei aut
Lazima akutaitishe tuπŸ˜‚
 
🀣🀣🀣 alitaka kunisababishia kesi
 
Mbuzi anaweza akawa anatafuna kitu hicho kitu ni kama vile hakiishi hapo yupo bandani ambapo hamna majani lakini unamuona anatafuna kitu kama.mtu anavyotafuna bigijii
 
Unafugia wapi ndugu.
 
πŸ˜…πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ ukifuga mbuzi unakuwa kichaaa et unamng’ata masikio una matatizo ya akili
 
Mbuzi anaweza akawa anatafuna kitu hicho kitu ni kama vile hakiishi hapo yupo bandani ambapo hamna majani lakini unamuona anatafuna kitu kama.mtu anavyotafuna bigijii
Wana matumbo manne , mchana huwa wanapakia , usku ndo wanatafuna
 
Mbuzi ni viumbe wazuri ila wasumbufu .
Nafuga mbuzi ila ni mgeni kwenye haya mambo wiki mbili mbuzi wangu wanne wamefariki kisa kilikuwa hivi .

Ninaye kijana anawafuga ila jioni anawaleta kwangu hivyo alfajiri anawafuata pia , sasa siku hiyo wamerudishwa jioni nilisahau kufunga stoo ya mahindi .

Usiku wakaingia hao wanne wakala mahindi kwa kiasi walichopenda .

Asubuhi naamka nakuta hao wanne wanataabika kwa kupumua kwa shida na pia matumbo yao yamevimba sana .

Basi nikaamua niulize kwa watu kuwa hiki ni nini wakasema hao wamekula mahindi makavu na hapo wasinywe maji wakinywa maji watakufa , hivyo wanadai niwalishe magadi ili watoe gesi tumboni nikajisemea wacha niwape hayo magadi ila mpaka inafika mchana mbuzi wanapumua kwa shida na ni kama wanataka kufa .

Nikiwaza kumpiga bwana mifugo naogopa maana siku mbili nyuma tuligombana kisa pombe huko bar maana mimi niliwahi kufika hapo bar nikakuta kuna uhaba wa bia kulikuwa na bia tisa tu kwenye ile bar na hapa kijijini inatokeaga bar zote hazina bia hivyo ni mpaka ushuke mjini .

Hivyo nikamwambia muhudumu aziache kwenye friji na pia nikalipia nikawa nachukua moja moja nafurahia maisha alipokuja bwana mifugo naye anaforce apewe tatu wanamwambia zimenunuliwa haelewi anaforce ikabidi niingie front kumwambia nakuzingua sio mda hivyo tuliza tamaa zako .

Akapoa sana ila kwa vile ananiogopa na kuniheshimu , sasa nakuja kupata story mtaani ananikandia naringa sana .

Hivyo hata kumpigia sikuweza nikawa najua hatoweza kuwasaidia mbuzi wangu .
Basi saa saba ndiyo muda watoto wangu mbuzi walianza kupukutika , alianza mwanangu Celine , akaja mtoto wangu Cloude , akafuata Chriss na mwisho binti yangu mdogo Chyna alifariki saa kumi na moja jioni .

Ilikuwa siku ya huzuni sana kwangu na nyumba ilikuwa kubwa sana , niliwazika pembezoni na nyumba yangu nikiwa na ndugu zao wakubwa sita ila pia mbwa wangu kipenzi Chizika alikuwepo na alishuhudia mazishi yale mwanzo mwisho , pamoja na rafiki yangu na msiri wangu paka bwana Cherish naye aliona kila kitu .

Ni hivyo ndugu kuhusu usumbufu sijui lolote nawaona ni wazuri tu kikubwa wawe na kamba na pia uwe na sehemu maalumu ya kufugia japo sikatai kuwa ni viumbe wenye resistance sana wakiamua .

Endeleeni kupumzika nawakumbuka sana Celine , Cloude , Chyna na Chriss njia ni yetu sote .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…